USHAIRI
Ushairi ni mtungo wa kisanaa wenye mpangilio maalumu wa lugha ya mkato katika usemi, maandishi, wimbo unaoelezea wazi juu ya mawazo, hisi au tukio juu ya maisha na ambao hufuata utaratibu wa urari na muwala maalum unaoheshimu na kuzingatia kanuni za utunzi wa mashairi unaohusika. Kwa hivyo, kwa kifupi, shairi ni mtungo , wimbo au maandishi yaliyoandikwa kwa kufuata sharia Fulani za utunzi ambazo huitwa arudhi.
Ushairi pia ni sanaa ya utunzi wa mashairi , tenzi, ngonjera nk
MAKUNDI YA WASHAIRI
Aina za washairi zimetokana na mitazamo tofauti ua washairi , kuna makundi mawili ya washairi :-
(.a.) WANAMAPOKEO
Hawa ni washairi wa jadi wanaoshikilia kuwa ili mtungo Fulani uweze kuingia katika kundi la washairi, ni lazima mtungo hufuate sharia au kanuni Fulani kama vile urari wa vina, mizani , idadi ya mishororo katika beti nk,ambazo huitwa arudhi.Kutokana na mtazamo wa kundi hili ,kukaibuka aina ya mashairi yaitwayo mashairi ya arudhi, mashairi ya jadi na mashairi ya kimapokeo.Haya ni mashairi yanayoshibisha kanuni zote zilizokubaliwa katika utunzi wa mashairi.

Sifa za mashairi ya kimapokeo/mashairi ya arudhi :-
1.Huwa na urari/usawa/ulinganifu wa mizani.
2.Huwa na urari wa vina.
3.Huwa na urari wa mishororo
4.Huwa na muundo ulio rahisi kufuatika ukilinganishwa na wa mashairi huru.
5.Huwa na beti zinazofanana isipokuwa katika bahari ya sarakani inayochanganya aina mbali mbali za washairi
6.Hutumia lugha ya mkato na yenye mnato
7. Hutumia tamathali za usemi kwa wingi

(.b.) WANAMAPINDUZI
Hawa ni washairi wa kisasa wanaoaminu kuwa ili mtungo Fulani weze kuingia katika kundi la washairi, si lazima uzingatie arudhi kama vile urari wa vina, mizani, idadi ya mishororo katika bet ink. Kundi hili husisitiza kuwa la muhimu katika mtungo sio sharia/kaida hizi bali ni ujumbe au maudhui ua walemhwa kwa hadhira yake.Kutokana na mtazamo wa washairi kawa kukaibuka aina nyingine ya mashairi yaitwayo mashairi huru, mauve, zuhali au mashairi mlegezo.
SIFA ZA MASHAIRI HURU
1.Hayazingatii arudhi kama vile urari wa vina ,mizani ,idadi ya mishororo katika bet ink
2.Huwa na beti tofauti tofauti yaani hamna idadi maalumu ya mistari katika ubeti mmoja.
3.Huweza kuwa ma sehemu za ubeti ambazo zimeingia ndani kama njia ya kuzifanya zionekane wazi kwa msomaji kwa nia ya kusisitiza
4.Hutumika takriri kwa wingi ili kusisitiza ujumbe.
5.Huhusisha matumizi ya mishororo (mistari) inayokamilika na inayojitosheleza kimaana iitwayo mistari toshelezi au mistari ambayo haijakamilika kimaana iitwayo mishata, na kwa hivyo humbidi msomaji asome mstari unaofuata ili aweze kuipata ,aama kamili.

