TASWIRA YA JAGINA KATIKA TENDI: ULINGANISHI WA FUMO LIYONGO

                                       

                                             SURA YA KWANZA ................................................................................................................... 1 1.0 Utangulizi.................................................................................................................................. 1 1.1 Tatizo la Utafiti......................................................................................................................... 5 1.2 Madhumuni ya Utafiti............................................................................................................... 6 1.3 Nadharia tete .............................................................................................................................6 1.4 Maswali ya Utafiti..................................................................................................................... 6 1.5 Sababu za Kuchagua Mada....................................................................................................... 6 1.6 Upeo na Mipaka........................................................................................................................ 7 1.7 Msingi wa Kinadharia............................................................................................................... 9 1.8 Yaliyoandikwa Kuhusu Mada................................................................................................. 15 1.9 Mbinu za Utafiti...................................................................................................................... 22 1.10 Hitimisho............................................................................................................................... 22 SURA YA PILI: HISTORIA YA FUMO LIYONGO NA SHUJAA ISA PAMOJA NA ILE YA JAMII ILIYOWAZAA NA KUWAKUZA........................................................................ 24 2.0 Utangulizi................................................................................................................................ 24 2.1 Historia ya Waswahili............................................................................................................. 24 ix 2.2 Historia ya Fumo Liyongo...................................................................................................... 30 2.3 Misukosuko ya Kivita Iliyomzua Fumo Liyongo................................................................... 33 2.4 Historia ya Wayahudi hadi Kuzaliwa kwa Nabii Isa .............................................................. 36 2.5 Misukosuko ya Kivita Iliyowakumba Wayahudi ................................................................... 38 2.6 Historia Ya Nabii Isa .............................................................................................................. 40 2.7 Hitimisho................................................................................................................................. 46 SURA YA TATU: KULINGANISHA NA KUTOFAUTISHA SIFA ZA KIJAGINA ZA NABII ISA NA FUMO LIYONGO........................................................................................... 47 3.0 Utangulizi................................................................................................................................ 47 3.1 Kuzuka kwa Mashujaa............................................................................................................ 48 3.1.1 Utabiri wa Kuzaliwa kwa Majagina .................................................................................... 48 3.1.2 Jagina kwa Kawaida ni Mwanamume ................................................................................. 50 3.1.3 Utoto na Ujana wa Jagina .................................................................................................... 