UTAFITI:UFASIHI SIMULIZI KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad
SURA YA KWANZA
UTANGULIZI KWA UJUMLA
1.0 Utangulizi Sura hii ni sura tangulizi inayobainisha usuli wa tatizo la utafiti lililofanyiwa uchunguzi katika utafiti huu. Kwa hivyo, sura hii inabanisha na kueleza usuli wa tatizo, tatizo la utafiti, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, ambayo utafiti huu ulikusudia kuyajibu na umuhimu wa utafiti, masuala ya maadili ambayo yalizingatiwa kabla, wakati na baada ya utafiti. 1.1 Usuli wa Utafiti Wataalamu mbali mbali wameelezea na kufafanua maana ya riwaya. Kutokana na ukweli huo ni dhahiri kuwa kuna maoni mbali mbali yanayohusu dhana ya riwaya, Maneno ambayo yamekaririwa na watalamu wote, ni kuwa riwaya ni utanzu wa fasihi andishi, ikiwa ni pamoja na ushairi na tamthiliya. Matteru (1976) anafafanua kuwa riwaya ni hadithi ndefu ambazo zimeandikwa. Kutokana maana hii tunaweza kuona mambo matatu makuu katika dhana ya riwaya, kwamba riwaya ni hadithi, hadithi ni lazima iwe ndefu na ni lazima iwe imeandikwa. Mphalale (1976), anasema riwaya ni hadithi ndefu za maneno kati ya 35,000 na 50,000. Tunaweza kusema kwamba kuna riwaya ndefu na riwaya fupi, kulingana na idadi ya maneno yaliyotumiwa na mwandishi. 2 Mulokozi (1996) anaeleza kuwa, riwaya ni kazi ambayo inakuwa na sifa mbali mbali, kuwepo na ubunifu, usimulizi (ni hadithi ya kisimulizi la kinathari), mpangilio au msukumo fulani wa matukio (ploti), mfungamano wa wakati, visa vinatendeka katika wakati fulani, inatakiwa iwe na maneno mengi na itakapokuwa na maneno pungufu ya elfu tatu (3000), yaweza kuitwa Novela, pawepo na mawanda mapana (kwa upande wa yale yanayozungumzwa, wakati na mahali pa matukio hayo), na pia pawepo na uchangamani katika visa, dhamira, tabia, wahusika n.k. Senkoro (1982) na Wamitila (2002) wanaeleza kuwa riwaya ni kisa mchangamano ambacho huweza kuchambuliwa na kupimwa kwa mapana na marefu kifani na kimaudhui. Kisa ambacho urefu unaoruhusu kisa kitambe na kutambaa vizingiti vingi vya maisha kama apendavyo mwanadamu. Hivyo riwaya ni hadithi ndefu ya kubuni, yenye visa vingi, wahusika zaidi ya mmoja na yenye mazungumzo na maelezo yanayozingatia kwa undani na upana, maisha ya jamii. Kuhusiana na chimbuko au chanzo cha utanzu huu wa fasihi, wataalamu wengi au wote wanakubaliana na chanzo cha riwaya ni hali halisi ya kijamii, pia wanakubaliana kuwa utanzu huu ni mchanga, ukilinganisha na tanzu kama ushairi, michezo ya kuigiza au tamthiliya. Ndungo na mwenzake (1991) wanasema kuwa, miongoni mwa riwaya za mwanzo kuzuka ilikuwa ni riwaya ya Robinson Cruisoe (1719) ya Daniel Defoe. Riwaya hii ilizuka kutokana na maendeleo na mabadiliko ya uvumbuzi wa viwanda. Ukoloni na uvumbuzi wa viwanda ulileta haja ya kueleza mambo kwa njia ya hadithi na ngano 3 ambazo zilikuwepo kwa wakati huo. Wanaendelea kusisitiza kuwa, kuzuka kwa miji na viwanda kulistawisha uandikaji wa riwaya na usomaji kupanuka. Maendeleo katika vipengele vyote vya maisha kama vile kiuchumi, kisiasa na kijamii, yalizusha haja ya kuwa na utanzu wa fasihi ambao uchangamano wake wa kifani na kimaudhui ungedhibiti nyanja hizi zote. Akijadili kuhusu kuzuka kwa riwaya Mulokozi (1996) anasema