Majambazi wa nne sugu wamekamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za uporaji wa kutumia silaha,Morogoro.
Jeshi la polisi mkoa wa morogoro
limefanikiwa kukamata majambazi sugu 4 risasi 20 na bastola moja kwa
tuhuma za kuhusika na uporaji wa kutumia slaha na wengine kupora pochi
za wanawake na simu kwa kutumia pikipiki katika maeneo mbalimbali.
Kamanda wa polisi mkoa wa morogoro Leonardi Paulo amesema mnamo
februari 26 mwaka huu eneo la kilakala mjini morogoro kwenye geti la
kampuni ya BH LADWA wakati kijana Bhayik Peter 26 akiwa na wenzake saba
kwenye gari wakisubiri kufunguliwa geti ghafla majambazi walifyatua
risasi hewani na kupora shilingi milioni 56 na hundi ya shilingi miloni
tano na kutokomea kusikojulikana.
Katika hatua nyigine kamanda paulo amesema mnamo machi 26 eneo la
nanenane mjini morogoro watu watatu wakiwa kwenye pikipiki walimgonga
kwa nyuma Mwanahawa Athuman29 akitokea kwenye kibanda cha huduma ya
M-Pesa wakitaka kumnyan’ganya pesa ambapo alipiga kelele kuomba msaada
wasamalia wema walifika katika eneo hilo na kufanikiwa kumkamata
mtuhumiwa mmoja abubakari salum.
Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi
kukamilika na jeshi la polisi linaendelea na msako kuwakamata wale wote
wanaojihusisha na uhalifu huo.