VIPENGELE VYA FANI KATIKA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI
AFRIKA
Niko nikiishi kwa matumaini ya kuona siku moja Afrika iko huru. Siku hiyo, nitafurahia kuuona uhuru wa Afrika! Siktt hiyo, siku ambayo Afrika yote itakuwa huru, nitaimba nyimbo za kufurahia uhuru kwa shangwe ua vingorimbo! Nitacheza ngoma zetu! Siku hiyo ni taimba nyimbo kwa Lugha zetu zote za Afrika! Nitaamuru Mandela ua wenzake watolewe kifungoni Robben (kisiwam) ili waje waungane ua familia zao ambazo wametengana nazo kwa siku nyingi. Pia, nitamwomba Mungu huku kunakosemekana kupo awafufue machujaa wa Afrika walioanzisha vita vya ukombozi ili waje wafurahie uhuru wao walioupigania hata wakafa. Nitataka Mkwawa afufuliwe! Nitataka. pia Chabruma, Makita, Mputa, Songea wafufuliwe... Nitataka Kinjeketile, Isike, Milambo, Ng'wanamalundi, na wengine wafufuliwe!! Wakisha fufuliwa, nitaomba waniamuru niwasomee risala yangu. Nami nitai soma: Mababu zetu. Tunayo furaha kuwa pamoja, nanyi. Kazi mliyotuachia tumeimaliza. Tutalinda uhuru wetu! Mababu hawa watanipongeza na kusema... Wanetu wa Afrika, kumbukeni kuishi katika umoja unaounganishwa ua damu yetu. Lakini hili ni jambo kubwa! Epukeni kuuana wenyewe kwa wenyewe kama wanyma mwitu. Tunaahidi kuja kusherehekea siku ya MUUNGANO WA AFRIKA." Nitashukuru.30
Katika kifungu hiki kumekuwa na mbinu ya Kimonologia ikiwa na ufafanuzi uliotolewa pale awali. Aidha, uandishi wake hapa umekuwa u wa kawaida sana, hasa kwa vile umetumia wakati uliopita kidogo ua sehemu kubwa ni wakati unaokuja. Uandishi wa aina hii si wa kawaida sana katika hadithi za Kiswahili. Mpaka sasa (1990), ni hadithi moja tu katika Kiswahili imetumia maelezo yake kwa kuzingatia wakati unaokuja. Hadithi hiyo imeandikwa na J.R.R. Mkabara na inaitwa Mbio za Kipofv.31 Ni muhimu pia kusema hapa kuwa Monologia hutumia nyakati mbalimbali kama vile, muda uliopita, muda uliopo, na muda unaokuja.
Mbinu za Kidialogia
Dialogia ni mazungumzo ya watu wawili au zaidi yanayowakilishwa kimaan-dishi katika kazi za sanaa zitumiazo lugha, hususan, hadithi fupi. Kwa kawaida, dialogia haitumiki katika kazi za kitaaluma kama vile Fizikia, Hisabati, Jiografia, Historia n.k. Taangalie mfano ufuatao unaoonyesha matumizi ya dialogia ulioandikwa na E. Kezilahabi.
Rosa alijipaka mafuta Iddogo. Baada ya muda mfupi taa ilizimishwa. Giza liliingia. Rosa alikaa juu ya kitanda. Thomas alisikia kitanda idnalia. Rosa alikuwa Jdtandani. Thomas, akiwa na shauku kubwa alimtu-pia mkono. Aliona kwamba Rosahakuwa na nguo hata moja. Thomas alimvuta ili amsogeze karibu. Mara moja mkono wake ulishikwa ua kurudishwa kwa nguvu.
"Si kawaida yangu," Rosa alisema
"Kwa nini?"
"Huwa sipendi. Si leo siku ya kwanza."
"Sasa!"
"Tuzungumze tu."
"Mpaka lini?"
"Mpaka mimi nipende.''
"Utapenda lini?"
"Vumilia kidogo."
"Haiwezekani."
"Kwa nini huwezi?"
"Mwenzio sijiwezi. Lakini kwa nini hupendi?"
"Hali yangu hainiruhusu."
"Hali gani?"
"Mimi mwanafunzi wako."
"Sahau uanafunzi."
Thomas alimtupia mkono tena. Rosa aliurudisha.
"Basi mimi nakwenda kulala kitanda kingine."32
Katika mfano huu, maelezo machache yanatangulia dialogia kali inayofanywa na watu wawili, Rosa Mistika na Mwalimu Thomas, Mkuu wa Shule aliyokuwa akisoma Rosa Mistika.
Dialogia inavyotumiwa na waandishi wengi ina kazi mbalimbali muhimu za kisanaa katika hadithi. C.H. Holman anazitaja kazi hizo kuwa ni:
a
|
-
|
Kusaidia kuyasukumia matukio upande ule ambao mwandishi ameukusudia. Mbinu hii hutumika pia kama pambo la hadithi kisanaa.
|
b
|
-
|
Dialogia inazingatia tabia, hali, uhusika na ujumla wa ujenzi wa mhusika katika hadithi fupi (na hadithi kwa ujumla). Kama mhusika anaanza ua tabia fulani, ataonyeshwa na tabia hiyo, labda kama mwandishi anaibadilisha tabia kwa makusudi maalumu ya kutaka kupata athari fulani. Wahusika hao watahusiana na pia kuonyesha tofauti kati yao, wataonye-sha tofauti ya kitabia, kitaifa, kitabaka, kila mhusika ataionyesha rejesta au lahaja yake, kazi yake na uwezo alionao.
|
c
|
-
|
Dialogia hujaribu kuiga hali halisi ya maisha kimazungumzo kama ilivyo katika jamii.
|
d
|
-
|
Dialogia huonyesha uhusiano mkubwa wa kimawazo uliopo kati ya watu wanaozungumza au kujibizana katika hadithi huku wakitoa dhamira na maudhui muhimu yaliyokusudiwa na jamii.
|
e
|
-
|
Dialogia kati ya watu wawili au zaidi hujengwa na mwandishi ili waweze kutofautiana kimaumbile na ki-mazungumzo. Mwandishi huwaonyesha wahusika hao kwa kuzingatia utabaka wao. Mambo kama maneno, ridhimu na mwendo wa sentensi na matamshi pia yanatofautiana.
|
f
|
-
|
Kwa wasomaji wa hadithi, mbinu hii husaidia kupunguza uchovu wakati wa kuisoma hadithi.
|
Mbinu hii ya kidialogia inachanganya nyakati kama tulivyoona katika Monologia. Aidha, mbinu hizi zote hutumiwa na mwandishi akihoji, aki-fafanua au akijadili masuala mbalimbali katika jamii.
Msuko au Muundo wa Matukio Katika Hadithi Fupi
Muundo au msuko wa matukio ni kipengele kingine muhimu katika kuiangalia fani ya hadithi fupi za Kiswahili. Wanataaluma, baadhi yao, walioelezea maana ya muundo wamekubaliana kuwa msuko nijumla ya mpangilio, uteuzi na uelezeaji wa vipengele mbalimbali vya matukio katika kazi ya kubuni ya sanaa, hususan hadithi fupi. Muundo huipa kazi ya sanaa fani na umoja wa kimantiki, kama anavyosema Walter Blair33 na wenzake. Wakati mwingine, vitu kama lugha itumikayo, utanzu utumikao, aina ya sentensi, huelezwa kama violezo vya kimuundo. Mfuatano au mtiririko wa vituko vinavyojenga mgogoro katika hadithi unatakiwa uunde mantiki na mafundisho kwa jamii.
