Sadiki alia na wezi wa maji Dar
KATIKA kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya maji
Duniani, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiki amesema Mamlaka
ya Maji Safi na Majitaka inatarajia kuanza kuzalisha maji kiasi cha lita
710milioni zaidi ya mahitaji ya sasa ambayo ni lita 450milioni ifikapo
mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari kuhusu namna Serikali itakavyoshiriki maadhimisho hayo, Sadick
amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto kama vile uhaba wa vyanzo vya
maji, Ukame, uchafunzi wa vyanzo vya maji pamoja na wizi wa maji
Serikali imeendelea kubuni mbinu mbadala wa kukabiliana na changamoto
hizo.
Amesema Upanuzi wa mitambo ya Ruvu juu na Ruvu
chini, uchimbaji wa visima virefu vya maji , ujenzi wa bwawa la Kidunda
na upanuzi wa mifumo ya majisafi na majitaka ni moja ya mikakati ya
kuhakikisha kuwa malengo ya kuzalisha maji kwa kiwango kinachohitajiwa
yanafikiwa.
“Mkoa wa Dar es Salaam unatekeleza jumla ya
miradi 41 ya visima vya maji katika halmashauri zote, pia tunatekeleza
miradi mingine 15 chini ya ufadhili wa Ubelgiji, miradi yote hii
imebuniwa ili kuhakikisha kuwa zaidi ya wananchi 3.8 milioni wanapata
maji safi na salama”, amesema Sadiki.
Amesema shughu za
maadhimishi zimeanza leo kwa kuelimisha wananchi kuhusu sera ya
maji ikiwa ni pamoja na kuzindua bomba la maji na kupanda miti katika
mtaa wa Mongolandege Kata ya Ukonga Manispaa ya ilala, jiini
Dar-es-saalam.
Sadiki ametoa wito kwa wananchi wa Dar es Salaam
kutunza kulinda na kuheshimu miradi yote ya maji kwa kuzingatia kauli
mbiu ya maadhimishi ya mwaka huu ianyosema Maji kwa maendeleo endelevu
Amesema
miradi iliyo kamilika kwa sasa na iliyoanza kutoa huduma ni miradi
14 ambayo ni Ilala miradi 5 ya segerea ugombolwa,pugu kimani , Temeke
miradi 5 ya kijichi, kibonde majiB na Uwazi, Kinondoni miradi 4
ya Tandale, Mburahati na Kwembe”
Amesema zaidi ya
asilimia 50 ya maji yanayozalishwa kwa siku hupotea ama kuibiwa na watu
wasiokuwa na mapenzi mema , hivyo aliziagiza mamlaka husika kuhakikisha
kuwa inachukua hatua kali dhidi ya wale wote watakaobainika kuiba maji
kwa njia moja ama nyingine.
Pamoja na hayo Sadiki
aliitaka Dawasa kuhakikisha kuwa inakarabati mara kwa mara mifumom yake
ya maji ili kupunguza kama si kumaliza kabia upotevu wa maji unaotokana
na miundombinu iliyochakaa.
Aidha Sadiki ametoa wito
kwa wawekezaji kujitokeza na kuwekeza katika sekta hiyo kwani ni moja
ya sekta muhimu kwa ustawi wa taifa.