UTAFITI :UTAFITI: UFASIHI SIMULIZI KATIKA RIWAYA ZA SHAABAN ROBERT: Mifano kutoka Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad


SURA YA TANO 

MUHTASARI, 

HITIMISHO NA MAPENDEKEZO 

5.0 Utangulizi 

Sura hii ni ya mwisho ambayo inatoa muhtasari, hitimisho na mapendekezo ya utafiti huu. Sura hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni; sehemu ya kwanza inahusu muhtasari, sehemu ya pili inahusu hitimisho la utafiti huu na sehemu ya tatu ni mapendekezo ya utafiti huu. 5.1Muhtasari Utafiti huu ulilenga tathmini ya mwingilianomatini katika utunzi wa Shaaban Robert kwa kuangalia vipengele vya Fasihi Simulizi ndani ya riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad Kuchunguza ufasihi simulizi katika riwaya za Shaaban Robert kwa kutumia mifano ya riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti binti Saad, ili kuona ni jinsi gani msanii huyo anatumia vipengele vya fasihi simulizi kama mali ghafi ya utunzi wa riwaya ya Kiswahili. Vile vile kubaini jinsi mtunzi huyo anavyofumbata mbinu ya mwingilianomatini katika kazi zake za fasihi na namna mbinu hiyo inavyotumika kuibua dhamira za riwaya hizo. Utafiti huu ulikuwa na malengo mahsusi mawili ambayo yalijibiwa na maswali mawili. Malengo hayo ni; Kubaini vipengele vya fasihi simulizi vinavyojitokeza katika Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad na kubainisha dhamira zinavyowasilishwa na matumizi ya vipengele vya fasihi simulizi katika riwaya za Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Tatizo la utafiti huu limetokana na uelewa wa mtafiti baada ya kupitia mapitio mbalimbali na kubaini kuwa hakukuwa na utafiti wa kina ambao umejikita katika kuchunguza na kubainisha vipengele vya fasihi simulizi ndani ya fasihi ya fasihi andishi 79 kwa kutumia nadhari ya mwingilianomatini katika kazi za riwaya. Kwa hiyo, tatizo la utafiti huu lilikuwa ni, kuchunguza vipengele vya fasihi simulizi vinavyojitokeza katika riwaya za Shaaban Robert ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad, ili kubaini jinsi vipengele vipi vya fasihi simulizi vilivyotumiwa na mtunzi kama mali ghafi ya utunzi wa riwaya ya Kiswahili. Hivyo utafiti huu umetumia nadharia ya mwingiliano matini katika kuchunguza, kuchambua, kubainisha na kujadili data na matokeo ya utafiti huu. Katika utafiti hii mbinu za utafiti zimejadiliwa kwa kina katika sura ya tatu. Katika sura hiyo, imebainishwa kuwa eneo la utafiti huu ni Dar es salaam (Chuo Kikuu Huria) na Pemba (Zanzibar). Vile vile kutokana na maeneo hayo ilikuwa rahisi kuwapata watu ambao waliwahi kuziangalia kazi zake, kwa kuandika makala au kuzifanyia utafiti. Kwa hiyo tulitegemea kupata data za kutosha. Kwa upande wa Pemba itakuwa rahisi kupata data za mwandishi wa kitabu cha Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad, kwasababu vitabu hivi viliwahi kutumiwa mashuleni na bado vinatumika na pia watu wa kawaida wanaendelea kuvisoma. Hivyo, Dar es Salaam na Pemba ndio maeneo tuliyoyaona kuwa ni muhimu na kufaa kukamilisha utafiti huu. Walengwa katika utafiti walikuwa ni wanafunzi wa umahiri katika fasihi ya Kiswahili katika Chuo Kikuu Huria waliteuliwa kwa kigezo kuwa ni wanafunzi wanaosoma fasihi, wana maarifa ya nadharia za uchambuzi wa kazi za fasihi na pia