MISEMO YA KISWAHILI


Lenye mwanzo lina mwisho
Msemo huu unamaanisha kuwa jambo lolote lililo na mwanzo lina mwiso. Msemo huu una maana sawa na hakuna ndefu lisilokuwa na mwiaso.
         Zunguo la mtukutu ni ufito
Msemo huu unatufunza kuwa njia ya kumfunza mtoto mkaidi ama asiyesikiliza ni kumpa adhabu.
       Maji usiyoyafika hujui kina chake
Msemo huu unamaanisha kwamba jambo ambalo hujalifanya hujui ugumu wake. Pia, msemo huu una maaana sawa na kitanda usichokilalia hujui kunguni wake.
             Ukiwaona ni watu moyoni hawana utu
Msemo huu unamaanisha kuwa usifikiri kwamba kila uliyekuwa karibu naye anakupenda kwa dhati  wengine ndio maadui zako namba moja na ni vigumu kuwatambua.
       Afadhali jirani mbuge kuliko jirani mwenye mdomo mrefu
Msemo huu una maana kuwa mtu anayefitini wengine ni hatari kuliko hata mlafi.
Misemo ni muhimu sana katika jamii. Kwanza, ni njia ya kupitisha mafunzo kutoka kazazi kimaja hadi kingine. Pia, misemo huwafunza wanajamii kuhusu utamanduni wao, ni njia ya kujiburudisha na pia hutumika kuonya au kushauri.
Kwa hivyo, ni vyema wanajamii kuitumia misemo kila siku kwani itawajenga kielimu na pia kimaadili.

Powered by Blogger.