Fasili Za Vidahizo Vya Kamusi Ya Kiswahili Sanifu
Fasili Za Vidahizo Vya Kamusi Ya Kiswahili Sanifu
Utangulizi
Baada ya miaka mingi ya kutumia kamusi za lugha mbili ambazo zinahusika hasa nautoaji wa visawe vya vidahizo kutoka lugha moja hadi nyingine, tulitumaini kuwa Kamusi ya Kiswahili Sanifu (KKS) ikiwa ni ya iugha moja, itatuwezesha kukifahamu Kiswahili kwa nndani na mapana zaidi.
Fasili zenye maneno magumu
Pasili na visawe vingi vya KKS ni toshelevu isipokuwa tu baadhi yake hukosa mifano ya kuelezea matumizi. Mifano ya fasili toshelevu ni kama ifuatayo:
(1)
|
kifumbu
|
ji vi-
chombo kama kikapu chenye umbo la duara kitengenezwacho kwa miyaa na kutumika kuchujia nazi; kumto, kung'uto, kichujio. |
kifundo
|
ji vi-
1. sehemu ya mwili ambapo mifupa inaungana na kutokeza 2. aina ya uvimbe kama jipu unaotokeza mwilini. |
Baadhi ya maneno katika fasili ya kifumbu ni magumu kuelewa, k.v miyaa na kumto; kwa jumla fasili zote ni toshelevu isipokuwa tu kwamba zinakosa mifano ya matumizi. Kama tulivyokwisha tamka hapo juu fasili zilizo nyingi katika KKS ni toshelevu isipokuwa chache ambazo zitahitaji kurekebishwa. Katika kuchambua utoshelevu wa fasili katika KKS, kwanza tutatoa mifano michache ya fasili na visawe visivyotosheleza. Halafu tunazungumzia umuhimu wa kutumia maneno rahisi katika fasili, uainishaji wa vidahizo na mifano ya matumizi. Kisha, tunatoa maoni kuhusu tasili za sinonimu na mifano ya matumizi ya vidahizo. Mwishowe tunagusia dhima ya sifa za kisarufi za vidahizo katika kukamilisha fasili.
Fasili ya Visawe Visivyotosheleza
Fasili za Mzunguko
Baadhi ya fasili za KKS zina maneno ambayo ndiyo yanayofasili.
(2)
|
kifu ji vi- kitu kilichokufa
|
kifuasi ji vi- kitu kinachofuata
| |
kifukizio ji vi -
| |
kitu kitumikacho wakati wa kufukiza; kifukizo
|
Fasili za aina hii hazimsaidii mtu kuelewa maana ya kidahizo. Kwa mfano fasili ya kifu haimwezeshi msomaji kuelewa maana yake iwapo hajui maana ya kufa. Fasili nzuri ingekuwa: "kitu ambacho kimetok wa au kimeishiwa uhai". Halikadhalika, tasili ya kifo kama ilivyo katika KKS haitoshelezi: "tukio au tendo la kufa, mauti" sinonimu mauti ni neno gumu zaidi kueleweka kwa mtumiaji wa kamusi. Fasili nzuri ya kifo ambayo ipo pia katika KKS ni: "uondokaji wa roho kiwiliwilini, mwisho wa uhai". Aidha, mfano wa matumizi unaotolewa wa neno kifo, haueleweki kwa urahisi kwa sababu ni methali: "- - - - cha wengi harusi". Methali na nahau ni vipengele vya lugha ambavyo vinatatiza sana, hasa kwa wale ambao lugha inayolengwa ni lugha ya pili au ya tatu. Waandishi wa kamusi sharti wajitahidi kutotumia nahau na methali kuelezea matumizi ya vidahizo kwa sabubu nahau na methali zenyewe hazieleweki mpaka zifasiliwe.
Fasili Zisizoleta Maana Iliyokusudiwa
Fasili nyingine hazitoi maana iliyodhamiriwa. Mathalani. fasili za kidahizo utamu na uchungu hazileti maana iliyokusudiwa.