kuwa riwaya haikuzuka hivi hivi tu, bali ilitokana na fani za masimulizi (za hadithi) zilizokuwepo kabla. Hivyo fani hizo zilikuwemo katika fasihi simulizi iliyokuwepo kabla ya kuzuka utanzu wa riwaya katika fasihi andishi, na ziliigwa na watunzi wa mwanzo wa riwaya. Watunzi hao walisukumwa na mabadiliko ya kijamii ya karne ya 16-18 huko Ulaya. Fani ya jadi ambazo zilichangia katika kuchapuza riwaya ni ngano, hekaya, tendi, visa kale, historia, siasa, masimulizi ya wasafiri, insha na tafsiri. Hoja za Ndungo mwenzake (1991) pamoja na Mulokozi (1996) zinadhihirisha kuwa, riwaya ilianzia huko Ulaya, kutokana na mabadiliko mbali mbali ya kijamii, yaliyotokea nchi za Ulaya na kuathiri wanajamii. Masimulizi yalikuwepo kabla ya mabadiliko hayo ndiyo yaliyotumika kuweza kuonya, kuburudisha, kuliwaza, kutunza historia ya jamii, kwa kutumia mfumo wa maandishi, ambapo yalikuwa ni maendeleo mapya katika dunia. Hali hii inayothibitisha kuwa fasihi ni lazima kuendana na mabadiliko ya jamii. Mulokozi (1996) anasisitiza kuwa kufika karne ya kumi na sita (16), fani zilizotajwa kama vile ngano, hekaya, tendi, visakale, historia, insha na tafsiri, zilikuwa zimeshaenea 4 pia kufahamika na mataifa mengi. Hivyo kulihitaji msukumo wa jamii kiteknolojia na kiuchumi, ili ziweze kuwa za riwaya. Kutokana na maelezo hayo ni dhahiri kuwa, palikuwepo mambo yaliyopelekea kuenea kwa vitu hivyo ndani ya jamii. Hivyo ukuaji mkubwa wa shughuli za kiuchumi huko Ulaya. Ukuaji huo ulishikamana na biashara za masafa marefu za baharini, kutoka bara moja hadi bara jengine. Vile vile msukumo mwengine ni kuvumbuliwa kwa Mabara ya Amerika pamoja na kukua kwa vitendea kazi kazi (nyenzo) vya uzalishaji wa viwandani barani Ulaya. Hali iliyosababisha mapinduzi ya viwanda. Chanzo cha riwaya katika fasihi ya Kiswahili ni fani za kijadi ni ngano, hekaya, tendi, visa kale, historia, sira, masimulizi ya wasafiri, insha na tafsiri. Watoto na wazee walikuwa wanakutana na kutambiana hadithi kwa nia ya kushauri, kuonya, kutahadharishana na kuelezana mambo ya mbali mbali kuhusu jamii. Hadithi hizi zilipokezanwa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine (tazama Ndongo na Mwai na mwenzake 1991 na Mulokozi (1996). Wataalamu hawa wanakubaliana kuwa majilio ya wazungu kama majilio wa wageni waliotangulia katika nchi za Afrika ya Mashariki, yalikuwa na athari kubwa katika fasihi ya Kiswahili. Kwani hati za kilatini zilianza kutumika 1890 kwa watu wa Afrika Mashariki, na yale yaliyoandikwa na waalimu wenyewe kwa kutumia mila na tamaduni za kwao. Kulikuwa hakuna yaliyoandikwa na Waafrika kwa wakati huu. Hivyo hadithi za Waafrika zilikuwa katika masimulizi. Maelezo hayo yanathibitisha kuwa riwaya ni mazao ya fikra na mawazo ya wageni wa kizungu. Mara nyingi vitabu hivi vilikita kuelezea tajriba yao ya maisha, silka, malezi, 5 na mtazamo kuhusu maisha. Pia waliendelea kutunga vitabu vya hadithi vya Kiarabu na kizungu, baadhi ya vitabu hivyo ni kama Alfu lela Ulela (1313), Safari ya Gulliver (1932, Mashimo ya Mfalme Suleiman (1929), Hekaya za Abunuasi (1915) n.k. Waafrika walitunga hadithi kwa kutumia maudhui na mtindo katika mtiririko wa visa na mengineyo yaliyoegemea katika kuendeleza