51 3.1.4 Shujaa Hutokana na Ukoo wa Kifalme................................................................................ 52 3.1.5 Utetezi wa Cheo................................................................................................................... 53 3.1.6 Maadui wa Shujaa................................................................................................................ 55 3.1.7 Shujaa huwa Kipenzi cha Wanajamii ................................................................................. 57 3.1.8 Jina la Shujaa ....................................................................................................................... 59 3.1.9 Shujaa Huwa na Akili Pevu ................................................................................................. 60 3.2.0 Kugura kwa Shujaa ............................................................................................................. 63 3.2.1 Mashujaa kwa Kawaida Huwa ni Washairi......................................................................... 64 3.2.2 Maisha ya Shujaa Huwa ni Dhiki Tupu............................................................................... 65 3.2.3 Maisha na Matendo ya Shujaa Huwa ni ya Kimiujiza......................................................... 66 x 3.2.4 Shujaa Huwa Hawaeleweki kwa Uwazi .............................................................................. 68 3.2.5 Mapenzi ya Mama kwa Shujaa ............................................................................................ 69 3.2.6 Kimo na Nguvu za Shujaa ................................................................................................... 70 3.2.7 Majagina Aghalabu Huwa Magwiji Katika Vita ................................................................. 72 3.2.8 Shujaa na Suala la Ndoa ...................................................................................................... 74 3.2.9 Kifuasi cha Shujaa ............................................................................................................... 75 3.3.0 Shujaa Huhusishwa na Zaidi ya Jamii Moja........................................................................ 76 3.3.1 Usaliti na Kifo cha Shujaa ................................................................................................... 78 3.3.2 Anamoishi Jagina na Kurudi Kwake Safari ya Mwisho.................................................... 800 3.4 Hitimisho................................................................................................................................ 82 SURA YA NNE: UMUHIMU WA FUMO LIYONGO NA NABII ISA KWA JAMII ZAO. 4.0 Utangulizi ................................................................................................................................83 4.1.1 Kitambulisho cha Kitaifa/Kijamii........................................................................................ 89 4.1.2 Ukombozi na Muungano wa Jamii ...................................................................................... 83 4.1.3 Kioo cha Jamii/Historia ya Jamii......................................................................................... 85 4.1.4 Mabadiliko Katika Mfumo Mzima wa Jamii....................................................................... 84 4.1.5 Ruwaza Bora ya Kufuatwa na Wanajamii........................................................................... 88 4.1.6 Fahari ya Jamii Zao.............................................................................................................. 89 4.2 Hitimisho............................................................................................................................... 911 SURA YA TANO: HITIMISHO NA MAPENDEKEZO........................................................ 92 5.0 Hitimisho................................................................................................................................. 