Aidha, wakati wakiangalia hadithi kwa ujumla, Penina Muhando na Ndyanao Balisidya34 wameijadili misuko ya hadithi ndefu na kuitaja kuwa ni Msuko wa Kioo, Msuko wa Msago (Msuko wa moja kwa moja), n.k. Japokuwa misuko au miundo hii imetajwa kuwa ni ya riwaya, kwa upande mwingine inatumiwa na hadithi fupi pia. Tofauti muhimu kimatumizi ipo katika upana wa mawanda. Misuko katika hadithi fupi inaambaa katika mawanda yasiyo mapana, na kwa hiyo huifanya hadithi isiwe na uwanja mpana wa kuelezea vituko na vitukio vyake. Tuangalie misuko hiyo ya hadithi kwa undani kidogo.
Msuko wa Msago
Katika aina hii ya msuko, matukio yanasimuliwa na kuonyeshwa kuwa yanafuatana na kuhusiana kimantiki kutoka mwanzo hadi mwisho. Matukio hayo yanakwenda sambamba na wakati. Kila tukio katika msuko au muundo huu linafanyika mahala pake na kwa wakati wake. Angalia Kielelezo Na. 3.
Kieldezo 3: Msuko wa Msago
Katika kielelezo hiki, hadithi inaanzia penye A. Wakati unaonyesha baada ya saa moja. Hadithi inaendelea ua kufikia upeo B wakati muda unaonyesha saa sita. Kisha hadithi maendelea na kufikia mwisho penye C wakati muda unaonyesha saa kumi na mbili.
Msuko wa Kioo
Katika msuko huu, matukio yanasimuliwa kutoka mwanzo kwa kutumia kanuni na taratibu za miundo mingine kama vile Msuko Msago, Mwanzo-Kati, Kati-Mwisho, Mwisho-Mwanso, n.k. Katika usimulizi wake, msuko huu husimulia matukio kwa kurudia jambo lililowisha kuelezwa1 mwanzo. Ni matukio ya kudakiyana. Baadhi ya wanataaluma, kama vile F.E.M.K.Senkoro,35 wameutaja msuko huu kawa unatumia mbinu za viona nyuma na viona mbele. Wengine kama vile F.V. Nkwera36 wanauelezea msuko huu kuwa ni wa rukia Angalia Kielelezo Na. 4.
Kielelezo 4: Msuko wa Kioo
Hadithi inaanza penye A. Matukio yake yanasimuliwa kwa kudakiyana kupitia B hadi mwisho C. Ukichunguza kwa makini utaona muda wa matukio hauoam vyema ua mwendo wa matukio kama ilivyo katika Msuko Msago. Msuko huu umechangamana.
Msuko Mwisho-Kati-Mwanzo
Msuko huu huanza na matukio ambayo m ya kumalisia hadithi, au yale ambayo yangepaswa yawe mbele zaidi mwa hadithi.
Msanii akisha yaeleza matukio hayo yaliyotakiwa yawe mwisho mwanzoni, halafu huelezwa matukio ya katikati, hatimaye huelezwa yale ambayo yangepaswa yawe mwaazoni. Wakati mwingme mwandishi huelezea. matukio yanayomalizia hadithi kama mwanzo, baada ya kuendelea na hadithi huelezwa baadaye kidogo. Kisha hadithi hiyo huendelezwa na ifikapo nwisho, inarudia tena kueleza yale matukio yaliyoelezwa mwanzo. Baadhi ya wataalamu wameuita msuko huo kisengerenyuma37 Tazama Kielelezo Na. 5.
Mfano wa hadithi kama hu ni ile ya Mzimu wa Watu wa Kale38 ily otungwa na M.S. Abdulla.
Msuko Mwanzo-Kipeo
Mwandishi maweza kuandika hadithi asifikie mwisho, bali kileleni. Hadithi kama hii kwa kawaida hutumia taratibu za msuko wa kawaida, yaani msuko wa msago ama wa moja kwa moja. Mwandishi huionyesha hadithi yake ikikua huku mhusika wake mkuu akionyesha mambo na matendo muhimu yanayozidi kuijenga dhamira muhimu aliyoikusudia. Mara hadithi ikifikia kileleni inakatishwa ghafla ua kumwacha msomaji katika taharuki kali. Tazama Kielelezo Na. 6(a) kwa ufafanuzi.
Kielelezo 5: Msuko Mwisho-Kati-Mwanzo
Katika hali ya kawaida sehemu BC ilipaswa isimuliwe, lakini katika hadithi hii inaonyesha haikusimuliwa. Badala yake iko sehemu AB tu!
Aidha, badala ya kuanza mwanzo kama ilivyoonyeshwa katika Kielelezo Na. 6(b) hadithi yaweza kuanza na kilele hadi kufikia mwisho.
Katika kielelezo hiki sehemu AB ilipaswa iwe imesimuliwa kabla ya BC. Sehemu BC imeanza na kipeo B, na halafu hadithi husimuliwa hadi mwisho.
Tunaweza kuhitimisha sehemu hii inayohusu misuko ya hadithi kwa kusema kuwa kimsingi, mwandishi anaweza kuwa na mpango wa msuko wa hadithi yake ambao atautumia katika kuelezea mwendo au maendeleo ya matukio katika hadithi nzima. Aidha, msuko wa mwandishi unaweza usitumie kila tukio analolifanya mhusika wa hadithi anayokusudia kuielezea kama inavyoonyeshwa katika Kielelezo Na. 7.
Matumizi ya Mashairi na Nyimbo
Katika kuimarisha kazi ya fasihi mwandishi anaweza pia kutumia nyimbo ama mashairi katika hadithi fupi. Jambo hili linasaidia katika kujenga fani ya aina fulani na kutoa ufafanuzi zaidi wa maudhui. Kwa upande mwingine hilo huingilia utaratibu wa msuko wa hadithi ambao hujikuta umetengeneza vifungu mbalimbali vinavyofanana na vidato katika hadithi nyingine.
Kielelezo (6a: Msuko Mwanzo-Kipeo)
Kielelezo 6b: Msuko Kipeo-Mwisho
Kilele na Mpomoko katika Hadithi fupi
Kilele katika hadithi ni mabali ambapo panaonyesha mabadiliko katika mkondo mzima wa hadithi. Ni mahala ambapo mkwezo wa mawazo yanayosimuliwa katika hadithi hufikiwa kilele. Kwa mfano katika hadithi fulani-labda ya kukata mkonge kulikuwa na tatizo ama mgogoro juu ya vijana kukimbia kufanya kazi ya kukata mkonge, sasa hawakimbii tena kwa sababu labda wamepewa vivutio. Au katika hadithi ya mapenzi, kama kulikuwa na watu wawili: msichana na mvulana waaataka kuoana, pale wanapokubaliana kuoana patakuwa ni kipeo au kilele.
