Zao la muhogo linavyoweza kuwa na manufaa kiuchumi
Kadri siku zinavyozidi kwenda kumekuwepo juhudi za makusudi za uendelezaji wa zao la muhogo nchini.
Imeshuhudia
taasisi kadhaa zinazojihusisha na kilimo zikitilia mkazo kilimo cha zao
hilo na hata kuwafahamisha wakulima umuhimu wake.
Hivi
karibuni Asasi ya Wanawake ya Kupambana na Umasikini (Iwapoa) na Umoja
wa Wanawake Wanasiasa (Ulingo), iliendesha mafunzo ya matumizi ya unga
wa muhogo kwa wanawake wa Wilayani ya Temeke ikilenga kuwakwamua
kiuchumi kupitia zao hilo.
Kupitia mafunzo hayo,
wanawake wakaelimishwa juu ya umuhimu wa zao la mhogo na kiwamba
likitumika vizuri laweza kuwa na manufaa mengi kuliko aina nyingine za
mazao na hasa ikizingatiwa kuwa bei yake ni nafuu.
Faida za muhogo
Wakufunzi
mbalimbali waliweka bayana faida za zao hili, miongoni zikiwa ni majani
yake kutumika kama mboga na kiazi chake, kutumika kama chakula kwa
namna mbalimbali.
Katika viwanda, mazao yanayopatikana
katika mzizi (mhogo), miti na majani huweza kuzalisha bidhaa anuwai.
Baadhi ni vifaa vya nguo, karatasi, mafuta, kilevi, dawa za binadamu na
plastiki.
Vilevile, wanasema wanga wa muhogo hutumika kutengeneza dawa za madoa, gundi katika samani, rangi za awali za ukuta na sukari.
Unga wake nao hutumiwa kutengeneza vitu mbalimbali vikiwamo vitafunwa vinavyopendwa na watu wengi nchini.
Baadhi ya vitafunwa hivyo vinatajwa kuwa ni pamoja na keki, mikate, skonzi, biskuti na mandazi.
Umuhimu wa muhogo umekuwa ukiwachochea wadau wa kilimo nchini kuhakikisha kuwa zao hilo linatumika kuleta tija kwa mtu mmoja.
Wakufunzi
wanaeleza kuwa muhogo kwa kawaida huchukuliwa kama zao la ziada lisilo
la muhimu na ni jamii chache ambazo hulitegemea kwa chakula na biashara.
Ni
ukweli usiopingika kuwa hapa nchini hata katika nchi nyingine za
Afrika, muhogo umekuwa ukichukuliwa kama zao la chakula kwa watu
maskini.
Wakulima wengi, japo wamekuwa wanapanda muhogo kwenye mashamba yao lakini huyapa kipaumbele, mazao mengine.
Mwenyekiti
wa Iwapoa, Paskazia Sezari anasema: “Unajua awali watu wengi walikuwa
wakifahamu kuwa unga wa muhogo unatumika kwa ugali na kuchemsha au
kukaanga jambo ambalo sio kweli. Kupitia unga wake, tunaweza kupata
vitafunwa vingi kama vile keki, maandazi, tambi na hata bagia,” anasema.
Kwa
wale wanaopenda kutengeneza tambi, anasema unga huu utakuwa ndio
suluhisho, kwani awali kina mama wengi walikuwa wakikwamishwa na bei ya
unga wa dengu hasa wanapoamua kujikita kwenye biashara hiyo.
Bei ya unga wa muhogo ni kati ya Sh800 hadi 1000 kwa kilo, huku bei ya kilo moja ya unga wa dengu ni Sh2000 hadi Sh2400.
Anashauri
wanawake wajasiriamali kujifunza namna ya kutumia mihogo kama chanzo
cha kipato. Iwapo wengi watakuwa na taaluma hiyo, anasema itasaidia kwa
kiasi kikubwa kupandisha thamani ya zao hilo na hivyo kuwapa hamasa
watanzania kulilima kibiashara kama ilivyo kwa mazao mengine.
Ofisa
usimamizi mafunzo na tathmini kutoka shirika la Chakula na Lishe, Loyce
Murusuri anasema mhogo ni chakula chenye faida nyingi kiafya.
Kwa sababu hiyo anasema pamoja na faida nyingi za kibiashara, zao hilo ni muhimu kwa afya za walaji.
“Taasisi
ya chakula na lishe ni miongoni mwa wadau wakuu wanaohamasisha kilimo
cha zao la muhogo, kutokana na kufahamu faida zake kiafya,” anasema
akifafanua:
“Tumekuwa tukiandaa mafunzo kwa lengo la
kuwajengea uwezo wananchi na pia kuwahamasisha watu wengi kutumia zao
hili lililopuuzwa kipindi cha nyuma”.
Wajasiriamali
Maria Mapunda kutoka Buza anasema kuwa mafunzo hayo yatamuwezesha kupiga hatua kwenye shughuli zake za ujasiriamali.
“Kwani
baada ya kuelewa matumizi mbalimbali ya unga wake, sasa naweza kuchagua
aina moja ya kitafunwa kwa mfano tambi na kutengeneza kwa ajili ya
kuuza”.
Halima Hamad kutoka Yombo Makangarawe anasema
kuwa awali alikuwa akifanya biashara ya kuuza matunda, hivyo baada ya
kupata mafunzo hayo, sasa ameamua kubadilisha muelekeo.
“Najipanga kutengeneza tambi, kwani najua naweza kuziuza shuleni na kujiingizia kipato zaidi, tena kwa gharama nafuu”
Zao kimataifa
Kilimo cha muhogo ni zao, linalohamasishwa kitaifa na kimataifa.
Mwaka
2008, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa, (FAO) lilitangaza kuwa,
ulimaji wa muhogo waweza kuepusha mabaa ya njaa na kuwa chanzo cha
nishati katika nchi zenye matatizo ya chakula na kukabiliana na bei ya
mafuta ya nishati.
Hata hivyo zao hili liliendelea kudharauliwa na kuonekana ni mzizi wa hamu na chakula kwa maskini.
Baada
ya muda mfupi, Afrika imeshuhudia, watu zaidi ya 11 milioni wakikumbwa
na janga la njaa katika pembe ya Afrika (Somalia, Sudan, Kenya) mwaka
huu ilhali suluhisho lilikuwepo mikononi mwetu.
Posted Thursday, March 19, 2015 | by- Maimuna Kubegeya