Dar es Salaam yaongoza kwa kuvutia wawekezaji
Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam limetajwa kuwa la kwanza
kati ya majiji 20 yenye fursa zaidi barani Afrika likiongoza katika
kipengele cha kuvutia wawekezaji na kipengele kidogo cha ukuaji wa pato
la taifa (GDP).
Kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa juzi na Shirika
la Ukaguzi wa Mahesabu la PwC, Jiji la Dar es Salaam pia lina sifa ya
ukuaji wa kasi wa idadi ya watu kwa kuwa na alama 19 kati ya 20, ukuaji
wa kundi la watu wenye kipato cha kati (alama 15 kati ya 20), huku
likiboronga katika vipengele vya urahisi wa ufanyaji biashara (9), na
mvuto wa uwekezaji wa kigeni (8).
Katika eneo hilo, jiji hilo ambalo ni kitovu cha
biashara nchini, linafuatiwa na majiji ya Lusaka (Zambia), Nairobi
(Kenya), Lagos (Nigeria), Accra (Ghana) na nafasi ya 10 katika kipengele
hicho ikishikwa na Jiji la Cairo (Misri).
Katika nafasi ya jumla ya kifursa barani Afrika,
Dar es Salaam limetupwa katika nafasi ya 15 nyuma ya majiji ya Nairobi,
Kigali, na Kampala, katika nafasi ya 10.
Katika ripoti hiyo iitwayo ‘Ndani ya Afrika:
Majiji yenye fursa’ na kusainiwa na Paul Monekosso Cleal, Pierre-Antoine
Balu na Jonathan Cawood, PwC katika fursa za jumla ilichambua hali ya
miundombinu, nguvukazi, uchumi na jamii pamoja na sifa za watu wa majiji
husika.
“Jambo la msingi ni kwamba maendeleo ni suala la
hatua mbalimbali katika kipindi fulani. Lakini hatua hizo ni lazima
ziratibiwe vizuri na kutekelezwa kwa wakati.
“Tunaamini kuwa uchambuzi ulioanishwa katika
ripoti yetu utawapa fursa watunga sera, wafanyabiashara na wawekezaji
kuendelea na mikakati yao ya kimaendeleo yenye tija katika majiji
husika,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.
Ripoti hiyo ilieleza kuwa kuwapo kwa fursa hizo
hakumaanishi hakuna changamoto katika majiji hayo na kwamba kila jiji
lina mazuri yake na mabaya yake na kuongeza kuwa uchambuzi wa namna hiyo
ni kazi endelevu