VIPENGELE VYA FANI KATIKA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI
VIPENGELE VYA FANI KATIKA HADITHI FUPI ZA KISWAHILI
KATIKA sura hii nyadala wetu utazingatia uchambuzi wa vipengele vya fani ns kuonajinsi gani vinaleta athari mbalimbali katika hadithi fupi za Kiswahili. Tutaangalia sifa muhimu zinazohitajika katika ujenzi wa fani ya utanzu huu wa hadithi fupi. Ni muhimu kusisitiza hapa kuwa fani itakayojadiliwa hapa ina uhusiano mkubwa na maudhui, na kwamba hapa vimetenganishwa kwa ajili ya uchambuzi tu.
Vipengele vitakavyojadiliwa na kuchambuliwa ama kuchanganuliwa hapa ni wahusika, lugha na matumizi yake, muundo, mtindo na mandhari. Katika mjadala wetu tutaangalia jinsi vipengele hivyo vinavyotegemeana na kuhusiana katika kuandaa ama kuunda na kuikamilisha fani ya hadithi fupi ili iweze kutoa maudhui yanayoihusu.
Wahusika: Uumbi ama Ujenzi Wake
Wakati wa kuelezea maana ya hadithi fupi, tulisema kuwa wahusika, (pamoja na mengineyo, k.v. tukio) ni muhimu katika kuiunda kazi ya kifasihi ya hadithi. Lakini hatukuwa tumeelezea maana y'a wahusika hao katika kazi hiyo ya hadithi fupi. Pia hatukuwa tumeelezea mbinu za uumbi au ujenzi wake na jinsi wahusika wanavyoathiri mkondo wa hadithi kutokana na ujenzi wake. Katika sehemu hii tutavichambua vipengele hivyo kwa mapana.
Kwanza kabisa tuanze kwa kufafanua kwa nini wahusika wamewekwa kama sehemu ya fani na sio sehemu ya maudhui. Ukweli ni kwamba kuna hoja ambazo zimetolewa na baadhi ya wataalamu kuwa wahusika ni sehemu ya maudhui. Hawa wana sababu zao. Nia ya kuwaweka wahusika upande wa fani si kwa sababu hawachangii katika maudhui. Uamuzi wa kuwaweka upande wa fani unatokana na sababu kadhaa. Kwanza, tumefikiria, ujenzi wa wahusika m muhimu katika kutoa maudhui kwa hadhira. Mhusika hujengwa kwa namna mbalimbali-ikiwemo jinsi aonekanavyo, atendavyo na kusema. Kwa kuwa fani ni jinsi kazi ya faaihi ilivyojengwa, tunafikiri wahusika watafaa kuwa sehemu hii ya fani.
Kwa upande mwingine, wahusika ni muhimu sana katika kutoa na kufikisha dhamira kwa hadhira. Kutokana na nafasi muhimu ya wahusika katika kazi ya kifasihi, na kutokana na ukweli kwamba umuhimu wake uko' katika upande wa fani na maudhui, labda mahali panapostahili pangekuwa katikati ya pande hizo mbili-ambazo kimsingi hazipo. Tunafikiri upande wa fani ndio unaostahili kuwekwa wahusika.
Baada ya maelezo hayo mafupi, sasa tuangalie maana ya wahusika katika kazi ya- kifasihi. Wahusika katika kazi yoyote ya sanaa itumiayo lugha ni watu, wanyama ama vitu. Wahusika hao husawiriwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii. Kwa hiyo, mwandishi huwasawiri wahusika kwa wasomaji wake kwa kutumia sifa pambanuzi walizo nazo, naimna gani walivyo, mambo gani hawayapendi na yapi wanayapenda, maisha yao n.k. Wahusika hao hutumia misemo, nahau, tamathali za usemi, na methali, katika mazungumzo yao tli kujenga tabia na hali ya kisanaa.
Wahusika wa kazi za sanaa huwa na tabia zinazotofautiana kati yao kwa sababu mbalimbali. Kwanza kabisa, inategemea mwandishi ana lengo gani analotaka kulionyesha katika kazi yake ya sanaa. Pili, aina ya kazi ya sanaa inaweza kuathiri aina ya wahusika: jinsi walivyosawiriwa, kuaminika kwao, wanavyohusiana wao kwa wao, uwakilishi wao na majina yao. Wahusika katika hadithi ni mhimili mkubwa katika fasihi andishi na hata simulizi.
Utofauti mwingine wa wahusika katika hadithi unatokana na mbinu za uumbi wao, ambao kwa upande mwingine unategemea kwa kiasi kikubwa uwezo wa usanii alionao mwandishi pamoja na dhamira anayoielezea kama tulivyosema.
Msanii anaweza kuamua kuwa anataka wahusika wanaowakilisha tabia na matendo fulani tu katika jamii na kwa hiyo atawaumba wahusika hao ili kukamilisha nia na lengo lake. Katika kuzipata tabia na hali za wahusika, msanii analazimika kutumia mbinu za kuwapa majina wahusika wake, kama wakati mwingine anavyofanya Shaaban Robert katika baadhi ya vitabu vyake kama vile Kusadikika1 na Adili na Nduguze2 Katika kazi hizo za Shaaban Robert, majina yanaonyesha moja kwa moja tabia ya mhusika mwenye jina linalolingana na tabia ambayo mwandishi anataka kuielezakwajamii. Wakati mwingine mwandishi anaweza kuwaelezea wahusika jinsi walivyo.
Penina Muhando na Ndyanao Balisidya3 wanasema kifupi tu kuwa wahusika wanaweza kuumbwa kinafsia, kiakili na kimwili. Kutokana na ujenzi wa aina hii, mhusika huonyesha wasifu wake wa ndani na nje, au anaweza kuonyesha mabadiliko yake kila anapokutana na mazingira tofauti. Hii inamaanish a kuwa mhusika ataonyesha mabadiliko na ataonekana katika uhalisia wake kwa kuzingatia nguvu zinazomzunguka kama vile za utamaduni, siasa, uchumi na kadhalika.
Ikibidi wakati mwingine, mwandishi anaweza kumjenga mhusika mmoja kwa njia ambayo ni tofauti na mhusika ama wahusika wengine katika kazi yake ili aweze kuijenga dhamira iliyokusudiwa. Kwa kuzingatia sababu hiyo, mwandishi analazimika kuwatumia vyema wahusika wake.
Hii vilevile madhihirisha kuwa mwandishi huyapisha mawazo aliyonayo juu ya ulimwengu kwa wahusika wake. Mwandishi anayo nafasi ya kuwajenga wahusika wake kadiri anavyopenda, lakini ana mipaka katika utanzu huu wa hadithi fupi kama ilivyodokezwa hapo awali.
Kila msanii kimsmgi ana mbinu za kuumba wahusika wake. Anaweza kutumia mbinu ya aina moja, au anaweza kutumia mbinu mbalimbali katika kazi moja.
Mbinu za kuwaumba wahusika zinategemea pia uwasilisho wake kwa wasomaji. Katika kuwawasilisha wahusika kwa wasomaji, msanii anaweza kutumia njia mbalimbali. Kwanza, anaweza kuwawasilisha kwa kuwaumba kidhahiri (exposition). Katika mbinu hii sifa na matendo ya mhusika yanaelezwa waziwazi. Njia hii ya kuwaumba wahusika husaidia kumfanya msomaji asipate taabu katika kutambua kiini cha kisa, wazo au dhamira. Msanii hapa anamjenga na kumtumia mhusika huyo kutoka mwanzo hadi mwishoni mwa hadithi yake. Uwasilishaji dhahiri kwa upande mwingine huambatana na mbinu nyingine za usimuliaji wa hadithi. Kwa kawaida uwasilishaji dhahiri hutokea wakati hadithi inaposimuliwa na mhusika au msimulizi wa nafsi ya kwanza. Mfano wa hadithi zenye aina hii ya usimulizi zinaweza kupatikana katika kitabu cha Nitakuja kwa Siri.4 Katika usimulizi wake, mhusika mwenyewe huelezea kila kitu anachokitenda.
Udhahiri pia unajitokeza wakati hadithi inaposimuliwa na msimulizi Mmaizi. Msimulizi Mmaizi ni wa nafsi ya tatu ambaye anazijua siri zote za wahusika wote. Huyo ni msimulizi anayeweza kuwako kila mahali kwa wakati mmoja na anayejua tangu mwanzo mambo yote katika dunia yake ya h dithi. Uumbaji huu unaweza kutumia utangulizi ambao mwandishi anaweza kuuweka mwanzoni mwa hadithi yake
Msanii anaweza pia kumwuumba mhusika kimatendo na kumwasilisha kwa hadhira yake. Katika aina hii ya uwasilishaji msanii hutumia ufafanuzi mchache wa maoni yake na sehemu kubwa humwachia msomaji anayetakiwa afasiri maana na sifa za mhusika aliyeumbwa kutokana na matendo yake. Msanii huwaumba wahusika kwa kutoa matendo nusunusu, hafcoi maelezo juu ya matendo yote kwa mara moja.
Msanii anaweza pia kumwasilisha mhusika kwa kutumia mbinu za kihisi. Mawazo au hisi hizo hutokana na nafsi ya mhusika huyo5Wakati mwingine msanii hutumia mbinu za mazungumzo baina ya wahusika wake, yaani wahusika huwekwa wazungumze wao kwa wao. Hapo kadiri wanavyoendelea, wazo la mhusika pamoja na tabia yake hujulikana taratibu katika kazi hiyo. Kwa kuyaunganisha mawazo, matukio na matendo ya mhusika huyo tabia na pengine maumbile ya mhusika katika hadithi hudhihirika.
Aina ya Wahusika
Katika hadithi fupi kuna wahusika wakuu na wahusika wasaidizi ama wadogo. Hebu tuwaangalie wahusika hao kwa undani.
Wahusika Wakuu
Wahusika wakuu kwa kawaida ni mmoja ama wawili katika hadithi fupi. Wahusika hao hujitokeza kutoka mwanzoni hadi mwishoni mwa hadithi. Mara kwa mara wahusika wa aina hii hubeba kiini cha dhamira kuu na maana ya hadithi yote. Vituko na matendo yote hujengwa kuwahusu ama kutokana nao.
Kwa kawaida, wahusika hao huonyesha mabadiliko mengi ikiwa ni pamoja na kupoteza nafasi kubwa kama walikuwa nayo: mhusika hufikia kilele, anaanguka. Au inawezekana mhusika akaibuka ghafla mwishoni mwa hadithi na kuonekana kuwa ni mtu maarufu baada ya kuwa duni katika hadithi akionyesha tabia mbalimbali.
Wahusika wa hadithi fupi hawasawiriwi kwa mapana kutokana na sababu ya mawanda. Mawanda ya hadithi fupi si mapana kama yale ya tamthiliya ama riwaya.
