Theobald Mvungi: Raha Karaha
SURA YA TANO
Kitangulizi
Raha Karaha si diwani pekee ya Mvuogi kwani ameshaandika pia diwani nyingine, Chungu Tamu, (TPH, 1986) ambayo inashabihiana sana kifani na kimaudhui na hu ya Raha Karaha.
DHAMIRA KUU
Katika diwani ya Raha Karaha mshairi ameshughulikia dhamira kadhaa ambazo zinahusu masuala mbalimbali ya jamii, uchumi, siasa, na utamaduni. Kati ya hizo, muhimu ni:
1. Kupmga dhuluma na kutetea haki za wanyonge
2. Upotofu na uongozi mbaya
3. Umuhimu wa kazi na uwajibikaji
4. Marudi na maonyo
5. Mapenzi
6. Maana na dhima ya sanaa
7. Maana ya maisha
8. Tambo
9. Mengineyo.
Tutazichambua dhamira hizi moja baada ya nyingine, kabla ya kuyaangalia masuluhisho anayoyatoa mshairi kuhusu migogoro iibukayo katika dbamira hizo. Sebemu ya mwisho ya sura hii itachambua kigezo cha fani.
Kupinga Dhuluma na Kutetea Haki za Wnyonge
Dhamira ya kupinga dhuluma na kumtetea mtu mnyonge imejitokeza sana katika fasihi za Afrika si tu kabla ya uhuru wa bendera wakati ambao Waafrika waliteswa na kunyanyaswa na wakoloni, bali pia baada ya kupatikana kwa huo uhuru wakati ambapo mwananchi wa kawaida alizidi kudidimia katika liodi la dhiki na kuoDewa.
Katika diwani hii baadhi ya mashairi yaliyoshughulikia dhamira hii ni: "Madhumuni" (uk. 7-8), "Mkulima Furahia" (uk. 33), "Hali Halisi" (uk. 42), "Watu" (uk. 49-50), "Vita" (uk. 53), na "Tulokataa Zamani" (uk. 60).
Shairi la "Madhumuni" linatetea uhuru wa kusema na wa kudai haki; na zaidi ya hivyo linatetea kupatikana kwa mahitaji ya lazima kwa wananchi. Jambo hili tunaliona hasa katika ubeti wa 13:
Dunia yataka raha, wengi wapate chakula
Waseme bila karaho, wapate na pa kulala
Wasifanyiwe shabaha, hawa ni watu si swala
Nyingine ipi dunia, tuweze kulinganisha?
Hili ni shairi linalipinga pia ubaguzi pamoja na siasa za mataifa yenye nguvu kuikalia dunia, kama asemavyo mshairi:
Naililia dunia, hii dunia nyomavu,
Woga umetuingia, twahofu miti mikavu,
Wawili watukalia, twaf'ata kama pumbavu
Sauti hii ya kumtetea mnyonge inajitokeza vizuri sana katika shairi la "Mkulima Furahia" ambamo mshairi - kwa kutumia kejeli, dhihaka na tashtiti - ameonyesha dhiki za mkulima, na kwa hakika neno "furahia" limetakiwa humu lichukuliwe katika kiuyume chake kabisa. Makasisi, mashehe, maprofesa, wanasiasa na wafanyabiashara wanaonyeshwa wanavyoshughulika na maneno tu na hata kutoa "nadharia za kulima" na kumpangia mkulima bei ambaye jasho lake ndicho hasa chanzo cha wao kupata raha na anasa. Na hata mstari wa mwisho'wa shairi hili usemao: "Wewe na jembe wao na kalamu" umekusudiwa uipige muhuri kejeli ya shairi hili.
Dhiki hizi za mtu mnyonge, hasa za mkulima, zimeonyeshwa zilivyo na mismgi yake katika utabaka wa jamii katika shairi la "Watu". Ubeti wa pili wa shairi hili unalieleza jambo hili waziwazi:
Mambo yao mengi sana, ya furaha na huzuni
Wengine shida hawana, wengine ni masikini
Maisha yana hiana, na mvutano wa kani,
Dunia ni pande mbili, wenyecho na wasonacho
Baada ya kutupa taswira ya utwana na ubwana uliopo katika dunia (beti za 3 na 4), mshairi anamalizia shairi lake kwa kusisitiza juu ya dhiki za mkulima:
Kazi wanapozifanya, jua linavyowachoma,
Sawa kukaanga nyanya, migongo imeinama,
Majasho yajikusanya, misuli inatetema
Mifereji yachimbika, mgongo chanzo cha mito.
Shairi la "Vita" linapinga vita hasa kwa vile mtu mnyonge ndiye aumiaye vita vinapofumka. Katika shairi la "Tulokataa Zamani," mshairi anapinga kuzoka kwa aina mbalimbali za "michango" na "kodi" ambazo madhumuni yake ni kujengea majumba ya fahari yasiyomsaidia mtu mnyonge; hali ambayo si tofauti sana na ile wananchi waliyoipinga wakati wa enzi za ukoloni walipodaiwa kodi za "kichwa".
Mashairi yote haya yanayotetea haki za wanyonge hapohapo yanaungana na yale yanayochambua dhamira ya upotofu na uongozi mbaya, kwani dhamira bizi mbili zinashirikiana: ni pande mbili za sarafu hiyo hiyo moja.
