Stara Thomas Awaponda Wasanii na Maproducer wa Bongo Flava


Msanii wa muziki Stara Thomas amefunguka kwa kusema kuwa wasanii wanashindwa kufika mbali kutokana na uoga na kutokuwa serious na kazi zao.

Stara ameiambia Bongo5 kuwa wasanii wa sasa wanashindwa kujitanua zaidi.

“Asilimia kubwa ya wasanii waoga, bado wamekuwa na akili za kujiangalia hapa walipo, wengi bado hawajapata akili ya kutoka na kujitegemea wenyewe nje, hii inawafanya wasanii wengi wasikue wabaki pale pale,” alisema Stara.

Pia Stara alisema watayarishaji wa muziki wanachangia kuuangusha muziki kutokana na kushindwa kuwa wabunifu.

“Wapo maproduce wazuri lakini njia wanazo zitumia zinafanya muziki unafanana, wengi wanakuwa wanaandika juu wa beat tofauti na zamani sisi tunaandika kwanza ndo beat inatengenezwa, kwahiyo unakuta anayeandika anakuwa controlled na beat, kwahiyo kama producer alitengeneza beat inafanana katika watu watatu au wanne basi hata kile kinachokuja kuimbwa kitapenya katika ile melody,” alisema Stara.

Pia Stara ameongeza kuwa sasa amerudi rasmi kwenye muziki huku akiwataka mashabiki wa muziki wake kuendelea kusupport kazi zake.
Powered by Blogger.