Mwanamke Aliye Mrekodi Video Ya UCHI Mtangazaji wa Runinga ya TV1, Ezden Akamatwa na Jeshi La Polisi
JESHI la polisi jijini Dar limemkamata binti anayefahamika kwa jina
la Moza kwa kosa la kudaiwa kumdhalilisha Mtangazaji wa Runinga ya TV1,
Ezden Jumanne ambapo anatarajiwa kuburuzwa mahakamani muda wowote baada
ya uchunguzi kukamilika.
Moza ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji huyo kisha
kuachwa, anadaiwa kumrekodi video ya utupu Ezden kipindi walipokuwa
kwenye uhusiano mzuri kisha kuisambaza mitandaoni walipogombana.
Chanzo makini kimedai kuwa, Moza alikamatwa na kuwekwa mahabusu
katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar kufuatia msako mdogo
uliofanywa na polisi saa chache baada ya mrembo huyo kuvujisha video
hiyo.
“Wameshamtaiti
pale Oysterbay, wanakamilisha tu taratibu za ushahidi kisha anaburuzwa
mahakamani muda wowote kuanzia sasa,” kilisema chanzo chetu, juzi
Jumatano.
Moza amedaiwa kuiachia video hiyo mapema wiki hii kutokana na chuki za kuona Ezden ana mwanamke mwingine hivyo akaona akivujisha video hiyo atakuwa amemkomoa mtangazaji huyo kijana aliyewahi kuwa mume wa Mtangazaji Khadija Shaibu ‘Dida’.
Moza amedaiwa kuiachia video hiyo mapema wiki hii kutokana na chuki za kuona Ezden ana mwanamke mwingine hivyo akaona akivujisha video hiyo atakuwa amemkomoa mtangazaji huyo kijana aliyewahi kuwa mume wa Mtangazaji Khadija Shaibu ‘Dida’.
Akizungumzia sakata hilo, Ezden alisema yeye ni mtu anayejiheshimu,
anajitambua hivyo kitendo cha mwanamke huyo kumrekodi video hiyo
hakikuwa cha kiungwana.
“Hakunitendea haki, Nimeshalifikisha suala
hili polisi, taratibu za kipolisi zikikamilika anaburuzwa mahakamani,”
alisema Edzen.