92 5.1 Mapendekezo ya Utafiti.......................................................................................................... 95 MAREJEO................................................................................................................................... 96 1 SURA YA KWANZA 1.0 Utangulizi Mada tunayochunguza inahusu taswira ya jagina katika tendi mbili teule; Utenzi wa Nabii Isa ulioandikwa (1977) na Musa Mzenga, Almaarufu, Ustadh Shirazi, na Utenzi wa Fumo Liyongo, wake Mohamed Kijumwa, kama ulivyoelezwa katika Tenzi Tatu za Kale (1999), kitabu kilichohaririwa na Mulokozi. Tumewalinganisha na kuwatofautishaa Fumo Liyongo na Nabii Isa, ambao ndio majagina wakuu wa tendi hizi, kwa mujibu wa sifa bia za mashujaa. Kazi hii vilevile imelenga kuonyesha umuhimu wa majagina hawa kwa jamii zao. Jamii tofauti zina mitazamo anuwai kuhusu taswira ya jagina. Taswira ni neno lenye matumizi mbalimbali katika uhakiki wa fasihi. Kulingana na Njogu na Chimera (1993), taswira ni mkusanyiko wa picha zinazotokana na ufundi wa msanii katika kuteua na kupanga maneno yake ya kazi fulani ya kifasihi. Wanasema pia, taswira ni mkusanyiko wa picha anazozipata msomaji au msikilizaji wa kazi fulani ya kifasihi. Picha hizi huwa na mafunzo au jumbe fulani. Katika Kamusi ya Kiswahili sanifu (2002), tunaelezwa taswira ni picha ya mambo au vitu vinavyomjia mtu akilini mwake; maono, picha. Pia ni mchoro au sanamu. Kutokana na maelezo yaliyotolewa hapo juu, tunaweza kusema kuwa maana ya kijumla ya neno hili ni mkusanyiko wa picha zinazoundwa na maelezo ya msanii katika kazi yake ya fasihi. Katika utafiti huu, tumejikita katika tendi hizi mbili kufafanulia picha za majagina hawa wawili kama kielelezo, hata ingawa tumerejelea matini zingine ambazo zinawazungumzia, ili kujenga taswira pana ya majagina hawa. Sifa za kimsingi za majagina nyingi ila zinajitokeza kwa viwango tofauti, kwa majagina wa aina mbalimbali na wa mazingira mbalimbali. Majagina 2 wanaweza kutofautiana kimaeneo, lakini ukweli ni kwamba zipo sifa ambazo ni bia kwa majagina wote. Wamitila (2003) amejadili utendi kama shairi refu la kisimulizi linalozungumzia kwa mapana na kwa mtindo wa hali ya juu, matendo ya mashujaa au shujaa mmoja. Anasema kuwa utendi huwa na sifa nyingi na huweza kuleta pamoja hadithi ya shujaa, visasili, historia, pamoja na ndoto za taifa fulani. Fasili hii inatupatia utata inapoeleza utendi kama shairi refu la kisimulizi. Utata unajitokeza katika kupima urefu wa ushairi ulio katika masimulizi.Tutatumia kipimo gani kupima urefu huo? Na mpaka wa ushairi mrefu na mfupi unaanzia wapi na kuishia wapi? Fasili hiyo inahitaji maelezo zaidi ya kipimo kipi kinafaa kutumika. Mulokozi (1996), anaeleza utendi kama ushairi wa matendo. Ni utungo mrefu wenye kusimulia matukio ya kishujaa yenye uzito wa kijamii au kitaifa. Matukio hayo yanaweza kuwa ya kihistoria na visakale. Ufafanuzi huu wa Mulokozi umepiga hatua mbele kwa kueleza utendi kama ushairi wa matendo. Utendi hufungamana na matendo wakati wa utendaji wake. Matendo hayo huathirika utendi unapokuwa katika maandishi. Kutokana na fasili za wataalamu hawa, tunaweza kusema kuwa utendi ni ushairi unaosimulia tukio fulani kwa matendo. Usimuliaji wa tukio huambatana na matendo ambayo hufanywa na msimuliaji. Utenzi unaweza kuhusu tukio lolote la kijamii ambalo laweza kuwa la kishujaa au lisiwe la kishujaa. Utafiti huu unakusudia kufafanua taswira ya jagina katika utendi kwa kumrejelea Nabii Isa, ambaye ni shujaa wa kidini (anayefahamika kama Yesu miongoni mwa Wakristo), kama alivyoelezewa katika Utenzi wa Nabii Isa, na Fumo Liyongo (ambaye ni shujaa 3 wa kihistoria), kama alivyoelezewa katika Utenzi wa Fumo Liyongo. Nia yetu katika utafiti huu ni kuthibitisha kuwa sira za majagina katika ulimwengu mzima zinafanana sana. Nitaangalia maisha ya majagina hawa wawili na kuangazia sifa zao za kishujaa kwa kuzilinganisha na sifa bia za mashujaa. Kulingana