Pazia la tuzo za Kili Music lafunguliwa

 
Msimu mpya wa tuzo za Kilimanjaro Music Award‘KTMA’ umezinduliwa rasmi jana utatumia sh1 bilioni hadi kukamlika kwake.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro ambao ni wadhamini wa tuzo hizo PamelaKikuri alisema kuwa shindano hilo mchakato wake utaanza rasmi Machi 30, fainali zake zimepangwa kufanyika Juni 13.
.“Chini ya Kilimanjaro wasanii 400 wamenufaika na tuzo hizo ambazo mwaka huu ni mwaka wa 14 tangu kuanzishwa kwake,”alisema Kikuri.
Alisema zoezi la kupendekeza wasanii watakaoshiriki tuzo hizo litaanza rasmi Machi 30 hadi Aprili 19 na kwamba tuzo ya mwaka huu zina jumlaya vipengele 34.
“Kutakuwa na njia tatu za kupiga kura, facebook, WhatsApp, na njia ya website ya KTMA, na mshindi atapatikana kutokana na asilimia 70 ya kura zitakazopigwa na wananchi na asilimia 30 zitatoka kwa majaji.
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mungereza alisisitiza umuhimu wa wasanii kujisajili kwenye baraza hilo kwa kuwa mwakani hakuna msanii atakayehusishwa kwenye zoezi la tuzo kama hatakuwa amejisajili.
Meneja udhamini wa TBL, George Kavishe alisema msimu uliopita walifanyia maboresho kasoro zilizojitokeza kwa wasanii kujiondoa kwa kuwapa elimu ikiwa ni pamoja na kuwaalika usiku wa tuzo hizo
 posted Tuesday, March 24, 2015 | by- Vicky Kimaro
Powered by Blogger.