Makalio Yampaisha Marekani Agness Masogange.....Mitandao ya Nje Yasifia Kiuno Chake
Staa aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na makalio yake, Agnes
Gerald ‘Masogange’ sasa amepaa kimataifa zaidi na kuwa gumzo hadi
Marekani baada ya hivi karibuni mtandao mmoja wa watu maarufu nchini
humo kumpa shavu.
Masogange aliripotiwa na mtandao wa Media Take Out na kumuelezea kuwa
ni staa mwenye makalio makubwa barani Afrika akitokea Tanzania.
Mbali na
maelezo kibao ya kusifia wowowo lake, mtandao huo uliposti picha kibao
za mwanadada huyo ambaye sasa anaishi Afrika Kusini akiweka mapozi
tofauti ya kimitego.
Hata hivyo, baadhi waliponda maelezo hayo kwa kusema kuwa, Afrika ina
mabinti wenye maumbo tata kuliko Masogange hivyo mtandao huo ungefanya
uchunguzi kabla ya kuripoti habari hiyo.