Kinana abanwa, Nape ampiga kijembe Dk Slaa


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto), akichimba mtaro na viongozi wengine wa chama katika Kijiji cha Ilindi, Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma. Picha na Habel Chidawali.     
Bahi. Wananchi wa Kijiji cha Msisi katika Tarafa ya Mundemu, juzi walizuia kwa mabango msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapiduzi (CCM), Abdulrahman Kinana wakilalamikia shule yao kutelekezwa tangu 2011.
Hata hivyo, majibu ya Kinana yaligeuza hasira za wananchi na kuwa shangwe zilizoambatana na kumsindikiza kwa msafara.
Wananchi walizuia msafara huo wakati ukitoka Kijiji cha Chonde na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliamuru wananchi wasikilizwe.
“CCM ni chama chetu, lakini mbona watendaji wa Bahi wametusahau na kufanya watoto wetu wasome kwa shida, iko wapi CCM madhubuti ya Nyerere,” yalisomeka baadhi.
Mmoja wa wananchi hao alimweleza Kinana kuwa shule hiyo tangu ilipoezuliwa paa lake mwaka 2011, wamekuwa wakipigwa danadana na kufanya watoto wao kusoma chini ya mti.
Alipotakiwa kutoa maelezo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi, Hussein Kamau alikiri kuwapo tatizo katika shule hiyo na halmashauri kutochukua hatua mapema.
Majibu hayo yalimfanya Kinana kuanzisha harambee kwa viongozi wote waliokuwa kwenye msafara huo na kupatikana fedha za kununua mabati 100 na mifuko 75 ya saruji kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Nape adai Dk Slaa ni mzushi
Katika ziara hiyo, Nnauye aliitumia pia kumpiga kijembe Katibu wa Chadema Dk, Willibrod Slaa akidai amekuwa akisema mambo mengi yasiyo na ukweli.
Nape alimtaka katibu huyo kumrudia Mungu mapema kabla hajaharikibiwa zaidi.
Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo jana mjini Dodoma alipokuwa akijibu tuhuma kuwa baadhi ya vigogo wa CCM walipanga kumuua.
Hivi karibuni, Dk Slaa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabele Marando walidai kuwa mlinzi wake alikuwa akishirikiana na makachero na wanaCCM ili kumuua.
Hata hivyo, Dk Slaa aliibuka tena na kusema analindwa na nguvu za Mungu.
“Sio tu uongo bali tuhuma hizi ni upuuzi na uongo wa mchana,” alisema Nape.
Alisema Dk Slaa anarekodi nzuri ya uongo ingawa pia ni mwepesi wa kusahau.
Aliyata baadhi ya matukio ni kutabgaza kuwa lilikamatwa lori lililokuwa na kura za Urais mwaka 2010 lakini ulikuwa uongo.
Nyingine ni kiongozi huyo kudanganya Rais Jakaya Kikwete alikwenda Mwanza kwa lengo la kuiba kura jambo lililothibitika ni uongo.
“Jamani mambo ya Slaa ni mengi sana ikiwemo kuwaambia Watanzania kwamba alokuwa na matokeo ya vituo vyote wakati ni uongo kwa alishindwa nini kuwasilisha,”alihoji.
Nape aliwataka Watanzania kupuuza uongo huo kwakuwa CCM na viongozi wake hawana .ia hiyo.
Hata hivyo alisema hiyo ni mbinu ya mfa maji.
Kwa upande mwingine kiongozi huyo alimshukia Marando kuwa ni mvurugaji anayepaswa kupiuzwa.
Aliwaambia waandishi kuwa Marando ndiyo aliyesambaratika Chama cha NCCR na mkakati wake ni kuua Chadema.
Alimtaka Marando kuwatangazia Watanzania ni lini aliacha kazi ya ukachero na kwa barua ipi kwani amekuwa bingwa wa kuvuruga.
Powered by Blogger.