Muuguzi anayedaiwa kutekwa wiki iliyopita apatikana, ahojiwa na polisi
Dar es Salaam. Muuguzi wa Hospitali ya Mwananyamala, Pili
Amiri aliyetekwa Machi 12, amepatikana usiku wa kuamkia jana baada ya
watekaji hao kudaiwa kumtupa katika pori moja lililoko Dar es Salaam.
Hata
hivyo, gazeti hili lilishindwa kufanya mahojiano na muuguzi huyo jana
kwa kuwa alikuwa akihojiwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay,
kuanzia saa nne asubuhi hadi mwandishi alipoondoka kituoni hapo saa 11
jioni.
Kwa mujibu wa shangazi yake Pili, Fatuma Mbasa,
muuguzi huyo alirudi nyumbani saa 10 alfajiri jana akiwa katika hali ya
kulewa na makovu kadhaa shingoni.
“Inaonekana walimpa
dawa za kulevya kwa sababu alikuwa kama teja, hajiwezi na ana majeraha
kadhaa na alikuwa akilalamika kuwa na maumivu shingoni,” alisema Mbasa.
Alisema licha ya kuwa Pili alikuwa hawezi kuzungumza vizuri, lakini alisema watekaji hao walimpa mateso makali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema Pili pamoja na watu wengine saba wanahojiwa kuhusu tukio hilo.
“Kuna mambo mengi tumeyagundua kuhusu utekaji huu,
lakini tutayaeleza baada ya kuwa tumeshawahoji. Ingawa amepatikana
lakini hatuwezi kutoa ripoti nusu nusu,” alisema Wambura na kuongeza:
“Matukio
ya utekaji yapo, sisi kazi yetu siyo kulifanyia kazi tukio hili moja,
lakini tutahakikisha kupitia tukio la pili, tutajua kwa kina mchezo
unavyofanyika na kuuzuia ili usijirudie tena.”
Mjomba
yake Pili, Amiri Kangile alisema siyo kwamba familia hiyo ni ya watu
wenye uwezo wa kifedha lakini waliamua kutoa kiasi hicho cha fedha kwa
watekaji ili kumuokoa ndugu yao.
Alisema kwa mujibu wa
maelezo ya awali ya Pili, watekaji hao walikuwa wakimwamuru akatoe fedha
katika akaunti yake ya NMB akiwa chini ya ulinzi mkali.
“Anasema
walikuwa wakimsindikiza mpaka kwenye ATM na kumsimamia ili atoe fedha
na kisha kumfunga tena kitambaa na kuondoka naye kusikojulikana,”
alisema.
Kangile alisema kwa mujibu wa Pili, watekaji
hao walimtoa katika pori ambalo halifahamu na kumfikisha kwenye barabara
kubwa na kumuamuru akimbie bila kugeuka.
Posted Thursday, March 19, 2015 | by- Florence Majani