Wazee waandamana tanga kufuatia kunyang’anywa mashamba yao bila kulipwa fidia.
Wakazi
zaidi ya 300 ambao wengi wao ni makundi ya wazee hasa akina mama
wameiomba serikali kuingilia kati kufuatia mashamba yao waliyopewa na
baba wa taifa hayati mwalimu jullius nyerere mwaka 1973 kunyang'anywa
bila kulipwa fidia yeyote hatua ambayo imesababisha wazee hao kuishi
katika mazingira magumu na hatarishi kwa maisha yao.
Wakizungumza baada ya maandamano hayo wazee hao wamesema maeneo
hayo ya mwakidila walipewa kisheria na mwalimu nyerere na hakukuwa na
hati yoyote yenye kuonesha kuwa wao hawana haki ya kufanya shughuli zao
za kilimo katika eneo hilo na badala yake wameomba watafutiwe maeneo
mengine kwanza ya kufanya shughuli zao badala ya kuwaondoa kwa nguvu
kama vile sio raia wa Tanzania.
Hata hivyo baadhi ya viongozi wa wazee hao wameiomba serikali
kuangalia suala hilo kwa jicho la huruma kwa sababu kama sheria za
mipango miji zinawabana na kuwataka kuondoka katika eneo la''mwakidila
kwa ramsingi'' wao wangeanza kupewa kipaumbele kwanza kwa kupimiwa
maeneo ya ujenzi wa nyumba za kudumu badala ya kuwanyng'anya na kuwauzia
wafanyabishara kutoka nje ya eneo hilo waliloishi kwa zaidi ya miaka
miaka zaidi ya 50.
Kufuatia hatua maafisa mipango miji wa jiji la tanga wamesema kuwa
wao hawawezi kulizungumzia suala hilo kwa sababu eneo hilo ni la jumuiya
ya umoja wa vijana ccm mkoa wa tanga kama jinsi alivyonukuliwa
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa tanga Bwana. Salim Perembo
wakatiakizungumza kwa njia ya simu akiwa safarini kutoka mjini dodoma
kurejea mkoani tanga.