Kielelezo 7: Uteuzi wa Matukio katika Uandishi wa Hadithi
Wakati mwingine huwa si suala la mgogoro kuchukua upande wa pili, bali kipeo paweza kuwa mahali popote ambapo migogoro ya kazi ya sanaa ya kifasihi inayohusika inaonyesha maana kamili. Kwa hiyo kilele kinaweza kiwe mwanzoni niwa hadithi - hasa katika msuko wa hadithi wa kioo - au kinaweza kuwa katikati ya hadithi au hata mwishoni mwa hadithi. Kwa ujumla hii itategemea na mawazo ya msanii mwenyewe.
Kimsingi, kilele wengine huita kipeo na ni vitu vinavyohusiana katika hadithi. Kuna aina mbili ya vilele: kilele chajuu ua kilele cha chini. Tumetaja na kujadili kilele cha juu hapo awali. Tuone kilele cha chini ni nini? Kilele cha chini kinaonyesha tabia iliyo tofauti au iliyo kinyume na ile ya kilele cha juu. Kilele hiki ni mashuko ya mawazo, mahali ambapojambo au wazo hulegezwa mkazo wake wa kusisitizwa. Kilele cha chini hujitokeza wakati ambao msanii anaijenga kazi ya kifasihi na kuleta hisia iliyo kinyume na matazamio ya wengi. Msamiati wa Muda wa Fasihi ya Kiswahili39 unatoa mfano wa mhusika Kmjeketile wakati anapokabiliana na wakinzani wake, anakusanya wananchi wake ili wapigane na maadui hao. Lakini kinyume na matarajio ya wasomaji, Kinjeketile anakataa kwenda vitani. Mahali hapa ndipo panaonyesha kileie cha chini, ambacho istilahi yake iliyotolewa na BAKITA * ni mpomoko.
* BAKITA = Baraza la Kiswahili la Taifa
Vilele katika kazi za sanaa za kifasihi huundwa na wasanii kwa madhumuni mbalimbali, na kuweko kwa vilele hivi kumezua mawazo tofauti kwa wanafasihi. C.H. Holman40 kwa mfano anasema kuwa katika baadhi ya kazi za fasihi vilele vya chini huwa ni udhaifu wa kazi zao. Lakini katika kazi nyingine za kisanaa, hususan hadithi fupi za Kiswahili, kilele cha chini kimekusudiwa hivyo na msanii ili kuleta athari iliyokusudiwa naye. Hali hii ya pili hutokea katika hadithi fupi ambapo kipeo au kilele cha chini hutumiwa kuwa mbinu ya kuipa hadhira mshangao mkubwa, yaani taharuki. Sifa hii ya kitaharuki ni muhimu sana katika kazi ya sanaa ya kifasihi, ua hasa hadithi fupi.
Suala la Migogoro
Hadithi yoyote ile lazima iwe na migogoro. Migogoro katika hadithi husaidia kujenga aina mbalimbali ya misuko ya hadithi. Migogoro ni nini hasa? Migogoro ni mivutano ama mikinzano katika kazi za fasihi. Mgogoro unaweza kutokea ua kukuzwa na uhusiano uliopo kati ya mawazo mbalimbali na matendo mbalimbali. Mgogoro pia unaweza kuwa baina ya wahusika wawili, au unaweza uwe kati ya mhusika na mazingira yake au kati ya wazo na wazo41 Yote hiyo ni migogoro inayoweza kuwa katika kazi ya sanaa ya kifasihi.
Mgogoro katika kazi ya fasihi ni muhimu kwa sababu ndio unaojenga mvu-tano baina ya wahusika na kujenga maudhui yanayohitajika.
Migogoro inayojitokeza katika kazi ya fasihi inaweza kuwa katika mafungu makuu matatu. Migogoro hiyo ni ya kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa. Migogoro hiyo ikiangaliwa kwa undani inatokana ua utawalaji wa nyenzo za uzalishaji mali katika jamii. Kwa mfano kama kuna wale walionacho hawawajali wasionacho, wasionacho wataamua kudai haki yao kwa nguvu, na hivyo kuunda mgogoro wa kiuchumi.
Mgogoro mwingine ni ule wa kisiasa. Katika aina hii ya mgogora mtu anaweza kuwa hakubaliani ua siasa ya nchi yake na mwandishi wa kifasihi anamwonyesha kama mpinzani. Mgongano huu unaweza kuonyeshwa kama kitu kidogo kinachoenea kwa watu wengine kutokana na uwezo wa kipropaganda anaoweza kuonyesha na labda kuwa nao mtu huyo.
Mkondo mwmgine wa migogoro un akuwa katika kundi la utamaduni. Huko tunakuta migogoro kama ile ya mapenzi ndoa; Jini ua imani malezi na tabia nyinginezo.
Tukiondoa migoro hiyo tuliyoitaja na kuizungumzia hapo juu, kuna mgogoro mwingine muhimu ambao tunafikiri ni bora kuutaja hapa. Huu ni mgogoro wa mtu binafsi. Wakat: wote mhusika akiwa katika jamii anaonekana kuzongwa na hali mbili: kutenda au kutotenda. Hali hii itamjengea mivutano mbalimbali kila pale atakapokutana na mazingira fulani katika maisha yake. Kwa kuzingatia hilo, mwandishi wa hadithi fupi anatakiwa kuwajenga wahusika wake kwa kuzingatia pia aina hii ya migogoro.
Mianzo, Kiwiliwili, na Miisho ya Hadithi ya Hadithi Fupi
Tumesema msuko wa hadithi fupi umegawanyika katika sehemu kuu tatu, yaani nawanzo, kati, na mwisho. Lakini tulitoa tahadhari kuwa si kila hadithi fupi hufuata utaratibu huo kwa sasa kutokana ua mabadiliko kadhaa ya kisanaa yaliyokwisha tokea katika fasihi. Kama tulivyokwisha dokeza, ziko hadithi zinaweza kuanza ua mwisho, ukafuata mwanzo, na kumalizia na sehemu nyinginezo. Aidha, bado kuna hadithi zile zenye kuzingatia utaratibu wa mianzo ileile ya awali iliyosemwa na wakongwe wa Kiyunani akina Plato na Aristotle. Katika sehemu hii hatutaingilia mjadala juu ya mianzo hiyo, lakini tutataja vipengele hivyo vya mianzo katika hadithi fupi kama vilivyo kwa sasa, kwa kuzingatia kuwa zina asili ya kimapokeo ama ni za kisasa.
Mianzo
Tutaigawa mianzo ya hadithi fupi katika mafungu mawili ya msingi. Mgawanyo huu umefanywa kwa kuzingatia mikondo ya hadithi hizo fupi zi nazoandikwa kwa Kiswahili ua ni za Kiswahili. Mianzo hiyo ni (a) ile inayotokana na mkondo wa hadithi za Kiswahili za simulizi, hadithi za kingano (b) mianzo ile inayotokana na mkondo wa hadithi za kubuni za kisasa.