(3)
|
uchungu ji
|
hali anayuhisi mtu kinywani baada ya kuramba au kula kitu k.v. shubiri, kwinini, mchunga
|
utamu ji
|
hali ya kunoga kwa kitu au mambo.
|
Tukizingatia vitu ambavyo hunoga tunaona kwamba ni vingi: chumvi. kilimo. kazi. n.k. Si lazima kitu kiwe na utamu ili kinoge, Mtu asiyejua kuwa uchungu huhusiana hasa na urambaji au ulaji wa vitu vyenye mwonjo au ladha ya chumvi au asidi anaweza akaongezeaasali au sukari kwenye orodha iliyotolewa katika kitomeo cha uchungu. Kwa hakika vidahizo utamu na uchungu havistahili fasili sawa ila zinahitaji kutofautishwa kwa kuongeza usukari na uchumvi kutika kidahizo utamu na uchungu.
Fasili ziwe na Maelezo Rahisi
Maana ya wa kidahizo haina budi kufafanuliwa kwa maelezo kisha ifuate sinonimu. Fasili ya neno haina budi kuwa na sifa semantiki sawa sawa na sifa semanliki za kidahizo. Baadhi ya vidahizo vya KKS vimefasiliwa kama ilivyoelezwa juu. kwa mfano:
(4)
|
angalau - ku neno litumikalo kueleza lililokuwa afadhali, japokuwa, walau. lau. Pengine angalao, ngaa, angaa, angao.
| |
kubali kt
|
l.sema ndiyo; ridhika: kiri
| |
2.toa ruhusa: ruhusu.
|
Vidahizo vingine vimetasiliwa kwa sinonimu tu. kwa mfano: kiri kt kubali, ungama. Kidahizo hiki kingefafanuliwa vyema zaidi iwapo fasili ingeanza na maelezo: sema kuwa umefanya kosa kabla ya visawe kubali na ungama.
Kategoria zote za maneno zishughulikiwe
KKS haikuzishughulikia aina zote za maneno. Kwa mfano, vionyeshi na vimilikishi havikutajwa kabisa katika kamusi nzima, hata katika utangulizi. Ingefaa ielezwe katika utangulizi kuwa ni vigumu kwa aina hizo za maneno kuingizwa kama vidahizo pekee katika kamusi kwa sababu maumbo ya kimofolojia ya maneno ya aina hizo yanatawaliwa sana na maneno yanayoyatawala kiasi kwamba bila upatanifu wa namna hiyo maneno hayo yanashindwa kujitegemea. Kwa mfano. tamko kama: watu -hutamhulika tu baada ya kukamilishwa kwa upatanifu wa kisarufi kuwa. watu hawa. Mzizi h- wa kionyeshi hautambuliki mpaka umbo lake linapodhihirishwa wakati wa kuwiana na nomino watu. Vilevile kimilikishi: angu hakijitegemei mpaka kinapotawaliwa na kukamilishwa kiumbo na nomino inayokitawala. Kwa mfano. mdomo + u-angu. huwa mdomo wangu.
Vihusishi pia havitajwi ingawa tuna maneno kama na na kwa ambayo kwa vyovyote vile ni vihusishi katika mifano ifuatayo:
(5)
(a) Aliuawa na majamhazi
(b) Tulikuja kwa basi.
Kifupisho (kw) hutumika katika vitomeo vya maneno kama mimi, yeye. n.k. bila shaka kinamaanisha kiwakilishi lakini hakitajwi katika orodha ya vifupisho iliyoko katika utangulizi. Vijalizo pia havitajwi kabisa ingawa kwa kweli yipo katika sintaksia ya Kiswahili kama tunavyoona katika mifano namba (6):
(6)
(a) Ni uwongo kuwa tunataka kumtoa.
(b) Hivi hamna habari kama ninakuja leo?
(c) Alikuwa na imani ya kuwa kutofanikiwa ni hak-i.
(d) Jibu alilolipata kwa wote lilikuwa ati nyumba yake ilikuwa na nuksi.