wana ujuzi na maarifa katika matumizi ya nadharia na mbinu za uhakiki wa kazi za fasihi. Vile vile kigezo cha kuwa wanafunzi hawa wanasoma riwaya kwa Kiswahili kililifanya kundi hili kuwa ni rasilimali ya kutosha katika utoaji wa data za utafiti huu. 80 Walimu na wahadhiri wa fasihi wa muda mrefu ni kundi muhimu katika utafiti huu kwa sababu wao ndio wanaofundisha kozi ya fasihi, wana ujuzi na maarifa ya kutosha katika nadharia na vitendo kuhusu fasihi ya Kiswahili na uhakiki wa kazi za fasihi kwa jumla. Kwa upande mwingine, Walimu wa fasihi wa muda mrefu ni kundi muhimu katika utafiti huu kwa sababu wao ndio wanaofundisha kozi ya fasihi, wana ujuzi na maarifa katika nadharia na vitendo kuhusu fasihi ya Kiswahili na uhakiki wa kazi za fasihi kwa jumla. Vile vile uliwahusisha wazee na vijana wanaoishi nje ya eneo la Mkoani – Pemba, wazee ambao ni kawaida hutamba hadithi kwa vijana na pia vijana ambao hutolewa hadithi za kale, ambao huwa na uzoefu wa kutoa hadithi na wanosimuliwa kuweza kuhifadhi hadithi hizo na kusimulia wenzao. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kwa kutumia mbinu ya uteuzi wa madhumuni maalumu. Data za utafiti huu zilikusanywa kwa kutumia mbinu nne ambazo ni mbinu mbinu ya usaili, mbinu ya majadiliano ya vikundi, Mbinu ya Dodoso na Mbinu ya usomaji wa machapisho ilikuwa ni mbinu kuu ambayo iliyotusaidia kuchambua riwaya zote mbili na kubainisha mbinu ya mwingilianomatini ilivyotumika katika riwaya hizo. Vilevile mbinu ya dodoso, usaili na majadiliano ya vikundi zilitumika kama mbinu jazilizi ambazo zilitumika kujaliza data zilizopatikana kutoka katika mbinu kuu. Uchambuzi wa data za utafiti huu umefanyika kwa kutumia mbinu ya uchambuzi maudhui. Utafiti huu umetumia mbinu zisizo za kitakwimu katika kuwasilisha, kuchambua na kujadili data za utafi. 81 Kulingana na malengo ya utafiti huu maswali mawili yalijibiwa, ambayo yalitokana na malengo mahususi. Kwa hiyo matokeo ya utafiti huu ni kama ifutavyo. Swali la kwanza lililenga kubaini matumizi ya vipengele vya fasihi simulizi vinavyojitokeza katika Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad, kwa kutumia mbinu ya mwingilianomatini, vipengele hivi vimeonyeshwa katika jadweli nambari (2.). Aidha, Kubainisha dhamira zinavyowasilishwa na matumizi ya vipengele vya fasihi simulizi katika riwaya za Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Vipengele hivyo vimeonyeshwa katika jadweli nambari (3). Utafiti huu umebaini kuwa riwaya zote matokeo ya mapokeo simulizi ambayo msanii aliyapata kuhusu visakale vya fasihi simulizi ya Kiswahili. Masimulizi yametumika katika viatabu vyote viwili vya Shaaban Robert: Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Aidha, utafiti huu ulibaini kuwa matini zote ni matokeo ya mapokeo simulizi ya visakale vya fasihi ya Kiswahili. Pamoja na kuwa zote zimetokana na masimulizi lakini matini hizo zinatofautiana katika matumizi ya vipengele vya fasihi simulizi katika misingi na kanuni za utunzi. Hii ina maana kuwa, Adili na Nduguze na masimulizi ya visakale wakati Wasifu wa Siti Binti Saad msingi wake wa kutungwa kumsimulia mwanamke aliyekuwa maarufu Afrika Mashariki pamoja na Dunia ambaye alikuwa ni Siti Saad, na aliishi Zanzibar katika uhai wake. Kwa ujumla utafiti huu uligundua kuwa, riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad zinafanana katika vipenhele vya fasihi simulizi ijapokuwa havikutumika sawa sawa katika kuibua dhamira. 