Upotofu na Uongozi Mbaya
Dhamira ya upotofu na uongozi mbaya imejazana katika baadhi kubwa ya vitabu vya fasihi ya Kiswahili. Hii tunaiona hasa katika vitabu vilivyojaribu kutathmini kufaulu ama kushindwa kutekelezwa kwa maadili ya matamko mbalimbali ya kisiasa, hasa yale ya Azimio la Arusha (1967) na Mwongozo (1971). Matamko haya yalionyesha dira ya uongozi bora, na wasanii wengi walionyesha ari ya kuufuatilia utekelezaji wake.
Msomaji anashauriwa asome, kati ya maandishi mengi yashughulikiavo dhamira hii, kazi za Oabriel Ruhumbika za Parapanda: Wali wa Ndevu na Hadithi Zingine (Nairobi, EALB, 1976), na Uwike Usiwike Kutakucha (EAPL, 1981); riwaya ya W.E. Mkufya, Kww Hiki(TPH, 1976); Isaack Mruma, Nguzo ya Uhondo (TPH, 1981); George Liweriga, Nyota ya Huzuni (TPH, 1981); na ya Harrison Mwakyembe, Pepo ya Mabwege (Longmans Tanzania, 1982). Pia inafaa kusoma tamthilia za Paukwa Theatre Association, Ayubu(Kampala: Documentation and Publication Centre, 1984), Penina Muhando, Ndyanao Balisidya na Amandina Lihamba, Harakati za Ukombou (TPH, 1984); Amandiana Lihamba, Hawala ya Fedha (TPH, 1980), Penina Muhando, Lina Ubani (DUP, 1984) na ile ya E. Kezilahabi ya Kaputula la Marx (Itatolewa na EAPL).
Kazi zote hizo zihusuzo dhamira ya upotofu na uongozi mbaya zinasaidia sana kuyaelewa mashairi yaliyoko katika diwani ya Raha Karaha yanayoishughulikia pia dhamira hii. Kati ya mashairi bayo ni yale ya "Madhumuni", "Chama Kikumbuke Hayo" (uk. 9-10), "Adui" (uk. 11-13), "Joho la Maisha" (uk. 31-32), "Nani Atuponye" (uk. 33-34), "Kelebu Nyie Wabishi" (uk. 37-39), "Utumwa" (uk. 40-41), "Utawala si Urithi" (uk. 41), "Shambani" (uk. 43), "Miazi ya, Misituni" (uk. 44-45), na "Tulokataa Zamani" (uk. 60). Yote haya yanaonyesha jinsi ambavyo suala la uongozi mbaya limeathiri maendeleo ya jamii nyingi na Afrika.
Shairi la "Chama Kikumbuke Hayo", kwa mfano, linapinga vikali siasa za midomoni ambazo zimejaa unafiki (ubeti wa 4), ushirikina na umbea (ubeti wa 5), uzembe (ubeti wa 7), na wizi (ubeti wa 9). Labda ubeti wa 2 unawakilisha muhtasari wa yale asemayo mshairi:
Masikio yalituna, hotuba kutuzidia,
Tukawa twaulizana, kipi wanakusudia,
Katika kusema sana, kazi zinajilalia,
Mapinduzi ni kwa kazi, sio kwa kuhutubia.
Shairi la "Adui" linaendeleza maoni ya lile la "Chama Kikumbuke Hayo" kwa kupiga mbiu ya mgambo dhidi ya maadui watano: magendo, rushwa, bei za kuruka, wizi na upendeleo. Hata hivyo inakuwa vigumu kuifuatilia mbiu hii kwani mshairi hatuonyeshi hasa ni akina nani wataendesha vita hivyo, na chini ya uongozi wa nani!
Mashairi ya "Joho la Maisha", "Utawala si Urithi" na "Shambani" yanashughulikia suala au tatizo la viorigozi wanaong'a-ng'ania madaraka na vyeo. Hawa wameugeuza uongozi kuwa usultani, na kwao cheo si dhamana. Viongozi hawa wanatoa ahadi za uongo ili tu wapate vyeo. Siasa hizi za kusema uongo zinawafanya viorigozi hawa wasiwaruhusu wananchi wafikiri wala kutoa maoni, na pia wanajidai kuwa wao wamechaguliwa na Mungu, kama beti mbili za mwisho za "Joho la Maisha" zinavyoeleza:
Tena uwe mkasuku, asemayo uyakiri
Asije akakushuku, ati nawe wafikiri
Au waandika buku, jamii kuipa ari
Mvaaji kesha vaa, kumvua kwa mivv.
Asema yeye ajua, ni yeye alijulia
Wengine hawajajua. Ni Mola kamchagua
Wengine watachafua, joho hili la maua,
Joho la uzi mwekundu, sijui lavaliwaje.
Mshairi anaendelea kuonyesha kejeli iliyopo katika uongozi wa Afrika kwa kutupa laswira ya kiongozi anayedai kuwa raha na starehe zote azipatazo ni kwa niaba ya wananchi wote. Hili linajitokeza katika shairi la "Lakini Haridhiki" (uk. 41). Jambo hili limerudiwa pia katika shairi la "Shambani" ambamo "meneja" wa shamba anakula mazao yote na kunenepeana wakati wananchi walioshiriki katika kuyalima, kuyapanda na kuyavuna wanazidi kukondeana. Tatizo hili la uongozi mbaya Unazidishwa mara dufu na kitendo cha kuwahamishahamisha tu wale wanaofanya makosa katika sehemu zao za kazi kama ubeti wa mwisho usailivyo:
Shamba akilifilisi, na jingine atapewa,
Yeye hakosi nafasi, wenzake wanamjuwa,
Je wanyonge wanahisi? nani anayewajuwa?