ukoloni na utamaduni wa kigeni. Riwaya ziliendelea kutungwa kwa kuziba pengo la ukosefu wa riwaya katika fasihi ya Kiswahili. Palianzishwa mashindano ya uandishi na taasisi ya kusanifisha lugha ya Kiswahili kwa utungaji wa hadithi fupi pamoja na vitabu vidogo vidogo na lugha iliyotumiwa ni ile iliyokubaliwa na taasisi hiyo, na mfano wa vitabu ni Mjomba Remus (1935), Safari ya Juma (1949), Safari ya Sungura (1926) n.k. Hadithi na vitabu vilivyotungwa havikusaidia ila kukuza nadharia za kuendeleza na kudumisha ukoloni na kudunisha utamaduni wa Kiafrika, ijapokuwa havikusaidia kwa kiasi fulani lakini hali hii ilipelekea kuibua waandishi wa riwaya za Kiswahili. Maelezo hayo yanadhahirisha kuwa chanzo cha riwaya za Kiswahili, ni mchango mkubwa uliotokana na biashara na mapinduzi ya viwanda huko Ulaya. Hali hii ilianza Ulaya na kuja Afrika, kwa kutumia biashara ya baharini. Ambapo biashara hii ilipotokea Ulaya kuja Afrika iliathiri kwa kiasi kikubwa mila, silka na desturi za Waafrika. Hali iliyopelekea kufuata uhalisia wa Kiafrika na kuwa mchanganyiko kati ya Uafrika na Uzungu. Ndipo palipopatikana kitu kiitwacho riwaya inayotokana na fasihi andishi badala ya hadithi inayotokana na fasihi simulizi. Hata hivyo tukirejelea mwazo ya Mulokozi (1996), yanaonyesha kuwa riwaya ya Kiswahili imechimbuka katika fasihi simulizi. 6 Kutokana na utalii huo kuhusu riwaya na chimbuko lake. Utafiti huu unaona kuwa ipo haja kuchunguza ufasihi simulizi katika riwaya ili kuona ni jinsi gani vipengele vya fasihi simulizi vimeingizwa katika utanzu wa riwaya kama mbinu ya kisanii inayotumika kujenga riwaya za Kiswahili. Kwa kufanya hivi tunaweza kubaini nafasi ya fasihi simulizi katika riwaya za Kiswahili. Kwa hiyo utafiti huu ulichunguza riwaya mbili za Shaaban Robert ili kubaini ufasihi simulizi uliojitokeza katika riwaya hizo. 1.2 Tatizo la Utafiti Kama tulivyoona hapo awali kwamba chanzo cha riwaya ya Kiswahili ni fasihi simulizi, Swali linalotatiza utafiti huu ni je kuna athari yoyote ya fasihi simulizi katika riwaya za Kiswahili? Je, vipengele vya fasihi simulizi hujitokeza katika riwaya za Kiswahili? Kutokana na maswali hayo, tatizo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza vipengele vya fasihi simulizi vinavyojitokeza katika riwaya za Shaabn Robert ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti binti Saad, ili kubaini jinsi vipengele vipi vya fasihi simulizi vilivyotumiwa na mtunzi kama mali ghafi ya utunzi wa riwaya ya Kiswahili. 1.3.0 Malengo ya Utafiti Utafiti huu una malengo ya jumla (kuu) na malengo mahsusi. Kama yanavyojionyesha katika sehemu ifuatayo; 1.3.1 Lengo Kuu Kuchunguza ufasihi simulizi katika riwaya za Shaaban Robert kwa kutumia mifano ya riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad, ili kuona ni jinsi gani msanii huyo anatumia vipengele vya fasihi simulizi kama mali ghafi ya utunzi wa riwaya ya Kiswahili. 7 1.3.2 Malengo Mahsusi Utafiti huu una malengo mahsusi mawili. 1) Kubaini vipengele vya fasihi simulizi vinavyojitokeza katika Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. 2) Kubainisha dhamira zinavyowasilishwa na matumizi ya vipengele vya fasihi simulizi katika riwaya za Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. 