NADHARIA YA UFEMINISTI ( Mtazamo wa kike)

(Williady, 2015) Nadharia hii inahistoria ndefu duniani, ikimaanisha ni moja ya nadharia zilizopata kutokea miongo mingi iliyopita. chanzo cha kuibuka kwa nadharia hii ni vuguvugu la kutaka kufuta kabisa uonevu wa mwanaume kwa mwanamk. nadharia hii inadai kuwa chimbuko lauonevu na ukandamizaji unaofanywa na wanaume kwa wanawake ni uroho wa mwanaume katika kumtawala mwanamke. Kwaufupi, ajaenda kuu ya ufeministi na mafeministi ni kumaliza kabisa utawala wa mwanaume kwa mwanamke.

moja ya wadau waliochangia sana kuendelea kwa nadharia hii kwa kasi ni Adrew Dworkin. Mwaka 1976, akiwa katika mji mkuu wa Uingereza, London, alitoa mapendekezo makali katika kukomesha utawala wa mwanaume kwa mwanamke, Dworkin anasema: Ili kufanikisha, tunahitaji kubomoa kabisa muundo wa mihimili ya utamaduni wa jamii kama vile sanaa, kanisa, sheria, kaya zinazodhibitiwa na baba, jamii na taswira zote za asasi, mila, desturi ambazo zinamwona mwanamke kuwa mtu ovyo.

WATAALAMU MBALIMBALI WALIVYOZUNGUMZIA MAANA YA UFEMINISTI

Nadharia ya Ufeministi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kama vile:
Wamitila (2003:253), hii ni nadharia ambayo imewekewa msingi na msukumo mkubwa pamoja na nia ya kupigania ukombozi wa mwanamke kutokana na pingu za kiutamaduni, kidini, kijamii, kisiasa na kiuchumi. Hii ni nadharia ambayo inasaili na kudadisi itikadi ya kiume ambayo imekuwepo katika jamii kwa kipindi kirefu. Kudadisi pia fasiri za kiume za fasihi pamoja na mikabala ya kiubabedume.
Ntarangwi (2004:45), ni nadharia ambayo inajaribu kukiuka mitazamo ya kiume ambayo yaelekea inatumiwa sana katika jamii.
Mukobwa M. nadharia ya ufeministi imetokana na mkondo na harakati za kutetea haki za wanawake ulimwenguni na imejikita katika imani ya usawa wa kijinsia, kijamii, kisiasa na kiuchumi. 
(Williady, 2015) Ninadharia iliyojaribu kuvunja mwiko wa mfumo dume hapa dunia kwa kuanzisha mapambano ya usawa wa kijinsia, bilashaka majaribio haya bado hayajafanikiwa.
Kwa jumla, nadharia ya ufeministi ni nadharia iliyojikita katika kupinga ukandamizaji wa mwanamke katika jamii hususan katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, na kiutamaduni.


KUIBUKA KWA UFEMINISTI NA HARAKATI ZA KUIENDELEZA NADHARIA HII
Uhakiki wa kifeministi ulishika kasi miaka ya 1960 na kuendelea kukua na kuishia kuwa muhimu katika miaka ya hivi karibuni. Zipo kazi kadhaa zilizoandikwa kabla na kulimulika suala hili kwa namna moja ama nyingine. Kazi kuu mbili zinazorejelewa hapa ni A Room of One’s Own ya Virginia Woolf na A virdiction of the Right of women ya Mery Wollsto Necraft.
Hata hivyo, kazi iliyoishia kuwa na mchango mkubwa katika kuuweka msingi wa uhakiki wa ufeministi ni kazi maarufu ya mwandishi wa Kifaransa, Simone de Beauvoir iitwayo, The Second sex, 1952 katika kitabu hiki, mwandishi huyu anachukuwa mkabala wa kiharakati kwa kushambulia na kukosoa baadhi ya asasi zinazochangia katika kumdhalilisha au kumdunisha mwanamke. Asasi kuu anazozishambulia ni ndoa, dini na utamaduni.
Nadharia ya ufeministi ilichimbuka huko Marekani katika harakati za kukomesha biashara ya utumwa mwaka 1830. Wanawake wakaanzisha harakati za kupigania haki za mwanamke.
Wamitila (2006:160-161) na Ntarangwi (2004:52-56) wamebainisha malengo mbalimbali ya ufeministi.
