NYANZA: Walimu kortini kwa kuuza mafuta ya albinoADVERTISEMENT Mwanza. Walimu wawili wa Shule ya Msingi Maalumu Mtindo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo wilayani Misungwi mkoani Mwanza, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuuza mafuta ya ngozi kwa ajili ya albino. Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) wilayani Misungwi, iliwapandisha kizimbani juzi kwenye Mahakama ya Wilaya Misungwi washtakiwa hao kwa tuhuma ya makosa manne ya uhujumu uchumi. Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Mwema Mella aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Fredrick Mworo (42) ambaye ni Mwalimu Mkuu Msaidizi na Mtunza Stoo, Velentina Ngodoki (34) mkazi wa Kijiji cha Misasi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Ngodoki Ginnery Supply, Mwenyekiti wa kamati ya shule, Kalunde Kushamba (60) na aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo mwaka 2012, Edesta Nshekanabo (32). Mella alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja kati ya Julai na Novemba 2012, walikula njama za kutenda kosa la kughushi mafuta aina ya Neutrogena chupa 200 yaliyotolewa msaada na Hospitali ya Rufani Bugando (BMC) kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) shuleni hapo na kuyafanyia zabuni ya thamani ya Sh5.6 milioni. Mshtakiwa wa kwanza na wa tatu, wanadaiwa Julai 19, 2012 wakiwa shuleni hapo, walighushi muhtasari wa kikao cha kamati ya shule kwa kuidhinisha ununuzi wa mafuta hayo, yaliyopokelewa ukiwa ni msaada kwa albino. Shitaka la pili na la tatu linawahusu mshtakiwa wa kwanza na wa tatu wanaodaiwa kuwa Novemba 2, 2012, walitumia vibaya nyaraka kwa lengo la kudanganya na kujipatia fedha, au faida kwa kughushi hati bandia ya ununuzi namba 32/11 ya chupa 200 za mafuta aina ya Neutrogena. Shitaka la nne, tano na sita kwa washtakiwa wa kwanza na wa tatu, wanadaiwa Novemba 11, 2012 walitumia nyaraka za uongo za kudadisi bei kwa Kampuni bandia ya Madudi Ginnery Enterprises kwa Sh6 milioni, huku kampuni nyingine bandia ya CJC Lab and Surgicals (T) kwa Sh5.6 milioni. Pia, mshtakiwa wa kwanza na wa pili wanadaiwa Novemba 12, 2012, kwa kutumia nyaraka bandia kwa lengo la kudanganya na kujipatia Sh5 milioni kwa kutumia hati ya malipo namba 11/15 kulipa Kampuni ya Ngodoki kwamba wamepokea mafuta hayo. Shtaka la nane kwa mshtakiwa wa kwanza, tatu na wa nne, wanadaiwa kutumia vibaya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri kwa kuitisha zabuni hewa ya Kampuni ya Ngodoki ya Misasi na kununua chupa 200 za mafuta hayo ya ngozi kwa albino, yaliyotolewa bure na BMC. Washtakiwa wote walikana mashtaka, wapo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Hakimu Mfawidhi, Godfrey Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 13, itakapoanza kusikilizwa.
Mwanza. Walimu wawili wa Shule ya Msingi
Maalumu Mtindo na mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo wilayani Misungwi
mkoani Mwanza, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuuza mafuta ya
ngozi kwa ajili ya albino.
Taasisi ya Kupambana na
Kuzuia Rushwa (Takukuru) wilayani Misungwi, iliwapandisha kizimbani juzi
kwenye Mahakama ya Wilaya Misungwi washtakiwa hao kwa tuhuma ya makosa
manne ya uhujumu uchumi.
Mwendesha Mashtaka wa
Takukuru, Mwema Mella aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Fredrick Mworo
(42) ambaye ni Mwalimu Mkuu Msaidizi na Mtunza Stoo, Velentina Ngodoki
(34) mkazi wa Kijiji cha Misasi ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Ngodoki Ginnery Supply, Mwenyekiti wa kamati ya shule, Kalunde Kushamba
(60) na aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo mwaka 2012, Edesta
Nshekanabo (32).
Mella alidai kuwa washtakiwa kwa
pamoja kati ya Julai na Novemba 2012, walikula njama za kutenda kosa la
kughushi mafuta aina ya Neutrogena chupa 200 yaliyotolewa msaada na
Hospitali ya Rufani Bugando (BMC) kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi
(Albino) shuleni hapo na kuyafanyia zabuni ya thamani ya Sh5.6 milioni.
Mshtakiwa
wa kwanza na wa tatu, wanadaiwa Julai 19, 2012 wakiwa shuleni hapo,
walighushi muhtasari wa kikao cha kamati ya shule kwa kuidhinisha
ununuzi wa mafuta hayo, yaliyopokelewa ukiwa ni msaada kwa albino.
Shitaka
la pili na la tatu linawahusu mshtakiwa wa kwanza na wa tatu wanaodaiwa
kuwa Novemba 2, 2012, walitumia vibaya nyaraka kwa lengo la kudanganya
na kujipatia fedha, au faida kwa kughushi hati bandia ya ununuzi namba
32/11 ya chupa 200 za mafuta aina ya Neutrogena.
Shitaka
la nne, tano na sita kwa washtakiwa wa kwanza na wa tatu, wanadaiwa
Novemba 11, 2012 walitumia nyaraka za uongo za kudadisi bei kwa Kampuni
bandia ya Madudi Ginnery Enterprises kwa Sh6 milioni, huku kampuni
nyingine bandia ya CJC Lab and Surgicals (T) kwa Sh5.6 milioni.
Pia,
mshtakiwa wa kwanza na wa pili wanadaiwa Novemba 12, 2012, kwa kutumia
nyaraka bandia kwa lengo la kudanganya na kujipatia Sh5 milioni kwa
kutumia hati ya malipo namba 11/15 kulipa Kampuni ya Ngodoki kwamba
wamepokea mafuta hayo.
Shtaka la nane kwa mshtakiwa wa
kwanza, tatu na wa nne, wanadaiwa kutumia vibaya nyaraka kwa lengo la
kumdanganya mwajiri kwa kuitisha zabuni hewa ya Kampuni ya Ngodoki ya
Misasi na kununua chupa 200 za mafuta hayo ya ngozi kwa albino,
yaliyotolewa bure na BMC.
Washtakiwa wote walikana mashtaka, wapo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Hakimu Mfawidhi, Godfrey Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 13, itakapoanza kusikilizwa.