na Gaster, kama anavyonukuliwa na Gichamba (2005), jagina ni mtu ambaye humiliki uwezo zaidi kuliko uwezo wa watu wa kawaida na hutumia uwezo huu kiujasiri na huwa tayari kuyahatarisha maisha yake kwa manufaa ya watu wengine. Nayo Kamusi ya Tuki (2004), inasema kuwa, shujaa ni mtu mwenye moyo thabiti anayeweza kukabili mambo, hata kama ni hatari. Ni jasiri, nguli, jogoo, jabali, abtali, ghazi, nyamaume. Kwa jumla, tunakubaliana na maoni ya wataalamu hawa na kufafanua shujaa kama kiumbe aliye na sifa za kiajabu, anayekuzwa na wanajamii na pia kujikuza mwenyewe ili ajinufaishe na kuwanufaisha watu wengine. Mutiso (1999:1), anaainisha majagina katika makundi matatu. Anasema jagina wa kwanza ni kiumbe wa kweli ambaye amekuzwa na amejikuza mwenyewe hata akaonekana kiumbe wa ajabu. Kiumbe huyu huwa ni mashuhuri na husifika kwa ujasiri, nguvu, (hata kama amelemaa ulemavu huu ni onyo kuwa baadaye atakuwa na nguvu za ajabu) na kwa kila jambo lionekanalo kubwa au la ajabu katika jamii husika, hata kama jambo hilo twaliona ni la kipuuzi. Mabadiliko yote mazuri yatokeayo katika jamii, jamii husika huamini ya kwamba yameletwa na jagina wao, hata kama jagina huyo hahusiki kamwe. Kwa kawaida, jagina huyu hutokana na familia maskini lakini jamii yake huamini ya kwamba ametokana na familia tajiri ya kifalme. Maisha yake huwa 4 ni ya taabu na dhiki na ya kutangataga. Yumkini, watu humwabudu baada ya kifo chake (kwa kawaida hata akifa huaminika ya kwamba yu hai na anayaona yote tuyatendayo). Mutiso (khj), anaendelea kufafanua aina ya pili ya jagina kama kiumbe wa kihurafa, ambaye ameumbwa na jamii yake. Kiumbe huyu pia huwa na sifa ambazo si za kawaida na ghalibu awe ni Mungu au yote mawili. Yumkini iaminike ya kwamba jagina huyu ndiye mzazi wa jamii husika. Jagina wa tatu ni mhusika mkuu katika utenzi, tamthilia, riwaya, hadithi, ngano, sinema, kitendo au jambo. Mpaka kati ya aina hizi tatu za majagina ni mwembamba, kwani mhusika mkuu anaweza kuwa ni mmojawapo wa aina mbili zingine za majagina. Kwa sababu hii, tunapomjadili jagina Isa ambaye ni shujaa wa kidini na kulinganisha sifa zake na za Fumo Liyongo ambaye ni jagina wa kihistoria na majagina wengine, hatunuii kukuza au kumdunisha shujaa wa jamii yoyote ile, bali kwa maoni yetu, sifa za majagina wote, wa kidini au la ni karibu sawa. Utendi ni ushairi unaosimulia tukio fulani kwa matendo. Usimuliaji wa tukio huambatana na matendo ambayo hufanywa na msimuliaji. Utendi unaweza kuhusu tukio lolote la kijamii ambalo laweza kuwa la kishujaa au lisiwe la kishujaa. Katika makala haya, istilahi ambayo imetumika ni tenzi ambayo ina maana sawa na tendi. Hivyo, istilahi zote zimetumika sawa. Tendi nyingi huwajenga mashujaa wake katika hali ya kuwafungamanisha na matatizo ya kijamii yanayoikabili jamii husika. Hufanya hivyo kwa malengo mbalimbali. Kwanza, kwa lengo la kuonyesha kuwa shujaa ni zao la jamii, na kama ni zao la jamii hana budi kukumbana na 5 matatizo kama wanajamii wengine. Pia, hufanya hivi kwa lengo la kuwaonyesha wanajamii ushujaa wa shujaa katika kukabiliana na matatizo mbalimbali, kwamba hutofautiana na watu wa kawaida. Aidha, hufanya hivyo kwa lengo la kuwaondolea wanajamii hofu na kuwahakikishia usalama wao pindi wapatwapo na matatizo, kuwa, wanaye mwokozi atakayewaokoa katika matatizo yao. Katika kuyathibitisha haya tutajikita katika kuchambua ujagina wa wahusika wetu kama unavyojitokeza katika Utenzi wa Nabii Isa, na Utenzi wa Fumo Liyongo. 