Ni kweli kwamba kuna baadhi ya malengo ya ufeministi yanakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika lakini baadhi ya malengo hayo yanasawiri maisha halisi ya mwanamke wa kiafrika kama ifuatavyo:
Kubainisha umuhimu wa mwanamke, kutokana na mwanamke kukulia katika jamii zenye mfumodume. Umuhimu wake haukuonekana, ndiyo maana ikaanzishwa nadharia ya ufeministi ambayo yenyewe iligundua umuhimu wa mwanamke katika jamii. Umuhimu wake upo katika Nyanja zote za kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni. Mfano, katika nyanja ya kisiasa mwanamke anaweza kuwa kiongozi bora na mwenye ushauri. Hili linajidhihirisha katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ (1994). Mwandishi anathibitisha hili anaposema:
“Tunayo karibu miaka ishirini ya uhuru! Lini tutampata mwanamke wa kwanza awe waziri atakaye husishwa na maamuzi yatakayoongoza nchi yetu huko tuendako? Kumbe nguvu walizonazo wakina mama, uwezo wao wa kupambana, na kujihusisha kwao bila kutegemea kupata faida yoyote ni mambo ambayo hayahitaji tena kuthibitishwa. Wanawake wamewainua wanaume wengi kwenye ngazi za juu.” (uk.82)
Katika nyanja ya kijamii, mwanamke ni mlezi wa familia. Mfano, Ramatulayi anailea familia yake kwani ameweza kulipa bili ya maji, umeme bila hata kumtegemea mwanaume. Mfano, mwandishi anasema:
“Licha ya mzigo niliokuwa nao tangu zamani, nikaubeba na ule uliokuwa wa Modu. Ununuzi wa vyakula muhimu ulinishughulisha kila mwisho wa mwezi. Nilihakikisha kwamba sikuwa na upungufu wa nyanya au mafuta, viazi mviringo na vitunguu wakati ambapo vyakula hivi viliadimika sokoni… Nilikuwa mwangalifu kuzilipa bili za maji na umeme pindi zilipofika.” (uk.69)
Lengo hili la ufeministi linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwa kuwa mwanamke wa Kiafrika anaonekana hana umuhimu katika jamii, pia anaonekana kuwa dhaifu ambaye hawezi kuiendesha familia yake bila msaada wa mwanaume hii ni kutokana na jamii nyingi kuendeshwa na mfumodume.
Kuorodhesha kuwa kihistoria wanawake wamekuwa ni tegemezi na wasaidizi wa wanaume, ni kweli kihistoria wanawake wamekuwa wategemezi na wasaidizi wa wanaume. Mfano katika tamthiliya ya Nguzo Mama iliyoandikwa na Penina Muhando (2007) tunaona mhusika BI MOJA alivyokuwa akimtegemea mume wake na kutaka anunuliwe kanga. Mwandishi anasema:
“BI MOJA: (kwa Shaabani): Kama ulijua kufika sasa hivi nipe hela ya kanga bwana meli meli hii hainikosi leo utanipa hela hizo kanga nikakate. Mwezi wa tatu huu kanga sizijui.
Shaabani: Nimekuambia mimi hela sina. Sasa unataka nikaibe?”(uk.31-32)
Ni kweli kwamba mwanamke wa kiafrika amekuwa tegemezi katika jamii, kwani humtegemea mwanaume katika mambo mbalimbali ya kifamilia. Kwa mfano kutafuta au kununua mahitaji ya nyumbani kama vile chakula, mavazi yake na watoto wake au kulea watoto wake.
Kuondoa ukandamizaji wa mwanamke kutokana na pingu za kiutamaduni, kijamii, kidini, kisiasa na kiuchumi. Jamii nyingi za Kiafrika zimejengeka katika mfumodume, hivyo basi jamii zinamkandamiza mwanamke kutokana na pingu hizo. Katika kulithibitisha hili waandishi wa kazi za fasihi nao hawakuwa nyuma kulizungumzia katika kazi zao na lengo ni kuondoa mfumodume uliojengeka muda mrefu katika jamii.