Wahusika wakuu wanaweza kuwakilisha vikundi mbalimbali katika jamii, au wanaweza kuwakilisha tabia za mtu binafsi, n.k. Ikitokea labda mhusika mkuu amekufa wakati hadithi haijafikia mwisho, itambidi mwandishi kumleta mhusika mkuu mwingine atakayebeba uzito wa mhusika aliyekufa. Kama hafanyi hivyo, hadithi italazimika kuishia pale ilipofikia.
Wahusika Wasaidizi
Katika hadithi fupi, wahusika wadogo sio muhimu sana kama wahusika wakuu, na hujitokeza hapa na pale katika hadithi inayohusika. Wakati mwingine wahusika wa namna hii hujengwa sambamba na mhusika mkuu, huku wakihusishwa na migOngano mbalimbali. Mbinu ya aina hii ya kuwasawiri wahusika inajitokeza sana katika hadithi fupi za kisasa.
Ukiwalinganisha wahusika wadogo (wasaidizi) na wahusika wakuu hawa sio muhimu sana, lakini kuwako kwao kunasaidia kufafanua dhamira za hadithi na kuipa mwelekeo muhimu wa kisanaa na kimaudhui. Wahusika hao hujitokeza mara moja moja. Kwa ujumla wahusika wote katika hadithi wanahusiana. Wahusika wasaidizi wanasaidia kukuza, kudumaza au kufanya maamuzi muhimu ya hadithini.
Katika makundi mawili ya wahusika tuliyoyaona hapa juu, tunaweza kuwa na aina tatu nyingine za wahusika muhimu. Wahusika hawa ni bapa, duara (mviringo) na wahusika wafoili (shinda).
Wahusika Bapa
Wahusika bapa huwakilisha aina moja tu ya tabia kutoka mwanzo hadi mwisho wa hadithi. Wahusika hao wanazingatia kuishi katika wazo moja kuu waliloanza nalo kutoka mwanzo hadi mwisho. Wahusika bapa hawawezi kubadilishwa na mazingira au na matukio ya wakati wanayokutana nayo. Wala uhusiano wao na wahusika wengine wa hadithini haubadiliki kutoka mwanzo hadi mwisho. Kwao, inategemea wameanza na uhusiano wa aina gani.
Kimsingi, wahusika bapa wanatumika kama chombo maalumu kilichoan-daliwa rasmi na msanii ili kutimiza lengo fulani bila ya kujali hali za kawaida za maisha ya binadamu. S.A.K.Mlacha6 anawagawa wahusika hawa katika mafungu mawili, wahusika bapa-sugu na wahusika bapa-vielelezo.
Wahusika bapa-sugu ni wale ambao wanaonyesha msimamo wao kutokana na maelezo ya msanii. Wanakuwa sugu katika hali kwamba hawabadiliki, kila wanapoonekana, hali zao huwa ni zilezile, hawahukumiwi bali wao huhukumu tu, hawashauriwi bali wao hushauri tu, hawaongozwi bali wao huongoza tu. Wanakuwa kama madikteta!
Wahusika bapa-vielelezo kwa upande mwingine ni wale ambao pamoja na kutobadilika kwao, wamepewa majina ambayo humfanya msomaji aielewe tabia na matendo yao. Mfano wa wahusika hao ni ule wa majina kama Boramimi, Majivuno, Karama n.k. Shaaban Robert anatumia sana mtindo huu.
Katika aina hii ya wahusika, msanii anatilia mkazo katika aina moja ya tabia inayotawala, na ambayo anataka iwafikie wasomaji kiasi ambacho sehemu nyingine zote za sifa za mhusika huyo hazionyeshwi. Wahusika bapa hawawakilishi hali halisi ya tabia za watu wanaoishi. Kwa kawaida huonyesha kipengele kimoja tu cha tabia hata kama wanakutana na mazingira mbalim-bali.
Wahusika Duara
Wahusika wa aina hii vilevile huitwa wahusika mviringo. Hao wanaonyesha tabia mbalimbali kila wakiwepo katika hadithi Wahusika hao ni hai zaidi na wanavutia kisanaa. Kwa kawaida mhusika mmoja anajengwa akionyesha tabia mbalimbali kila anapokutana na mazingira fulani, japokuwa tabia hizo nazo haziwi zote. Ni wahusika wenye kubadilika kitabia, kimawazo, kisaikolojia, n.k. Wahusika wa aina hii hukua, huugua, hufa hucheka, hununa n.k., kila paaapopaaa. Kwa hakika wahusika hao wanawakilisha maisha ya watu katika uhalisi wake. Wahusika duara' wanavutia kisanaa ukiwalinganisha na wahusika bapa tuliok wisha kuwaona hapa juu. Kila tukio watendalo wahusika duara hufanya hadithi ijisogeze mbele kisanaa na kidhamira, na huifanya badithi ikubalike katikajamii na kuaminikajuu ya ukweli wa kutendeka kwake. Vwezekano wa kuwaonyesha wahusika duara kwa mapana katika riwaya ni mkubwa sana kuliko katika hadithi fupi.
Wahusika Wafoili
Wahusika wa aina hii wapo katikati ya wahusika duara na wahusika bapa. Hawakujaa kama wahusika duara, lakini ni hai zaidi kuliko wahusika bapa.
Wahusika wafoili wakati mwingine hujulikana kama wahusika shinda, Ili waweze kujengeka vizuri, wahusika hao huwategemea wahusika duara na wahusika bapa. Wanaendeshwa na mawazo ya wengine.
Kwa kawaida wahusika hao wana tabia na matendo ama msukumo wa nafsi ulio tofauti na wahusika wakuu ama wahusika wengine muhimu katika kazi ya sanaa. Mwandishi huwajenga na kuwatumia wahusika hao ili kupambanua zaidi sifa pekee walizo nazo wahusika wakau ama wahusika muhimu katika kazi ya sanaa inayohusika. Kwa mfano, weupe wa nguo uaavyojitokeza ukiwa katikati ya nguo nyeuni, au nguo nyeusi hiyo inavyojitokeza ikiwa katikati ya nguo nyeupe. Mguo nyeusi itakuwa nyeusi zaidi ikiwa katikati ya nguo nyeupe, na nguo nyeupe itakuwa nyeupe zaidi ikiwa katikati ya nguo nyeusi.
Ujengaji huu wa wahusika unafanywa na msanii ili kuipa nguvu zaidi kazi ya kisanaa inayohusika. Wahusika kama vile wababe, wapinzani, n.k. wanaweza kuwako katika kundi hili pia.
Wahusika wafoili (au hata wahusika wengine) sio lazima wawe katika kila hadithi fupi (ama hadithi kwa ujumla). Hadithi inaweza kuwa na wahusika wale ambao msanii ameamua wawe katika kazi yake.
Aina za wahusika zilizojadiliwa hapa juu zinaathiriwa katika ujenzi wake na matakwa ama uamuzi wa msanii mwenyewe katika kuwajenga wahusika hao. Msanii waweza kuamua kuonyesha kuwa wahusika wake wanawakilisha utaifa fulani: Mwafrika, Mwingereza, Mmarekani, Mrusi, Mchina na wengineo. Au, mhusika anaweza kuwakilisha hali yake katika jamii: Bachela, na wengineo. Mwisho, anaweza kuwakilisha tabia mbalimbali: jasiri, kichaa, mwisi na nyinginezo.
Hata hivyo, wahusika hao wote wana jambo moja mahimu: kwamba si watu halizi wanaoishi, bali ni mkusanyiko wa tabia za watu halisi wanaoishi, walioishi au watakaoishi siku sijazo na kujazilizwa kwa wahusika hao ili waweze kujenga dhaaa fulani anayoitaka msanii.
Kutokana na umuhimu wa wahusika katika hadithi fupi (na hata katika kazi nyingine za kisanaa za fasihi) msaii yapasa afanye uchunguzi mkubwa kabla ya kufanya uchaguzi wa wahusika anaotaka kuwatumia katika kazi yake ya sanaa. Jambo litakalomwongoza, pamoja na mengine, ni dhamira aliyoichagua, mbinu za uwasilishaji anazotaka kutumia, usisimko wa aina ya kazi anayoisanii n.k. Mbinu hizo zitamfanya mhuaika kuwa mzuri au duni kisanaa. Wahusika katika ujumla wao, huarifu, hufundisha, hufurahisha, au vyote hufanywa kwa pamoja.
Kuaminika na Kutoaminika kwa Wahusika
Katika kazi ya sanaa, mhusika anayeaminika m yule ambaye masimulizi yake katika hadithi yanaaminika kutoka mwanzo hadi mwisho. Hata hivyo, kuna baadhi ya usimulizi katika hadithi unafanya masimulizi yake yasiwe ya kuaminika. Mara nyingi wahusika wa kuammika ni wa aina mbili: Msimulizi Mmaizi wa nafsi ya tatu ambaye katika usimulizi wake anaelekea kujua kila kitu. Pia, msimulizi wa nafsi ya kwanza naye ana nafasi ya kuaminika.
Mwandishi anawajenga wahusika wa kuaminika nje au ndani ya hadithi yake kwa madhumuni maalumu wakati mwingine. Kuaminika kwa wahusika kutakuwa ni kule kukubalika kwao kimatendo katika mkondo wote wa hadithi yenyewe au maisha ya kawaida ya binadamu.
Wakati mwingine msanii huwajenga wahusika wake visivyoaminika kwa makusudi ya kuonyesha dhamira na lengo fulani, au kwa kutodhamiria na kutokuelewa jinsi ya kuwajenga wahusika wake.
Aidha, maelezo mengi yaliyotolewa kuhusu wahusika yanahusu pia wahusika wa riwaya. Wahusika wa hadithi fupi wanatakiwa wawe wachache sana na wajengwe kifupi na kirahisi, tofauti na riwaya.
Matumizi ya Lugha
Majadiliano na maelezo juu ya maana ya lugha yamekwisha fanywa na wataalamu mbalimbali. Lugha, kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu "ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au kabila fulani kwa ajili ya kuwasiliana."7 Tutaitumia maana hii katika auala lote la mjadala wetu kuhusu lugha katika kazi ya sanaa. Hata hivyo, japokuwa Lugha inatumika kama chombo cha mawasiliano, mawasiliano hayo yanatofautiana kulingana na mazingira. Kuna mawasiliano rasmi ambayo hufanywa sehemu fulani fulani, na kuna mawasiliano ya kisanaa ambayo hufanywa katika kazi za sanaa. Katika sura hii tutajadili zaidi juu ya mawasiliano ya kisanaa. Tutaangalia matumizi ya lugha katika hadithi fupi, na kwa kiasi fulani katika kazi nyingine kila tutakapoona kuwa ni muhimu kupambanua matumizi ya Lugha katika hadithi fupi. Vinginevyo, kazi za lugha hazihesabiki, na wala hatuwezi kuzieleza zote hapa.
Lugha katika hadithi fupi ya Kiswahili ni mtindo anaoutumia msanii kujieleza kimaandishi. Kwa hiyo, tutakapojadili matumizi ya lugha katika hadithi fupi za Kiswahili, tutazingatia mbinu mbalimbali zitumikazo katika kusanii maneno ambayo yanaleta athari matika maana iliyokusudiwa na watumiaji wake.