Mianzo ya Hadithi za Simulizi
Hadithi za namna hii zina mianzo ya aina tatu inayofanana. Aidha, ziko tofauti ndogo kati ya mwanzo mmoja na mwingine. Mianzo hiyo hutanguliwa na kifungu cha maneno maalumu, ambacho kimsingi hutamkwa na kiongozi kama hadithi inatambwa, au inaweza ikasomwa tu katika hali ya kawaida kama inasomwa na mtu yeyote yule. Baada ya kumaliza utangulizi huo, kiwiliwili cha hadithi ndicho kinachofuata. Mfano wa mwanzo wa aina ya kwanza ni kama ufuatao:
Paukwa! (Kiongozi)
Pakawa! (Hadhira)
Paukwa! ... ...
Pakawa! ... ...
Baada ya kumaliza utangulizi huo, masimulizi ya hadithi nzima yanafuata. Kwa kawaida huanza ua: 'Hapo zamani za kale... Kuliondokea mtu ua mkewe... Siku moja Chura na Ng'ombe... Paliondokea..." na kadhalika.
Mwanzo wa aina ya pili ni kama ufuatao:
Hadithi, hadithi! (Kiongozi)
Hadithi njoo! (Hadhira)
Hadithi, hadithi! ... ...
Hadithi njoo! ... ... ...
Baada ya kitangulizi hicho, masimulizi hufuata kama ilivyoelezwa hapa juu kaitka kifungu cha kwanza.
Mwanzo wa aina ya tatu ni kama ufuatao:
Atokeani! (Kiongozi)
Naam Twaib! (Hadhira)
Kaondokea Chenjagaa
Kajenga nyumba kakaa
Mwanangu Mwanasiti
Kijino kama Chikichi
Cha kujengea kijumba
Na vilango vya kupitia...
Katika kifungu hiki kiongozi huanzisha kwa kusema: Kaondokea Chenjagaa na hadhira huungana naye na kusema kifungu hiki kilichosalia. Wakishamaliza kifungu hiki ndipo hadithi iliyokusudiwa husimuliwa. Wakati mwingine mianzo hiyo inaweza kuwa katika mfumo wa kishairi kama inavy-oonyeshwa katika mfano huu ufuatao, ambao umechukuliwa kutoka katika gazeti la Mambo Leo42
KAKA SUNGURA
NA NAMNA ALIVYOPATA NYAMA
NA NAMNA ALIVYOPATA NYAMA
Masbairi ya kukaribisha:
Njoo tusimulie jamani
Hadithi zile za zamani
Njooni tukakaa rahani
Kuzunguka moto
Hadithi zile za zamani
Njooni tukakaa rahani
Kuzunguka moto
Hadithi zile za Mzee Ndovu
Hadithi kuondoa ucovu
Hadithi kututilia nguvu
Kuzunguka moto
Hadithi kuondoa ucovu
Hadithi kututilia nguvu
Kuzunguka moto
Mzee Simba, Kaka Fisi
Mjanja kweli ya halisi
Kila jambo kudadisi
Hadithi tamu zile
Mjanja kweli ya halisi
Kila jambo kudadisi
Hadithi tamu zile
Na Mzee Kobe, Catu, Nyota
Kutaja wote nitacoka
Sungura wote' kawapoka
Kwa zamani zile
Kutaja wote nitacoka
Sungura wote' kawapoka
Kwa zamani zile
Na Sungura yu mwerevu
Akili zake kweli mpevu
Kaka huyo mcekevu
Hadithi tamu zile
Basi tukakusanyika
Tutafurahia hakika
Mambo yalihadithika
Kwa zamani zile.
Akili zake kweli mpevu
Kaka huyo mcekevu
Hadithi tamu zile
Basi tukakusanyika
Tutafurahia hakika
Mambo yalihadithika
Kwa zamani zile.
IKATOKEA siku moja ya kuwa wanyama wote wakafanya shauri la kujenga nyumba kubwa wapate kukaa humo salama. Kila mmoja alifanya bidii nyingi sana lakini Sungura (Kaka) alisema moyoni kama kupanda ngazi mara kwa mara hucoshasana, basi yeye akashughulika shughulika tu anakwenda huko na kupima, na kurudi huko na kupima, lakini hafanyi kitu kabisa na kila mara kama wengine wanafanya kazi zao, yeye alikwenda kulala tu. Basi nyumba ilikwisha na Kaka Sungura alicagua cumba kimoja katika ghorofa juu kabisa. Akafanya werevu na walipotoka wote kutembea yeye akacukua bunduki na mzinga, na pipa kubwa la maji macafu, akayaweka cumbani mwake juu.Wanyama wakarudi na Kaka Sungura akaenda cini akakaa pamoja nao wakaongea mpaka Kaka Sungura akasema kama amecoka akapanda juu cumbani mwake. Basi alipofika juu akatoa kicwa dirishani akawaambia wale cini. "Je! ninyi, kama mtu mkubwa kama mimi anataka kukaa atakaa wapi?" Wale wengine uaceka wakaceka sana wakajibu. Kama mtu mkubwa sana kama wewe hawezi kukaa kitini basi afadhali akae cini." Kaka Sungura akajibu: "Vema, ninyi cini angalia nitakaa sasa." Basi akaishika bunduki akaipiga.Wanyama wale wakashangaa sana, wakasikiliza, wakasikiliza, mpaka wakaanza kuzungumza tena. Halafu Kaka Sungura akatoa kicwa dirishani tena akasema. "Je! kama mtu mkubwa kama mimi anataka kupiga cafya atapiga cafya wapi?" Na wale wanyama wakajibu, "Kama mtu mkubwa kama wewe hana wazimu, atapiga cafya apendapo. Kaka Sungura akajibu. "Vema angalieni ninyi cini! nataka kupiga cafya sasa." Akapiga mzinga wake.Looo, kila kitu kilistuka sana na wanyama wale Cini wakashangaa. Halafu kidogo wakasahau wakaanza kuongea tena, mara Kaka Sungura akatoa kicwa tena akasema, "Haya ninyi cini huko, kama mtu mkubwa kama mimi akitafuna tumbako yake ua akitaka kutema mate atatema wapi?"Basi sasa wanyama wale cini wakakasirika kwa ucungu."Kama mtu mkubwa, kama mtu mdogo, tema mate upendapo."Kaka Sungura akajibu. "Vema, hii ndiyo namna anavyotema mate mkubwa." Mara akamwaga maji yale rnacafu katika pipa lake yakashuka yakamwagika katika ngazi na katika vyumba cini na wanyama wale wote wakatoka mbio sana.Basi Kaka Sungura akafunga mlango, akafunga madirisha yote akalala usingizi. Wale wanyama wengine waliojenga nyumba hawakurudi tena, wakamwacilia Kaka Sungura na nyumba yake.43
Maelezo juu ya mianzo ya hadithi za simulizi yanaonyesha ukweli kuwa katika hali ya kawaida hadithi hizi hutegemea sana masimulizi ya mdomo, kusikia kwa masikio, kuona vitendo vinavyofanyika ua uhusiano kati ya mtambaji/msimuliaji ua hadhira ili kukamilisha uhusiano wa kimaudhui uliokusudiwa kutolewa. Ufanisi wa hadithi unategemea uwezo wa mtambaji katika hadithi hizo za simulizi. Kwa hiyo, hadithi hizo zinapoandikwa zinakosa mambo muhimu kisanaa yaliyokuwa yakipatikana wakati wa masimulizi. Hali hii huifanya hadithi nzima kuonekana kuwa chapwa.
