MISEMO YA KISWAHILI
Kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa
Msemo huu una maana kuwa unapewa sifa usizostahili. Msemo mwingine ulio na maana sawa ni kuvalishwa kilemba cha ukoka.
Chezea unyango wa kima
Msemo huu huweza kutumika kuonya mtu dhidi ya jambo fulani. Kwa mfano, ” wewe, utakiona leo, nitakuchezesha unyago wa kima”. Inaaminika kuwa kima huacheza ngoma (Unyago) ili kuwatoa vigori (Wali). Tendo hili hufantika kwa siri na endapo watagundua umewaona, lazma nawe uchezeshwe. Kwa hivyo, kuwa makini na mambo ya watu, usije ukachezeshwa unyago wa kima!
Bara yangu sibadili na rehani
Huu ni msemo ambao una maana lukuki, baadhi ya watu hutafsiri neno “bura’ kama kitu cha tunu kichakavu. Kwa hivyo msemaji wa msemo huu hunamaanisha kuwa hawezi badili kitu chake cha tunu kwa kipya.
Usiache “mbachao” kwa msala upitao
Katika msemo huu, wahenga wametumia neno “mbachao” linatamkwa “m-bachao,” yaani ni kifaa duni kinachotumiwa kufanyia ibada, Kwa mfano, mkeka au jamvi kuukuu (Kidukwa)..sasa wamesisitiza usije ukauacha kwa “Msala” upitao..msala nao ni sehemu ya kusalia lakini si duni kama ilivyo m-bachao. Pia, msemo huu un maana sawa na Usiyadharau madafu, maembe ni ya msimu.
Mwanya ni kilema pendwa
Wengi hawafahamu kuwa hata kama mwanya ni kilema, lakini ni kilema kinachopendwa na wengi. Vilema vya aina hii hutambulika kama ‘vilema pendwa’, vipo vingi kwa uchache ni baadhi ya matege ya miguu, makalio makubwa, vifua, na misuli mikubwa.
Mungu hakupi kilema akakunyima mwendo
Msemu huu una maana kuwa mtu anapaswa kuridhika na alicho nacho. Funzo kuu ni kuwa haina haja kutamani vitu ambavyo vimepiku uwezo wetu.
Mlevi haukubali ulevi
Msemo huu una maana kuwa hata anywe vipi hakubali kuitwa mlevi. Msemo hu umewalenga mahasidi na mafisadi ambao hukataa chungu ya ukweli.
Chongo kwa mnyamwezi kwa mswahili amri ya mungu
Wengne hutumia neno ‘chogo’ badala ya ‘chongo’, yote kheri alimradi haipotosha maana ya usemi huu.
Ushikwapo shikamana, si wengi wa kupendana
Maana ya msemo huu ni, endapo atatokea mtu akakupenda na akaomba muwe marafiki usikatae, kwani hapa ulimwenguni watu wachache sana wanaopendana