82 Halikadhalika riwaya hizi zimetungwa na mtunzi yuleyule, hivyo hiyo huweza kuwa ni miongoni mwa sababu zinazoleta mfanano wa karibu katika matumizi ya vipengele vya fasihi simulizi. Hii ni kutokana na kuwa mtunzi ameendelea kufumbata mbinu ya mwingilianomatini katika utunzi wake Utafiti huu ulibaini kuwa, mwingilianomatini ni mbinu ya utunzi wa Shaaban Robert kwa sababu mtunzi huyu anatumia fasihi simulizi ndani ya riwaya. Aidha, utunzi wake umedhihirisha kuwa ni matokeo ya athari ya mapokeo aliyoyapata kuhusu fasihi simulizi za Kiafrika hususani visakale. Utafiti huu unamtaja Shaaban Robert kama mwanamwingilianomatini ambaye anadhihirishwa na utunzi wa kazi zake za fasihi. Hivyo, mwingilianomatini ndiyo unampa upekee katika utunzi wa vitabu vyake. 5.3 Hitimisho Utafiti huu unahitimisha kuwa Shaaban Robert anatumia mwingilianomatini katika utunzi wake kwa kuingiza matini za fasihi simulizi katika utunzi wa riwaya ya Adili na Nduguze na Wasifu wa Siti Binti Saad. Katika riwaya zote mtunzi ameingiza vipengele vya fasihi simulizi ambavyo ni matokeo ya masimulizi na mapokeo ya visakale vya fasihi simulizi ya Kiswahili. Hii imetuthibitishia kuwa, mtunzi ameendelea kufumbata mbinu ya mwingilianomatini katika utunzi wa kazi zake za fasihi. Halikadhalika iligunduliwa na utafiti huu kuwa, mtunzi ameathiriwa na mapokeo simulizi ya fasihi simulizi, kwani riwaya zote mbili ni matokeo ya athari ya mapokeo simulizi ya ukweli katika Afrika. Hii inatokana na mtunzi kuchota malighafi yake ya kutungia riwaya hizi kutoka katika masimulizi hayo ya kimapokeo ya kusikia nayle yaliyotoka katika kinywa cha msimuliwaji wa kisa. Adili na Nduguze inatokana na 83 mapokeo simulizi ya kisakale cha ngano za wasafiri, na Wasifu wa Siti Binti Saad ni matokeo ya kisa cha kweli kilichowahi kutokea katika jamii ya watu Wazanzibar. 5.4 Mapendekezo Utafiti huu unahitimisha kuwa Riwaya ya Adili na Ndguze na Wasifu wa Siti Binti Saad ni Riwaya zinazotaka katika jamii yenye utamaduni mmoja. Utafiti huu, unapendekeza tafiti nyengine zifanywe katika kuchunguza ufasihi simulizi katika tanzu nyengine za fasihi andishi kama vile tamthiliya na ushairi. Hili litasaidia kuibua namna vipengele vya fasihi simulizu kama malighafi fasihi andishi. 84 MAREJELEO Balisidia, M. L. (Bi Matteru), (1987) “Tanzu na Fani za Fasihi Simulizi”: Mulika 19. TUKI: Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam. Bryman, A. (2004). Social Research Methods (Toleo la Pili - 2). Oxford: Oxford University. Chuachua na wenzake (2009). Shaaban Robert: Visa na Ukoloni, Katika Mulika. TUKI: Dar-es-salaam. Chuachua, R. (2011). Itikadi katika Riwaya za Shaaban Robert. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI): Chuo Kikuu Dar-es-salaam: Dar-es-salaam. Kenguru, P.J.M. (2013). Fasihi Simulizi katika kazi ya Utu Bora Mkulima, (M.A Kiswahili), Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya, Nairobi Kihore Y.M (1996). Kozi ya Maandalizi ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania: Dar-es Salaam, Tanzania. Kitula, M. (2010). Research Methodology for Postgraduate Students. The Open University of Tanzania: Dar-es-Salaam. Kombo, D. K. and Tromp, D. L. A. (2006). Proposal and Thesis Writing: Introduction. Paulines Publication Africa: Kenya. Kothari, C. R. (1990). Research Methods: Methods and Techniques. New Delhi: Wiley Eastern Ltd. Kothari, R.C. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques. New Delhi: New Age International (P) Limited, Publishers. Masebo J. A na Nyangwine (2004). Nadharia ya Fasihi Kidato cha (5) na Sita (6). Afro Plus Industries ltd .Dar-es Salaam: Tanzania. 85 Mateeru, M. L. (1976). Fani ya Hadithi na Riwaya: Makala katika kioo cha Lugha. Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam: Dar-es-salaam, Tanzanai. Msokilie, B. (1993). Miongozo ya Lugha na Fasihi: Uchambuzi na Uhakiki wa Riwaya. Dar-es- salaam University Press: Dar-es-salaam. Mulokozi M.M (1996). Utangulizi wa fasihi ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania: Dar-es Salaam Tanzania. Mulokozi M.M (2002). Tenzi Tatu za Kale. TUKI: Dar-es Salaam. Mulokozi, M. M. (1989). Tanzu za Fasihi Simulizi: Katika Mulika 21. TUKI: Dar- es Salaam. Mung‟eri, O. B. (2000). Utetezi wa Maandishi katika Fasihi: Nadhariya ya Shaaban Robert, Ripoti ya Tasnifu. Chuo Kikuu Nairobi: Nairobi, Kenya. Mwai, W. na Ndungo, W. (1991). Kiswahili Studies: Part Two. Nairobi: University of Nairobi. Ndugo C. M na Wafula R.M (1993). Nadharia ya Fasihi Simulizi (Kiswahili part III). The College of Education and External Studies: Nairobi. Ndugo C.M. na Wafula R.M. (1993). Tanzu za Fasihi Simulizi. University of Nairobi: Kenya. Ndungo, W. C. na Mwai, R. (1991). Misingi ya Nadharia ya Fasihi ya Kiswahili. Chuo Kikuu cha Nairobi: Nairobi, Kenya. Nkwera F.M.V (1979). Sarufi na Fasihi: Sekondari na Vyuo. Dae-es- salaam: Tanzania Publishing House. Ntarangwi, M. (2004). Uhakiki wa Kazi za Fasihi. Augustana College: Rock Island. Ponera, A. (2010). Athari za Ufutuhi katika Nathari za Shaaban Robert: Tasnifu ya Uzamili Chuo Kikuu Dodoma. Dododoma: Tanzania. 86 R, Shaaban (1951). Adili na Nduguze. Macmillan Publisher: London. R, Shaaban (1991). Wasifu wa Siti Binti Saad. Mkuki na Nyota Publisher: Dar es Salaam, Tnzania. Ruhumbika, G. (2003). “Tafsiri za Fasihi za Kigeni Katika Ukuzaji wa Fasihi ya Kiswahili.”Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili III (2003). TUKI: Dar-es-Salaam. Sengo T.S.Y na Kiango S.D (1977). Hisi Zetu. TUKI: Dar-es salaam, Tanzania. Sengo, T. S. Y. (1975). Shaaban Robert: Uhakiki na Maandishi Yake. Foundation Books: Nairobi. Senkoro, F. V. (1976). Utamaduni katika Riwaya za Kiswahili. TUKI: Dar-es-salaam. Senkoro, F. V. (1982). Fasihi. Press Publicity Centre: Dar-es-salaam. Taib, A. H. (2008). Mkabala wa Kiislamu katika Uchanganuzi na Uhakiki wa Fasihi ya Kiswahili. CHAKAMA: Dar-es-salaam. Taib, A. H. (2009). Maisha ya Shaaban Robert na Falsafa yake katika Maandishi. Katika Mulika. TUKI: Dar-es-salaam. TAKILUKI (1981). Hapa na Pale. TAKILUKI: Zanzibar. TUKI (1985). Journal of Institute of Kiswahili Research. TUKI: Dae-es- salaam. TUMI (1988). Kiswahili Sekondari. TUMI: Dae-es Salaam. Wamitila, K. W. (2002). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na Vipengele Vyake. Phonex Publisher Limited: Nairobi, Kenya

Powered by Blogger.