Mianzo ya Hadithi za Kubuni
Baada ya kuangalia mianzo ya "ngano" sasa tuangalie mianzo ya hadithi fupi za kisasa.
(1) Jina la Hadithi: WASUBIRI KIFO
Mwandishi: E. Kezilahabi
Kutoka: Uandishi wa Tanzania (J.P. Mbonde - Mhariri)
Mwandishi: E. Kezilahabi
Kutoka: Uandishi wa Tanzania (J.P. Mbonde - Mhariri)
Kijiji cha Mkalala - kijiji ambacho kwa muda mrefu kilikuwa hakijapewa nafasi ya kuingia katika mashindano ya maendeleo - kilikuwa hakijulikani. Yamkini utafikiri hakikuwa katika ramani ya Mkurugenzi wa Wilaya - ramani ambayo ilikuwa...44
(2) Jina la Hadithi: NDUMILA KUWILI
Mwandishi: J. Rutayisingwa
Kutoka: Gazeti la Mzalendo (Gazeti la Chama)
Mwandishi: J. Rutayisingwa
Kutoka: Gazeti la Mzalendo (Gazeti la Chama)
Ali Gihaza alikuwa chumbani kwake akisoma kitabu wakati mtu alipobisha hodi mlangoni na kuuliza. "Wenyewe humu ndani mpo?" Gihaza alishtuka na kuweka kitabu mezani, akaitikia huku akiwa amekunja uso kwa fikra, "Tumo, karibu mpaka ndani."45
Mianzo hii miwili imeonyesha tofauti zilizoko kati ya hadithi za kingano na hizi za kisasa. Mianzo ya hadithi za kisasa inabadilika kufuatana na lengo la mwandishi na dhamira yake.
Kiwiliwili au Katikati
Mara baada ya mianzo hiyo, kinachofuata ni kiini cha hadithi nzima. Kwa mfano tukiangalia hadithi ya "Kaka Sungura ua Namna Alivyopata Nyama,'' mwanzo unajionyesha waziwazi, katikati napo pameonyeshwa na mwisho unaweza kutambuliwa kirahisi tu'. Ni muhimu kusisitiza hapa kuwa hadithi za asili za simulizi hazibebi sanaa kama ile ya kimasimulizi kutokana na ukweli kuwa mambo mengi yanayofanywa na watendaji hai hayawezi kufanywa kwa maandishi. Hili, tutalirejea tena hapo baadaye.
Miisho
Kama ilivyo katika mianzo, miisho ya hadithi fupi za Kiswahili nayo tunaweza kuigawa katika makundi mawili - ya simulizi na ya kisasa.
Miisho ya simulizi husisitiza raha ama kutoa taarifa ya maisha ya wahusika walioijenga hadithi. Kwa mfano:
a - Hapo ndipo wakaishi raha mustarehe
b - Hapo ndipo hadithi yangu inaishia
c - Huu ndio mwisho wa hadithi yenyewe
Miisho ya aina ya pili, ile ya hadithi fupi za kisasa ni tofauti kimsingi na hii ya hadithi za kimapokeo. Hata hivyo wakati mwingine athari za hadithi hizo za kimapokeo katika hadithi za kisasa inajitokeza sana. Mifano ya miisho ya hadithi za kisasa imetolewa hapa chini.
(1) Jina la Hadithi: WASUBIRI KIFO
Mwandishi: E. Kezilahabi
Kutoka: Uandishi wa Tanzania (J.P. Mbonde - Mhariri)
Mwandishi: E. Kezilahabi
Kutoka: Uandishi wa Tanzania (J.P. Mbonde - Mhariri)
Walipotoka huko kilimani, mahali ambapo mifupa ya baba zao ilikuwa ikizikwa - walianza kufurukuta na kutafuta mayai ya utajiri, wakasahau kwamba katika kila jiwe la msingi wa majumba hayo kulikuwa kumelala mifupa ya baba zao maskini. Kwa hiyo wakawa watu wa maneno mengi na nadharia zisizokuwa ua mkia wala kichwa!46
(2) Jina la Hadithi: NDUMILA KUWILI
Mwandishi: J. Rutayisingwa
Gazeti la Mzalendo (Gazeti la Chama)
Mwandishi: J. Rutayisingwa
Gazeti la Mzalendo (Gazeti la Chama)
Kwamba nilimchukulia rafiki na papo hapo akawa rafiki wa mke wangu si jambo ambalo limetokea kwangu tu. Hutokea kwa wengi. Mimi namuombea apone ua nimemsamehe dhambi zake zote. Hatua yoyote ninayoweza kuchukua haiwezi kumfufua Sakina.47
Hii ni miisho ya hadithi fupi za kisasa. Kwa ujumla kuna athari tuliyoisema ya kimapokeo inajitokeza kwa kiasi fulani katika miisho hiyo. Aidha, bado kuna miisho ambayo haina athari za kimapokeo.
Tunaweza kuhitimisha sasa kwa kusema kifupi kuwa hadithi fupi za kisasa zina msingi wa kubuniwa. Mtu anayebuni na kuandika hadithi za aina hii anajulikana, na kwa hiyo kazi hiyo ya sanaa huwa ni mali yake.
Ngano kwa upande mwingine ni kazi ya sanaa yenye misingi yake katika mapokeo. Kwa muda mrefu ngano zimekuwa zikisimuliwa, na hivyo, kuhifadhiwa kichwani. Ingawa kwa sasa ngano huhifadhiwa kimaandishi, bado kuna mambo ya msingi ya kimasimulizi yanajitokeza katika hadithi hizo. Hadithi hizo zikichunguzwa zinafuata mikondo (pattern) katika usimulizi wake.
V. Propp48 anazigawa ngano kwa kuzingatia kazi ambazo hufanywa na wahusika waliomo katika ngano mbalimbali. Katika kusisitiza mikondo hiyo, Propp anasema kuwa:
· Katika ngano mhusika anatazamwa anafanya nini katika matukio yote· Kimsingi, kazi za wahusika katika ngano ya aina fulani itabaki kuwa ileile hata kama anapewa jina jingine.· Mfululizo wa matendo katika ngano za aina fulani unafanana· Hata kama ngano huwa ua miundo tofauti, kimsingi zote ni za aina moja kwani zina lengo na tabia zinazofanana.
Baadhi ya wataalamu huzigawa ngano kwa kufuata dhamira. S. Kichamu Akivaga na A. Bole Odaga49 wamezingatia utaratibu wa aina hii. Kufuatana nao, kuna hadithi za ngano za visasili, hekaya, ishara, kharafa, viada na kadhalika. Mgawanyo huu unaelekea kukubalika na wataalamu wengi, wakiwemo F. Senkoro,50 Ndyanao Balisidya na Penina Muhando,51 na J. Berg Esenwein.52 Kwa vile kazi hizi ni za kimapokeo, hakuna mwenye haki nazo, isipokuwa jamii nzima.
