Ukatili: Mama amtesa mwanae na kumpa majeraha mengi mwilini....
Mwanamke mmoja mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, Violet
Manyondo (40) anadaiwa kumtesa na kumfanyia vitendo vya kikatili mtoto
wake wa kumzaa, anayejulikana kwa jina la David (14).David ambaye ni
mwanafunzi wa darasa la tano katika shule moja ya msingi iliyopo
Mzambarauni, Dar kwa sasa haendi shule kutokana na majereha aliyonayo
kiasi cha kuwaliza majirani.
Akizungumza na Amani, mmoja wa majirani aliyeomba hifadhi ya jina
lake, alisema ni mara yake ya kwanza kushuhudia mama akimtesa mtoto
wake wa kumzaa kama anavyofanya mama huyo.
“Tunaomba vyombo vya haki za binadamu hata Jeshi la Polisi kushughulikia tukio hili haraka iwezekanavyo vinginevyo mtoto huyo ataathirika kisaikolojia, halafu cha kushangaza, ana watoto watatu, lakini ni huyu tu ndiye anayekutana na kipigo,” alisema jirani huyo.

Alisema katika kumsaidia kijana huyo, wamewahi kwenda kituo cha
polisi Gongo la Mboto, lakini polisi jamii walipokwenda nyumbani hapo,
waliambulia matusi.
Mtoto David alimwambia mwandishi kuwa ni kweli mama yake anamtesa kwa muda mrefu na kwamba hivi karibuni alikwenda kumshtaki katika kanisa lao liitwalo Universal Ufalme wa Mungu, Mzambarauni, Ilala, Dar na alipotakiwa kumwita mama yake alikataa kwenda.

“Baada ya mama kupata wito ule hata kanisani ameacha kwenda kwa
kuhofia kikao na ushauri wa viongozi wa kanisa. Sina cha kufanya wala
pa kwenda, namuomba Mungu anisaidie nimalize shule,” alisema kijana
huyo.
Kuhusu sababu za kuteswa, alisema hafahamu chochote, ingawa
alihisi huenda ni kwa sababu ya baba yake kutopeleka hela ya matumizi
nyumbani, kitu ambacho hata hivyo hafahamu kwani hamfahamu mzazi wake,
zaidi ya kusikia kuwa ni dereva wa daladala.
Katika hali ya kushangaza, mama huyo alipotafutwa na mwandishi, alijibu kijeuri;
“Yule ni mwanangu, naweza kumfanya lolote lile. Mimi ni mzazi wake,
natakiwa kumrekebisha kwa njia yoyote.”