Lugha kama kiini cha mawasiliano huifanya hadithi iwe hai na iweze kuelezea dhana mbalimbali katikajamii. Hadithi fupi nzuri inakuwa na lugha yenye mpangilio maalumu, lugha ya ujazo. Uzuri wa lugha hapo unazingatia ukamilifu wake katika sarufi, mofolojia (maumbo), fonolojia (umbosauti) na umbo maana katika uchangamano wake.
Msanii mzuri hutumia lugha kwa tahadhari kubwa. Katika usanii wake, msanii atalazimika kutumia lugha fasaha ambayo ina tamathali mbalimbali za usemi, methali, nahau, n.k. Tutazijadili semi na tamathali hizo kwa urefu hapa chini.
Methali na Misemo
Methali ni semi zinazotokana na ujuzi, sheria na tabia za jamii ambazo kwa kawaida hushauri na kufundisha mambo mbalimbali. Kwa muda mrefu methali zimekuwa zikihifadhiwa na fasihi simulizi kwa manufaa yajamii nzima. Ili kufanikisha mawasiliano na uhusiano katika jamii, methali hufuatilia maisha ya jamii ya kila siku na kujihusisha na upinzani ama usuluhishi mbalimbali. Kwa vile methali zinajitokeza katika vipengele vingi mno vya maisha yajamii tutazijadili hapa kwa kirefu kidogo ili kutoa tahadhari kwa watumiaji wake katika ujenzi na uandishi wa hadithi fupi za Kiswahili.
Mwandishi anapotumia methali katika hadithi ni vyema ajue kuwa licha ya uzuri wa kisanaa utokanao na matumizi mazuri ya methali, methali zina kazi nyingine zaidi hasa kwa upande wa maudhui.
Kutokana na kuhifadhiwa kwake kwa njia ya simulizi kwa kipindi kirefu, methali, zimekuwa na dhima ya kuueleza utamaduni kwa kupitia mifumo mbalimbali ya tamaduni na historia kwa jumla. Ni muhimu kwa mwandishi kufahamu matumizi ya kila methali anayoitumia. Kwa mfano, methali ya "Maskini na mwanaye, tajiri na mali yake," inayoonyesha kiburi cha walionacho cha kutojali wale ambao hawanacho kitu. Kiburi hicho kimeandamana na kebehi. Methali, hiyohiyo inawakatisha tamaa wale wasiona-cho! Methali ya "Kidole kimoja hakivunji chawa," au "Jiwe moja haliinjiki chungu, "inaonyesha umuhimu wa ushirikiano katika utendaji wa kazi katika jamii. Yawezekana kabisa kuwa methali hiyo imechimbuka wakati wa ujima, wakati ambapo kazi zilifanywa kwa pamoja na kwa manufaa ya watu wote. Uchambuzi ukifanywa kwa uangalifu, utaweza kueleza migongano au migogoro inayokuwepo miongoni mwa jamii, na kwa hiyo utumiaji wa methali hizo unaweza kulengwa kwenye dhima ya kuichambua na kuitatua migogoro na migongano hiyo.
Msanii anapozitumia methali katikajamii, awe na uhakika juu ya maana ya methali hizo. Baadhi ya methali zikitumiwa bila uangalifu zitaonyesha nadharia ya utengano ambayo inaweza kupotosha maana na kuleta athari isiyokusudiwa. Baadhi ya methali hueleza matatizo katika jamii tu, hazitaji chimbuko la matatizo hayo. Kwa mfano, methali, "Mkaidi huliwa na nzi... Mkaidi mngoje siku ya ngoma... Mkaidi hafaidi mpaka siku ya Iddi," ni ile inayosema tokeo la "ukaidi," lakini hatuambiwi kwa nini huyu "mkaidi" aliamua kuwa mkaidi. Pengine mkaidi alikataa kutii kwa sababu alitaka kulinda maslahi na maisha yake. Je, ni nani asiye na haki ya kulinda uhai wake? Wasanii wanashauriwa kwa hiyo wawe waangalifu wakati wa kuzitumia methali hizo ili ziweze kuleta maana inayokusudiwa.
Kwa upande mwingine, methali zimekuwa na matazamo muflisi wa udhanifu - mtazamo kama ule usio wa kisayansi. Katika dini ya Kikristo kwa mfano, kuna amri isemayo kuwa "usiibe." Lakini haielezwi kwa nini huyu mtu anaamua "kuiba". Hivyo ndivyo ilivyo kwa baadhi ya methali, kwamba haziangalii kiini cha tatizo kilichosababisha mtu kuleta "tatizo," bali zenyewe zinaonya au kukemea tu. Athari ya jambo kama hili ni kuwa hata ikisemwa namna gani, "wizi" au "tatizo" litaendelea kuwepo, mpaka pale kiini cha shida zilizosababisha wizi au tatizo kitakapotatuliwa. Tunategemea methali kama hizo zingechambua kiini cha matatizo na pengine kuonyesha uwezekano wa kutatuliwa kwa matatizo yanayosibu. Uchambuzi na uwasilishi wa namna hii m wa manufaa kuliko kutoa vitisho visivyosaidia.
Mwelekeo na mtazamo wa mjadala wetu hapa unatupa dhana moja muhimu. Dhana hiyo ni ile inayoifanya methali ionekane kama ni sanaa tegemezi ambayo matumizi na ukweli wake hutegemea muktadha (context). Kwa msingi huo, ni vigumu kupata methali ambayo ni "kweli" tu, au ni "uongo" tu wakati wote.
Jambo la mwisho kulitaja hapa ni kuhusu dhima ya methali kama kiungo au kichocheo muhimu cha kisanaa katika hadithi fupi. Kwa hakika methali na misemo hupamba hadithi kama matumizi yake yakiwa mazuri. Tuone mfano ufuatao:
GONZA KWAHERI
Gonza, tazama sasa giza limekufika! Umelala, umekufa, unadai machozi yetu ambayo hatuna hiyari ya kuyatoa. Uliponenewa ukishikwa shikamana hukusikia, na wala hukujali! Kwako, mwanzo na mwisho uliviweka pamoja. Watu husema, ukiona kongoni ana pembe uzeeni ujue amejitunza. Gonza, umeufikia mwisho kwa hiyari isiyo hiyari, huna mwanzo wala mwisho tena, bali litakutanda giza la milele. Ulitakiwa ujue kuwa anayekuzidi nguvu hukupiga na fimbo yako mwenyewe (...). Gonza! Mkaidi huliwa na nzi! Mbuku, kwa sababu ya ujinga wake hachagui vya kumeza (...) Funo kukuza pembe zake si ufahari bali ni kuepuka mitego ya wawindaji!8
Kifungu hiki kimetumia methali kadhaa zilizoko katika msisitizo ambazo zinaibusha'bisia kali kwa wasomaji na kuwafanya waathirike kwa viwango mbalimbali wasomapo kifungu hiki. Fani hapa imeongezewa uzito wa kisanaa ambao huzalisha taharuki na hisia kadiri ya matakwa ya msanii mwenyewe.
Matumizi ya methali wakati mwmgine huambatana na misemo kama vile misimu na nahau. Misimu na misemo kimsingi haihesabiwi kuwa m fasaha wala ya kufaa. Nahau kwa mfano hutumia maneno ya kawaida, lakini, yamesetiri maana iliyo tofauti na ni nzito katika maana. Angalia mifano ifuatayo kwa ufafanuzi zaidi:
a - Chichi ana mkono wa birika
b - Asha ana ulimi wa nge
c - Diana amevaa miwani
d - Leonila ana mate ya fisi
e - Zeituni ametutoka angali mbichi
Hivyo ndivyo ilivyo misemo ya kinahau. Katika misemo ya kawaida nahau hizi zingeweza kutamkwa kama ifuatavyo:
a - Chichi ni mchoyo/mnyimi
b - Asha ana maaeno makali sana
c - Diana amelewa (pombe)
d - Leonila anapenda nyama sana
e - Zeituni amekufa bado akiwa na umri mdogo sana
Tamathali za Usemi
Baada ya kuangalia matumizi ya methali na nahau ama misemo katika hadithi fupi, sasa tuangalie kipengele kingine cha semi na tamathali katika kuunda fani ya hadithi fupi. Umuhimu wa kipengele hiki ni kusaidia katika kutofautisha kazi ya sanaa itumiayo lugha na ile isiyo ya kisanaa kama vile hotuba n.k. Semi na tamathali zinaweza kugawanywa kama vile alivyofanya Casmir Kuhenga9 Aidha, tunatahadharisha kuwa tamathali za usemi ziko nyingi, na hapa tunazijadili baadhi yake tu.
Tamathali za Mafumbo
Fungu hili lina tamathali kama vile dhihaka, kyembe, tasifida na nyinginezo kama tutakavyoziona hapo baadaye. Kama tulivyokwis'ha kudokeza, tamathali hizo zinatumika kwa madhumuni maalumu. Tuiangalie kila tamathali peke, yake.
Dhihaka
Aina hii ya tamathali ni ya dharau na ina lengo la kumweka mtu katika hali duni kupita kiasi, lakini kwa mbinu za kifumbo. Mara nyingine mtu anayed-harauliwa hujifahamu, lakmi mara nyingi huwa hajifahamu. Wanaomsema kwa kawaida hujua bezo zote juu ya mtu huyo.
Mwandishi wa hadithi fupi anaweza kutumia tamathali za aina hii ili kuonyesha ubingwa wake katika sanaa anayoisanii. Matumizi bora ya sanaa yanategemea sana uwezo na ujuzi alionao msanii. Misemo kama hii huijenga hadithi inayohusika kimaudhui na kifani. Angalia mfano ufuatao kwa ufafanuzi:
Adella alikuwa msichana msafi mno. Ndiyo maana kila mara alipata kupaka mafuta yaliyonulda na kukaribisha nzi walioleta matatizo makubwa.10
Katika mfano tuliouona hapa juu, Adella anasemwa kuwa ni msafi sana kwa kuwa anapaka mafuta yanayokaribisha nzi kwa matatizo. Kusema kweli hii ni dhihaka, kwani hali ilivyo nzi hufuata uchafu mara nyingi. Au angalia mfano mwingine hapa chini:
Bwana Bwanyenye, wewe ni miongoni mwa matajiri nchini Tanzania. Ama labda nikuite kabaila. Nanyi makabaila wa siku hizi mu wakarimu sana. Juzi umetoa shilingi moja kama dawa ildwa ni mchango wako kusaidia ujenzi wa makao makuu ya TANU.11
Katika kifungu tulichokiona hapa juu, Bwanyenye anasifiwa kuwa m "mkarimu," na amepata kutoa shilingi moja katika mchango wake wa kusaidia ujenzi wa jengo la TANU. Shilingi moja kutoka kwa Bwanyenye ni kichekesho na dhihaka tupu!