Shamba hili nalisema, ni mfano mariflhawa.
Shairi la "Mizizi ya Mistuni" hali kadhalika linaonyesha jinsi ambavyo upotofu na wizi wa mali ya umma umesambaa mahali pengi, nao unaambatana na dhuluma inayoathiri hata sheria. Haya yanajitokeza hasa katika ubeti wa 3 usemao:
Ni wizi ulozidia, wa walioshika uzi
Twa walinda sheria, kortini watetezi
Hukodi na kulipia, mwenye mali hatumwezi,
Dhuluma yakandamiza, mwenyecho awa hanacho.
Suala hili la sheria kuwa chombo cha kitabaka linajitokeza pia katika shairi la "Unafiki" (uk. 51-52) ambamo twaonyeshwa jinsi viongozi wanaolaani mambo mengi majukwaani wakati 'gizani wanaya-halalisha, wanavyotumia madaraka yao kuikandamiza haki:
Ona sheria na haki, na halali kwa haramu
Leo sheria ni haki, keshoye yawa shutumu
Au kwake ya wa haki, na kwangu yawa dhulumu,
Wawili wakiamua, dhuluma yawa sheria.
Utumwa kuwa sheria, ikawa haki kwa bwana
Sheria kajitungia, na watumwa kuwabana
Ndio wongo wa dunia, bwana aupenda sana
Ukadai haki kwake, sheria ni za tabaka.
Shairi la mwisho katika diwani hii, "Tulokataa Zamani", ni wito kwa viongozi wasipitishe maamuzi yanayowakamua zaidi wananchi kwa miradi ya kianasa ambayo haiwafaidii wananchi hao.
Umuhimu wa Kufanya Kazi na Kuwajibika
Mashairi kadhaa katika diwani hii yanasisitiza kuhusu umuhimu wa kufanya kazi ili kuleta maendeleo ya jamii.
Shairi la "Tuwe Sote Makondeni" (uk. 54-55) ni la wito wa watu kufanya na kuheshimu kazi. Zaidi ya kusisitiza kuwa wakati umekwisha wa maneno matupu majukwaani na semina zisizo na mwisho, shairi pia linasisitiza umuhimu wa kiluno:
Si maneno mdomoni, kutangaza jukwaani,
Semina tupunguzeni, twajitia hatarini,
Tuwe wte macondeni, mijini na vijijini,
Semina tupunguzeni, twajitia hatarini,
Tuwe wte macondeni, mijini na vijijini,
Dawa ya njaa naona, ni kulima kwa mpango.
Shairi la "Pombe" (uk. 55) nalo linakataza ulevi unaoingiliana na utendaji kazi na kusisitiza kuwa kuna baja ya watu kuwajibika katika sehemu zao za kazi.
Marudi na Maonyo
Mashairi ambayo kidhamira yanaungana sana na hayo yanayosisitiza umuhimu wa kuheshimu kazi ni yale yanayotoa mawaidha, marudi na maonyo. Kati ya hayo yale ya "Hadhari" (uk. 27), "Pombe" na "Raha" (uk. 55) ndiyo yanayotoa maadili ya moja kwa moja. Shairi fupi, "Hadhari" linamtahadharisha msomaji aepukane na shari na ujeuri. Linasema:
Naona wafanya shari, mambo yako ya hatari,
Kwa nini hutaki shwari, sharti utafakari,
Ndugu fanya tahadhari, jitenge na ujeuri
Namna zako za adha, wenzio wawapa kero.
Shairi la "Pombe" pia linatoa mawaidha dhidi ya ulevi. Linapnyesha jinsi ambavyo pombe huleta hasara zaidi ya faida kwa jamii. Pombe husababisha ajali nyingi, huleta uvivu kazini, na pia humfanya mlevi awe mwizi wa mali ya umma ili aweze kupata pesa zaidi za kulewea. Haya yamerudiwa katika shairi la "Raha" ambalo linasisitiza kuwa badata ya raha, pombe huleta karaha.
Kati ya mashairi ya marudi na maonyo, shairi la "Mtoto Kukosa Fimbo" (uk. 23) lina umuhimu wake kwani ni dhahiri kuwa litazusha ubishi na mijadala baina ya wasomaji, juu ya malezi bora. Mshairi katika shairi hili anadai kuwa malezi hayana budi kuambatana na kuwacharaza watoto viboko, na anasisitiza kuwa mtoto akikosa fimbo maisha yake huharibika. Kwa mshairi huyu, maneno na maonyo yasiyoambatana na fimbo humfanya mtoto asahau kuhusu kosa lake; lakini maneno yakiwa na fimbo humfanya anayeonywa akumbuke baadaye na akwepe kurudia kosa.
Wanasaikolojia wamewahi kuongelea sana kuhusu jambo hili. Wengine wamedai kuwa nidhamu kwa njia ya bakora na machozi si nidhamu halisi bali ni woga mtupu. Na wengine wameeleza kuwa mzazi au mwalimu afikiapo hatua ya kutumia fimbo basi mzazi au mwalimu huyo anakiri kuwa kashindwa kulea au kufundisba, kwani angefaulu kulea au kufundisha vizuri asingehitaji kutumia fimbo. Huu ni mjadala ambao msomaji wa shain la "Mtoto Kukosa Fimbo" anaweza kuutumia katika kulichambua shairi hili.
