Wanamichezo wanaoutaka ubunge mwaka huu
Wakati vuguvugu la uchaguzi mkuu wa mwaka huu likiendelea
nchini, Tasnia ya michezo nayo imeanza kupata msukumo kwa wanamichezo
kujitosa katika kinyang’anyiro hicho kwenye uchaguzi utakaofanyika
baadaye mwaka huu.
Tayari wanafamilia wa michezo wanne, wametangaza
nia ya kuhakikisha wanachukua majimbo kwenye uchaguzi huo kupitia Chama
cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Wanamichezo hao ni: Wilhelm Gidabuday (anagombea kupitia Chadema)
Bondia Mada Maugo
Huyu ana kumbukumbu nzuri katika tasnia ya michezo hasa riadha kwani alikuwa mstari wa mbele kukosoa maandalizi waliyopewa wanariadha wa Tanzania walioshiriki michezo ya Jumuiya ya Madola mwaka jana nchini Scotland.
Gidabuday amejitosa kuwania ubunge wa Jimbo la
Hanang kwa tiketi ya Chadema, jimbo linaloshikiliwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Mary Nagu wa CCM.
“Kwa kuamini kwamba kugombea nafasi yoyote ni haki
ya msingi kikatiba, mimi kabla ya kujitathmini mwenyewe nimefanyiwa
tathmini na watu wa rika tofauti ndani ya jamii, makundi hayo
yakiwakilisha watu wenye busara katika jamii na kuniweka katika orodha
ya watu wenye sifa stahiki,” anasema Gidabuday.
Ataitetea michezo bungeni
“Wananchi wa Hanang pia wameridhishwa na harakati
zangu za kutetea wanamichezo, hususan riadha kitaifa, Watanzania wengi
wananifahamu kwa jina la (mwanaharakati wa michezo Tanzania). Harakati
zangu michezoni zimenifanya kuaminiwa na wadau wa michezo kote
Tanzania,” anasema Gidabuday.
“Sheria namba 12 ya Baraza la Michezo Tanzania
(BMT) ya mwaka 1967 licha ya kukosa meno, lakini pia imedharauliwa na
viongozi wa wizara, BMT wenyewe na taasisi zilizokusudiwa kusimamiwa na
sheria hiyo, na matokeo ya udhaifu huo umesababisha ufisadi ndani ya
vyama vya michezo, ndiyo maana Tanzania tumekuwa watalii katika viwanja
vya michezo kimataifa.
Ili kuondoa hali hiyo nitatoa hoja binafsi sheria
hii ibadilike sambamba na kuikumbusha Serikali umuhimu wa kuwa na
kijiji cha michezo,” anasema Gidabuday.
Mada Maugo (anagombea kupitia Chadema)
Bondia huyu anajitosa kwa mara ya kwanza kuwania
ubunge wa Jimbo la Rorya kwa tiketi ya Chadema, jimbo hilo sasa
linaongozwa na Lameck Airo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).