Tundu Lissu Atangaza Rasmi Kuhusu Kuvuliwa Rasmi kwa Uanachama wa Zitto Kabwe CHADEMA
Mwanasheria mkuu wa chama cha upinzani nchini CHADEMA,
Tundu Lissu leo ametangaza kuvuliwa uanachama kwa mbunge wa Kigoma
Kasikani Zitto Kabwe baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es
Salaam kutupilia mbali pingamizi la mbunge huyo la kuzuia asijadiliwe.
"Kwa mujibu wa katiba ya chama cha CHADEMA, mwanachama
yoyote anapofungua kesi mahakamani dhidi ya chama chake, endapo
atashindwa katika kesi hiyo atakuwa amejiondoa uanachama wake, kwahiyo
natangaza rasmi rasmi Zitto Kabwe sio mwanachama tena wa Chadema."Amesema Tundu Lissu
Kwa upande wake Zitto Kabwe amesema hawakuwa na wito wa
mahakamani leo na Jaji wa kesi kahamishiwa Tabora na hawana taarifa ya
Jaji Mpya, pia kaongeza kuwa Mwanasheria anafuatilia na atatoa
statement.