Kwa upande wa kiutamaduni mwanamke ameonekana kukandamizwa kwa kuonekana hana mamlaka hata ya kurithi mali za mumewe au zake mwenyewe, badala yake hata akifiwa na mumuwe anapigwa, anafukuzwa na kudhalilishwa. Penina Muhando anayathibitisha haya katika tamthiliya yake ya Nguzo Mama kwa kumtumia BI SABA pale anaposema:
“Akalia Bi Saba tena akalia
Hana wa kumsaidia
Mumewe kafa nduguze wakaja juu
Pesa wamechukua senti tano haikubaki
Vyombo na nguo zote wakagawana
Roho ilimpasuka Bi Saba kuwaona hao ndugu
Walivyogombania mali wasiyoichuma…
Sasa juu ya yote haya wamerudi kufagia
Hata ufagio wamebeba
Na lawama kumtupia eti pesa kazificha.” (uk.39)
Pia mwanamke anaonekana anajishughulisha na kazi mbalimbali za kujiletea maendeleo yake binafsi lakini anarudishwa nyuma kwa kukandamizwa na mwanaume. Penina Muhando anayathibitisha haya kwa kumtumia BI PILI ambaye alikuwa anapika pombe ili kujikwamua katika hali ngumu ya maisha lakini mumewe SUDI alizichukua hela zote alizokuwa alizozipata. Kwa mfano, mwandishi anasema:
“BI MSIMULIZI: Upishi wa pombe balaa ulimzushia
Visa na mikasa Bi pili havikumuishia
Pesa alizipata kutokana na hiyo pombe
Lakini visa vya pombe hiyo pesa hazikufidia”
SUDI: (kwa Bi Pili) Nani kalewa? Umeninywesha wewe?
Wee!hawara zako ndiyo wamekutia jeuri unaninyima pesa.
Toa pesa sasa hivi (Anampiga) Bi Pili anakimbia huku akilia.” (uk.16)
Vilevile, mwanamke alikuwa anakandamizwa kwa kulazimishwa kurithiwa na kaka au ndugu wa mume pindi anapofiwa na mumewe. Mwandishi analithibitisha hili katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii pale anaposema: 
“Tamsiri, zitapike hizo ndoto zako za kutaka kuniposa.
Umeshakaa nazo kwa siku arobaini. Kamwe sitokuwa mkeo.”(uk.81)
Kwa upande wa kisiasa, mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa kuonekana hawezi kuwa kiongozi bora wa kuiongoza nchi ndio maana hata nafasi za wanawake zilikuwa chache huko bungeni. Katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ mwandishi anayadhihirisha haya kwa kumtumia Ramatoulayi ambaye akilalamika kuhusu ukandamizwaji wa wanawake huko bungeni pale anaposema:
“Wanawake wanne, Dauda, wanne miongoni mwa wabunge mia moja uwiano gani huu wa kimzaha! Wala hakuna uwakilishaji wa kimkoa” (uk.81)
Kwa upande wa kijamii, mwanamke amekuwa akikandamizwa kwa kupigwa na mumewe bila sababu zozote za msingi. Hili linajidhihirisha katika riwaya ya Rosa Mistika iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi (1988) kwa kumtumia mhusika Zakaria ambaye alikuwa anampiga mkewe bila sababu. Mwandishi anasema:
“Regina tangu aolewe hakuwa na raha! Alikuwa akisumbuliwa na kuteswa na mumewe kwa kosa lisilokuwa lake. Katika kijiji chote cha Namagondo hapakuwa na mwanamke aliyekuwa akipigwa karibu kila juma kama Regina. Wanawake wengi kijijini walijiuliza kwa nini hakutaka kumuacha bwana wake. wengine walimuonea huruma, wengi lakini walimuona mjinga.” (uk.3)
Pi, mwanamke alikuwa anakandamizwa kwa kuonekana kuwa yeye ndiye mwenye majukumu ya malezi, kwa hiyo hata watoto wakiharibika anayelaumiwa ni mwanamke. Euphrase Kezilahabi analithibitisha hilo pale anaposema:
“Lete hiyo barua iko wapi? Pamoja na shilingi ulizopewa unafikiri sisi hapa maskini. Rosa alipigwa tena na tena. Makofi yalikwenda mfululizo hata damu zikamtoka puani na mdomoni. Baba nihurumie sitarudia tena… Zakaria hakujali alichukua fimbo na kuongozana na bintiye mpaka chumba cha watoto hali akinguluma lazima unioneshe barua hiyo unataka kuniletea umalaya wa mama yako hapa.” (Uk.7)
Vilevile, mtoto wa kike alikuwa anaonekana hana thamani katika jamii, na watoto wa kiume ndio waliopewa kipaumbele. Euphrase Kezilahabi anathibitisha haya katika riwaya ya Rosa Mistika kwa kumtumia Zakaria ambaye kabla ya kumpata mtoto wa kiume alikuwa anamnyanyasa sana mke wake lakini baada ya kujifungua mtoto wa kiume manyanyaso yaliisha na alimpenda sana mkewe. Mwandishi anasema:
“Zakaria alirudi nyumbani siku hiyo. Alikuwa amekwisha pata habari hizo njiani. Alimbeba mtoto. Alimpa pongezi mke wake. Regina sasa mji huu umekuwa wako. Asante Regina alijibu akitabasamu, alijiona anauwezo wa kuzungumza.” (uk.24)
Lengo hili linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwani mwanamke hatakiwi kurithi mali yoyote pindi wazazi wake wanapofariki au mumewe anapofariki. Pia mwanamke kushindwa kupewa nafasi ya kutoa maamuzi yoyote katika masuala ya kiukoo. Kwa upande wa dini mwanamke anakandamizwa na kuonekana dhaifu hivyo kutokuwa na nafasi ya kuongoza waamini. Mfano, dini ya Kiislamu na baadhi ya madhehebu ya Kikristo.
