Tanzania mwenyeji wa Jukwaa la vijana Afrika na China
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM ) ,Sixtus Raphael Mapunda
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete anatarajiwa kuzindua Jukwaa
la kimataifa la vijana kutoka nchi 43 za Africa na China lenye lengo
la kudumisha urafiki ,ushirikiano wa kimaendeleo katika Nyanja za
kiuchumi ,kijamii na kisiasa.
Mkutano wa Jukwaa hilo
ambalo Tanzania ni mwenyeji wake utahusisha pia vyama vya siasa 57,
wafanyabiashara vijana 32 ambao kwa pamoja watajadili ushirikiano kati
ya China na bara la Afrika katika kuleta maendeleo.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UVCCM ) ,Sixtus Raphael Mapunda
amesema jukwaa hilo litafanyika kuanzia machi 27 hadi 31 mwaka huu
katika ukumbi wa Hoteli ya Ngurudoto Mkoani Arusha
“Tunatarajia
kupokea ugeni mkubwa wakati wa mkutano wa jukwa hili, nchi 43 kutoka
Afrika zitahudhuria, vyama vya siasa 57 vitashiriki pia kutakuwa na
wafanyabiashara vijana 32 kutoka nchi mbalimbali za Africa.
Amesema
Tanzania itawakilishwa na vijana 70 na vijana wengine 50 watatoka
nchini China ambapo lengo kuu ni kujadili fursa zilizopo na jinsi ya
kuzifikia kwa ajili ya maendeleo ya Vijana wa Africa ikiwa ni pamoja na
kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza Afrika.
Mapunda
ameongeza kuwa hii ni mara ya tatu ya kufanyika kwa mkutano wa jukwaa
hilo ambapo mara ya kwanza lilifanyiak mwaka 2011 katika mji wa
Windhoek nchini Namibia na kufuatiwa mwaka 2012 Beijing China ambapo
walijadili uhusiano wa fursa katika biashara utumike kwa maendeleo.
Amesema
kuwa jukwaa hilo litajadili maendeleo ya mahusiano kati ya Africa na
China ,ushiriki uhusiano wa vijana katika maendeleo na wajibu wa asasi
zisizo kuwa za kiserikali katika kukuza mahusiano na maendeleo kati ya
china na Africa.
Aidha amesema mgeni rasmi katika
ufunguzi wa jukwaa hilo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh.Dr.Jakaya Kikwete ambapo ataambatana na Waziri wa mambo ya
ndani wa China, Waziri wa Biashara na Viwanda, Dk Abdallah Kigoda na
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene