Vipengele Vya Kisarufi Katika Kamusi YA Kiswahili Sanifu Utangulizi





Vipengele Vya Kisarufi Katika Kamusi YA Kiswahili Sanifu

Utangulizi
Kuzungumzia vipengele vya kisarufi katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu ni kuzungumzia hasa suala zima la uambishaji katika Kiswahili. Katika msamiati wa Kiswahili kama ilivyo katika lugha nyinginezo za kibantu kuna baadhi ya maneno ambayo hayabadiliki kimaumbo katika mazingira yote, kwa mfano:
(1)
"na"
(kiunganishi)

"kama"
(kihusishi)

"sana"
(kielezi)

"simba"
(jina)

"hodari"
(kivumishi)
Maneno kama haya hayanyambuliki na hayabadiliki kimaumbo kwa kuambishwa. Kwa hiyo maneno ya aina hii yanaingizwa kama yalivyo katika Kamusi. Lakini baadhi ya maneno mengine kama nomino, vitenzi na viambishi m yale yanayojulikana kuwa ni maneno yaliyonyambuliwa. Maneno ya aina hii hubadilika kimaumbo kwa kuambishwa. Uambishaji ni kipengele cha kisarufi kinachowatatiza watunga kamusi. Kwa maneno mengine, kushughulikia leksimu ni tatizo kubwa katika utungaji wa Kamusi ya Kiswahili, kama hali ilivyo katika lugha nyingine za Kibantu.
Jambo la msingi ni jinsi ya kuandaa leksimu za lugha hasa nomino na vitenzi katika kamusi. Suala hilo linatokana na hali ya mfumo wa kimofolojia wa lugha za Kibantu. Ngeli za nomino na mfumo wa unyambuaji wa vitenzi ni tatizo kubwa kwa mtunga kamusi wa Kiswahili kuamua leksimu zipi zinazoorodheshwa katika Kamusi na kwa njia ipi. Mfumo wa ngeli za nomino unazigawanya nomino katika ngeli kwa msaada wa viambishi awali vya nomino na mfumo wa unyambuaji wa vitenzi unaunda vitenzi vipya kwa msaada wa viambishi tamati vya unyambuaji. Uundaji wa nomino na wa vitenzi ni njia pekee za unyambuaji katika lugha. Majina yanaweza kuundwa kutokana na mashina ya majina au ya vitenzi au ya vivumishi, k.m.
(2)
mtoto
utoto

-soma
msomi

-fupi
ufupi
Kadhalika, vitenzi vinaweza kuundwa kutokana na mashina ya vitenzi au ya majina au vivumishi, k.m.
(3)
-kata
kukatisha

taifa
kutaifisha

-nene
kunenepa, n.k.
Maneno kama haya hayana budi yashughulikiwe ipasavyo katika kamusi kutokana na nadharia bainifu inayohusu leksimu. Tutajitahidi hapa kutazamajinsi suala la uambishaji na leksimu linavyojitokeza katika Kiswahili najinsi lilivyoshughulikiwa katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu (1981). Baada ya kuipitia Kamusi hiyo, ni dhahiri kuwa suala la msamiati (lexicon) halikushughulikiwa kwa kina na uwazi. Matokeo yake ni kwamba suala la uundaji wa maneno kwa ujumla halikushughulikiwa ipasavyo. Sababu ya hali hii ni kwamba hadi miaka ya 1970 nadharia nyingi za kiisimu zilikuwa hazitilii sana maanani hali ya msamiati (lexicon). Lakini kwa sasa kuna nadharia ambazo hufafanua msamiati kwa kina zaidi. Kwa mfano nadharia ya kileksika imeonekana kwa wanaisimu wengi kama mojawapo ya nadharia ambazo hufafanua msamiati ipasavyo. Msamiati unajitokezakuwa sehemu muhimu yautafiti na inakubalika sasa kuwa mofolojia nyambuaji ni ya kileksika. Dai kubwa katika nadharia hiyo ni kwamba kila faridi husika katika kuunda vipashio viambishi vipya vya kileksika ni sehemu ya msamiati.
Kwa hiyo viambishi awali na tamati ni muhimu sana katika uundaji wa faridi mpya (new items) za kileksika katika lugha ya Kiswahili. Ndiyo maana ni muhimu kupitia kwa muhstasari kanuni muhimu za uambishaji katika Kiswahili.
Uambishaji wa Nomino au Uundaji wa Nomino kwa Uambishaji.
Maneno mengi hapa yanatokana hasa na mzizi au shina la kitenzi lililoambatishwa viambishi awali na tamati (vinyambuaji)
a)
kiambishi nyambuaji -i kinatoa maana ya utendaji
k.m (4)m-somi u- som-i
u - som - i
Kiambishi hiki kinaweza kujitokeza baada ya kinyambuaji -aj- na kuleta maana ya tendo la kudumu au la kurudiarudia, k.m.
(5)
sema
m-sem-aj-i