(e) Nilivyoeiewa ni kwamba Bwana James hapingi mpango huu.
(f) Nakubali kwamba matatizo uliyoyapata ni makubwa.
VijaJizo katika data (6) Vina chapa ya italiki. Maneno kama hayo lazima yaelezwe katika kamusi toshelevu. Tunapenda pia kugusia hapa umuhimu wa kuwepo na ulinganifu wa kuyaainisha maneno. Uainishaji wa vidahizo vifuatavyo hauonyeshi ulinganifu wowotejapokuwa maneno haya ni sinonimu na yana dhima moja katika sentensi.
(7)
walau- kiunganishi
angalau- kiunganishi
japo- kiunganishi
ingawa- kiunganishi
katika- kiunganishi
na- kivumishi
bali- kiunganishi
Haieleweki kwa nini walau na angalau zimeashiriwa kategoria tofauti ilihali twafahamu kuwa zina dhima moja katika tungo. Vivyo hivyo kwa bali na na. Aidha KKS haina budi kutumia istilaln zilizosanifiwa kuashiria kategoria za manenu kama zilivyotumiwa katika Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. Iwapo Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha inazungumzia nomino itafaa pia KKS itumie nomino badala ya jina. Halikadhalika. kwa kuwa sasa tumeamua kutumia kijalizo (complement) basi vitomeo katika KKS visiendelee kutoa maelezo yanayozunguzia shamirisho kwa maana ile ile.
Vidahizo Vifasiliwe Vyote
Watunga kamusi wengi wamesisitiza umuhimu wa kufasili vidahizo vinavyoingizwa katika Kamusi. KKS ina vidahizo ambavyo havikufasiliwa, na badala yake msomaji anaelekezwa atazame kidahizo kingine katika kamusi hiyo hiyo. Vidahizo visivyofasiliwa havimsaidii mtumiaji kamusi kupata maana ya neno analolitatuta. Tazama Na. 8 chini.
(8)
Mbaruwae ji taz. mbayuwayu
Mbayuwayu —- Pengine barawai, mbaruwae.
Mbaa ji taz. mbawala.
Mbawala - - - Pengine mbawara
Pekee- - - -; pweke
Pweke - - - pekee: mtu - - - - ni uvundo(mt): Msema - - - - hakosi hajui ailiye (mt).
(Angalia: mbaa halitajwi tena)
Mambo kama haya yanamtatanisha na kumkatisha tamaa mtumiaji wa kamusi ambaye angependa kujua ule uhusiano baina ya mbaa na mbawala. Methali iliyoingizwa katika kidahizo pweke haikufasiliwa. Methali na nahau zinazotumiwa katika vitomeo sharti zifasiliwe.
Mifano ya Matumizi ya Neno
Kamusi ya Kiswahili Sanifu ina maelezo yanayoashiria nyanja za matumizi ya maneno: Kibaharia, kidini, kishairi, kizamani n.k. Taarita hii ni muhimu sana kwa mtumiaji wa Kamusi. Hata hivyo, KKS haina mifano ya matumizi ya neno. Mifano ya matumizi ni muhimu. Kwa mwanafunzi wa Kiswahili hususan k-wa vidabizn ambavyo vimefasiliwa kwa sinonimu. Kwa mfano:
i) afiki kt kubali.
ii) walau kl japo; ingawa:
iii) matakwaji; mahitaji; haja.
Kila seti ya maneno ina maana zinazokaribiana. Mifano ya matumizi inapokosekana, wanafunzi wa Kiswahili wanaweza kukosea kuyatumia vizuri katika lugha au kupata maana yake.
Sinonimu zieleze maana ya kidahizo
Sinonimu hazina budi kueleza maana ya kidahizo. Baadhi ya sinonimu katika KKS hazina maana sawa na vidahizo zinazovifafanua. Kwa mfano walau inafafanuliwa na: hata kama, japo na ingawa. Iwapo maneno haya ni sinonimu, hayana budi kubadilishana nafasi kama vile kuondoa hata kama na kuingiza walau badala yake.
