MWANAMKE JIJINI DAR AJIFUNGUA CHATU BADALA YA MTOTO
Mwanamke
mmoja, mkazi wa Mbezi- Maua jijini Dar aliyefahamika kwa jina moja la
Neema, amelea ujauzito wake kwa miezi tisa yenye matumaini lakini siku
ya kujifungua akaambulia kiumbe cha ajabu kilichofanana na nyoka aina
ya chatu
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, awali Neema alikuwa akisumbuliwa na pepo
wachafu hali iliyomfanya akatishe masomo ya sekondari na kuanza kwenda
kanisani kila wakati kwa ajili ya maombi.
MAUZAUZA KILA MARA
Chanzo kilisema kuwa, kipindi chote hicho, Neema alikuwa akianguka na kutaja majina ya watu wa mtaani anapoishi kwamba ni wachawi, wengine wanahusika kumchukua yeye usiku na kwenda naye makaburini ambako humlisha nyama na kumnywesha damu za watu.

“Neema
alikuwa akisumbuliwa na mapepo tangu akiwa mdogo na alikuwa anasumbua
kwelikweli. Alipokuwa akipandisha ‘madudu’ yake hayo hakuna aliyeweza
kumshika labda wanaume kama watano. Pia kuna wakati alikuwa akitaka
kujiua kwa kujichoma kisu,” kilisema chanzo hicho.
MAMA MZAZI ASIMULIA
Naye mama mzazi wa Neema ambaye hakupenda kujitambulisha kwa jina, alipozungumza na gazeti hili huku majirani wakifurika nyumbani kwake, alisimulia jinsi mwanaye huyo alivyokuwa akiteseka kipindi chote tangu alipokuwa mdogo mpaka ikafika hatua amepata ujauzito huo na hatimaye kujifungua kiumbe kinachofanana na chatu.

“Ni
mambo mengi ambayo tumeyapitia lakini siwezi kumkufuru Mwenyezi Mungu
kwa sababu mpaka leo hii tuko wazima japo mitihani ni kipimo cha maisha
na hata hili lililotokea karibuni ni mtihani pia, ila kikubwa ni
kuomba sana.
“Baada
ya kupata huu ujauzito kuna wakati tulikuwa hatulali, akianza kulia
ni usiku kucha, anasema kuna kitu kinambana kifuani. Tulipokuwa
tukienda hospitali kwa ajili ya uchunguzi, vipimo vilionesha mtoto
tumboni hachezi.
“Mimi
kama mzazi, hayo mambo yaliyokuwa yanamtokea mwanangu nilikuwa nayaona
kama maajabu f’lani hivi japokuwa kipindi hicho alikuwa mzima na mimi
mwenyewe nilikuwa nikimsubiri mjukuu wangu kwa hamu, kumbe tunakuja
kupokea kitu cha ajabu namna ile,” alisema mama huyo.
SIKU YA KUUMWA UCHUNGU
Iliendelea kudaiwa kuwa, kipindi chote cha ujauzito, Neema alikuwa mtu wa maombi, lakini siku ya kuumwa uchungu alikimbizwa hospitali (haikutajwa jina) na kujifungua kiumbe cha ajabu. Ndipo familia ikaamua kukaa kikao na kuamua kukizika kiumbe hicho kama chatu.

Mama
Neema anasema: “Mwanangu alijifungua kiumbe cha ajabu, kilikuwa kama
chatu halafu kina magamba na meno mawili marefu lakini hakikuwa hai.
Tulishtuka sana, tukaona ni mkosi katika familia lakini tuliamua
kukizika kile kiumbe.“Sikuona sababu ya kuwaonesha majirani zangu kwa
kuwa kilikuwa kinatisha. Ila naona ni bora niwape taarifa kuwa, mwanangu
alijifungua kiumbe cha ajabu.”
ALICHOSEMA ALIYEJIFUNGUA
Naye Neema mwenyewe alipozungumza na Amani kuhusu tukio hilo la ajabu, alikuwa na haya ya kusema:“Mimi mwenyewe sikupenda kuzaa chatu jamani, nimepitia mambo mengi ya ajabu, wazazi wangu ndiyo wanajua fika hali niliyokuwanayo huko nyuma, lakini sina namna.

“Labda
niwaulize mama zangu ambao tayari walishazaa kama tumbo huwa linapanda
juu mpaka kifuani badala ya kushuka? Na nilikuwa nakabwa sana kuanzia
kifuani mpaka kwenye koo, usiku sikuwa nalala kutokana na maumivu
niliyokuwa nikiyapata mpaka nilipojifungua hicho kiumbe.
“Usione
watu tunatembea, hatujijui tuna nini kwenye miili yetu. Leo hii
yamenikuta mimi, kesho mtu mwingine. (huku akiwaangalia majirani) mi
nawaomba ndugu zangu tukazane kumwomba Mungu kwani mimi maombi
yamenisaidia sana.”