Ukawa kujadili mvutano wa majimbo Ijumaa
>
Viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)
Viongozi wa ngazi za juu wanaounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) watakutana Ijumaa wiki hii kutafuta mwafaka katika
mvutano uliopo katika majimbo 19 ya uchaguzi, yakiwamo manne ya Dar es
Salaam, Mwananchi limedokezwa.
Taarifa kutoka ndani ya
wanachama wanaounda umoja huo, zinaeleza kwamba, viongozi watakaokutana
ni wenyeviti wa vyama, makamu wenyeviti, makatibu na wajumbe wa
sekretarieti kutoka ndani ya vyama hivyo.
Umoja huo
ulioanzishwa Februari mwaka jana wakati wa Bunge Maalumu la Katiba,
ukiundwa na vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD kabla ya kusaini
makubaliano (MoU) kwa ajili ya kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi
zote kuanzia udiwani, ubunge na urais.
Siku chache
zilizopita, kamati maalumu ya Ukawa ilikamilisha kazi ya ugawaji wa
majimbo 170 lakini ukawapo mvutano katika majimbo 19 ambayo vyama zaidi
ya kimoja vinayataka, yakiwamo ya Segerea, Kinondoni, Kigamboni na
Ukonga ya Dar es Salaam, Morogoro Mjini na mengine ya mikoa ya Mwanza,
Shinyanga na Kagera.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bara,
Magdalena Sakaya alithibitisha kuwapo kwa kikao hicho na kuwa kitakuwa
na ajenda ya kukusanya maoni na mapendekezo ya wanachama, kujadiliana
kwa pamoja ili kufikia muafaka wa majimbo hayo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa pia alithibitisha kuwapo kwa mkutano huo.
“Mkutano utakuwapo na utafanyika Zanzibar kwa mujibu wa ratiba za Ukawa,” alisema Dk Slaa bila kutaka kuingia kwa undani.
Alipoulizwa
kuhusu utata katika mgawanyo wa majimbo, Dk Slaa alisisitiza kwamba,
busara pekee ndiyo itatumika kumaliza mvutano uliopo. Hata hivyo, Dk
Slaa alikanusha kuwapo kwa mvutano katika majimbo 28 huku akilalamikia
upotoshaji uliofanyika kwa vyombo vya habari. “Hizo taarifa siyo za
kweli na tumekuwa na utaratibu wa kutoa tamko la pamoja, nisingependa
kueleza lolote zaidi ya hapo ila tusubiri vikao vya Ukawa, ni hatari
sana kutoa taarifa ambazo siyo sahihi na zisizokuwa na lengo la kujenga
umoja huu,” alisema Dk Slaa.
Katibu Mkuu wa
NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema katika hatua za kutafuta
maridhiano ya majimbo hayo, vyama vyote vinapaswa kutambua kila nafasi
ya chama kilichoshiriki kwenye makubaliano ya Ukawa.
“Tukifuata
kanuni nadhani kuna vyama ambavyo havitakuwa na nafasi Ukawa na
haitakuwa na maana ya kuungana, kwa hivyo lazima busara itumike zaidi
haiwezekani chama fulani kilazimishe kuchukua majimbo mengi kuliko
kingine,” alisema Nyambabe.
posted Tuesday, March 24, 2015 | by- Kelvin Matandiko