1.4 Maswali ya Utafiti Utafiti huu unaongozwa na maswali yafuatayo: 1) Je, ni vipengele vipi vya fasihi simulizi vinavyojitokeza katika riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad? 2) Je matumizi ya vipengele vya fasihi simulizi katika riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad yanaibua dhamira zipi? 1.5 Umuhimi wa Utafiti Umuhimu wa utafiti huu umejikita katika nyanja kuu tatu: Kwanza, utafiti huu utatoa mchango katika taaluma ya fasihi kinadharia na vitendo. Kwa kueleza na kuchambua fasihi simulizi iliyomo katika kitabu cha Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad, tutaweza kuona ni jinsi gani msanii huyu alivyotumia mbinu za fasihi ndani ya kazi zake; Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Pili, utaongeza maarifa katika nadharia na mbinu za utunzi wa riwaya hususani riwaya za Kiswahili. Aidha, utafiti huu utaweza kutumika katika taaluma ya fasihi, hususani 8 riwaya. Hivyo, utafiti huu utatumika kama marejeo na kwa maana hiyo, utawasaidia wanafunzi na watafiti wengine kupata marejeo kuhusu riwaya za Kiswahili na riwaya kwa ujumla wake. Vile vile, utafiti huu utakuwa ni changamoto kwa watafiti wengine kutupia jicho katika riwaya za Kiswahili. Hivyo basi, utafiti huu utawapa changamoto watafiti wengine waweze kuchunguza na kuchumbua ufasihi simulizi katika kazi zingine za fasihi ili kuona jinsi gani vipengele vya fasihi simulizi vinatumika katika kujenga tanzu zingine za fasihi ya Kiswahili. Tatu, utafiti huu ni malighafi, kwani utatoa mchango mkubwa katika historia ya riwaya na fasihi chambuzi kwa ujumla na vile vile utatajirisha maktaba ya chuo. 1.6 Mipaka ya Utafiti Utafiti huu ulilenga kuchunguza na kuchambua ufasihi simulizi katika riwaya za Kiswahili. Pamoja na kuwawapo waandishi na watunzi wengi wa riwaya kwa hivyo utafiti huu, kuwa haikuwa rahisi kuchunguza riwaya za waandishi wote, utafiti huu ulijikita katika kuchunguza na kuchambua ufasihi simulizi katika riwaya za Shaaban Robert tu. Sababu ya kumchagua Shaaban Robert ni kwa sababu ni mtunzi mwenye athari kubwa katika fsihi ya Kiswahili. Shaaban Robert ana riwaya nyingi lakini utafiti huu uliamua kuteua zake mbili yaani riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti binti Saad. Hii ni kwa sababu isengekuwa rahisi kuchunguza riwaya zote alizotunga Shaaban Robert. 9 Hivyo utafiti huu ulichunguza na kuchambua kazi mbili tu Shaaban Robert. Kwa maana hiyo kazi zake nyengine za kifasihi hazitoshughulikiwa isipokuwa riwaya zilizotajwa. Kazi za Shaaban Robert na zile za wasanii wengine ambazo hazikushughulikiwa katika utafiti huu, bali ziliweza kurejelewa hapa na pale kwa lengo la kuchunguza na kuchambua vipengele mbali mbali vya fasihi vilivyomo katika kazi hizo. 1.7 Hitimisho Sura hii imeajadili kuhusu usuli wa utafiti, vile vile limejadiliwa tatizo la utafiti. Aidha sura imezungumzia kuihusu malengo ya utafiti, pamoja na kuzungumzia lengo kuu la utafiti. Sura hii vile vile imezungumzia malengo mahsusi yaliyomo katika utafiti huu, na pia yamejadiliwa maswali ya utafiti. Aidha katika utafiti huu imejadiliwa kuhusu umuhimu wa utafiti pamoja na mipaka inayohusu utafiti. Sura inayofuata inahusu nini?