Nay Afunguka: ' Sina Mke Sijaoa na sina mahusiano ya kimapenzi na Mwanamke yoyote Yule'

Msaniii Emmanuel Elibarick alimaarufu kama Mr Nay ameonesha dalili ya wazi kuwa hana mpango tena wa kuwa katika mahusiano na Mchumba wake huyo Siwema ambaye amezaa nae mtoto wa kiume aitwae Curtis miezi kadhaa iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instgram Nay wa mitego siku mbili zilizopita aliweka post ambayo ilikuwa inasema kuwa kwa sasa ana watoto watatu na ana mapenzi ya kweli na watoto wake lakini hana mpango wala hana mahusiano ya kimapenzi na mama wa watoto wake hao bali anawaheshimu wanawake hao kama wazazi wenzake.

"Mr_Nay Baba wa watoto watatu... Sina Mke I mean Sijaoa na sina mahusiano ya kimapenzi na Mwanamke yoyote Yule... Kati ya niliozaa nao. Nawapenda watoto wangu nawaheshim mama zao..SingleBoy am in love with my son and daughters... Rishma, Curtis na Munie"
Powered by Blogger.