Tasifido
Tamathali bu iko katika kundi la "adabu," ama "ficho." Yako baadhi ya maneno fulani katika maandishi yanakiuka misingi ya utamaduni wa jamii. Maneno hayo hujulikana kama Lugha safihi. Maneno hayo hayapendezi kusikika hadharani, hasa ikiwa hadhara hiyo ni ya makundi ya watu mbalimbali. Ashakum, tuangalie mifano kadhaa ili kupata ufafanuzi zaidi wa suala zima la tamathali hiyo. Katika mfano huo, mwanafunzi anataka kwenda haja. Anamwendea mwalimu wake anayemfundisha kwa muda huo na kumwambia akiomba aruhusiwe kwenda nje kwa shughuli hiyo. Anasema:
a - Mwalimu naomba kwenda haja
b - Mwalimu naomba kwenda kujituma
c - Mwalimu naomba kwenda kunya
d - Mwalimu naomba kwenda kukojoa
Katika mifano minne iliyotolewa kuna aina ama namna mbili ya kusema jambo lililomsibu mwanafunzi huyo aliyeko darasani kwa sasa. Mifano a na b imekuwa ya "adabu" au "ficho" kuhusu shughuli anayotaka kufanya mwanafunzi huyo nje ya darasa. Lakini mifano c na d haina "adabu" na kusema kweli haipendezi kusikika masikioni. Tasifida ni tamathali inayosema kitu, tamathali inayoambaa kitu ili kupunguza ukali wake kama ilivyofanywa hapa juu. Mifano zaidi imetolewa hapa chini.
a
|
-
|
Mariamu ni mwizi
|
a1
|
-
|
Mariamu ana mkono mrefu
|
b
|
-
|
John amekufa
|
b1
|
-
|
John ameaga dunia
|
b2
|
-
|
John ametutupa mkono
|
b3
|
-
|
John amefariki dunia
|
b4
|
-
|
John amerudisha namba kwa Mungu
|
b5
|
-
|
John ametutoka
|
b6
|
-
|
John si mwenzetu tena
|
b7
|
-
|
John ametutangulia
|
b8
|
-
|
John ameitikia mwito wa Bwana Mola wetu
|
b9
|
-
|
John amefumba macho
|
b10
|
-
|
John amesafiri njia ya wote
|
c
|
-
|
Hamida amezaa mtoto wa kiume
|
c1
|
-
|
Hamida amejifungua mtoto wa kiume
|
c2
|
-
|
Hamida ameshusha tumbo lake
|
Katika mifano iliyotolewa hapa juu, misemo a,b, na c ni mikali. Lakini misemo a1, b1 - b10, na c1 - c2 ni misemo ambayo ina adabu.
Matumizi mazuri ya semi kama hizo yanaweza kuiweka hadithi kuwa bora zaidi. Hata hivyo baadhi ya wataalamu wanaona hali ya kutumia tasifida kuwa ni upungufu fulani katika kazi ya sanaa. Mmoja kati ya wanataaluma hao ni C.H. Holman12 ambaye anasisitiza kuwa wasanii wawe na mtazamo wa kuyatamka mambo kihalisia kama vile yalivyo bila ya kujali yanaumiza ama kufurahisha. Inadaiwa kwa ujumla kuwa mtazamo wa fasihi ni kuelekea kwenye uhalisia, na kwamba mambo yanatakiwa yasemwe bila ficho - yasemwe waziwazi.
Shitizai (Kinaya au Kejeli)
Tamathali hii imekusudiwa kuleta maana iliyo kinyume na ile iliyokusudiwa ama kinyume na ukweli ulivyo. Lengo hasa la shitizai ni kujaribu kuzuia matatizo na migongano pindi itumikapo kwa lengo maalumu la kufundisha na kuasa. Tazama mifano ifuatayo kwa ufafanuzi wa kauli hii:
a
|
-
|
Mtu ni mchafu, lakini anaambiwa
|
a1
|
-
|
Sijamwona mtu msafi kama wewe
|
b
|
-
|
Mtu ni bepari, lakini anaambiwa
|
b1
|
-
|
Wewe ni mjamaa ambaye hajapata kuonekana
|
c
|
-
|
Mtu ni adui. lakini anaambiwa
|
c1
|
-
|
Wewe ni rafiki mpenzi, (cf Raisi Nyerere alimwita Fashisti Idd Amin Dada rafiki yake wakati anatangaza vita mwaka 1978).
|
Katika mfano wa kwanza mtu "mchafu" anayesifiwa anaridhika, haleti matata. Ni hivyo pia katika mifano mingine ya b na c. Wakati mwingine, kejeli pia ina maana ya kuchekelea mtu, kumdharau na kumchusha kwa mzaha. Ni usemi ambao maana yake ya ndani ni kinyume chake, na inabeua maana yake halisi. Ni kebehi, ambamo kisemwacho sicho kikusudiwacho.
Innuendo (Kijembe)
Huu ni usemi wa mzunguko, ni usemi wa kifumbo na humsema mtu kwa ubaya. Katika kusemwa kwa mhusika fulani, msemaji mmoja hudokeza kidogo tu hali ya ubaya juu ya mwmgine. Kunakuwa na hali ya tafakari baina ya wahusika, na halafu hufanya hukumu juu ya mambo muhimu katika hadithi. Maamuzi mara nyingi yanakuwa katika hali ya ubaya.
Tamathali za Mlinganisho
Katika kundi la tamathali tulilolijadili hapa juu tumeona kuwa kundi hilo linatumia mafumbo katika tabia mbalimbali. Kundi tunalolijadili hapa linahusu tamathali za ulinganisho. Kama lilivyo kundi jingine tuliloliona, kundi hili ni muhimu katika ujenzi wa fani ya hadithi fupi za Kiswahili. Tamathali kama vile sitiari, tashibiha, tashihisi, na nyinginezo zinajumuishwa katika kundi hili. Tuangalie baadhi ya mifano ya tamathali hizo hapa chini:
Sitiari
Hii m tamathali ya usemi ambayo kwa kawaida inahusisha matendo, kitu au tabia ya vitu vyenye maumbile tofauti. Ulinganisho huu unazingatia misingi au sifa inayopatikana au zinazopatikana katika vitu vyote viwili, lakini sifa hizo haziwi wazi kati ya kitu na kitu. Angalia mifano ifuatayo:
a - Maisha ni moshi
b - Mtu kinyonga
c - Ana mwendo wa kobe
d - Mchuzi wa kukata na shoka
e - Mwogafisi John
f- John alikuwa mbogo
g - Wakati wa vita alikuwa simba
h - Mwatumu ana jicho la kinyonga
i - Ulimi wako Maria Magge ni ua la waridi
j - Petro ni mwamba, juu yako nitajenga imani yangu
k - Lydia amekuwa sungura
l - Salma ni mbwa kabisa
Katika mifano hiyo, mfano (a) kwa mfano umefananishwa maisha na moshi. Moshi ni kitu kinachodumu kwa muda mfupi sana toka pale unapojitokeza. Kwa hiyo, "mtu" ambaye amefichwa katika neno "maisha" anaishi kwa muda mfupi sana kama vile maisha ya moshi yalivyo. Mfano wa (b) unamlinganisha "mtu" na "kinyonga." Kinyonga ni mnyama aliye na tabia ya kubadili rangi kila awapo katika mazingirs. mapya. Kutokana na dhana hii, mtu anafikiriwa kuwa kinyonga kw» sababu hatabiriki, wakati wowote anaweza kubadilika na kwenye mazingira yoyote yale. Katika mfano wa (c) kobe anatembea polepole. Mtu mwenda pole hulinganishwa na kobe, ndipo tunapopata methali ya "Taratibu ya kobe humfikisha mbali." Kwa kufuata utaratibu huo, sitiari nyingine zote zilizolinganishwa hapa juu zinaweza kufafanuliwa vile. Ni muhimu kusisitiza bapa kuwa sitiari ni tamathali ya usemi ilinganishayo vitu bila kutumia viunganishi kama vile: mithili ya, mfano wa, sawa na, kama kwamba, na kadhalika.
Tashibiha au Mshabaha
Tamathali ya aina hii hutumia mhnganisho wa mambo ama vit.u kwa kutumia viunganishi: "kama," "mfano wa," "mithili ya," "sawa na," "mfano wa," n.k. M.M. Mulokozi na K.K. Kahigi,13 wakijadili tashibiha katika ushairi wanasema kuwa katika tashibiha, kama ilivyo katika sitiari, kuna vitu vitatu vinavyofananishwa ambavyo wataalamu wameviita kizungumzwa, kifananishi na kiungo. Kizungumzwa ni kitu halisi ambacho huzungumzwa na kitu kinachofananishwa kwa fumbo. Kifananishi kipo katika mawazo na huzingatia maana dhahnia. Kiungo m sifa zipatikanazo katika kitu kinachozungumziwa na hivyo kuhusisha vitu vyote viwili. Maelezo kama hayo pia yanaelezwa na wataalamu wengine kama vile Walter Blair14 na wenzake. Kwa kutumia tashibiha, msanii wa hadithi fupi anaweza kuifanya sanaa yake kuwa bora na nzuri. Mifano ifuatayo inaonyesha tamathali za kitashibiha.
a - Alikuwa mweusi kama mpingo
b - Ana sauti tamu sawa na ya chiriku
c - Kiuno chake ktnatetemeka kama cha mbuni
d - Mwantumu, akiwa amechukia mithili ya mbogo, alinitupia shoka
e - Alianza kukoroma kwa kunguruma mfano wa radi
Katika mfano (a) mtu anasemekana yuko mweusi. Ufafanuzi zaidi wa weusi huo unaelezwa uko kama mpingo. Mpingo ni mti mweusi sana na unapatikana katika sehemu kadha wa kadha za Afrika. Kutokana ua sifa hii ya weusi sana, ndipo inaposemekana kuwa mtu ni mweusi kama mpingo. Kwa maelezo ya kawaida tungeaema hivi:
a - Alikuwa mweusi sana
b - Ana sauti nzuri sana
c - Alichukia (Mwantumu) sana
e - Alinguruma sana
Ukilinganisha semi zile za awali na hizi za pili, hali ya kisanaa imejitokeza sana katika semi za awali kuliko hizi za pili.
Tashihisi au Uhaishaji
Tamathali hii ni ile ya kunafsisha vitu, yaani kufanya vitu viwe na maumbile na kusema au kutenda kama mtu. Katika tamathali ya aina hii vitu kama mimea, maji, moto vinapewa uwezo wa kimtu. Angalia mifano ifuatayo:
a - Chtriku mpenzi usilie! Nibusu mashavu yote ili nafsi yako itakatike.b - Ua, langu, sema kauli ya mwisho ili nami nitulie.c - Ningekuwa na uwezo, ningekuamuru nyota ua waridi langu ufunue ktdari changu ili ujionee mwenyewe jinsi ulivyofotolewa na papi za moyo wangu mchanga!d - Kimya kiliukumbatia moyo wa Maria Florence, msichana msomi wa Jangwani, Dar es Salaam, uliokuwa ukivuja machozi mazito ya damu kwa mapenzi.e - Kiburi husafiri juu ya mgongo wa ngamia kwa furaha na shangwe, lakini hurudi kwa 'aibu kikitembea kichwa chini na kuomba mahali pa kujisetiri.f - Mauti u kttu gani wewe? Kwa nini huwezi kuamua, unakuwa hujali nani au nani. kila mtu unamchukua tu? Hata mtoto unamchukua tu? U kitu gani wewe usiyejali umri7
Maneno yaliyo kwenye italiki hapa juu yamepewa uwezo wa kutenda ua kusimama badala ya binadamu.
