MISEMO YA KISWAHILI
Midundo ikibadilika ngoma huchezwa vingine
Maana kuu ya msemo huu ni kuwa, mabadiliko yanapotokea katika mazingira yako, huna budi kubadili mbinu ili kukabiliana na mabadiliko hayo. Funzo kuu ni kuwa wanajamii wanapaswa kukubali mabadiliko badala ya kulalamika.
Bata mtaga mayai usichinje kwa tamaa ya wingi
Msemo huu una funzo nzuri sana kwa wanajamii. Maana yake ni kuwa tamaa za haraka za kukifaidi kitu zisituponze tukaharibu manufaa makubwa zaidi ya kitu hicho hapo baadae.
Samaki mkunje angali mbichi
Msemo huu ni muhimu sana katika jamii yetu. Unatufunza kwamba ni vinzuri kuwaonya watoto wetu tangu utotoni mwao ili kwafanya waelewe mambo na kujirekebisha kwa urahisi.
Bahati ikibisha hodi sharti ufungue mlango mwenyewe
Msemo huu unamaanisha kuwa unapopata fursa ama nafasi ya kutenda jambo yakupasa uitumie vema na si kuipuuzia au kukata usaidiwe kuipokea. Kwa hivyo, ni vyema wanajamii wajifunze kutumia fursa tofauti tofauti kama inavyohitajika.
Kipenda roho hula nyama mbichi
Msemo huu una maana kuwa, mtu hujitosa hata kuyatenda mambo yasiyo ya kawaida au magumu bora apate anachokipenda.
Dunia tambara bovu ukivuta utachana
Msemo huu untuonya dhidi ya kuwaamini sana wanadamu. Maana yake ni kuwa, usiwaamini sana walimwengu au kuwategemea sana kwani wanaweza kukutenda.
Cha mchama huchama cha mgura hugura
Msemo huu una maana kuwa asiyekuwepo kulinda mali yake au kutunza mali yake huishia kutumiwa vibaya ama kumalizwa na wengine ambao labda hawana.
Akopaye akilipa huondokana na lawama
Huu ni msemo ambao una funzo nzuri sana kwa wanajamii. Una maana kuwa anyekopa akilipa hujiondolea lawama. Kwa hivyo, ni wajibu wate kuhakikisha tumeiondolea lawama kwa kulipa madeni yote yanayotukabili.
Achezaye na tope humrukia
Msemo huu una maana kuwa unaposhiriki kutenda uovu si ajabu mabaya hayo yakakudhuru mwenyewe. Kwa hivyo, msemo huu unatuonya dhidi ya kushiki katika kutenda uovu.
Waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba
Pemba ni mji fulani wa pwani na waswahili wanoishi huko huvalia vilemba. Msemo huu una maana kuwa watu a tabia moja hujuana kwa mambo wanyofanya.