HII NDIO VIDEO MPYA KUTOKA KWA DIAMOND PLATNUMZ AFANYA NA HANSCANA


Maneno yaliyosemwa na director mkenya Kevin Bosco mwanzoni mwa mwaka huu (Hanscana is the director to watch) kuhusu director mpya anayekuja juu kwa sasa, Hanscana yanazidi kutimia.
 
Baada ya kutisha kwenye video mpya ya Barnaba & Vanessa Mdee, sasa Hanscana amepata shavu la kushoot video mpya ya Diamond Platnumz.

Kupitia kipindi cha ‘Clouds e’ cha Clouds TV, kimeoneshwa kipande kidogo cha wakati wa utengenezwaji wa video (BTS) ya wimbo mpya wa Diamond na Khadija Kopa ambayo kwa mujibu wa chanzo chao imefanyika Dar na Zanzibar. Video hiyo inatarajiwa kutoka wiki moja kuanzia sasa.

Diamond kuamua kufanya kazi na director mpya ambaye anaonekana kukua kwa kasi, Hanscana ni ishara ya kuwa ameamini uwezo wake kupitia video chache ambazo tayari ametoa.

Itakumbukwa kuwa Baada ya Diamond kufanya kazi na producer wa audio Sheddy Clever ndipo milango mingi ya mafanikio ilifunguka kwa producer huyo kutokana na kupewa njia na staa huyo.

Video zingine ambazo Hanscana amefanya ni ‘Moyoni’ ya Navy Kenzo, ‘Siri’ ya Vanessa na Barnaba, WCD ya Vanessa, Nahreel, Aika, Barnaba+, ‘Morale’ ya G-Nako, ‘Tiririka’ ya Adam Mchomvu na zingine
Powered by Blogger.