(9)
(a) Hata kama watakubali, sidhani kama watasema kuwa waliteka nyara teksi mbili.
(b) Mimi nitahakikisha kuwa haki inatendeka hata kama polisi haitaki kunisaidia.
(c) Nitawatafuta hata kama itakuwa sababu ya kifo changu.
(d) Hata kama akinioa nitakuwa nikiona haya kutembea naye.
Walan haiingii katika sentensi hizo. Isitoshe. haiwezekani kuweka walau badala ya ingawa katika sentensi zifuatazo:
(10)
(a) Mimi sikupenda kabisa kujiingiza katika mambo haya ingawa niliyajua.
(b) Ingawa kwa sasa nasikitika na kujuta kufanya kitendo hicho, lakini sijilaumu.
(c) Alifika mpakani kwenye saa moja nusu ingawaje aliambiwa Rais angefika hapo saa tatu.
Sinonimu japo ndiyo inayotoa maana ya walau mara moja. Katika mfano ya (11) walau inaweza kukaa vizuri badala yajapo:
(11)
(a) Kwa nini wasitoe taarifa hiyo japo kwa siri.
(b) Lakini jaribu kula - japo kidogo shikashika hivyo hivyo.
Ingawa ijapokuwa/japokuwa hayatolewi kama sinonimu za walau ni dhahiri katika mifano ya (12) kwamba zina maana ya walau:
(12)
(a) Sasa sadfa imemletea hahati nzuri ili kumpoteza ijapokuwa kwa uchache. ijapokuwa kwa muda - kwani bila ya Maimuna, furaha ya Maksudi haikutimilika.(b) Wakati huo naweza kukuaminisha kwenda japokuwa kwa kusema nacho kiherehere cha moyo wangu.(c) Seyyid Ahmed. naamini ulikuwa huyajui mambo haya yalivyojiri; lakini sasa unayajua japokuwa kijuujuu tu kwa muhtasari wake.
Sinomimu angalau na lau pia hukaribiana sana kimaana na walau lakini hazitajwi kahisa katika kitomeo cha walau. Kukosekana kwa visawe kama hivyo kunakifanya kidahizo walau kisieleweke barabara maana yake.
Sinonimu Zijalizwe na Mifano ya Matumizi
Sinonimu zinazofasili kidahizo zijalizwe na mifano ya matumizi badala ya kuorodheshwa tu zenyewe. Kwa mfano, ikiwa kweli walauina maana ya hata kama na ingawa, ingelifaa mifano ya matumizi itolewe kudhihirisha vivuli hivyo vya maana ya walau. Lakini mfano mmoja tu ndio unaotolewa. na wenyewe unaeleza tu maana ya walau inayokarihiana na maana ya japo.
(13) Kama huna shilingi tano basi nipe walau mbili.
Mifano ya matumizi ya vidahizo si jambo la ziada au pambo tu ni sehemu muhimu ya fasili ya kidahizo mahsusi. Vivyo hivyo, kwa kidahizo afiki chenye maana tatu: 1) kubali 2) kubaliana 3) faa. Ni bora kila kivuli cha maana kieleze kwa sentensi inayodhihirisha waziwazi maana yenyewe.
Maana za Kisarufi za Vidahizo
Fasili za Nomino
Pamoja na kutoa tasili za nomino na kuonyesha ngeli zinamokaa twapaswa pia kuonyesha vile vigezo au sifa ambazo hutawala namna zinavyotumika katika muundo wa Kiswahili ili kumwezesha mtumiaji wa KKS kuendeleza na kupevusha weledi wake wa matumizi ya nomino mahsusi katika sarufi ya Kiswahili. Sifa za kuzingatia hapa ni maelezo kuhusu miundo ya vipashio mbalimbali vya kisintaksia. Sifa hizo za kisintaksia hutambulisha vipashio vinavyoweza kufuatana kimantiki na vile visivyoweza kufanya hivyo.