Lengo lingine ni kuzitambua na kuzibainisha dhamira kuu katika kazi zilizoandikwa na wanawake. Dhamira kuu ni dhamira inayomsukuma mwandishi katika kuandika kazi ya fasihi. Baadhi ya waandishi wanawake wameonesha dhamira kuu katika kazi zao kama ifuatavyo:
Nguzo Mama iliyoandikwa na Penina Muhando (2007) imebeba dhamira kuu ambayo ni ukombozi wa mwanamke. Ukombozi huo upo katika nyanja mbalimbali kama vile kijamii, kiutamaduni, kiuchumi na kisiasa. Mfano, mwandishi ameonesha wanawake wanavyojishughulisha katika kuinua uchumi wao, kwani walikuwa wakiuza vitambaa na kupika pombe. Mwandishi anathibitisha haya kwa kusema:
“BI TANO: Yaani mnasema mimi mvivu siyo nimezunguka mji mzima na zigo hilo halafu mnaniambia mimi mvivu. Nawaambia watu hawataki kununua au mnataka niwagawie bure.”
BI NANE: Lakini kwa nini wakatae kununua hivi, mbona vile vya mwanzo walivinunua? (uk.16).
Vilevile, Katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii iliyoandikwa na Mariama Bâ (1994) suala la ukombozi wa mwanamke limejitokeza kama dhamira kuu. Ukombozi huu umejikita katika nyanja za kisiasa, kiutamaduni, kijamii na kiuchumi.
Mfano, katika nyanja ya kijamii, mwandishi ameonesha jinsi ya kumkomboa mwanamke kielimu, pale anaposema:
“…Shangazi Nabu anampeleka Nabu mdogo katika shule ya Kifaransa huko. Huko Nabu alijifunza aina mbalimbali za mapishi, matumizi ya pasi na zana za kutumia na kumenyea...” (uk.39)
Lengo hili linakinzana na maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika, kwa kuwa tangu mwanzo wanawake walikuwa hawaruhusiwi kuwa viongozi, badala yake wanaume ndio waliochukuwa jukumu hilo la uongozi katika jamii. Pia, wanawake hawakuruhusiwa kupata elimu wakitegemezwa katika majukumu ya nyumbani na kuandaliwa kwenda kuolewa na kuja kuwa walezi wa familia.
Kuichunguza historia ya kifasihi ya jadi ya kike na kuwamulika waandishi wa kike waliotambua hali za wanawake na ambao wanaweza kuchukuliwa kama vielelezo kwa wasomaji wao. Hapo awali kazi mbalimbali za kifasihi za jadi za kike zilielezwa na waandishi wa kiume. Lakini nadharia hii imemulika waandishi wa kike wanaotambua hali mbalimbali na wameamua kuandika kazi mbalimbali ambazo zinaelezea matatizo ya wanawake. Mfano, katika tamthiliya ya Nguzo Mama mwandishi anaelezea jinsi wanawake wanavyonyanyaswa na kuachiwa majukumu ya kulea familia, kuchukuliwa mali zilizoachwa na waume zao baada ya kufariki. Mfano, mwandishi anasema:
“…Haa! Shemeji mmerudi kuchukua hata kitanda! Hata sufuria! Nitalala wapi na nitapikia wapi jamani!” (uk.39)
SUDI: Haya nipe pesa ulizokwisha kupata.
BI PILI: Hee! Kwa nini nikupe?