Hadithi fupi za kisasa, zikilinganishwa na ngano, ni ndefu kidogo. Hii inatokana na mambo yanayoandikwa hadithini humo. Mambo hayo ni pamoja na kuwa na msuko ama muundo wa mtiririko wa matukio katika usimulizi wake. Masimulizi ya hadithi fupi yanazingatia uhalisia katika misingi ya muda na mahali maalumu.
Ngano husimulia kitu kilichokwisha simuliwa. Fanani anaweza kuongeza au kupunguza kitu katika usimuliaji lakini katika uandishi hawezi kufanya hivyo bila kupoteza uasili wa ngano inayohusika. Muda wake hauna mpaka (infinite past), hakuna uumbi mpana wa wahusika wake ua kadhalika.
Uzuri wa hadithi fupi unategemea uwezo wa msanii. Kama msanii ni mtaalamu na ana nyenzo zote za lugha, anaweza kutunga hadithi nzuri. Kinyume cha hapo, ataharibu. Ngano zinategemea hasa uwezo wa fanani wa kusimulia matukio ya hadithi.
Hadithi Fupi za Kibarua
Suala la mianzo, katikati na mwisho katika aina hii ya hadithi halina uzito sana, kwani hadithi nzima huwa, inachukua muundo wa barua za kawaida. Mwanzo huwa ni salaam na maamkizi, halafu huja maelezo yake, na humalizia na mwisho. Barua ina misingi yake.
Hadithi fupi za aina hii huwa ni masimulizi yanayohusu barua ziandikwazo na mhusika mmoja au wahusika zaidi. Mwandishi huwatumia wahusika kuelezea hisia na vionjo mbalimbali, lakini vyote vinajengwa na kuunganishwa katika "mkufu" wa dhamira kuu moja au wakati mwingine zaidi.
Kwa mfano, hadithi ya So Long a Letter53 ni nzuri na imepata kushinda Noma Award.
Hadithi za aina hii inasemekana kwanza zilianzia huko Uingereza, ua mwanzilishi wa kwanza wa hadithi hizo ni mtu aliyejulikana kwa jina la Samwel Richardson('s).54 Baada ya hapo, waandishi wengine walifuata kuandika aina hii ya hadithi.
Hadithi za aina hii si nyingi katika Kiswahili. Mwandishi Agoro Anduru amepata kuandika hadithi za aina hii katika gazeti laMzalendo.55 Mfano mwingine ni ule wa hadithi iitwayo "Barua kutoka Ufaransa" katika kitabu cha Chale za Kikabila.56
Kutokana na ukweli kuwa hadithi hizo ni chache, tumeona iko haja ya kuzihimiza. Katika diwani ya hadithi fupi ya kitabu hiki kuna mfano mmoja wa hadithi iitwayo "Uchungu." Tunategemea mfano huu utawasaidia wanafunzi na wale waandishi wanaokusudia kufanya hivyo.
Mfululizo wa barua hizo unaunda hadithi moja yenye mgogoro wa kimapenzi kati ya Dora Charles (msichana), na Richard m'Banza (mvulana). Mgogoro unaanza na kule kumwona Dora aigizapo mchezo wa Lina Ubani kule shuleni Kilakala. Changamoto ya mapenzi hayo inamfanya Richard m'Banza amweleze Dora nia ua lengo lake, ua kuwa ameshindwa kuvumilia bila kuwa ua Dora. Kinyume na matarajio ya Richard, Dora anapinga matakwa ya ndoa kati yake na Richard. Dora anasisitiza kuwa jambo hili haliwezekani kwa sababu yeye Dora ana mkataba mwingine wa mapenzi na mtu aitwaye Mm. Ni jibu la kusikitisha kwa Richard, na hadithi inaishia katika ushindi wa Dora na kushindwa kwa Richard. Tunaweza kuhitimisha mjadala wetu kwa kusema kuwa licha ya aina hii ya kuandika hadithi fupi za kibarua (ambayo imefafanuliwa zaidi hapa chini katika II) hutokea pia waandishi wengine wakaandika hadithi kwa kutumia aina nyingine za uandishi wa hadithi hizo fupi za kibarua. Aina hizo zimefafanuliwa hapa chini:
I. Hadithi ya Kibarua inayosimuliwa na mtu mmoja:
(i) Katika aina hii ya hadithi ya kibarua, mhusika ama mwandishi mmoja humwandikia mtu mmoja tu. Mfano kama huu uliwahi kuandikwa pia ua Agoro Anduru katika gazeti la Mzalendo (1982).57
(ii) Wakati mwingine mwandishi huandika hadithi ya kibarua kwa watu wawili au zaidi. Katika lugha ya Kiswahili hatujawahi kuwa na mifano ya aina hii ya hadithi.
II. Watu wawili au zaidi kuandikiana:
(i) Katika hadithi nyingine, watu wawili huandikiana barua wakijibizana kama ilivyofanywa katika hadithi yaUchungu katika kitabu hiki.
(ii) Yawezekana pia watu wengi wanaandikiana barua katika aina nyingine ya barua, na wanaungwa na dhamira zinazotofautiana.
(iii) Wakati mwingine katika aina nyingine ya hadithi fupi za kibarua, mtu mmoja huandikiana na wahusika wengi ambao wote humwandikia yeye majibu.
III. Watu zaidi ya wawili husimulia ama huandika barua lakini hawajibizani:
Aina nyingme ya hadithi fupi ya kibarua ni ile ambayo huwa ua waandishi wengi wa barua hizo, ambao lakini hawajibizani. Aina hii ya masimulizi kwa kweli hufanana na aina ya I na II, bali hutofautiana na hii ya III kwa kipengele kuwa katika aina hii ya hadithi, hakuna kupeana ama kujibizana/kubadilishana mawazo kama zilivyo hadithi za I na II. Hata hivyo, inasisitizwa hapa kuwa kundi III linakaribiana sana na kundi I kuliko na kundi II.
Mandhari ya Hadithi Fupi
Kwa mujibu wa C.H. Holman,58 mandhari au mazingira ya kazi ya sanaa ni hali ya maumbile ilivyo na inavyoonekana. Wakati mwingine, hali ya mizimu na kuzimu kwa ujumla; ni mandhari pia. Mazingira hayo hutumika katika kujenga masimulizi ya riwaya, drama, hadithi fupi na kadhalika. Mambo muhimu yanayounda mandhari au mazingira ya hadithi ni pamoja na (1) mahali palivyo: hali ya milima na mabonde, mpangilio wa vitu katika chumba, milango na kadhalika (2) kazi ua utaratibu wa maisha ya kila siku ya wahusika (3) muda au wakati ambapo tukio linatendeka k.m. kipindi gani cha kihistoria, majira katika mwaka na kadhalika (4) mahusiano ua maisha ya jumla ya wahusika wa kazi ya sanaa, kama vile dini yao, akili na mawazo katika masimulizi ya kazi ya sanaa na kadhalika.
M.H. Abrams59 anaelezea juu ya mazingira ya hadithi au tamthilia kuwa "ni pale yalipowekwa kulingana na mfumo wa kihistoria. Mazingira ya kazi inayosimuliwa yanahusu mahali ambapo matukio yanatendeka."
