Kili Music Award 2015?
Msimu wa utoaji tuzo kwa wasanii wa muziki Tanzania
wanaofanya vizuri umewadia huku mchakato wa awali wa mchanganuo wa tuzo
hizo za Kili Tanzania Music Awards 2015 (KTMA) ukianza rasmi wiki hii.
Wakati
mchakato huo ukisubiri mashabiki kuamua msanii yupi aingie katika
kipengele kipi, wasanii wengi watakuwa matumbo joto kwa kile
kinachoelezwa kwamba KTMA sasa zimekubalika zaidi kwao na mashabiki wa
muziki.
Hata hivyo, msimu huo unatojawa kuwa wenye
neema kwa wasanii, unazua maswali mengi vichwani mwa wasanii na
mashabiki wao moja likiwa; ni nani atavunja rekodi iliyowekwa na
mwanamuziki Diamond Platnumz mwaka jana?
Mbali na
Diamond kuvunja rekodi msimu uliopita, Bendi ya muziki wa dansi ya
Mashujaa pia iliwahi kunyakua tuzo tano mwaka 2013, huku wasanii, Kala
Jeremiah na Ommy Dimpoz wakinyakua tuzo tatu kila mmoja.
Shabiki
wa muziki wa kizazi kipya na mfanyabiashara katika Soko la Kariakoo,
Omary Shaban alisema ushindani kwa mwaka huu utakuwa mkubwa kwa tuzo
hizo, hasa ikizingatiwa uwepo wa wanamuziki wengi wazuri waliofanya kazi
tofauti, zenye ubora na viwango vya juu.
“Mwaka jana
Diamond Platnumz alinyakua tuzo nyingi kwa kuwa alijaribu kufanya kitu
tofauti, lakini alichokifanya na wengine wamefanya. Hivyo, ana ushindani
mkubwa, pia Alikiba ambaye alikuwa kimya amerudi. Hawa wawili ni
washindani wakubwa, hivyo video zao zitalumbana sana, yaani tunasubiri
kumjua mkali nani,” anasema Shaban.
Mshabiki mwingine,
Ally Elly wa Dar es Salaam alisema ni vyema kusiwepo ubabaishaji ili
wapatikane washindani na washindi halisi wa tuzo hizo kwa mwaka huu.
Mchakato utakavyokuwa
Waandaji
wa mashindani hayo walisema kuwa kwa mwaka huu kuna ongezeko la baadhi
ya mambo, lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa tuzo hizo na kuwapa fursa
Watanzania kupendekeza wasanii watakaowania tuzo hizo kwa kuwapigia kura
waingie kwenye kinyang’anyiro kwa njia tatu kuu.
“Tumekuwa
na juhudi za makusudi za kutenga fungu kubwa na kuongeza ushiriki wa
wataalamu kwenye fani husika ili kuziendeleza, kuzikuza na kuziongezea
thamani na umaarufu wa tuzo hizi kimataifa mwaka hadi mwaka,” alisema
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli. Bia hiyo ndiyo wadhamini
wakuu wa tuzo hizo
“Wananchi watapata fursa ya kupiga
kura kupendekeza wasanii katika vipengele mbalimbali kwa kutumia njia
tatu; kwa mfumo wa website ya www.ktma.co.tz, mfumo wa mtandao wa
WhatsApp na kwa njia ya SMS.”
Alisema katika WhatsApp,
mpigakura ataweza kutumia namba ya simu na SMS kwa kutuma ujumbe wa neno
KTMA au KILI na kisha kufuata maelekezo kwa ajili ya kukamilisha zoezi
hilo litakaloanza rasmi Machi 30 hadi Aprili 19, mwaka huu
litakapositishwa.
Kwa mujibu wa waandaji, baada ya
upigaji wa kura kutakuwa pia na michakato mwingine wa kuwatafuta
washindi, mpaka mwisho wa utoaji wa tuzo hizo ikiwamo kuchuja
wapendekezwa kabla ya kuwarudisha tena kwa wananchi na kupigiwa kura za
ushindi kuanzia Mei Mosi
posted Wednesday, March 25, 2015 | by- Herieth Makweta