TANZU ZA USHAIRI
Kuna tanzu (branches) mbili za ushairi :- 1. Mashairi Andishi 2. Mashairi Masimulizi
• MASHAIRI ANDISHI
Haya ni mashairi yaliyoandikwa m Mashairi haya hushughulikiwa katika fasihi andishi na yanaweza kuwa mashairi ya arudhi au mashairi huru.
• MASHAIRI SIMULIZI/ MASIMULIZI
Haya ni mashairi yanayowasilishwa kwa kutumia ala yam domo, Huwasilishwa kwa njia yam domo kwa kuimba, kughani au kukariri.Baadhi yao hayaimbwi bali huwasilishwa kwa kalmia-kwa maneno ya kawaida kama vile maghani. Mashairi haya hushughulikiwa katika fasihi simulizi.Yanahusisha nyimbo,maghani,ngonjera na sifo. Ni muhimu kutaja kuwa kaitka kitabu hiki tutajifunga kwenye mashairi andishi, mashairi ya arudhi na mashairi huru.Kwa hivyo,mwanafunzi anashauriwa kurejea kazi yake ya fasihi simulizi kwa maelezo zaidi juu ya mashairi mawasimulizi.

SIFA ZA MASHAIRI KWA UJUMLA
• Ni tungo za kubuni zinazoelekeza maisha ya jamii kisanaa.
• Hutumia maneno machache kuwakilisha dhana pana mno
• Hutumia picha au taswira zenye uwezo wa kutoa maelezo kamili.
• Hutungwa kwa lugha ya kitamathali ,luhja inayoficha maana na hivyo hutumia tamathali za usemi kwa wingi.
• Baadhi ya mashairi hufuata sharia /arudhi katika utungwaji wake (mashairi ya arudhi) ilihali mengine hayafuati sharia hizo bali huzingatia maudhui (mashairi huru)
• Baadhi ya mashairi huwa na kibwagizo
• Hufungamana na hisia kwani hugusa moyo wa msomaji.
• Huwa na mpangalio maalumu wa maneno ,mizani ,vina ,mishororo na beti (mashairi ya kimapokeo)
• Huelezea hisia za watu kutoka ulimwengu halisi wa kila siku.
• Huelezea mambo yanayohusisha itikadi na imani za mwatu katika jamii
• Hutumia lugha mkato.
DHIMA YA USHAIRI
Dhima ni wajibu, jukumu ,kazi au umuhimu wa ushairi kwa wanajamii
Mashairi huwa na dhima zifuatazo:-
1.kutoa wasia, nasaha au mawaidha kwa wanajamii
2.kuelimisha hadhira lengwa.
3.Kutahadharisha mtu/ watu kuhusu ulimwengu na malimwengu
4.Kukashifu, kejeli Tania mbovu/hasi katika jamii
5.Kusifia tabia au mienendo miema katika jamii
6.Kuburudisha ,kufurahisha au kuchekuesha msomaji au msikilizaji (hadhira)
7.Kukuza na kuisarifu lugha husika
8.Kukuza kipawa cha mtu katika sanaa ya lugha ,kwa mfano , uwezo wa kuandika au kuimba kwa mahadhi.

ISTILAHI MUHIMU KATIKA USHAIRI
MALENGA – ni mtungani stadi wa mshairi
MANJU – ni mtu stadi wa kutunga na kuimba mashairi au nyimbo katika ngoma.
DIWANI – ni kitabu cha mkusanyiko wa mashairi hususani ya mtu mmoja.
URARI – ulingano au usawa haswa wa vina na mizani.
MUWALA/MWALA/UTOSHELEZI –ni upatanisho ,mtiririko au mkatamatano wa kuridhisha wa fikira kutoka ubeti hadi mwingine au ni muoanisho wa fani na maudhui
UBETI : (wingi ,beti ) ni jumla ya mishororo/mistari inayobeba wazo moja kuu katika shairi.
VINA :ni silabi zinazojitosheleza katika kipumuo, katikati ya ushairi au mwishoni mwa shairi, idadi ya vina katika mshororo hutegemea bahari ya shairi.Kwa mfano , bahari ya utenzi huwa na kina kimoja, bahari, bahari ya mathinawi huwa na vina viwili, china cha kati (kwa ukwapi) na kina cha mwisho (utao).