Mapenzi
Mashairi ya "Ujue" (uk. 25) na "Jibu" (uk. 25) yanatoa mjadala unaoongelea suala hili, Shairi la "Ujue" linaonyesha vile ambavyo wakati watu wengine hulewa pombe, mshairi kalewa penzi ambalo limemjaza kiu ya kukutana na kuongea na yule ampendaye. Shairi la "Jibu" linatoa jibu kwa lile la "Ujue" na kutahadharisha kuwa yote yang'aayo si dhahabu, kwani huyo anayemlevya mshairi "Ni kweli anavutia, ila wcrigi wamemwacha." Hata hivyo jibu hili halimridhishi mshairi kwani bado katika "Zuzuo" (uk. 25) anasisitiza anavyovutiwa na huyo amtamaniye na ambaye anamuona kuwa "ni waridi maridhawa." Hatimaye shairi la "Fumbua" (uk. 25) linamaliza mjadala kwa kutueleza kuwa kupenda ni kitendawili:
Ama pindu hupindua, nalo pindo lapindika,
Pinduo likiingia, mengine yanatukuka,
Baadhi yadidimia, kukidhi tunayotaka,
Kitendawili fumbua.
Katika shairi la "Furaha na Huzuni", licha ya kutuonyesha pande mbili za maisha, papo hapo shairi linatoa hisia za wapenzi wanaoachana baada ya miaka mitano ya kuvumiliana. Ukali wa kutengana unajitokeza humu, nao unaonyesha kuwa wapenzi hawana budi kuwa kufu ili mapenzi yao yaweze kudumu.
Maana na Dhima ya Sanaa
Yako mashairi kadhaa katika diwani hii ambayo yanatoa mawazo ya Mvungi kuhusu nafasi ya sanaa (hasa ushairi na muziki) katika jamii. Baadhi ya hayo ni: "Jibu" (uk. 48), "Sanaa na Ufundi Je?" (uk. 52), "Shairi" (uk. 53), na "Muziki" (uk. 57).
Katika mashairi ya "Jibu" na "Shairi", mshairi anasisitiza kuwa japokuwa kuna "vipawa" katika usanii, kwa hakika kila mtu ana vipawa hivyo, bali wengi hawataki kuvitumia. Kwa hiyo Mvungi anatueleza kuwa ushairi ni mazoea, uzoefu na utundu wa mtu kujituma na kutunga mashairi, Mshairi anasema:
Vipaji vipo kichwani, kila mtu kavibana,
Kuviajiri kazini, ni hapo vyaonekana,
Vikilala akilini, twasema fulani hana,
Vipaji sawa na nywele, kila mtu ana zake.
Haya ni mawazo yanayopinga mtazamo wa baadhi ya wana-nadharia, hasa wale wanaoshikilia "ujadi" katika ushairi wa Kiswahili ambao husisitiza kwamba "ushairi wa Kiswahili na wenyewe", nadharia ambayo inajaribu kwa kila njia kumwonyesha mshairi kuwa kajawa na hekima amazo zinamfanye awe tofauti na wanajamii wengine "wa kawaida".
Mshairi anaendeleza wazo lake katika shairi la "Shairi" ijapokuwa humu amedhanifisha pia kipaji cha ushairi. Anasema:
Ushairi ni kipaji, chaletwa na Mwumbaji,
Mithili yake dibaji, kukuza ni kazi kuji,
Mwenye huu ujuaji, sheriaze zatuhoji,
Vipaji wengi tunavyo, kuviona ni juhudi.
Pamoja na mashairi haya yanayoongea kuhusu "vipaji", yamo mawili ambayo yanajaribu kueleza ni vipi kazi ya sanaa yatakiwa iwe. Yote haya yameelekezwa hasa upande wa bendi zetu za muziki ambazo, twaambiwa na mshairi, badala ya kutulia na kutunga nyimbo nzuri kifani na kimaudhui, zimebaki kuwa vipaza sauti vya matamko ya kisiasa majukwaam kwa namna ambayo ndani ya nyimbo zitungwazo hakuna sanaa na ufundi wowote. Mshairi katika shairi la "Sanaa na Ufundi Je?" anasisitiza kuwa wanamuziki wetu hawana budi kuwa na makini ya kiufundi ili wasisitize tu upande wa maudhui na kuusahau ule wa fam. Kwa hiyo, katika shairi la "Muziki" anasisitiza kuwa kuna haja pia ya kufanya mchujo wa maudhui ili badala ya kuwa muziki wa kuzikariri botuba za wanasiasa, tupate chombo kinachosaidia kuisahihisha jamii, wakati huohuo kikiifurahisha hadhira kwa upande wa ufundi na sanaa.
Labda ingefaa tu Mvungi aelewe kuwa huu "ufyatuaji" wa muziki si kitu kilichotokea kwa ajali tu bali ni sehemu ya maisha ya kipesa yanayogeuza kila kitu kuwa bidhaa ya kuuzwa harakaharaka sokoni. Kwa hiyo itaonekana dhahiri kuwa hata kwa upande wa fasihi, kwa mfano, katika miaka ya sabini na themanini kumetokea vitabu mbalimbali vinavyojaribu tu kumsisimua msomaji kwa visa vya mapenzi na upelelezi ambavyo havishughulikii undani wa matatizo ya jamii. Vitabu hivi vinatungwa harakaharaka mradi tu viuzwe na kuingiza pesa za harakaharaka pia.
Maana ya Maisha
Swali ambalo limekuwa likishughulisha bongo za watu tangu kuwako kwa jamii ya mwanzo ya binadamu ni lile la maana ya maisha. Swali hili limeshapatiwa majibu mengi yanayotofautiana na hata kupingana, tangu yale ya kidini yatoayo nadharia za "kuumbwa" na kuona chanzo cha uhai kuwa ni Mungu au nguvu zilizoko nje ya upeo wa mawazo na maarifa ya mtu, hadi yale ya kisayansi yatokanayo na utafiti na majaribio mengi kuhusu evolution; na pia yale ya kifalsafa ambayo mengine, mathalani ya kiexistentialism, yamedai kuwa zaidi ya kutokuwa na maana, wakati mwingine maisba yanawazika tu, hayako.
Katika Raha Karaha, Mvungi anakiri kuwa maisha yapo. Lakini pia anayaona kuwa ai usumbufu, dhiki na karaha tupu kama adaivyo katika shairi fupi la "Maisha" (uk. 27):
Lo maisha ya taabu, moyoni ninaungua,
Lo hii kali arlhabu, akili yanipungua,
Lo haya yanonisibu, hata sijayulia
Dunia jama dunia! Mbona haina huruma?
Hata hivyo, katika shairi la "Furaha na Huzuni" mshairi anaonyesha kuwa mara nyingi maisha yana pande kuu mbili; iwapo kuna huzuni, na furaha ipo pia; na pale penye majonzi wakati mwingine pana vicheko pia.
Kutokana na mashairi yashughulikiayo dhamira zingine tulizokwishazichambua, kwa ujumla tunaweza kusema kwamba mshairi anayaona maisha kuwa bado hayajawa na usawa baina ya watu; kwamba bado yamejazana harakati za kutafuta usawa na haki.
Mashairi ya Tambo
Katika shairi la tambo huwa mna fumbo ambalo mshairi kalifumba ndani ya taswira na ishara, na kwa kuitumia lugha kiufundi.
Mashairi ya namna hii si mengi katika diwani ya Raha Karaha kwani mara nyingi mshairi ametumia lugha ya moja kwa moja. Tunayoweza kuyataja hapa ni: "Fumbua", "Miti" (uk. 37) na "Wembe" (uk. 58).
Shairi la "Fumbua" linatupa tambo la maana ya mapenzi wakati ambapo lile la "Miti" linaweza kuwa na maana nyingi. Kwa baadhi ya wasomaji miti huweza kuwakilisha watu ambao katika jamii wana wategemea wenzao kwa kila kitu; watu waliolemazwa na uvivu wao. Ubeti wa 5 unasema:
Miti yajaa unene, kwa mbao haitufai,
Haitoshi meta nane, ila kulishwa yadai,
Miti haina mapana, wala haitoi tui;
Twaing'ang'ania miti, miti yaleta hasara.
Kama tutaichukulia "miti" hii kuwa inawakilisha wanyonyaji, basi ubeti huo wa 5 unatoa taswira ya mtu aliye tayari kula tu bila kukitolea jasho chakula alacho; mtu ambaye hana faida yoyote kwa jamii. Mstari wa mwisho wa ubeti huo unatoa wito ambao tutauchambua vizuri zaidi wakati wa kuyaangalia masuluhisho anayoyapendekeza mwandishi kuhusu migogoro inayoibuka katika ushairi wake.
Shairi la "Wembe" lina utata kidogo. Inawezekana kuwa mshairi alipoliandika ni kweli kuwa alikuwa kakerwa hasa na nyembe ambazo zilikuwa butu hata katika upya wake. Lakini pia inawezekana kuwa mshairi hapa anaongea kuhusu viongozi ambao japokuwa wananolewa na kupitia katika "vinu" mbalimbali vya misasa ya kisiasa kama vile katika Vyuo vya Chama, bado wanapoanza uongozi hawana "makali" yoyote ya mwamko, na badala yake wanaonyesha "ubutu" mwingi katika uongozi wao mbaya uliojaa upotofu.
Shairi la "Nyoka Gani" (uk. 20) hali kadhalika ni tambo zuri ambalo linatufanya tukune vichwa tukijiuliza kama "nyoka", "chura" na "kobe" wanaweza kuwakilisha nini katika maisha halisi yajamii.
Isije ikaeleweka kuwa kila shairi la tambo huwa na jibu moja tu. Msomaji mmoja huweza kupata maana ambayo itatofautiana na ile aipatayo msomaji mwingine wa shairi hilohilo moja. Jambo linalotakiwa na kila msomaji ni kujenga hoja zake na kuithibitisha maana aionayo ndiyo kwa kuitolea mifano dhahiri kutoka katika shairi linalohusika.
Dhamira Nyioginezo
Mashairi tuliyoyatumia wakati wa kuzichambua dhamira mbalimbali za Raha Karaha ni mifano na vielelezo tu. Bado msomaji anaweza kuyagundua mengine ambayo ni vielelezo pia vya dhamira hizo. Hata hivyo yako mashairi kadhaa ambayo hatukuyataja lakini yanao umuhimu wake katika diwani hii. Mojawapo ya hayo, ni lile la "Uzulufu" (uk. 34). Shairi hili linaonyesha athari za mfumo wa uchumi ulioambatana sana na kuabudu fedha. Kutokana na utabaka wa jamii, wanakuwapo watu wa juu wenye fedha na ambao wanatumia fedha hizo kununulia kila kitu, hata watu. Wengi wao ni wazee (wa kiume na kike) ambao wanatumia utajiri wao kuwapotosha na kuwaharibu vijana.