omba
u-omb-aj-i
b) kiambishi tamati -u chenye kumaanisha hali (state), k.m.
(6)
tulia
m-tuliv-u
u-tuliv-u
c) kiambishi tamati -o. Kina maana kubwa mbili: utekelezaji wa tendo na matokeo yake, k.m.
(7)
ziba
ki-zibo

enda
mw-end-o
d) kiambishi tamati -e. huwa na maana ya kutendewa jambo au tendo linalofanyika, k.m.
tuma
m-twn-e
kata
m-kat-e
Aina nyingine za unyambuaji
a) Baadhi ya maneno vinyambuo huundwa kwa kuambatishwa kiambishi awali cha nomino kwenye shina la kitenzi, k.m.
(8)
-ganga
m-ganga

-wiwa
m-wiwa

-tata
ma-tata
b) Maneno maungamfu
Maneno ya aina hii huunda hasa kundi la kisintaksia litokanalo na kuambatisha kiambishi awali cha ngeli kwenye shina la kitenzi pamoja na yambwa; k.m.
(9) - uza samaki mw- uza samaki - la
riba ni - ia riba
Maneno mengine maunganifu huundwa kwa kutanguliza neno - ana kwa nenojingine.
(10)
mw - anafunzi
mw - anachama
Maneno machache sana huundwa pia na kivumishi kuu ambacho hujitokeza katika umbo lilojisawazisha kimatamshi kama -ku-likiwa sehemu ya kwanza ya neno unganifu husika,
(11) m - kufunzi, m-kulima
Aidha kuna pia umbo la zamani la kiambishi * kuru (litokanalo na Mame Bantu) * kodo ambalu bado hutumika katika neno mkurugenziambapo genzi hutokana na kinyambuaji -i ya gend-a ambayo ni umbo la kale la - enda. Maneno mengine maunganifu hutokana tu na kuunganisha maneno mawili fulani,
(12)
gugu mwitu
- askari kanzu
Uradidi pia hujitokeza kwa nadra katika unyambuaji wa nomino na kuleta maana ya mkazo,
(13) ki -zunguzungu
Uambishaji wa vitenzi
Uundaji wa vitenzi unahusu uambatishaji wa Viambishi tamati kwenye mzizi wa kitenzi. Viambishi vinavyohusika hapa ni viambishi tamati nyuambuaji. Mzizi wa kitenzi hufuatwa na kiambishi tamati kimoja au zaidi kwa utaratibu mahsusi. Katika muktadha fulani, mizizi ya vitenzi iliyovutika na kiambishi tamati kimoja au zaidi inaweza kuwa msingi wa mifululizo mipya ya vinyambuaji; maumbo kama haya hujulikana kuwa m mashina ya vitenzi.
(14)
piga
pigwa
piganisha
piganishwa
Viamhishi tamati ni vingi lakini ni muhimu kuvichunguza kwa makini ili kuvishughulikia ipasavyo katika kamusi. Kabla ya kutazama taratibu za unyambuaji ni muhimu kutazama kwanza mfumo wa mzizi wa kitenzi katika Kiswahili. Umbo la msingi la mzizi ni:
(a) - KIK - (konsonanti - Irabu - Konsonanti) -kat- na vibadala vyake:
(b) - K n IIK - (Konsonanti- nusu Irabu-Irabu -konsonanti) -twet-
(c) -KINK (Konsonati - Irabu - Nazali Konsonanti) -vimb - n.k.
Kuna pia mizizi mifupi, kama:
(d)
K-
ku - f - a
(e)
- I-
ku - u - a
(0
-IK-
ku - ib - a
(g)
-INK-
ku - imb - a n.k.
Taratibu za unyambuaji
Uradidi
Baadhi ya mizizi pia hujitokeza katika umbo la kuradidiwa na hutoa maana ya kusisitiza tendo, k.m.
(15)
(peta)
pepeta

(gota)
gogota
Uradidi hapa unahusu silabi ya kwanza ya kitenzi.
Viambishi tamati
Viambishi hivi hujipachika kati ya mzizi na mofimu irabu ya mwisho wa kitenzi.
(a) kiambishi tamati -i- /e- na vibadala vyake. Viambishi hivi:
(i) hudokeza kuwa jambo linatendwa kwa ajili ya mtu au kitu fulani na
(ii) huonyesha uelekezi wa jambo, au lengo lake, n.k.
(16)
pig-a
pig-i-a

sem-a
sem-e-a
(b) Kiambishi tendwa -w- Kitenzi kinatoa kauli ya kutendwa. Mifano:
(17)
pend-a
pend-w-a

pig-a
pig-w-a
(c) viambishi tendeka -ik-/-ek- na kibadala chao -k- kinachojitokeza baada ya irabu za juu za nyuma. Viambishi hivyo huonyesha kuwa jambo lipo katika hali fulani au katika hali ya uwezekano.
(18)
fany-a
fany-ik-a

zim-a
zim-ik-a

tend-a
tend-ek-a

raru-a
raru-k-a

bomo-a
bomo-k-a

fung-u-a
fungu-k-a
(d) Viambishi tendeshi -ish-/ - esh- na vibadala vyao (~iz~, ~ez~, ~z~) vinaonyesha kwamba kiima huvifanyiza au huvitendesha vitu (watu) fulani kuasilisha au kusababisha.
(19)
-imb-a
-imb-ish-a

ot-a
-ol-esh-a

-tuli-a
-tuli-z-a n.k
(e) Viambishi geuza kinyume -u-/-o- na vibadala vyao.
(20)
-pind-a
-pind-u-a

- shon-a
-shon-o-a

- tib-u
-tib-u-a
Katikajozi hizi, kilajozi ina mzizi ule ule. Lakini maana ya kila neno katika jozi ni kinyume ya nyingine. Lakini katika baadhi ya jozi maana siyo kinyume cha kitenzi asilia bali jambo Jinasisitizwa, k.m.
(21)
-kam-a
-kam-u-a

-song-a
-song-o-a
(f) Kiambishi tamati -am- hutoa maana ya kudumu ya hali za iambo fulani.
(22)
-kwa-a
kwa-am-a

-gand-a
gand-am-a
Katika baadhi ya vinyambuo mzizi wa msingi hautumiki tena, k.m.
(23)
-chutam-a
* chut-a

- tazam-a
* taz-a
g) Kiambishi tamati -at- cha mgusano, k.m
(24)
-fumb-a
-fumb-at-a

-pdk-a
-pak-at-a

-kumb-a
-kumb-at-a
h) Kiambishi tamati -an- cha kufanyana au kutendana, k.m
(25)
-ju-a
-ju-an-a

-pend-a
·pend-an-a
i) Kuna pia dalili za kuwepo kwa kiambishi tamati -p-kinachotoa dhana ya kuweka jambo katika hali fulani, k.m.
(26)
-nene
-nene-p-a

-oga
-og (o)-p-a
Uradidi wa Sbina la Kitenzi
Uradidi wa aina hii pia huonyesha kuendelea kwa jambo fulani na kutiwa mkazo kwake, k.m.
(27)
tang-a
-tang-a tang-a

lew-a
-lew-alew-wa
Kama tulivyoona hapo juu viambishi vya unyambuaji vinahitaji vitomeo vyao pekee katika msamiati ambapo taarifa ya kikategoria. ya kinsintaksia, ya kisemantiki na taarifa nyingine ya kileksika zitabainishwa.
Jinsi ya kushughulikia viambishi nyambuaji na vinyambuaji vya kileksika katika Kamusi.
Ilionyeshwahapojuu kuwa viambishi nyambuaji vitazamwe kama leksimu kama ilivyo kwa mofimu nyingine ambazo siyo. Matokeo yake ni kwamba upangaji dhahiri wa faridi nyambuaji katika kamusi unahitaji pia upangaji bainifu na sisisi wa viambishi nyambuaji ili kuwezesha kutoa taarifa halisi juu ya vipengele vya kisintaksia, vya kileksika na vya kisemantiki vya faridi nyambuaji. Kwa hiyo, jitihada ya kufafanua mofolojia ya uambishaji haina budi kuchukulia viambishi nyambuaji kama msingi wa uundaji wa maneno mapya. Vinyambuo vitokanavyo na uambishaji wa nomino vinaweza kutolewa kama vitomeo huru kama ilivyokuwa katika Kamusi ya Kiswahili, lakini viambishi nyambuaji vikiwa vimechapwa katika alama maalum kama herufi za italiki. Maelezo dhahiri kuhusu unyambuaji, wa maneno yatoiewe katika utangulizi wa Kamusi. Kitomeo cha nomino nyambuaji kitakuwa kama ifuatavyo:
(28) m- sem- aj-i n.k.
Msingi wa uundaji wa vitenzi ni uambishaji wa viambishi tamati. Viambishi nyambuaji vya vitenzi ndivyo vinavyofanya kazi hiyo. Kila kiambishi tamati kitachukuliwa kama leksimu pamoja na kitomeo chake pekee. Pia itakuwa vizuri kuorodhesha chini ya kila kitomeo viambishi tamati vyote vinavyoweza kujitokeza na umbo hilo na kuunda neno jipya. Kwa mfano, chini ya som-a, viambishi tamati -w-, esh-, -ek-, -e- n.k vitaorodhesha. Lakini ikumbukwe kuwa kila unyambuaji unatoa leksimu mpya. Kutokana na hali hiyo ni muhimu kubadili kabisa jinsi ya kuandaa Kamusi ya Kiswahili. Majina yangeorodheshwa pamoja na viambishi vyao, vitenzi na viambishi viorodheshwe kwa msaada wa mashina yao na viambishi nyarabuaji vitaorodheshwa kiutaratibu wa sisisi kama leksimu tofauti. Viambishi nyambuaji vyote vitatofautishwa na faridi nyingine zisizo viambishi kwa kuvichapisha kwa alama pekee (k.v. italiki k.m.). Lakini kwa sasa mpangilio wa vitomeo katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu utaendelea lakini pamoja na mabadiliko kwa kuzingatia nafasi ya uambishaji na unyambuaji. Baadhi ya mapendekezo yetu ni kama yafuatayo:
(a) Kwanza, ingefaa viambishi vyote viandikwe kwa chapa tofauti na mzizi asilia wa neno ili kubainisha leksimu
(b) Kuhusu vitenzi. mzizi na irabu ya mwisho wa kitenzi kwa chapa ya pekee iliyo tofauti na ile ya viambishi nyambuaji. Katika kitenzi, mzizi wamsingi ni ule ambao ukiunganishwa na irabu ya mwisho ya kitenzi unatoa maana ya msingi ya kitenzi hicho. Irabu ya mwisho kwa hiyo itabidi isiambatishwe na kiambishi au sehemu yoyote ya kiambishi tamati nyambuaji, k.m
Nomino
(29)
m tu
m-som-i
m-som-aj-i
tunda/ma-tunda n.k.
Vivumishi (sifa)
Mashina tu ya vivumishi vya sifa yataingizwa yakitangutiwa na kistari kama kivumishi husika kmapatanishwa kisarufi, k.m.
(30)
- kubwa
- refu
lakini hodari n.k.
Vitenzi
Itakumbukwa kwamba katika Kiswahili irabu za mwisho za vitenzi visoukomo ni zifuatazo:
(31)
-a
-kat-a

- u
-abud-u

- i
-fik-i

- e
-stareh-e
Tuliona umuhimu wa kuchambua kwa kina mfumo wa mizizi ya vitenzi na wa viambishi nyambuaji vya Kiswahili. Hapa tutatoa tu kwa mifano baadhi ya mapendekezo yetu juu ya kushughulikia masuala hayo.
(32)
-kat-



-kat-ish -a-a

ahir -

-kat-an-a
fung-


-kat-w-a n.k
-fung-a
-ahiri-ish-a


-fung-i-a
-erevu-erevu-k-a


-fung-ish-a



-fung-an-a



-fung-u-a



-fung-aw-a
an-a n.k.
Unyambuaji wa maneno kutoka Kiarabu ufanyiwe uchunguzi ili wasomaji wa kamusi waelewe kanuni zilizotumika.
Mifano:
idara f mudiri / mudiria
abiria / abiri
ibada / abudu
ridhaa / ridhi
Katiba/ katibu/mkataba/maktaba/mkutubi/ kitabu.
karimu/kirimu
maliki/malkia
ridhika/mtaaridhi
tabibu/tibu/matibabu
Tunajiuliza pia kuwa sta- na ta- ni viambishi au vipi k.m.
m - staarabu/ mwarabu!4
stashahada/shahada
stakabadhi/? kabidhi
tadaraki / madaraka
tabibu /matibabu
tafakari/fikiri
tafaraji /faraja
tahariri/kuhariri
taratibu/ratibu n.k.
4 Katika (nantiki hiyo, je tunaweza kupata jozi za aina ya:
* Mstaafrika/mwafrika?
* Mstazungu/mzungu?
Hitimisho
Tumeona kwamba vipengele vya kisarufi katika kamusi vinahusu uambishaji na unyambuaji katika uundaji wa maneno. Tumeona pia kuwa tatizo mojawapo la watunga kamusi za Kiswahili linatokana na kutofanya utafanuzi wa kina kuhusu mofolojia ya viambishi vya Kiswahili. Imebainika pia kuwa uundaji wa majina na vitenzi katika Kiswahili unashughulikiwa vizuri sana katika leksimu ambapo kanuni za kileksika zinazotawala viambishi nyambuaji zitadhihirishwabayana. Kwa sababu hizi uundaji wa maneno na wa vitenzi vya Kiswahili ni suala la kileksika. Kutokana na hali hiyo utaratibu wa kuandaa Kamusi ya Kiswahili hauna budi ubadilishwe ili viambishi nyambuaji viingizwe kama vipashio vya kileksika pamoja na vitomeo vyao pekee katika kamusi.
Biografia fupi
1. DUBOIS, J. na wengine 1973. Dictionare de linguistique, Paris, Librarie,
2. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili 1981. Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Dar es Salaam: Oxford University Press.
3. BOUQUIAUX, L. na TOMAS, J.M.C. 1976. Enquete et description de langues a tradition orole. Vol. 1 L' Enquete de terrain et l' analyse grammaticale. Paris: SELAF. 2 ed, 258 p.
4. POLOME, E.C. 1967. Swahili Language handbook. Washington: Center for Applied linguistics 232 p.
5. KAPINGA, M.C. (Mtayarishaji) 1983. Sarufiya Maumbo ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.
6. NKWERA, F.M.V. 1985. Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: TPH.
7. Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, ISTILAHI (Isimu) mswada ambao haukuchapishwa.
8. BWENGE, M C.M.T., "Affixional Morphology and Dictionary design with particular reference to Swahili lexicography" (Unpublished) Exeter University.
Powered by Blogger.