Mifano mingi ya aina hii inajitokeza katika hadithi za masimulizi za mapokeo. Angalia kifungu cha hadithi ifuatayo:
Hapo zamani palikuwa na Chura na Nyigu. Chura alimwuliza Nyigu. Kwa nini una kiuno chembamba vile? Nyigu akajibu. Ni kwa vile miye sili, chakula chote wakimaliza weye! Ndiyo maana mimi ni mwembamba vile.
Katika mfano uliotolewa hapo juu, Chura na Nyigu ni kiwakilisho cha binadamu wenye uwezo wa kufanya mazungumzo kama hayo yaliyoonyeshwa.
Lakabu
Aina hii ya semi huelezea kitu kwa ubadilisho wa sifa. Uhusiano wa maneno mawili kisarufi hugeuzwa na pengine huwekwa kinyume na taratibu za kisarufi zilivyo. Angalia hapa chini.
a
|
-
|
Baridi kali ilimkaribisha
(Lakini mtu ndiye mwenye uwezo wa kukaribisha) |
b
|
-
|
Giza nene lilimmeza
(Lakini mtu ndiye anayemeza) |
c
|
-
|
Alididimia katika mawimbi ya furaha
(Lakini kudidimia mahali ni kupotea, si furaha kama ulivyosemwa hapa) |
Tamathali za Msisitizo na Nyinginezo
Kundi la tamathali za aina hii husisitiza mambo mbalimbali katika hadithi na hata kazi nyingine za sanaa. Katika kundi hili tuna mubaalagha, metonumia, majazi, na nyingine kama tutakavyoziona hapa chini.
Mubaalagha
Hii m tamathali ya chuku. Tamathali hizo hutia chumvi katika maelezo yanayofanywa katika kazi ya sanaa hususan hadithi fupi. Lengo la matumizi ya tamathali za aina hii ni kufurahisha, kuchochea, kuchekesha au kusisitiza hoja. Hoja mara nyingine zinaweza kujitokeza zile za kuibua hisia za kuchoma moyo, kuchochea furaha, huzuni n.k. Angalia kwa mfano semi zifuatazo:
a - Uso wake ulikuwa ua mito ya machozi ya uchungu baada ya mume wake kushikwa na askari wa usalama wa taifa.b - Mwangalie alivyo na mlima wa matiti! Amebeba mzigo wa matiti!c - Watu walijaa chumbani hadi chumba kikatapika.d - Ana ana tani za mapesa.
Mifano hii inaonyesha dhana ya chuku tuliyokwisha kuitaja hapa juu. Katika mfano (a) imeelezwa kuwa "mtu" alilia hadi kuunda mito ya machozi. Sote tunafahamu mto ulivyo na maji mengi. Na mto kuwa usoni mwa binadamu ni jambo lisilo la kawaida, na kusema kweli hili haliwezi kutokea. Hii ni chuku, ni usemi uliotiwa chumvi nyingi mno. Mfano (b) tunaambiwa "mtu" ana "mlima" wa matiti. Amebeba "mzigo" wa matiti. Kwa mara nyingine tena, sote tunaufahamu mlima ulivyo na jinsi binadamu asivyoweza kuubeba kifuani pake! Au mzigo ukiwa ni mkubwa sana, ni vigumu pia kuubeba. Kuhusu chumba kujaa hadi kutapika hii nayo ni chuku pia. Anayetapika ni mtu aliyeshiba sana. Ikiwa hii imesemwa kwa dhana ya kuwa kulikuwa ua watu wengi katika chumba kinachohusika, basi hii imetiwa chumvi nyingi mno!
Aidha, semi hizo zote zikichunguzwa hapa, zinaleta dhana ya kufanya kitu na kuvuka mpaka wa kawaida. Hii ni kufanya kitu kupita kiasi.
Metonumia (au Taashira)
Neno la Kiingereza la metonymy ni la asili ya Kigiriki lenye maneno mawili: meta na onyma yenye maana ya badiliko lajina la kitu. Katika Kiswahili, bado neno hili linadumisha asili yake ya Kigiriki na kubaki linaitwa "metonumia," kwa dhana ileile. Kwa kuzingatia hilo, tunaweza kusema kuwa metonumia ni tamathali itumiayo maneno kuwakilisha dhana, kitu n.k. Tamathali hii hutumia hasa ishara (ndiyo maana huitwa pengine taashira) kama alama ya kuwakilisha tukio fulani. Kwa mfano:
a - Kutabasamu huwakilisha furaha
b - Kitambi huwakilisha utajiri
c - Kukonda huwakilisha umaskini
d - Taji huwakilisha ufalme
e - Jembe huwakilisha ukulima
f - Mvi huwakilisha uzee
Majazi
Msemo huu huashiria maana ya kitu kizima mara ikitamkwa sehemu tu ya kitu hicho. Majazi na metonumia kimsingi ni tamathali zinazofanana, tofauti iko katika msisitizo tu. Ni aina ya sitiari, ambapo pia kitu kizima kikitajwa huwakilisha dhana ya sehemu ya kitu hicho. Angalia mifano ifuatayo:
a - Mbuzi: Mnyama/chombo
b - Paa: Mnyama/sehemu ya nyumba/tendo
c - Roho: Mtu
Tunaweza kufafanua tamathali hiyo kwa kutoa mifano ya sentensi mbal-imbali hapa chini.
a - Mbuzi amekataa kukuna nazi
b - Paa aliweza kuhangaisha umma
c - Roho yake imehama leo asubuhi
Taniaba
Huu ni usemi unaoonyesha kuwa kitu fulani ni badala ya kitu kingine. F.E.M.K. Senkoro anasema kuwa taniaba ni tamathali ambayo jina la mtu binafsi hutumiwa kwa watu wenye tabia, mwenendo na kazi ya mtu anayefanan-ishwa. Halafu anatoa mifano ya tamathali hiyo kuwa ni:
a
|
-
|
Yesu: Dhana ya mkombozi
(Raisi Nyerere ni Yesu wa Tanzania) |
b
|
-
|
Voster: Dhana ya ubaguzi
(Mavoster ni wengi katika Afrika hii) |
c
|
-
|
Amini: Dhaaa ya ujambazi
(Ma-Amini wanapatikana sehemu nyingi hapa Afrika)15 |
Msisitizo Bayani
Hii ni tamathali inayoonyesha ushindani wa mawazo. Ni tamathali inayosisitiza maana ya sentensi kwa kutumia kinyume. Kwa mfano tazama tungo zifuatazo:
a - Mwanadamu hupanga, Mungu hupaagua
b - Waitwa ni wengi, lakini wateule ni wachache
c - Tabia yake si mbaya, ni nzuri
d - Zeituni si mweusi, ni mweupe
Ritifaa
Hii ni tamathali ya usemi ambayo kwayo mtu huzungumza na kitu au mtu asiyekuwepo ambaye husikiliza katika fikra tu. Angalia mifano ifuatayo:
a
|
-
|
Ewe mwanangu Atuyane Tugalile! Lala vyema humo tumboni mwa mama yako Diana. Napenda akuzae siku zako zikifika. ili uje tnishi sote katika mtaa huu wa Takadiri hapa Magomeni!
|
b
|
-
|
Ewe marehemu babu yangu unayelala mbele yangu kwa uchungu nakuhurumia. Sit.wamba sioni uchungu kwa hilo lililonisibu, na natambua hungesita kusimama na kunituliza kama ungekuwa na uwezo huo. Lakini babu... tangulia... labda tutaonana wakati wangu ukifika. Msalimu marehemu mke wako, bibi yangu Bibiana.
|
c
|
-
|
Baba yetu marehemu Amani, Salaam sana. Habari za siku nyingi toka ututoke ghafla hapo mwezi Mei. Sisi uliotuacha nyama hatujambo. Vipi waliotangulia kabla yako? Je, mtoto wako Ignacio ulimkuta ana wajukuu? Na jee mdogo wake Ja-mir aliyekufa mwaka 1984 naye wameungana na mume wake baada ya kuachana katika kufa kwa mwaka mmoja na nusu? Siku hizi hawagombani tena? Je, yule mdogo wetu Joel naye ulimkuta anakaribia kuoa? Au ameoa? Ana wajukuu wake huko akera? Je, kawa majirani zetu waliokufa. kabla yako nao hawajambo?
Tana hamu ya kukueleza machache ya. huku duniani. Kwanza kabisa, mtoto wako wa kiume yule mwalimu anayefundisha. pale Chuo cha Ualimu Songea ameendelea kudhibiti mali safi ua mama. Yule mtoto wako anayefundisha Chuo Kikuu, ambaye ulimwacha amechumbia sehemu za Mbangamao uchumba umevunjika. Hii ni kazi ya majirani zetu, hasa huyu mjukuu wa Ndenda, anayefanya kazi pale Songea. Madai yao hasa m kuwa mtoto wako Shitete wanadai ni mhuni, eti aaa wasichana wengi ua anatunga vitabu vya kihuni na ha-dithi sa kihuni. Jambo hili Ulimwudhi sana Shitete, alikuwa amepanga kufanya mauaji makubwa. Kwanza angemng’oa yule wa Lindi ua kumalizia na huyu. Lakini ushauri wa mama umesaidia na kumrudisha nyuma. Shitete kwa sasa ameoa huko sehemu za Mpapa... Huwezi kuamini, LAKINI mtoto wako Shitete sasa ana maisha mazuri. Watoto wako wengine wote ua wajukuu zako hawajambo.
Mwisho, tunakuomba uendelee kutukumbuka kwa kuja katika njia za ndoto. Sisi kama kawaida, tutakutambikia pale ktiegeoni kila baada ya miezi sita. Tafadhali tusalimie marehemu babu zetu Manyuka aa Msokile. Tusalimie bibi zeta Bibiana Kuhangaika na Kilwambo Kitunda. Tusalimie ndugu zetu wote«walioko huko. Tutakutana sisi tutakapobadilisha maisha yet«kwa kifo. Tunakutakia heri!
Familia yako
Kijijini Mtakanini
|
Mifano hii yote inajaribu kufafanua mjadala wetu kuhusu tamathali hiyo ya kiritifaa iliyotajwa hapajuu. Pengine tungeona tena mfano mmojajuu ya suala hilohilo. Mfano huu ni wa shairi la Shaaban Robert liitwalo AMINA aliloliandika kumlilia mke wake baada ya kufariki dunia.