SUDI: Leta pesa upesi kabla sijakukong’ota.” (uk.13)
Mariama Bâ naye ni kielelezo kwani ameelezea matatizo mbalimbali yanayowakumba wanawake na namna wanavyokabiliana na matatizo hayo. Mfano mwandishi anasema:
“… Ramatulayi, Acha nisikilize mimi zaidi; Redio ya Kankan ilinifahamisha kwamba ulikataa kuolewa na Tamsiri. Ni kweli? Ndio.” (uk.87)
Mwandishi anaonesha jinsi mhusika Ramatulayi alivyojitambua na kukataa kurithiwa na Tamsiri, pia anamkataa Dauda ambaye alitaka kumrithi baada ya kufiwa na mume wake.
Kupitia lengo hili tunaona wanaufeministi wameongelea kuhusu wanawake tu ambao ni vielelezo katika kazi za fasihi, lakini wapo wanaume ambao wamezungumzia masuala mbalimbali yanayowahusu wanawake. Mfano, Shaaban Robert aliyeandika Wasifu wa Siti Binti Saad.
Kudhihirisha kuwa kuna sifa fulani za kike na uzoefu fulani wa kike katika uwazaji, hisia, kutathmini, kujiangalia na kuuangalia ulimwengu wao wa nje. Uzoefu fulani wa kike unajitokeza katika uwazaji na jinsi wanavyousawiri uhalisi. Kazi ambazo zinamsawiri mwanamke kwa njia chanya, mfano ni riwaya ya Kiwasifu ya Shaaban Robert Wasifu wa Siti Binti Saad. Kuna mashairi kadhaa aliyoyatunga mwandishi ambayo yanaendeleza suala hili la uchanya wa wanawake katika jamii. Mfano wa usawiri wa wahusika linathibitishwa pale mwandishi anaposema:
“Siti binti Saad,
Ulikuwa mtu lini,
Ulitoka shamba,
Na kaniki mbili chini,
Kama si sauti,
Ungekula nini?” (uk.22)
Hisia: mfano, katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii kupitia mhusika Daba alivyomwambia mama yake kuhusu Benetuu. Mwandishi anasema:
“Hasira ya Daba iliongezeka zaidi jinsi alivyozidi kuichambua hali ilivyokuwa. “Mama! Vunja ndoa yako! Achana naye mtu huyu hajatuheshimu, si wewe wala si mimi… sitaki kukuona unagombania mwanaume na mwanamke mwenye umri sawa na mimi.” (uk.52)
Lengo hili la wanaufeministi, linaendana na hali halisi ya wanawake wa Kiafrika, kwa kuwa mawazo ya mwanamke jinsi anavyojiwazia yeye mwenyewe au kuwawazia wanawake wenzake hutofautiana . vilevile, hisia za mwanamke zinaweza kudhihirika katika maandishi na kuonesha jinsi wanavyowaza katika hali ya kawaida.
HITIMISHO
Lengo la nadharia ya ufeministi lilikuwa ni kuondoa unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa mwanamke. Hivyo basi, malengo ya ufeministi yalijikita katika kumnasua mwanamke kutoka katika pingu za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Malengo haya ndiyo yanayoleta ukinzani wa maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika. Hali hii imeleta mabadiliko katika maisha ya wanawake wa kiafrika, kama vile kutaka haki ya elimu, kumiliki mali, kurithi mali, kutaka nafasi za uongozi, pia kuwa na maamuzi ya kifamilia au kiukoo, katika kupingana na pingu za maisha.


Nadharia ya Uhemenitiki

Uhemenitiki ni taaluma inayohusiana na uelewaji na kutafsiri matini. Chimbuko la nadharia hii ni katika uchambuzi wa falsafa katika matini za kidini, hususani dini ya Kikristo. Waasisi wanaohusishwa na chimbuko la nadharia hii ni kama vile Friedrich Schleiermacher (1768-1834),Wilhem Dilthey (1833-1911) na Martin Heidegger (1889-1976).

Msingi mkubwa wa nadharia ya Uhemenitiki ni imani ya kwamba matendo ya binadamu yanaathiriwa kwa njia mbalimbali na asasi tofauti zilizoko katika mazingira yake. Msingi huo unatupeleka katika dhana ya kuibua umuhimu wa kuelewa njia au mbinu za uelewaji wa maana za matini. Madai ya msingi ya nadharia ya Uhemenitiki yanahusisha dhana mbalimbali kama vile duara la kihemenitiki, utukuzaji pamoja na ile ya ufufuaji wa kisarufi, kisaikolojia na kimuktadha (Senkoro, 1987; Wamitila, 2002 katika Ponera, 2010).
Powered by Blogger.