Kwa mfano, sifa za kuwa hisivu zina umuhimu wa kisarufi katika Kiswahili. Baadhi ya vitenzi vinabeba tu viwakilishi vya nomino yambwa ikiwa ni hisivu. Mifano ya vitenzi vyenye mtindo huo huonyeshwa katika mifano ifuatayo:
(14)
(a) Macho yalikuwa yamemwiva
(b) Punde si punde. Ema alijirudi.
(c) Alimpita mkewe kwa umri wa miaka kumi na minne.
(d) Gauni ile ilimkaa vyema
Hivyo itasaidia sana KKS ikiziwekea msimbo (his) nomino hisivu.
Umoja na Wingi
Nomino nyingi zinaonyesha maumbo ya umoja na wingi yakiwa yamefungamana na viambishi vya ngeli. Kwa hivyo hakuna haja ya kutaja hali ya umoja na wingi kwa kila nomino isipokuwa kwa nomino za ngeli ya 9 - 10 ambazo hazibadiliki umbo zikiwa katika umoja au wingi. Mathalani, zipo nomino chache kama nyama ambayo hutumika katika umoja au wingi kama katika mifano ifuatayo:
(15)
(i) Nyama imeoza
(ii) Nyama zimeoza
Ni bora kuziwekea alama zote mbili za Umoja na Wingi (U/W) nomino kama damu na nyama. Pia zipo nomino za ngeli ya 9-10 ambazo zinatumika katika umoja tu: chai, sukari, chumvi, n.k. Hizi pia zapaswa ziwekewe alama (U). Na nomino nyinginezo ambazo hutumika tu katika wingi, kama vile: maziwa, mate, masurufu pia ziwekewe alama ya (W).
Kwa vile ni jambo la kawaida kwa nomino kuwa vivumishi vya nomino nyingine hakuna haja ya kuziwekea alama ya kuzitambulisha nomino zenye uwezo wa kutenda hivyo kwa sababu ni nyingi sana, kama vile: kivumishi arifu, nomino yambwa, baba mzazi, mame mtu, kishazi rejeshi, paka shume, askari kanzu, n.k. Itatosha tukitoa tu mifano michache katika vitomeo vya vidahizu vinavyohusika.
Lakini zipo numino ambazo huwiana na vijalizo maalum ambavyo vyaslahili kuelezwa kwa msimbo katika vitomeo mahsusi. Mara nyingi vijalizo vinavyotawaliwa na nomino huwa ni sentensi ya aina ya kwamba kama tunavyoona katika mifano namba (16) (nomino tawazi zimechapwa kwa herufi nzito):
(16)
(a) Ni uwongo kuwa tunataka kumtoa
(b) Hivi hamna habari kama ninakuja leo?
(c) Alikuwa na imani ya kuwa kutofanikiwa ni haki.
(d) Tunataka kuwa na hakika kuwa anajua kwamba vita siyo lelemama
(e) Ni kweli kuwa sasa mamia ya askari wanakimbia jeshi kusalimisha maisha yao.
(f) Kwa msichana kurudishia kumwuliza mvulana jina ni dokezo kuwa anampenda.
Nomino zilizochapwa kwa herufi nzito na nyinginezo zinazowiana na sentensi za aina ya kwamba zafaa ziwekewe msimbo kama (+ kwamba S). Lakini nomino viarifu haziteui aina moja tu ya vijalizo; sentesi namba (17) yaonyesha kijalizo cha aina nyingine.
17. Tuwe vielelezo kwa wengine.
Hivyo. nomino kama kielelezo yafaa ziwekewe msimbo kama (+ kwa PN) nomino ruhusa pia hufuata suluhu ya kikwake kama unavyoona katika namba (18):
18. Yeyote atakayekuja ana ruhusa ya kuingia ndani amngojee.
Kufuatana na mfano huo ruhusa yaweza kupewa mshnbo (+ a FN): ila tu labda hakutakuwa na haja ya kufanya hivyo kwa vile karibu kila nomino huweza kuwiana na vivumishi vya (+ a FN).