AMINA
Amina umejitenga., kufa umetangulia
Kama ua umefunga, baada ya kuchanua
Nakuombea mwanga, Peponi kukubalika
Mapenzi tuliyofunga hapana wa kufungua
Kama ua umefunga, baada ya kuchanua
Nakuombea mwanga, Peponi kukubalika
Mapenzi tuliyofunga hapana wa kufungua
Nilitaka unyanyuke, kwa kukuombea dua
Sikupenda ushindike, maradhi kukuchukua
Ila kwa rehema yake, Mungu amekuchagua
Mapenzi tuliyofunga kapana wa kufungua
Sikupenda ushindike, maradhi kukuchukua
Ila kwa rehema yake, Mungu amekuchagua
Mapenzi tuliyofunga kapana wa kufungua
Majonzi hayaneneki, kila nikikumbukia
Nawaza kile ua hiki, naona kama ruia
Mauti siyasadild, kuwa mwisho wa dunia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Nawaza kile ua hiki, naona kama ruia
Mauti siyasadild, kuwa mwisho wa dunia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Nasadiki haziozi, roho hazitapotea
Twafuata uokozi, kwa mauti kutujia
Nawe wangu mpenzi, Peponi utaingia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Twafuata uokozi, kwa mauti kutujia
Nawe wangu mpenzi, Peponi utaingia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Jambo moja nakumbuka, sahihi ninalijua
Kuwa sasa umefika, ta'bu isokusumbua
Kwayo nimefurahika, nyuma nilikobakia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Kuwa sasa umefika, ta'bu isokusumbua
Kwayo nimefurahika, nyuma nilikobakia
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Ninamaliza kutunga, kwa kukuombea dua
Vumbi tena likiunga, roho likirudishiwa
Mauti yakijitenga, mapenzi yatarejea
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Vumbi tena likiunga, roho likirudishiwa
Mauti yakijitenga, mapenzi yatarejea
Mapenzi tuliyofunga, hapana wa kufungua
Usomapo shairi hili mtu unaweza kuona picha ambayo inajitokeza mbele ya Shaaban Robert ya marehemu mke wake Amina. Maneno hayo ya kishairi yanasemwa kana kwamba Shaaban Robert mwenyewe angetaka Amina amjibu na kumsemesha. La! Imeshindikana... Shairi hili liko kwenye tamathali ya kiritifaa.
Tabaini
Huu ni usemi unaosisitiza jambo kwa kutumia maneno ya ukinzani. Angalia mifano ifuatayo:
a - Amekuwa mrefu si mrefu, mfupi si mfupi, ni wa kadiri.
b - Hali yake ni ya ugeugeu, nzuri si nzuri, mbaya si mbaya.
c - Binadamu kinyonga, atakusemesha mazuri, kumbe rohoni. kweusi!
d - Usimwamini mtu. Yu acheka machoni, rohoni ana mabaya juu yako.
e - Ngamia afe, mzigo wa bwana ufike.
f - Sura inacheka, moyo unalia.
g - Yanga si timu mbaya, wala Simba si timu mbaya.
h - Hatukuwa tusio na furaha kwa kuondoka jioni hiyo.
Mbinu Nyingine za Kisanaa
Kimsingi, tamathali za usemi huambatana na matumizi ya mbimu nyingine za kisanaa ambazo hutunuwa na wasanii. Mbinu hizo kwa baadhi wameziweka katika kundi la tamathali za usemi. Hapa tumeziweka katika kundi hili kwa msingi kwamba mambo yanayojitokeza siyo ya ulinganisho katika zote, bali husisitiza ua kupamba kazi ya sanaa. Katika kundi hili kuna takriri, tashtiti, mjalizo, mdokezo, na kadhalika.
Takriri
Takriri ni urudiaji wa maneno, silabi au sauti zinazolingana katika kazi ya sanaa. Mwandishi huamua kwa makusudi kurudiarudia maneno au vipengele hivyo kwa lengo maalumu la kulisisitizajambo ama kulitia mkazo jambo linaloelezwa. Angalia hapa chini kwa ufafanuzi zaidi.
Maria Magge aliamua tena kumfuata Manda. Alikwenda, hakufika. Jua lilizidi kunyonya maji ardhini. Jua lilinyonya, likanyonya ua mvutano ukazidi. Hakukata tamaa. Alikwenda mbele hakufanikiwa. Hakukata tamaa, alikwenda mbele tena ajaribu bahati yake. Mwisho alifika ukingo wa tumaini lake. Hakufantkiwa! Alimwomba Mungu mchana na usiku, hakufanikiwa. Imani juu ya Mungu ikapungua. 'Mwisho alitoa sauti ya kukata tamaa iliyojaa masikitiko akisema: "Mwalimu wangu mpenzi, usiponioa nitakufa ... Nitakufa ningali mbichi usiponioa mwalimu wangu! 16
Maneno yote ya msisitizo yameandikwa kwa italiki. Tunaweza kufafanua zaidi kwa mifano mingine kama inavyoonyeshwa hapa chini:
a - Haba na haba hujaza ki baba
b - Baraka haraka haina baraka
c - Padogo pako si pakubwa pa mwenzio
Katika methali hizi tatu tunaona takriri katika maneno na herufi zilizo kwenye italiki. Ukichunguza zaidi, utaona kuwa methali hizo zina takriri za aina nyingi.
Ukariri wa sauti au silabi pia unaweza kuonekana katika mfano ufuatao wa shairi la Abdilatif Abdalla:
Kuno kunena kwa nini
Kukanilomeya kuno
Kwani kunena kunani
Kukashikwa kani vino
Kani isiyo na kiini
Na kuninuya mno
Kanama nako kunena
Kwaonekana ni kuwi17
Katika andiko hili takriri inajidhihirisha kwenye silabi - ku -, herufi - k -, - n -, - m -, n.k.
Mtindo huu wa msisitizo una lengo la kufanya jambo limwingie msomaji vyema. Aidha, takriri pia inatumiwa kupambanua dhamira zilizoko katika hadithi. Wakati huohuo pia takriri inapamba hadithi kisanaa na kusaidia kuweka kumbukumbu ya baadhi ya mambo muhimu. Takriri pia hutumika kwa nia ya kutaka kukazia jambo fulani, ikiwa jambo hilo litatajwa mara nyingi na kurudiwarudiwa kirefu, ama kutajwa peke yake.
Mdokezo
Wakati mwingine hutokea kuwa mwandishi anamjenga mhusika wake akisema mawazo yake kwa njia ya mdokezo. Kuna mifano mingi katika kitabu hiki, hasa katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. Mifano michache imetolewa hapa chini:
Ah! Naye asijaribu kukuvika kilemba cha ukoka! Kwani... Mwanaume hanalo moja likuaminishe! Na ukimpa ndiyo yako;nakuambia, ah! ... na tukae tu... Tusubiri ukweli wa historia usiopingika...18
Tashtiti
Huu ni mkazo wa maneno yasemwayo ama kuaadikwa. Katika mbinu hii, mwandishi hutumia mbinu za kuuliza maswali kwa jambo ambalo anafahamu jibu lake. Msanii hufanya hivyo kwa lengo la kusisitiza jambo, kuleta mshangao, n.k. Angalia mifano michache inayofuata:
a
|
-
|
Msickana Diana amefariki. Jambo hili linamshtusha msichana Luiza, kwa hiyo anataka kujua zaidi kitu anachokijua. tayari. Anasema kwa mshangao mkubwa ua kujiuliza:
Diana na uzuri wake amekufa? Looh! Sadakta! Ametu-toka? Hatakuwa nasi tena! Masikini... |
b
|
-
|
Jambazi limekatwa mguu hapa kijijini wakati lilipokuwa likiiba mali ya kijiji. Baadhi wamepata habari na wala hawaamini kuwa tukio hili ai la kweli. Kwa hiyo wanasisitiza kwa kuuliza maswali mbalimbali.
Jitu limekatwa mayu? Masalale! Shaash...! Bughudha sasa imekwisha? Hatuonewi tena na jitu? Na tuone...
|
Ukiangalia maswali yale yanayoulizwa katika mifano iliyotolewa hapo juu, majibu yake ni wazi na yanafahamika vyema kabisa kwa yule anayeuliza maswali hayo. Kitu ambacho anachokitaka hapo ni msisitizo tu utakaotokana na kujibiwa kwa maswali hayo. Mifano mingine ni kama hii inayofuata:
a
|
-
|
Saumu malaika Aziz muhibu wa moyo wangu! Looh! Nikupe nini uniamini kuwa kwato niko radhi kujitosa ba harini nikikukosa? Sadakta!
|
b
|
-
|
Astaghafirulahi! Mwanaharamu maluuni huyu jizi asiyejua kupenda! Limekwenda na kila kitu changu? Ole! Litanikoma.
|
Nidaa
Huu ni msemo ambao unaonyesha kushaogazwa kwa jambo fulani. Misemo ya aina hii huambatana na matumizi ya alama za mshangao, kukubali jambo, kuchukia ama kuonyesha heshima maalumu. Angalia misemo inayofuata:
a
|
-
|
Ah, maskini moyo wake, mbona nakupenda vile?
|
b
|
-
|
Zeituni mpenzi wangu! Ningekuwa. na uwezo ningekuandalia harusi ya ndovu kumla mwanawe!
|
c
|
-
|
La! Hasha! Puka chaka! d - Lahaulaa! Alaaa! Ama!
|
Mjalizo
Wakati mwingine mwandishi huaadika sentensi zake bila kutumia viunganishi kama vile: "ya", "na" "wa" '"kwa" n.k. Hii ni mbinu mojawapo ya kisanaa ambayo wasanii hupenda kuitmnia katika kuongeza uzuri wa kisanaa katika kazi zao. Tazama mifano ifuatayo:
a - Niliimba, nikanuna, nikachoka,
b - Nilivuna, nikatuta, nikashindwa
c - Mwenye kusamehe, asiye ua kinyongo
d - Fundi wa kuogelea, moyo usio woga, mwenye kupenda kusaidia, tayari, kujitoa mhanga
Wigo
Mbinu za aina hii huiga sauti ama milio mbalimbali katika kazi za sanaa. Mwandishi huwa na juhudi ya kujaribu kuiga kitu kama kinavyojitokeza katika mazingira ya kawaida. Katika fungu hili tuna mbinu za matumizi kama vile onomatopeia, mwigo-lafudhi, n.k.
Onomotopeia av Tanakali-sauti
Katika aina hii ya wigo mwandishi hujitahidi kuiga sauti za milio mbalimbali. Milio hii m ya wanyama, magari, simu, n.k. Tazama mifano hapa chini:
a - Alitumbukia bwawani, "Chubwi"
b - Alidondoka chini "pu!"
c - Chura alilia, "Korodoodoo! Mungu mkubwa!"
Maneno chubwi!, pu! korodoodoo! m onomatopeia. Mifano ya namna hii pia tunaweza kuipata katika methali za Kiswahili.
a - Chururu si ndo! ndo! ndo!