Athari za fedhapia zinajitokeza katika hongo wazipokeazo viongozi kama ielezwayo katika shairi la "Twakimbilia Gizani" (uk.39). Wakati huohuo uchumi huu wa kifedha unawafanya watu waziabudu fedha na kuzifanya Mungu pekee wa jamii; na katika kufanywa hrvyo, fedha imeleta ubadhirifu na ufujaji mali ya umma kama beti mbili za mwisho za shairi la "Twakimbilia Gizani" zinavyoonyesha:
Na matumizi mabaya, wayapendelea sana,
Wengi wafanywa mabaya, na wachache wajibuna,
Tumebaki tunagwaya, hatuthubutu kuguna,
Tunaichemsha mianzi, ndio dawa madhubuti.
Kwa nini iwe lazima, watu kuhonga mapesa?
Na haki yafanywa bima, baharini mwatutosa,
Watu mso na huruma, dunia mwajaza visa,
Tumetoka mwangazani, twakimbilia gizani.
Japokuwa mstari wa mwisho wa ubeti huu una utata ndani yake kwani inakuwa vigumu kuelewa huko "mwangazani" tulikotoka ni wapi hasa, hata hivyo ni dhahiri kuwa suala la athari za fedha limesisitizwa na mshairi katika beti hizi mbili.
Shairi la "Lugha Yangu" (uk. 14) hali kadhalika ni muhimu katika diwani hii. Zaidi ya mshairi kutueleza katika shairi hili kuwa iliyopo si kuisubiri lugha hadi ikue na kuweza kutumika katika taaluma mbalimbali bali inabidi kujitosa na kuikuza lugha hiyo kwa kuitumia katika hizo nyanja, mshairi anakiri kuwa ni kweli kwamba lugha ngeni zinayo manufaa yake. Hata hivyo anapinga kasumba za Waswahili za kuudharau na kuuhujumu utamaduni wao (beti za 7 na 8) na kusisitiza umuhimu wa Kiswahili karna lugha ya Afrika (beti za 9 na 10).
Shairi la Raha Karaba
Jina la diwani hii limetokana na shairi la "Raha Karaha" ndani ya diwani hii na kwa sababu shairi hili lina umuhimu wake tumelipa nafasi ya pekee katika kulichambua.
Shairi la "Raha Karaha" (uk. 28-30) linatoa muhtasari wa karibu dhamira zote kuu alizozishughulikia Mvungi. Kwanza linatuonyesha hali zilivyo baada ya Azimio la Arusha kwa kueleza jinsi ambavyo mali ya umma imegeuzwa kuwa ya watu binafsi. Katika ubeti wa 5 mshairi analilia huduma za umma ambazo sasa zimekuwa mwanzo wa unyonyaji. Anasema:
Tumeona mashirika, kuunda tumekazana,
Kama nakala yatoku, tena kwa haruka sana,
Na fedha zinatutoka, vema kusahihishana,
Umoja utio raha, umegeuzwa karaha.
Mashirika ayatumiayo kuwa vielelezo ni yale ya UMITA, UDA, Relwe, Posta, mamlaka mbalimbali, na biashara ya Mkoa, Mshairi anaonyesha jinsi yote haya yalivyogeuka kuwa karaha kwa mtu mnyonge, hasa mkulima, kwani raha imebakia huko mijini wakati dhiki imetanda vijijini. Haya na mashirika mengine yamegeuka kuwa ya "walaji waso huruma" (ubeti wa 19), na yamejaa wizi unaowakera wananchi.
Beti za 15 na 16 zimetumia taswira ya usongaji ugali kuwa ishara ya kulijenga taifa, na zimejaa pia malalamiko kwamba imekuwaje hata kabla "ugali haujawiva, wengine waanza kula." Hawa ndio wale washerehekeao ushindi mdogo ("ushindi wa moja bila") na kusahau kuwa safari ya kujenga nchi bado ni ndefu sana.
Kwa hivo basi shairi hili ni muhtasari wa kilio cha mwandishi Mvungi dhidi ya mabaya mbalimbali yaliyojaa katika jamii; mabaya ambayo mshairi pia amegusia ufumbuzi wake kama tutakavyoona katika sehemu ifuatayo.
Masuruhisho ya Migogoro
Mwandishi aandikapo kaa yake ya fasihi si lazima atoe masuluhisho na majawabu ya migogoro anayoishughulikia. Wakati mwingine uchambuzi wake na namna anavyousawiri uhalisi wa maisha ya jamii katika kazi yakc ya fasihi huweza kuchochea mijadala na majadiliano baina ya hadhira, hadi hadhira yenyewe ikayavumbua majawabu ya migogoro hiyo.
Hata luvyo, hutokea wakati mwingine msanii akatoa masuluhisho na majawabu ayaonayo kuwa yanafaa. Afanyapo hivyo, wasomaji na wahakiki wake wanao uhuru wa kuyachambua masuluhisho hayo pamoja na kuyatathmini.
Katika Raha Karaha, mshairi ameonyesha hapa na pale majawabu ya migogoro anayoichambua. Mathalani, katika beti mbili za mwisho za "Raha Karaha" anasema:
Maneno yametutosha, maneno yaso vidonda,
Walaji wanayapisha, ni mizizi itashinda,
Vizuri kuichemsha, mganga awe kakonda,
Umoja ulio raha, umegeuzwa karaha.
Mchimbaji kibarua, mpikaji mkulima,
Mnywaji ni mnywa bia, karani ndiye mpima,
Meneja anywe kwa nia, mambo yasende mrama.
Kidogo jawabu hili linapwaya kwani linabaki katika anga la nadharia tu la "kuchemsha mizizi" bila hasa kuonyesha kiuhalisi kuwa "mizizi" hiyo ni kitu gani. Utatuzi huu unaokanganya wa "mizia" unajitokeza pia katika shairi la "Mizizi ya MisitunP', hasa katika beti mbili za mwisho ambazo nazo pia hazituelezi kuwa mizizi hiyo ni nini.
Katika shairi la "Shwari Itaumuka" (uk.46), mshairi anazungumzia ukimya ambao umewanogea wanajamii hadi ukawafanya mabwege ambao hawako tayari kujitokeza kupinga dbuluma. Mshairi anaona kuwa msingi wa ukimya na "shwari" hii ya bandia ni woga wa kukemea hali zilivyo. Beti mbili za mwisho za shairi hili zinagusia tatizo na ufumbuzi wake:
Kule ng'ambo nimeona, kutengana kumezidi,
Kuna wale walonona, anasa zimewazidi,
Wengine wanajikuna, chakula kimekaidi,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.
Shwari nayo manoga, sijui mpaka lini.
Hii nishwariya woga, ndani yake kuna kani,
Mwenye njaa akichaga, nyokaatokapangoni,
Shwari isiyo na dhati, naona itaumuka.
Ubeti huu wa mwisho unaonya kuwa ijapokuwa masikini amenyamaza lakini kimya chake ni cha mshindo mkuu kwani iko siku "atachaga" na kumtoa nyoka (tajiri) pangoni. Hata hivyo njia hii ya ukombozi wa mtu mnyonge, hali kadhalika imcachwa ikielea hewani bila kudhihirishwa wazi wazi.
Katika shairi la "Tuwe Sote Makondeni", mshairi amejaribu pia kuonyesha jawabu la migogoro kwa kulikabidhi "wimbi" jukumu la mabadiliko. Anasema:
Wimbi lete tumaini, nchi iwe na amani,
Dhuluma nao uhuni, tusikutane njiani,
Kiongozi na karani, kau waache utani,
Pendeleo ifutike, ni rushwa yenye makeke.
Badiliko la imani, karibu kwetu nchini,
Na kila mwenye idhini, ajue twamdhamini,
Ajitenge na shetani, akalewa ofisini,
Tujenge nidhamuyetu, taifa liende mbele.
Katika beti hizi pamoja na mbili za mwisho za shairi hili utatuzi wa migogoro ni wa kidhanifu kwani mshairi anaamini kuwa kwa kuwahubiria watu watageuza nyoyo zao na kutupilia mbali uovu uletwao na "shetani"! Uvivu, wizi, dhuluma na kutumia cheo vibaya si mambo yatokanayo na shetani: ni mabaya yanayotokana na mwanadamu mwenyewe pamoja na mazingira yake; na ili yaondolewe haya hatuna budi kuushughulikia mfumo wa jamii inayohusika. Kutokana na mshairi kutolizingatia jambo hili mwishoni mwa shairi lake la "Pombe" anaishia katika mahubiri tu ya kuwasihi walevi waache pombe bila hasa kuchimba na kuchimbua chanzo cha ulevi huo.
BAADHI YA VIPENGELE VYA FANI KATIKA DIWANI YA RAHA KARAHA
Baadhi kubwa ya mashairi ya Raha Karaha yametumia mtindo na muundo wa kimapokeo ulio na mpangilio mahsusi wa beti (hasa za unne - mistari minne minne), mizani kumi na sita kila mstari, mpangilio wa vina ambao mara nyingi una vina vya kati na vya inwisho vinavyofanana katika nustari mitatu ya mwanzo wa kila ubeti, na vina tofauti katika mistari ya mwisho wa beti. Kwa sababu mshairi wa namna hii amezoeleka miongoni mwa wasomaji wengi hatutashughulikia fani yake humu. Badala yake tutaangalia vigezo vinginevyo vya fani na pia yale mashairi yaliyotumia miundo na mitindo tofauti na ya kimapokeo.
Mara nyingi mshairi ametumia lugha ya moja kwa moja isiyo na mficho wa kiishara wala wa kutumia tamathali. Jambo hili kwa baadhi ya wasomaji huonekana kuwa ni udhaifu kwani wengi huhitaji ushairi uwafanyao wakune bongo zao kabla ya kuyumbua ujumbe alioukusudia mshairi. Hata hivyo, hapa na pale mshairi ametumia taswira na ishara nzuri zenye kuyakamilisha maudhui vizuri zaidi.
Kwa mfano, katika shairi la "Chama Kikumbuke Hayo" mwandishi katumia "karakana" kuwa ishara ya nchi au taifa, na amewakemea "wakuu wa karakana" (viongozi) wanaoiangusha nchi kwa uzembe wao. Katumia lugha nzuri kuijenga kejeli yake na kutoa taswira inayosadifu hali zilivyo anaposema kuwa wengi wa hawa viongozi wameng'ang'ania kutoa maneno matupu tu majukwaani bila kuyatekeleza kivitendo. Anasema:
Lakini wamekazana, majukwaa kuinua,
Na watu kuandamana, mkuu kumsikia,
Hujuma za kiuchumi, vpo za aina nyingi.
Ni wazi kuwa kiuhalisi viongozi hawa hawainui majukwaa, bati hii ni lugha iliyotumiwa tu kiufundi kueleza ubaya wa siasa za midomoni zisizoambatana na utendaji.