Kwa upande mwingine, Kamusi ya Kiswahili Sanifu60 inasema kifupi tu kuwa mandhari "ni sura ya mahali, aghalabu ardhi, panavyoonekana."
Tukitathmini maana zote tatu zilizotolewa, maana ya Holman ni pana na imezama kwa undani katika kulifafanua suala zima la maana ya mandhari ama mazingira. Maana nyingine mbili zinazofuatia ile iliyotolewa ua Holman si pana sana. Kwa msingi huo, tutakapojadili dhana ya mazingira tutapenda kukubaliana na Holman zaidi kwa sababu hawa wengine mawazo yao yameisha jumuishwa katika maana yake.
Kwa msanii yeyote yule, mandhari anayoitumia inatakiwa izingatie ile misingi mmne iliyotolewa pale awali. Hadithi inaonekana kuaminika kama ina mismgi hiyo.
Ujenzi mzuri wa mazingira au mandhari una nafasi ya kuleta athari mbalimbali katika hadithi. Tunajaribu kufafanua athari hizo kama ifuatavyo:
(a) Mandhari kama kitu kinachodhibiti maelezo ya matukio katika hadithi fupi.
Maelezo mazuri na ya wazi kuhusu mahali ambapo hadithi inatendeka yanasaidia kuonyesha mwelekeo wa hadithi. Maelezo hayo kwa kawaida huonyesha kwanini mambo fulani huwa yanatokea baadaye katika hadithi hiyo. Angalia mfano ufuatao kwa ufafanuzi.
Katika kutafuta uhuru na furaha, Elena Chiku Ntale aliamua jambo la mwisho kulifanya katika nafsi yake: "Kuhama huko shamba kwenye maisha duni na ovyo na kwenda kula vya wajinga mjini." Alishaona viumbe wa kike na kiume waliowanda juu ya wingu furaha juu ya fedha. Yeye ndivyo alivyo- uona ulimwengu wa jijini. Shamba - mahali ambako hakuna raha - mahali ambako kumejaa sauti za kila aina za ndege mashambani, na mende, panya na mijusi majumbani, huku wakishindana kung'arisha macho kila wakipigwa na mwanga wa taa za vibatari vya wakazi wa huko shamba, wakazi wa mbavu za mbwa!" (Tazama Nyota ya Chiku, sehemu ya Diwani ya Hadithi).
Tukisoma maelezo hayo, tunaona uwiano uliopo wa mandhari na yale yanayotokea ama atakayoweza kuyafanya mhusika katika hadithi hiyo.
(b) Mandhari kama (nguzo) ya msuko na ujenzi wa wahusika wa hadithi fupi.
Wakati mwingine, mazingira ya hadithi fupi yakiwa yameelezwa vizuri yanasaidia kuimarisha msuko wa hadithi pamoja na uumbi mhusika/wahusika wake. Mazingira yakiumbwa ovyo, wahusika ua matukio yote yanaweza kuonekana ovyo. Mfano ufuatao unaonyesha mazingira yanavyoweza kushika-manisha matendo ya mhusika na hadithi yote kwa ujumla.
...Miguu yake ya kuchonga ilibeba kiwiliwili chake cha mwili mwororo bila wasiwasi. Mara pale miguu ilipoishia, kiuno cha ubapa na kinene kidogo kilikuwa kimebeta kwa nyuma. Utadhani cha mbuni, ndege wa fahari katika mbuga za Afrika! Tumbo lake lililokuwa limeteremka kwa chini kidogo halikuwa kubwa! Aidha, lilituna kwa mbele kidogo... Mabega yake ya kadiri yalining'iniza mikono ya mbinu huku katikati ya mabega hayo kukiwa kumehifadhiwa kifua chembamba chenye kubeba titi changa zilizotuna na kuwachungulia vijana wa kila aina - wenye kustahili na wasiostahili. Lakini wote waliziona... Utadhani titi hizo zilikuwa zikiwakonyeza! Na vijana wasivyokuwa na dogo, wakawa wanamtania na kumbeza ana titi chonge kama mdomo wakuku... Ukiwauliza wenyeji wa jiji la Mwanza juu ya msichana huyu wa damu mchanganyiko ya Kimalaba na Kingoni, watakuhadithia mengi..." (Tazama Nyota ya Chiku Sehemu ya pili ya kitabu hiki).
Maelezo hayo yanaonyesha kuwa ujenzi wa mhusika Chiku Ntale umesaidiwa sana na mazingira ya tabia na mahali alipo. Kwa hiyo, tunaweza kukiri hapa kuwa mandhari yanaimarisha ujenzi wa wahusika pia.
(c) Mandhari na uibuaji wa hisia katika hadithi fupi za Kiswahili.
Mwandishi anaweza kuyatengeneza mandhari ambayo yanapohusishwa ua wahusika na matukio yake huibua hisia maalumu kwa msomaji wake. Kwa mfano, katika tamthilia inayoigizwa, jinsi taa zinavyowashwa, jinsi maelezo ya mahali, hali ya nchi inavyoelezwa inaweza kuibua hisia. Tazama mfano wa andiko lifuatalo:
Baada ya mwito wa kuanzisha kijiji cha ujamaa huko Msota, kulitokea mldkimkiki mkubwa. Kukawa huku shoka lakata miti, jembe lang'oa magugu, mitungi na maji, ua mwiko ua kuta za nyumba. Si muda mwingi kijiji kikajengeka. Mawingu ya mvua yalipotuna, watu wakawa mashambani viakishika jemhe, kila siku hadi jua linapomezwa na mawingu. Wakati wa msinu ulipofika, watu wakaandamana sokoni na magunia ya nafaka. Baada ya kukunja noti; wananchi wakakimbilia madukant wakajinunulia mashuka ya Marekani, kanzu za China, na kofia za Japani. Wapenda mambo ya starehe wakanunua radio, asubuhi wakafurahia nyimbo wafunguliapo akina Salum Abdalla au akina Mbaraka Mwinshehe. Ili mradi kila nyumba ikawa ua furaha."61
Lugha iliyotumika katika masimulizi hayo inajenga mandhari bora pamoja ua kuibua hisia kwa msomaji wake. Mwandishi ametumia lugha fasaha, lugha ya ishara. Matendo yanayoelezwa na kusimuliwa yanawakilishwa vyema katika ishara hizo.
Matumizi ya vifaa katika ujenzi wa mandhari yanatakiwa yawiane ua wakati. Kama masimulizi hayalingani na mazmgira yake, hadithi ama kazi ya sanaa yoyote ile itapwaya. Kwa mfano, mwandishi anapoandika hadithi kuhusu Dar es Salaam, si busara kusema kuwa Jijt la Dar es Salaam lilijaa barafu.kama kawaida yake. Hii si kweli, kwani kila mtu anajua kuwa Dar es Salaam hapawezi kuwa na barafu hata siku moja kutokana ua mazingira ya kijiografia ya Dar es Salaam.