Hivyo ndivyo yanavyoigwa maji yadondokavyo katika ndoo. Na mchanja kuni naye anapobanda vibanzi kwa shoka hujipa tumaini kuwa:
b - Bandu! bandu! huisha gogo!
Hii ni baadhi tu ya mifano ya tamathali hizo zinazoiga sauti. Bado kunaweza kuwa na mifano mingi mingineyo kama tutataka kuisema na kuitambua ili itumike katika kazi zetu za sanaa.
Onomatopeia au tanakali sauti ina kazi kadhaa. Pamoja na kazi nyinginezo, kwanza ni kukaziajambo linalosemwa limetendeka. Kazi nyingine ya onomatopeia m kukomaza kitendo kinachoelezwa. Mwisho, huvutia usikivu katika taaluma za hotuba.
Tanakali- lafudhi
Hutokea pia kuwa mwandishi katika kusanii kazi yake huiga sauti ya lafudhi ya lugha fulani fulani katika taifa ama mataifa. Angalia mfano huu ufuatao:
"Watataka kwenda kunizika mtu wao. Watakuwa tayari kulipia gharama zote."'Tukupe ngapi?" atauliza mmoja kumwuliza yule mlinzi wa maiti wa kabila la Kimakonde. Naye atajibu:"Kupungua kabati tu, nataka njulupu mia unusu yake!Uchilete nchezo njomba. Tapachali kweli wewe tapachali."19
Maneno ya lafudhi ya Kimakonde yameandikwa kwa italiki ili kuonyesha tanakali lafudhi tunayoisema.
Usambamba
Huu ni mtindo wa maelezo ambapo kauli zenye kufanana kimaana au kisarufi huwekwa pamoja - huwekwa sambamba. "Kukinzana" katika usambamba hutokea mara chache sana. Angalia mifano ifuatayo:
a - Kikubwa kikipinduka na kifupi huwa kirefu
b - Mwanadamu hupanga, Mungu hupangua
c - Wengine wakicheka, yeye ananuna
Ukiangalia mifano yote hii, utaona kuwa inafanana na tamathali zile zina-zozingatia dhana ya kinyume au msisitizo bayani, tuliyoiona hapajuu.
Tauria (Mchezo wa Manena)
Hii ni mbinu pia ya kisanaa ambayo kwayo msanii hupenda kutumia maneno ya tahajia moja. Tahajia huwa katika herufi, vina, n.k., lakini maana ya maneno hayo huwa ni tofauti. Maneno hayo aghalabu huwa yamepangwa vizuri katika sentensi moja. Tazama kwa mfano sentensi zifuatazo:
a - Kaa alikalia kaa la moto
b - Paa alipaa juu ya paa la nyumba
c - Chungu alifia kwenye chungu
d - Mbuzi alikalia mbuzi ya kukunia nazi
e - Meza alimeza dawa iliyokuwa juu ya meza
f - Alimfinya kucha usiku kucha
g - Ana ana kichwa kidogo
Matumizi ya Ucheshi
Mbinu hii imejadiliwa kirefu sana ua F.E.M.K. Senkoro katika kitabu chake kiitwacho Fasihi.20 Hatutajadili hapa kwa urefu kuhusu mbinu hii. Isipokuwa tunasema kuwa mtu mcheshi si msununu, ua msanii anapoingiza mbinu hii katika kazi ya sanaa ana malengo mengi. F.E. M.K. Senkoro anataja faida za ucheshi kama: husaidia kuondoa uchovu, huburudisha, husaidia kujenga taswira, hufuta uchovu.
Hii ni baadhi ya misemo, tamathali za usemi ua mbmu za kisanaa ambazo zikitumiwa katika kazi za sanaa na msanii ubora wake huongezeka. Sehemu hii imejadili matumizi ya tamathali mbalimbali katika kazi ya sanaa. Inasisitizwa kuwa hizi ni baadhi tu ya semi zinazoweza kutumika katika kazi za sanaa. Utafiti zaidi ukifanywa zinaweza kupatikana tamathali nyingine nyingi ambazo ni muhimu na zinaweza kutumika katika kazi za sanaa.
Ishara
Waandishi pia wanaweza kutumia mbinu hii katika kujenga taswira na picha mbalimbali katika kazi zao za kifasihi. Ishara kwa kawaida katika fasihi ni za aina mbili. Kwanza kuna zile ambazo zinahusu maana ya kitu kinachoelezwa, yaani kama kinavyojitokeza katika akili za msomaji ama msikilizaji wa kazi ya sanaa pamoja na mtazamaji. Lakini pia ishara inaweza kuwa na maana ya kitu kingine kabisa katika mazingira ya jamii. Ishara ya safari kwa mfano inaweza kuwa ua maana iliyo tofauti na safari yenyewe. Inategemea msanii anaitumia vipi ishara hiyo ya safari.
Katika fasihi kwa mfano, mhusika anaweza kujengwa akitoa ishara fulani - kama kukonyeza. Mtazamaji atapata wazo na kutenda kufuatana na kukonyeza huko. Au anaweza kutoa ishara inayoonyesha kumeza kitu. Maana yajambo hilo halitakuwa kumeza pengine, bali litakuwa na maana ya kushikwa na njaa kali.
Katika hali zote hizo, ishara bado zinatumika katika kujenga picha mbalimbali ambazo hatimaye huibua hisia kwa wasomaji wa kazi za kifasihi zinazohusika.
Mitindo ya Hadithi Fupi
Baadhi ya wataalamu na wananadharia wanaona mtindo kuwa ni mchanganyiko wa mambo makubwa mawili. Mambo hayo ni wazo (maudhui) la msanii linaloelezwa najinsi wazo hili linavyoelezwa na msanii. Nadharia hii inauangalia mtindo kama kitu chenye mchanganyiko uelezao uhusiano uliopo kati ya mfanyakazi (nisimuliaji/msanii/mwandishi) na kazi anayoifanya21 Jinsi jambo linavyosemwa husaidia kuelezea ua kufafanua maana ya kile kinachosemwa.
Mtazamo huu umepata pia kuelezwa na H.J.M. Mwansoko22 wakati anapochunguza mitindo mbalimbali ya uandishi.
Katika uandishi wa kifasihi, mtindo pia unaweza kuwa ni tabia ya uandishi katika kipindi cha mfumo fulani wa maisha ya mtu. Kwa mfano mwandishi aliyekuwa akiandika kwa Kiswahili karne ya 17 - 18 alikuwa akitumia mtindo ulio tofauti na huu wa sasa. Hii inatokana na hali, mfumo, kanuni ua taratibu za maisha zilizokuwapo kwa wakati huo na zile ambazo ziko kwa sasa ambazo zinaonyesha ukweli kuwa maisha ya jamii yanabadilika kulingana na historia. Ni wazi kuwa mambo yalivyokuwa yakielezwa kama yalivyotendeka kwa wakati huo yatakuwa tofauti na jinsi yanavyoelezwa kwa sasa.
Wakati mwingine mtindo unaangaliwa kama tabia ya mtu binafsi juu ya ufundi, umahiri na hisia za kibinafsi katika kutenda mambo yake anayokutana nayo. Kwa mfano kama kuna wachezaji wawili wa timu ya mpira, nao wana-toka katika timu moja, wanatumia mtindo mmoja wa kucheza wakiangaliwa kama watu wanaotoka katika timu moja. Lakini pia kila mchezaji kutoka katika timu hiyohiyo moja ana mtindo wake wa kucheza. Ndivyo ilivyo katika suala la uandishi. Waandishi wanatofautiana katika mitindo kwa kuzingatia utofauti wa dhamira, nafsi ya msanii na kipindi alichoandikia hadithi ama kazi yake ya sanaa. Ingawa waandishi wa Kiswahili wanatumia lugha ya Kiswahili, kila mwandishi ana mtindo wake wa kuyaelezea mambo yake.
Kwa upande wa mwandishi, mtindo unatawaliwa na mambo kadhaa. Kwanza, ni nia ama lengo lake mwandishi. Pili, ni mtazamo na msimamo wa mwandishi. Mtazamo wa mwandishi unahusu maono yake juu ya suala zima au masuala anayoyaangalia katika kazi yake. Wako waandishi wenye mtazamo wa kidhanifu (ambao msingi wake wa mtazamo ni kudhani) ambao hawakubaliani katika mabadiliko ya kisayansi. Waandishi hao wanaangalia ulimwengu kwa kuhusishwa ua nguvu za Mungu, miungu, n.k. Kutokana na jambo hilo kila mtu anachokieleza mwandishi huyo kitakuwa na udhanifu mwingi.
Mtazamo wa kisayansi ru tofauti na huu. Mtazamo huu huuangalia ulimwengu kuwa ni kitu kinachobadilika kufuatana na historia ya wakati, mahali, n.k. vikitawaliwa ua kanuni za asili zinazotawala maisha ya binadamu. Mtazamo huu ni wa kihalisia unaogusa maisha ya mtu ya kila siku.
Wakati mwingine mtindo unaweza kutokana na mazingira yake ya kielimu. Katika suala kama hili, inategemea mwandishi amepata elimu ya aina gani? Amepata elimu ya vitendo ama nadharia tu? Makusudio ya elimu hiyo ni yepi? Kiwango cha elimu pia kinaweza kuongeza ufanisi wa uandishi wa hadithi fupi. Mwandishi, kwa kutumia stadi alizojifunza katika elimu yake, anaweza kuziandika hadithi vizuri.
Kwa kuhitimisha maelezo hayo yajumla kuhusu mtindo, tunaweza kusema kuwa mitindo inahusu mambo mengi. Kama H.J. M. Mwansoko23 anavyosema kuwa, "mitindo m mifumo ya zana za kilugha inayotokana na maendeleo ya kukua kwa lugha ambayo hutofautiana kufuatana na kutumiwa kwake katika mawasiliano yahusuyo nyanja mbalimbali za kazi ua shughuli za jamii."
Kutokana na fasiri hii ni wazi kuwa kutakuwa na tofauti ya mitindo kati ya utanzu na utanzu, kati ya mtu ua mtu, dhamira ua dhamira, n.k.
Vipengele vya Mitindo
Uchaguzi wa Maneno
Suala hili limekwisha gusiwa hapo mapema kwenye vipengele tofauti tofauti. Ukweli ni kuwa matumizi ya mambo kama tamathali za usemi na misemo mingine, matumizi ya methali n.k. ni mambo yanayokwenda pamoja na jinsi mwandishi anavyochagua maneno katika uandishi wake.
Hiki m kipengele cha lugha kijumla. Unapozungumzia mtindo wa kazi ya sanaa tunazungumzia matumizi ya lugha, kile kinachosemwa kinaweza kilazimishe aina ya matumizi ya maneno. Kwa mfano, mwandishi anapoelezea jambo fulani anaweza kuamua atumie maneno yenye maana nasibishi tu. Maneno ya aina hii yana maana inayofananishwa ua maana halisi ya jambo lililotajwa. Kwa mfano maana nasibishi ya bendera ni uhuru, uzalendo n.k. Maana yake halisi m kipande cha nguo kinachotundikwa ulingoni kikapepea. Maneno yenye maana halisi yanapotumiwa yanaeleza uwazi wa kile kinachoelezwa.
