Penny adaiwa kunywa sumu baada ya kupigwa chini na mpenzi wake...
Mtangazaji maarufu Bongo na aliyekuwa mpenzi wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amedaiwa kunywa sumu kufuatia kunyang’anywa bwana na shosti yake aliyefahamika kwa jina la Diana.
Kwa mujibu wa chanzo, Penny na
Diana walikuwa marafiki lakini wakatofautiana baada ya Diana kumteka
akili mwanaume wa rafiki yake huyo na kumkoleza mapenzi hadi kufikia
hatua ya kumtangazia ndoa.
“Diana kampagawisha mwanaume wa
watu, jamaa akatangaza ndoa na hivi ninavyokwambia siku siyo nyingi
Diana anaolewa hicho ndicho kikasababisha Penny apandwe na presha hadi
kufikia hatua ya kunywa sumu, alikimbizwa hospitali, akalazwa lakini
sasa ametoka anaendelea vizuri,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo,
mwanahabari wa Gpl alimtafuta Penny ili kujua anazungumziaje habari hizo
za kunywa sumu hadi kulazwa hospitali ambapo alikanusha madai hayo.
“Sijanywa sumu, suala la mimi kulazwa huwa linatokea sababu nasumbuliwa na pumu mara kwa mara,” alisema Penny.