Taarifa za Kisaruifi za Vivumishi
Vivumishi vingi hutokea baada ya nomino zinavyoeleza katika FN, na pia baada ya kitenzi. au baada ya kitenzi na yambwa yake. Hiyo ni miktadha yake ya kawaida kwa hivyo hakuna haja ya kuviundia msimbo maalum vivumishi vinavyo utekeleza mtawanyiko huo wote. Vivumishi ambavyo vinajifungia katika nafasi moja kimtawanyiko ndivyo vinavyostahili kuwekewa msimbo. Kwa mfano vivumishi kama: kila, a/kina, takriban, na baadhi ya hutangulia nomino siku zote.
Vivumishi vingi kiasi pia hutumika kama viarifu baada ya vitenzi vishirikishi. Na katika mazingira hayo baadhi ya vivumishi pia hujiteulia vijalizo. Tunawajibika kuviandikia vivumishi vinavyotenda hivyo misimbo inayoonyesha vijalizo mahsusi. Kwa mfano, kivumishi tayari kinateua vijalizo vya (ku S) tu kama katika sentensi namba (19):
(19) Na sisi tulikuwa tayari kukubali usuluhishi.
Hivyo twapendekeza kiandikiwe msimbo: (+ ku S) Vivumishi kama mtovu na mvivu vinateua sulubu nyingine ya ujalizishaji kama tunavyoona katika mifano namba (20)
(20)
(a) Hakuna mtovu wa Fedha
(b) Alikuwa mvivu wa masomo
Kufuatana na hayo tungeweza kupendekeza kuwa kuwepo msimbo (+ a N). Lakini kwa vile karibu nomino zote zaweza kupatana na vijalizo vya aina ya(- a (FN, KL) haifai kuziwekea msimbo.
Vivumishi wazi na dhahiri pia huteua sulubu sawa za ujalizishaji kama katika namba (21):
(21)
Ni [ wazi ] kuwa bado kuna watu wengi wasiojua dhahiri kusoma na kuandika.
Vivumishi kama hivyu sharti viandikiwe msimbo (+ kwamba S).
Taarifa za Kisarufi za Vitenzi
Vitenzi vikuu vina sifa madhubuti za kiwiano ambazo zinaviwezesha kutawala, au kuathiri uteuzi wa mafungu mengine yanayotokea katika sentensi zinazohusika. Na kwa sabahu ya tabia hiyo ya vitenzi, twapaswa kuviainisha au kuvitambulisha kutuatana na kigezo cha idadi na aina ya FN na viarifu vingine ambavyo vyaweza kutokea pamoja na vitenzi mahsusi katika sentensi. Hata hali ya kitenzi kujitegemea katika sentensi inakuwa na umuhimu kisintaksia. Inafuatia kwamba cunawajibika kuuelezea uhusika wa vitenzi kwa mfumo kamili wa misimbo.
Kwa mfano, katika kitomeo cha kidahizo kama toroka, pamoja na kuonyesha kuwa ni kt kuna haja ya kuongezea kuwa ni kitenzi kisoelekezi kwa msimbo kama (SOEL). Msimbo huo sharti uonyeshwe kwa vitenzi vyote visoelekezi, k.v. lala, pona, choka, ishi, lia, weweseka, garagara, tahayari, barizi, furukuta, n.k. Aidha, vitenzi elekezi ambavyo sharti vifuatwe na yambwa tendwa inafaa vionyeshwe kwa msimbo (EL). Na kwa vile vitenzi elekezi hufuatwa na yambwa au vishazi ambavyo pia vyaweza kufuatana na vijenzi vya aina nyingine tunawajibika kuunda misimbo zaidi kuelezea habari kuma hizo.
Vitenzi vikuu vingi havituatwi moja kwa moja na vijalizo vya vielezi au nomino arifu, lakini vipo vichache ambavyo hufanya hivyo kama inavyoonyeshwa katika mifano iliyoko katika namba (22):
(22)
(a) Ugua pole. (KL)
(b) Kaa salama
(c) Nenda salama (KL)
(d) Umekuwa tajiri (N arifu)
Msimbo (+ KL /N ar.) utavifaa vitenzi vya aina hii.