Shairi la "Adui" limetumia tamathali ya tashihisi kwa kuyapa magendo, rushwa, wizi na upendeleo sifa za mtu. Kwa njia hii tunayaona matatizo haya kuwa ni maadui hasa wa kupigwa vita.
Mashairi yote ya tambo hapohapo yametumia ufumbaji ndani ya ishara. Kwa mfano, katika shairi la "Dawa Mizizi Mirefu", je huu "ugonjwa" waweza kuwa ishara ya matatizo ya kisiasa na kitamaduni yaliyopo katika jamii? Iwapo ni hivyo, ishara ya "dawa" ya hiyo "mizizi mirefu" nayo pia haina budi kuelezwa. Je, inawezekana ishara hii inawakilisha nguvu za umoja wa wanyonge?
Baadhi ya mitindo tofauti na ule wa unne na mizani kumi na sita tunaiona katika mashairi ya 10, 11, 12 na 13 ambayo yanategemeana kimjadala. Hapa dhana ya utoshelezi wa kila shairi inakiukwa. Mtindo wa kimjadala ndani kwa ndani mwa shairi unajitokeza kwa wingi katika shairi la "Kelebu Nyie Wabishi" (uk. 37-39). Huu ni mtindo mzuri kwani unasaidia kulifanya shairi lisimchoshe msomaji.
Katika baadhi ya mashairi, kwa mfano lile la "Raha Karaha", mwandishi kaamua kutumia kituo au kibwagizo kimoja kwa beti zote. Ijapokuwa wakati mwingine hili huweza kumchokesha msomaji, katika baadhi ya mashairi, mathalani hilo tulilolitaja, kituo hiki kimesaidia kusisitiza lile alielezalo mshairi kwamba umoja ambao unahitajiwa ulete raha kwa wananchi uemgeuzwa kuwa karaha.
Katika shairi hili hili tendo la kujenga nchi ili kuleta maendeleo limefananishwa na usongaji wa ugali; taswira ambayo kwa vile ni ya kawaida sana imefanya uJumbe hapa ueleweke vizuri.
Sauti ijitokezayo katika diwani hii ni ile ya chuki iliyojaa karaha kutokana na mambo ambayo hayaendi sawa-katika jamii. Hata hivyo hii haimaanishi kuwa Mvungi amenuna moja kwa moja, kwani katika baadhi ya mashairi yake katumia ucheshi na kejeli - vipengele vinavyotufanya tucheke au walau tutabasamu hata kama mambo yajadiliwayo ni mazito. Kwa mfano, shairi zima la "Macho" (uk. 27) limewekwa kiucheshi kuwasuta wale wanaoyasingizia macho kuwa hayana pazia ili watende mambo mabaya faraghani. Ucheshi unajitokeza pia mshairi awasutapo wale wanaosheherekea ''ushindi wa moja bila" bila kutambua kuwa uhuru si lelemama.
Kejeli pia imejengwa katika mkabala wa shairi zima la "Mkulima Furahia" ambapo ni dhahiri kuwa mshairi anapotumia maneno "wapenzi" na "marafiki" anatutaka wasomaji tung'amue kuwa haya yanasimamia kinyume chake kabisa. Kejeli ya namna hii imetolewa pia kiucheshi katika shairi la "Mtu Jini" (uk. 49) hasa mstari wa mwisho kabisa wa shairi hili: "Twasonga hatua tatu, twarudi hatua nne".
Ni dhahiri kuwa mtu anayesonga mbele hatua tatu na kurudi nyuma hatua nne anakuwa kichekesho kwani kiuhalisi huwa amerudi nyuma hatua moja kutoka pale alipokuwa mwanzoni.
Vipengele vingine vya fani ambavyo vinajitokeza katika diwani hii na awezavyo kuvichuBguza msomaji ni: matumizi ya tamathali (ubeti wa 1 wa "Nyoka Gani", ubeti wa 18 wa "Raha Karaha", na beti za 2 na 3 za "Pombe"); taswira mbalimbali kama vile ya maisha (kwa mfano mshairi asemapo "ganda litahama mti" katika ubeti wa mwisho wa "Sifa ya Mti si Ganda", uk. 41-42) na uchcshi wa dhihaka, dharau na kejeli (angalia beti za 3,4, 5 na 6 za shairi la "Shambani").
Maswali
1. "Diwani ya Raha Karaha ni kilio cha kudai haki za wanyonge." Jadili kauli hii ukithibitisha hoja zako kwa mifano dhahiri.
2. Mashairi ya Raho Karaha yanashughulikia masuala mbalimbali ya kijamii. Chagua uwanja mmoja kati ya zifuatazo ujadili ulivyo-chambuliwa katika diwani hii:
(i) utamaduni
(ii) siasa
(iii) uchumi
3. "Raha Karaha ni mkusanyiko wa mashairi yanayolalamikia kutokukutekelezwa kwa maadili ya Azimio la Arusha". Jadili kauli hii. Dhihirisha mjadala wako kwa mifano kutoka diwani hii.
4. Jadili masuluhisho anayopendekeza mshairi kuhusu migogoro inayojitokeza katika diwani va Raha Karaha.
5. "Katika Raha Karaha tunamwona mshairi aliyeiva kimaudhui 'aldni hajakomaa kifani." Una mawazo 'gani kuhusu kauli hii?
6. Chagua vipengelc vitatu kati ya vifuatavyo na ujadili vilivyojitokeza katika diwani ya Raha Karaha:
(i) Ushairi
(ii) Muundo na mtindo
(iii) Taswira na Ishara
(iv) Kejeli na ucheshi