Zitto Kabwe avuliwa rasmi uanachama Chadema
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akifurahia jambo na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walipokuwa kwenye kikao cha Bunge hivi karibuni ribuni. Picha na Mkataba
Baada ya Mahakama Kuu Tanzania kanda ya Dar es Salaam leo
kutupilia mbali kesi iliyokuwa imefunguliwa na Zito Kabwe dhidi ya Chama
Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ya kuhoji uhalali wa uanachama
wake ndani ya chama hicho…
Habari zilizotufikia hivi
punde zinaeleza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
maendeleo Tundu Lissu ametangaza kuvuliwa rasmi uanachama wa Mbunge wa
Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Akitangaza hatua hiyo ya
kumvua uanachama,Lissu amesema kanuni na sharia za chama hicho ziko wazi
na zinaelekeza kuwa endapo mwanachama yeyote atakishtaki chama hicho
mahakamani na iwapo atashindwa atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye chama