“Tumewatunuku vyeti vya kimataifa vya MBA wahudumu wa baa kutoka mikoa kumi nchini baada ya kuhitimu mafunzo ya mwezi mmoja,” alisema. Alisema mafunzo hayo yamewapatia ujuzi wa kuhudumia wateja, kuchanganya bia, kujua wajibu wao na aina ya vinywaji vikiwemo vya Barleys, Gordons, Grants, John Walker, Guiness, Smirnoff na jamii zote za bia za Serengeti. Alisema mafunzo hayo ya kimataifa kwa Afrika, yalianza kutolewa Februari 7, mwaka huu na kukamilika Machi 7 na yaliyolewa na wakufunzi kutoka Afrika Kusini. “Mafunzo hayo yalifanyika katika mikoa ya Dodoma, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Morogoro na Mbeya,” alisema. Kuanzia sasa wahitimu wote wameandikishwa katika shindano la kimataifa la Diageo Master Bar Academy na watahitajika kujibu maswali kwa njia ya simu ya mkononi. Alisema shindano la kuwapata washindi kumi wa juu (top ten), litafanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa Aprili 2015 na kila mmoja atapatiwa zawadi ya dola 1,000 (Sh milioni 1.7) za Marekani. Alifafanua kuwa mshindi wa jumla, atapata tiketi ya kushiriki shindano la kimataifa la ‘Diageo World Class’ litakalofanyika mwaka huu Johannesburg, Afrika Kusini.
Msanii
na mtayarishaji wa muziki wa Sharobaro Records, Bob Junior amesema
hayakuwa mapenzi yake kuacha ndoa yake ivunjike. Bob Junior amesema kuwa
kilichotokea ni majaliwa ya mwenyezi Mungu.
“Nitaoa lakini sio miaka ya karibuni ni miaka ya mbele sana kwa
sababu niliingia kwenye ndoa halafu mwisho wa siku ndo haikukaa muda
mwingi ikanishinda,” amesema.
“Yaani siwezi tena kusema niache halafu nione tena, simaanishi kwamba
ndoa ya kwanza nilikurupuka, ilitokea kwa neema za Mungu na bahati
mbaya kwa majaliwa ya Mungu ikavunjika. Watu wanauliza sana hili suala
lakini mimi nipo single kabisa. Mimi nashangaa watu wanaendelea
kuniuliza,” ameongeza.