Hitimisho
Katika sura hii tumejitahidi kuvichambua vipengele vya fani kwa undani kadiri ilivyowezekana. Tumejadili FANI ua vipengele vyake (...) hadithi fupi. Japokuwa mjadala umelenga hasa katika hadithi fupi, vipengele hivyo ni vya kawaida katika kazi nyingine za sanaa. Jambo la muhimu kufahamu ni kuwa wakati mwingine kunakuwa ua tofauti za mkazo au njia za matumizi ya vipengele hivyo vya kisanaa. Kwa kuunganisha mawazo yaliyotolewa na kufafanuliwa katika sura ya tatu, mawazo yaliyo katika sura ya nne yanakamil-ishwa zaidi. Wazo kwamba ili fani iweze kufanya kazi kama FANI isitenganishwe na MAUDHUI ni muhimu.
Kwa hiyo, mpangilio wa vitu kama mawazo, taswira, mandhari, (mazingira), wahusika, lugha na mengineyo unakuwa muhimu tu pale unapotumika ili kuleta maana dhahiri ya maudhui kwa ujumla. Hadithi yoyote inafanikiwa kifani kama fani na maudhui vinaoanishwa na kukamilishana vyema.
Mshikamano katika hadithi lazima upimwe kwa kuzingatia vipengele vya fani: msuko, wahusika, mazingira, mtindo, lugha na matumizi yake parnoja ua maudhui.
Maelezo
1. S. Robert, Kusadikika, EALB, Dar es Salaam: 1961.
2. Kama Na. 1.
3. P. Muhando na N. Balisidya, Fasihi na Sanaa za Maonyesho, TPH 1976: 69.
4. M.Msokile, Nitakuja kwa Siri, DUP, Dar es Salaam: 1982.
5. Kuna wahusika mbalimbali tunaoweza kuwaainisha katika fasihi ua hasa kwa upande wa hadithi, wakati wanaposimulia hadithi zinazohusika. Kwa mfano tuna wahusika wafuatao: Msimulizi tinde, msimulizi horomo, msimuhzi mkengeushi, msimulizi penyszi n.k. Kwa maelezo zaidijuu yajambo hili, soma Istilahi za Fasihi, katika kitabu hiki.
6. S.A.K. Mlacha, "Wahusika katika Riwaya za Kiswahili," (Makala), TUKI: 1983.
7. Kamusi ya Kiswahili Sanifu, TUKI - OUP, Dar es Salaam - Nairobi: 1981.
8. M. Msokile, Usiku Utakapokwisha, DUP, Dar es Salaam: 1990.
9. C. Kuhenga, Tamathali za Usemi, EALB, Dar es Salaam: 1975.
10. Mfano wangu.
11. KamaNa. 9.
12. C.H. Holman, A Handbook to Literature, Odyssey Press, New York. 1936.
13. M.M. Mulokozi ua K.K. Kahigi, Kunga za, Ushairi na Diwani Yeiu, TPH, Dar es Salaam: 1976
14. W. Blair (nawenzake), Literature, Scott, Foresman & Company: 1966.
15. F.E.M.K. Senkoro, Fasihi, PPC, Dar es Salaam, 1984. Katika kitabu chake hicho Senkoro anajadili pia dhana ya ucheshi inavyoweza kutumiwa kisanaa ili kuiimarisha kazi ya sanaa inayotumia lugha. Anasema kuwa ucheshi unaweza kutumiwa na msanii ili kujenga dhamira kuu, kufurahisha, kukejeli, ua kukebehi n.k. Kwa msingi huo, ucheshi ni kipengele muhimu sana kwa msanii kama atataka msanii huyo kazi yake iwe ua nguvu kisanaa.
16. Mfano wangu.
17. A. Abdalla, Sauti ya Dhiki, OUP, Nairobi Dar es Salaam: 1973
18. Mfano wangu.
19. Mfano wangu.
20. Kama Na. 15.
21. Kama Na. 12.
22. J.H.Mwansoko, "Mitindo katika Uandishi wa Kiswahili," (Makala ya TUKI: 1982).
23. Kama Na. 20.
24. Kama Na. 15.
25. E. Kezilahabi, Ushairi wa Shaaban Robert, EALB, Dar es Salaam: 1976.
26. BAMITA, Zaka la Damu, BAMITA, Dar es Salaam: 1976.
27. M. Msokile, Thamani ya Ukubwa, Meza Publications, Dar es Salaam: 1979.
28. E. Kezilahabi, "Wasubiri Kifo." Katika Insha J.P. Mbonde (mh) 1976.
29. G. Rwechuagura, Ufahamu wa Lugha ya Kiswahili, Heinneman, 1973.
30. Mfano wangu.
31. J.R.R. Mkabara, Mbio za Kipofu, Utamaduni Publishers, Dar es Salaam: 1981.
32. E. Kezilahabi, Rosa Mistika, East African Literature Bureau, 1972.
33. W. Blair (na wenzake), Literature, Scott, Foresman and Company, New York, 1966: 824.
34. P. Muhando na N. Balisidya, Fasihi ua Sanaa za Maonyesho, TPH, Dar es Salaam, 1976: 64-67
35. Kama Na. 15.
36. Kama Na. 7.
37. T.S.Y. Sengo, Mwalimu wa Fasihi (Mswada) (Haujachapishwa).
38. M.S. Abdulla, Mzimu wa Watu wa Kale, EALB, Dar es Salaam: 1962.
39. P. Mbughuni (Mratibu) Msamiati wa Muda wa Fasihi, TUKI, (1985).
40. Kama Na. 12.
41. Kama Na. 22.
42. Gazeti la Mambo Leo lilichapishwa Tanzania kwa muda mrefu kuanzia mwaka 1923. Hadithi nyingi zilichapishwa kwa jina la Mjomba Remus.
43. Hadithi hii imedondolewa kutoka Gazeti la Mambo Leo la mwaka 1925. Kiawahili kilichotumiwa wakati huo ni cha herufi -c- badala ya -ch- kama ilivyoonyeshwa.
44. E. Kezilahabi, "Wasubiri Kifo," katika Uandishi Tanzania:Insha (Mhariri: J.P. Mbonde).
45. J. Rutayisingwa, "Ndumila Kuwili," kutoka kwa mwandishi mweayewe.
46. Kama Na. 44.
47. Kama Na. 45.
48. V. Propp, Morphology of the Folktale, University of Texas Press, Austin + London: 1968 (3-16).
49. S. Kichamu Akivaga na A. Bole Odaga, 0ral Literature, HEB, Nairobi, 1985.
50. F.E.M.K.Senkoro, Fasihi Simulizi (Mswada) (1988).
51. Kama Na. 34.
52. Kama Na 8.
53. Kama Na. 12.
54. Mariam Ba, So Long a Letter, Heinemann, Kenya, Nairobi: 1980.
55. Gazeti la Chama cha Mapinduzi, huchapwa na Kiwanda cha Uchapaji cha Taifa.
56. S. Ousmane, Chale za, Ktkabila, TPH, Dar es Salaam, 1981
57. Kama Na. 12.
58. M.H. Abrams, A Glosary of Literary Terms, Norton University Libtary, New York: 1957.
59. Kama Na. 7.
60. C. Kuhenga, Tamathali za Usemi, EALB, Dar es Salaam: 1977.