Suala la uchaguzi wa maneno ni la muhimu kwa sababu kila neno linavyotumika lina athari zake mbalimbali katika kulela maana inayokusudiwa.
Kukiwa na uchaguzi mzuri wa maneno, kitu kinachofuatia ni jinsi mwandishi anavyopanga maneno yake. Pengine mwandishi hupanga maneno kwa kutumia sarufi sanifu. Lakini pia anaweza atumie mbinu ngeni kabisa; ambayo haizingatii misingi ya kisarufi. Angalia mfano hapa chini.
a - Twakiacha kiza kitumeze?
b - Kiza kitumeze twakiacha?
c - Kitumeze twakiacha kiza?
d - Hukiogopi kiza kati yetu?
e - Kiza kati yetu hukiogopi?
f - Kati yetu hukiogopi kiza?
g - Yetu kati, kiza hukiogopi?
h - Kikatapika, chumba kilijaa!
i - Chumba kilijaa kikatapika!
j - Kilijaa kikataika chumba!
Mifano hii inaonyesha mipangilio mbalimbali ya maneno katika sentensi. Iko mipangilio ambayo ni ya kawaida ua iko isiyo ya kawaida katika usemaji na uandishi wa lugha ya Kiswahili. Kila mpangilio hapa una athari zake katika kuleta maana ya hadithi.
Matumizi ya Taswira na Ishara (Jazanda)
Picha ama taswira ni kiwakilisho cha kitu kwa maneno au kitu halisi, na kiwakilisho hicho chaweza kufahamika kwa mtu mmoja au watu wengi zaidi. Kimaandishi, kiwakilisho hicho kinapambanuliwa kwa matumizi mazuri ya lugha. Picha za kisanaa zinajitokeza kwa misingi kuwa vitu vinavyowakil-ishwa kipicha vinafahamika. Kwa msingi huo picha ni kitambulisho maalumu cha lugha ya kisanaa. Athari za lugha humfikia msomaji kwa njia ya kusikia, kuona, kunusa ama kugusa. Kutokana na picha, msomaji anaweza kuathirika kwa furaha, kusisimka, kuogopa, kuvutika, kuchukia n.k.
Kwa kutumia lugha ya kisanaa, msanii anaweza kuwasilisha uzoefu wake kwa kiasi kikubwa, hisia zake n.k. lakini kwa njia ambayo ni tofauti ua ile ya kitaaluma. Picha si pambo tu, bali ni kitu muhimu katika kuleta maana ya dhamira mbalimbali zinazojitokeza katika kazi za sanaa.
Picha zinajitokeza kwa dhana mbalimbali. F.E.M.K.Senkoro24 na E. Kezilahabi25 wanaziainisha picha hizo kuwa ni za hisi, picha za maumbile na zile za matendo. Tena ziko picha ambazo zinaeleweka moja kwa moja na ziko nyingine ni ngumu kueleweka kirahisi.
Kwa picha zinazoeleweka kirahisi, wengi wanaosoma kazi za sanaa za kifasihi wanaweza kupata picha ya jumla. Lakini kwa zile picha ambazo ni ngumu kueleweka na zinategemea hali ya kimazingira, zinajitokeza katika kazi za sanaa na kutoa maana kufuatana na muktadha - hali ambapo hiyo kazi ya sanaa inasomwa. Picha za aina hii zinaweza kufasiriwa ama kutafsiriwa na msomaji kwa maana mbalimbali.
Jinsi ya Kusema Jambo
Njia zitumikazo zinatofautiana, na ukweli ni kuwa inategemea na nia ya mwandishi - anataka kusema nini, kwa nani na kwa jinsi gani? Njia muhimu ni pamoja na maelezo, masimulizi na kuhoji.
Maelezo
Aina hii ya maandishi hushughulikia mambo kama yanavyoonekana. Ni ufafanuzi wa maelezo kama mambo yalivyo. Kazi kubwa ya maelezo ni kufahamisha jinsi mambo yalivyo. Angalia mfano ufuatao kutoka kitabu cha Zaka la Damu.
Lyanda alikuwa mtu mwenye umbile kubwa sana, tena mnene kabisa mwenye tumbo kubwa mno. Lyanda maana yake tumbo kubwa sana. Kumbe ni jina alilopewa na Wafakiri. Macho yake yana njaa ya kitu fulani, siyo chakula bali kitu kingine, yana tamaa ya kitu fulani. Mgongo wake umepinda kidogo lakini hayo siyo maumbile yake ...Pale alipokuwa amekaa Ndatu alianza kuchunguza mazingira. Kwa upande wa magharibi wa ukumbi, palikuwa na meza moja kubwa ambayo ilifunikwa kitambaa kizuri chenye maua ya dhahabu na viti vikubwa sita vilivyozunguka meza hiyo. Hapana shaka ilikuwa ikitumiwa kwa maakuli...26
Ukichunguza maandishi hayo unaweza kugundua mambo mengi yanay-ofanya kazi iwe ya pekee kwa kuweka vivumishi au maneno yanayosifia mambo mbalimbli.
Kwanza, tukimchunguza Lyanda, tunaona picha ya mtu mkubwa - mwenye umbile kubwa tena mnene... na t.umbo kubwa sana. Tunaambiwa kuwa nyumba yake ni kubwa na nzuri - ukwasi uliomo na jinsi nyumba hiyo ilivyopangwa. "...upande wa magharibi... (pana) meza moja kubwa (yenye) kitambaa kizuri, chenye maua ya dhahabu, viti vikubwa sita vilizunguka meza hiyo.
Mfano huu unaonyesha kimsingi mbinu za maelezo ambazo hutumiwa na waandishi kwenye kazi zao za sanaa za kifasihi. Mwandishi wa hadithi fupi za Kiswahili anaweza pia kutumia mbinu hii ya maelezo katika kuelezea ayatakayo.
Masimulizi
Katika mbinu hii ya uandishi, msanii hutoa masimulizi yake juu ya mfululizo wa matukio kama yalivyotokea katika kipindi fulani cha maisha ya wahusika. Mwandishi husema nini kilitokea, jinsi gani kilitokea na mahali ambapo hayo yalitokea. Je, mambo hayo yalipotokea kati ya A na B kulikuwa na nini? Angalia mfano ufuatao kutoka Thamani ya Ukubwa.
Ninapoyaona maandishi hayo, ninatambua mara moja kuwa hii ni kazi ya Mama Tusi, mama ambaye ni majuma mawili tu yaliyopita amein-gizwa kwenye darasa la Kiingereza la masomo ya kujiendeleza ya Watu Wazima, baada ya kufuzu uzuri mtihani wa kisomo chenye manufaa katika hatua yake ya nne. Kwa mbali namwona mtu mwingine ambaye anafanya shughuli nisizozielewa. Anatembea polepole na kimya kimya kutoka kwenye mlango wa jengo hili ambapo nimejibana. Mara anatulia Halafu anaendelea tena...27
Katika kusimulia, yako mambo ya msingi ambayo huangaliwa sana na wasanii. Kwanza kuna yielezi. Matumizi ya vielezi yafanywe kwa uangalifu, kwani huathiri mfululizo wa masimulizi. Tazama.kwa mfano kifungu kifuatacho kutoka hadithi ya Wasubiri Kifo.
Mkoromo huu ulipoacha, mgonjwa alianza kuhema tena upesi upesi ua macho yake ambayo sasa yalionyesha majilio ya kifo takuwa sasa hayatembei ua kope zake zilikuwa hazipepesi. Lakini alikuwa bado akihema. Waliokuwepo walijua fahamu zake zilikuwa zimepotea.28
Jambo jingine muhimu ni kuwa mwandishi anatakiwa azingatie matumizi ya nyakati mbalimbali katika kazi yake ya sanaa. Baadhi ya wasanii hutumia muda uliopita, wengine muda uliopo. Nyakati zote zinaruhusiwa; jambo la muhimu m kuwa msanii ajue kuzitumia vizuri nyakati hizo.
Msimulizi wa hadithi anatakiwa kimsingi kuzingatia mantiki ya hadithi yake anayoisimulia. Mtiririko wa matukio ni muhimu ufuatane.
Katika kujenga mtiririko wa vituko, mwandishi anaweza kuweka hadithi ndani ya hadithi, barua, nyimbo na mashairi na kadhalika. Au hadithi yaweza kuwa mwisho-mwanzo, mwanzo-mwisho, mwisho-kilele, kilele-mwisho n.k. Masimulizi kimsingi hutawaliwa ua mazingira ya tukio linalosimuliwa, mwendo wa tukio (movement), wakati wa kutendeka tukio (time) na maana ya tukio (meaning).
Kuhoji
Hii ni mbinu ambayo kwayo mwandishi hujenga nyadala wake kwa kutumia hoja maalumu kuonyesha imani na msimamo alionao juu ya masuala kadhaa. Katika kufanya hivyo, mwandishi husimama upande mmoja. Au hutokea pia mwandishi husimama katikati, asijipambanue ua upande wowote ule.
Kazi za aina hii hutofautiana ikiwa mwandishi atajishirikisha upande mmoja.
Katika kuhoji, mwandishi atatumia lugha ya kumfanya msomaji aafiki mawazo ya msanii/mwandishi. Ni muhimu kwa mwandishi kuwa mchaguzi wa maneno vyema ili kuipa nguvu kazi yake, Mfano wa andiko la kuhoji ni hili lifuatalo; kutoka Ufakamu wa Lugha ya Kiswahili.
Zamani watoto wetu walisoma kipepepe wakavalishwa kipepepe, wakaiga mambo yote ya kipepepe kusoma, kula, mavazi, mila na hata tabia... Kwa hiyo, kale ikawa imepita na mambo yake. Tatizo likaletwa kwa kuwa watu wa vizazi hivi viwili - yaani watoto waliozaliwa wakati wa utawala wa mkoloni na dahari yetu tulipozaliwa; lazima kukaa pamoja...29
Mbinu hizi zikitumiwa, kazi ya kisanaa huimarishwa na kuwa bora zaidi.
Kuna mbmu mbili zaidi zitumikazo katika kusimulia ua kuelezea jambo. Mbinu hizi ni za matumizi ya monologia na matumizi ya dialogia.
Mbinu za Kimonologia
Monologia ni masimulizi yanayofanywa na mhusika mmoja katika hadithi au kazi nyingine za kisanaa.
Katika mbinu hii, hadithi, inajitokeza kama inasimuliwa na mhusika aliye hadithini. Mwandishi anaonekana kuwa hayuko. Pia hadithi inaweza kujitokeza ikisimuliwa katika nyakati mbalimbali.
Wakati mwmgine, mwandishi anaweza kujitokeza mara chache chache ili kumfafanua mhusika anayesimulia hadithi hiyo ya kimonologia. Angalia mfano huu ufuatao: