Nature apigia hesabu za mbali ubunge Temeke
> Juma Kassim Nature
Mwanamuziki mwenye uwezo na mvuto jukwaani, Juma Nature
amesema kuwa hana mpango wa kugombea ubunge katika Jimbo la Temeke mwaka
huu, licha ya awali kutangaza nia hiyo.
Nature ametoa kauli hiyo huku wasanii wengine wakitangaza nia ya kuwania ubunge majimbo mbalimbali.
Wasanii
watakaowania ubunge mwaka huu ni pamoja na Mr II ambaye atatetea ubunge
wake wa Mbeya Mjini, Afande Sele, Kalapina, Chopa Mchopanga, JB ambao
wametangaza nia zao kupitia vyama tofauti.
Nature
ambaye hajawahi kutangaza chama anachokipigia upatu, alisema kuwa ingawa
alifuatwa na watu wengi waliomshawishi kugombea nafasi hiyo, lakini
atafanya hivyo mwaka 2020.
“Ubunge Temeke, nitapita tu.
Wenyewe wanajua kwamba mimi naweza kuwasaidia. Kwa sasa nimewaachia
kina Profesa Jay na wengine wachukue nafasi hizo, ila miaka mitano
injayo usishangae ukanikuta pale mjengoni nimevaa suti nikiwakilisha
wananchi. Kwa sasa sijaamua na malengo yangu ni mwaka 2020,” alisema
Nature.
Alisema kuwa akipata nafasi ya kuwa mbunge,
jambo la kwanza kufanya kwa wananchi wake ni kushughulikia kero zilizopo
hasa Barabara ya Mbagala.
“Barabara ndiyo kipaumbele,
kwani mvua ikinyesha kidogo ni shida, ile hospitali ya Temeke ni ndogo,
kumwona daktari ni kazi ngumu. Pia, soko siyo safi, inatakiwa vichimbwe
visima na kujengwa vyoo kwani watu wanachafua sana mazingira. Temeke
mitaro ni mibovu, mvua ikinyesha ni maafa kwa sababu watu wamejenga
kiholela,” alisema msanii huyo.
Alifafanua kuwa wakati
wake ukifika atagombea ubunge kupitia chama chochote atakachoona kina
msingi mzuri. “Lakini kwa sasa bado sijaona ni chama kipi ngangari,”
alisema .
posted Tuesday, March 24, 2015 | by- Herieth Makweta