Vitenzi vingi zaidi huvipokea vijalizo vya Nomino aritu (N arifu), vivumishi, na vielezi vikiwa vinaandamana na yambwa fulani (iwe yambwa jirejee au ya kawaida) kama katika mifano namba (23):
(23)
(a) Kwa nini unatufanya wajinga? (N arifu)
(b) Ugomvi huo ulimwacha mnyonge na mchovu (Narifu) na (kv)
(c) Anajiona mkubwa (kv)
(d) Suti ile ilimchukua vyema (kl)
(e) Kutwa siku ile Kipwerere alikuwa akijihisi vibaya vibaya (kl)
(f) Alizoea kujiweka kimbelembele (kl)
Vitomeo vya vitenzi -fanya, -acha, -ona, -chukua, -hisi, na -weka vitastahili kuandikiwa mishnbo inayoonyesha kivuli cha maana na matumizi haya. Itakuwa kama ifuatavyo:
(+ yamb. + N arif/kv/kl)
Baadhi ya vitenzi huwa na vijalizo vinavyokuwa sentensi. Kiswahili kina aina kuu tatu za sentensi jalizishi. Na aina hizi tatu tutazitaja kwa misimbo maalum:
i) Vijalizo vya ku - (ku S)
ii) Vijalizo vya - e (-e S)
iii) Vijalizo vya kwamba (kwamba S)
Vitenzi vinavyoandamwa na vijalizo vya sentensi ni kama vinavyoonyeshwa katika namba (24).
(24)
(a) Alimwahidi kuwa nyuma yake.
(b) Niliwaamuru askari wangu waifungue reli
(c) Mwalimu ametueleza sana kwamba majina kama haya yanawadhalilisha wanawake.
Vitenzi ahidi, amuru, na eleza vitaandikiwa misimbo kama inayofupishwa .ifuatavyo: (+ yamb. + ku S/-e S/kwamba S) Mifano inayoonyeshwa katika data (25) inadhihinsha haja ya kuingiza msimbo kama (+ sw. S); yaani sentensi ya swali. katika mfumo wa misimbo inayoelezea vitenzi kama uliza, -ambia, jua, -ngojea. -staajabu n.k.
(25)
(a) Stella aliuliza kwa nini walitaka kumwua mama yake.
(b) Hatuna tena tatizo la kuwaambia watu wenye akili duniani m nini kimetokea.
(c) Unajua ni wangapi ulimwenguni wanaangamizwa kila mwaka na tabia kama hiyo?
(d) Mganga napenda kujua ni kitu gani kinachomdhuru mtoto wangu.
(e) Haijulikani vipi bibi huyu anaishi.
(f) Alingojea lini bahati ingalimsadifia uhuru huo.
(g) Alistaajabu ni kwa sababu gani Jero amteue yeye kati ya wasichana wote wale.
Sulubu za vijalizo vinavyovitambulisha vitenzi ni nyingi na hatuwezi kuzitaja zote katika makala hii fupi. Pia vigezo vinavyoelezea nomino na kivumishi kipekee ni vingi na hatungeweza kuvichambua kikamilifu kwa sasa. Hata hivyo natumaini kwamha maoni ambayo nimeweza kutoa yametudhi- hirishia haja ya kuingiza maelezo kama hayo katika KKS ili ijitosheleze zaidi. Katika makala hii fupi tumeonyesha kuwa inatuhidi kuzingatia taarifa za kisemantiki na kisarufi ili kupata utoshelevu wa fasili za vidahizo.
MAREJEO
Leech, G.N. 1980 Semantics and Pragratics. Amsterdam: J. Benjamins.
TUKl 1981. Kamusi ya Kiswahili Sanifu. DSM: OUP.
TUKI. 1990 Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. DSM: Educational Publisber and Distributors Ltd.