1.2 Tatizo la Utafiti Suala la mashujaa ulimwenguni limefanyiwa utafiti na watafiti wengi kama anavyosema Mutiso (1985 na 1999). Anaeleza watafiti hawa kama: Carlyle (1924), Kunene (1971), Butler (1979), Raglan (1965), Mberia (1989), na Gaster (1987). Wengi wa watafiti hawa kulingana na Mutiso (khj), wamezungumzia majagina kwa jumla. Baadhi yao kama Mutiso mwenyewe, na Mberia wamejaribu kulinganisha majagina wawili wa kidini au wa kihistoria. Watafiti hawa wametoa sifa kadhaa, ambazo ni bia na ambazo zinadhihirika kwa mashujaa wa jamii mbalimbali ulimwenguni, na kwa viwango tofauti tofauti. Sifa za majagina walizozitoa watafiti hawa sio za pekee na nyingine zinaweza kujitokeza iwapo ulinganishi zaidi wa mashujaa wa aina tofauti, na kutoka tamaduni na mazingira tofautitofauti ulimwenguni ungefanywa. Mashujaa huwa na umuhimu mkubwa kwa jamii zao. Fumo Liyongo ambaye ni shujaa wa kihistoria wa jamii ya Waswahili, na Nabii Isa, ambaye ni shujaa wa kidini wa Wayahudi, ni mifano mizuri ya majagina ambao wanaweza kutuzulia sifa zaidi za majagina, na ndio msingi wa utafiti wetu. 6 1.3 Madhumuni ya Utafiti Madhumuni ya utafiti wetu ni: a) Kubaini historia na mazingira ya kijamii yaliyowazaa na kuwakuza shujaa Isa na Fumo Liyongo. b) Kulinganisha na kutofautisha sifa za kishujaa za Isa na Fumo Liyongo. c) Kuchunguza umuhimu wa majagina hawa kwa jamii zao, na kwa ulimwengu mzima kwa jumla. 1.3 Nadharia tete. Utafiti wetu uliongozwa na nadharia tete zifuatazo: a) Liyongo na Isa ni mifano mizuri ya majagina wa kihistoria na wa kidini. b) Sifa za kishujaa za majagina hawa kwa kiasi kikubwa zinafanana. c) Mashujaa hawa wana nafasi muhimu sana katika historia ya jamii zao, na kwa ulimwengu mzima kwa jumla. 1.4 Maswali ya Utafiti. a) Ni mazingira yepi ya kijamii yaliyowazaa mashujaa Fumo Liyongo na Isa? b) Ni kwa kiwango kipi ambapo sifa za mashujaa hawa zinafanana na kutofautiana? c) Majagina hawa ni muhimu sana kwa jamii zao na kwa ulimwengu mzima kwa jumla. 1.5 Sababu za Kuchagua Mada. Majagina au mashujaa wa utendi wa Kiswahili wanaweza kuwekwa katika vikundi vitatu. Kikundi cha kwanza ni cha mashujaa wa kijadi wa Kiafrika, kwa mfano Fumo Liyongo katika 7 Utendi wa Fumo Liyongo, na Abushiri bin Salim katika Utendi wa Vita vya Wadachi Kutamalaki Mrima. Kikundi cha pili ni cha mashujaa wa kidini, kama mtume Muhamadi na masahaba wake katika Utendi wa Rasil Ghuli. Kikundi cha tatu kinajumuisha mashujaa wa kubuni kama vile Tajiri, katika Utendi wa Masahibu. Kuna uwezekano wa shujaa kuwa katika zaidi ya kitengo kimoja. Mpaka baina ya makundi haya ni finyu mno. Baadhi ya mashujaa wa kidini yumkini wawe ni wa kubuni kama Mungu na Shetani. Hata mashujaa wa makundi hayo mengine wanaweza kutiliwa chumvi sawa na ubunifu. Kama vile tumeonyesha hapa baadaye, tafiti ambazo tayari zimefanywa, zimewalinganisha majagina wa aina moja tu, wawe wa kidini, wa kubuni au wa kihistoria. Hakuna utafiti wa kina tuujuao unaomlinganisha jagina yeyote wa kidini na wa kihistoria au wa kubuni. Hivyo, utafiti huu umenuiwa kuliziba pengo hili. Utafiti huu ni wa kwanza kumlinganisha shujaa wa kidini na wa kihistoria, kutoa sifa zao kama majagina na umuhimu wao kwa tamaduni zao. 1.6 Upeo na Mipaka Ujagina ni mada ambayo ni pana mno ya kufanyia utafiti. Kwa sababu ya wakati, imetuhalisi kujifunga katika kuangazia masuala maalum. Tumechunguza sifa za kishujaa za Fumo Liyongo na shujaa Isa kwa mujibu wa sifa bia za mashujaa. Tumelinganisha na kutofautisha sifa zao na kuonyesha umuhimu wa kila jagina kwa jamii yake. Kuna kazi nyingi ambazo zimeandikwa kuwahusu Fumo Liyongo na Nabii Isa. Kazi za kimsingi ambazo tulizirejelea na ambazo tuliamini zingelifaa katika utafiti huu ni pamoja na Utenzi wa Fumo Liyongo, ulio katika Tenzi Tatu za Kale, kitabu kilichohaririwa na Mulokozi (1999), Miehe na wenzake (2004), ambayo ni kazi iliyokusanya mashairi na nyimbo zinazodaiwa 8 kutungwa na Fumo Liyongo; Takhmisa ya Liyongo, Utenzi wa Nabii Isa, Qurani na Biblia takatifu. Katika utafiti huu, japo jagina tuliyemrejelea ni Nabii Isa kama mhusika wa kifasihi katika Utenzi wa Nabii Isa, tumerejelea Qurani na Bibilia vilevile, ili kujaribu kutoa taswira pana ya ujagina wake, na hali kadhalika kuangazia umuhimu wake kwa jamii yake. Katika utafiti huu, hatujajiingiza katika mjadala iwapo Isa bin Maryamu wa Qurani ndiye Yesu Kristo, mwana wa Mungu wa Bibilia. Tumechukulia kuwa haya ni majina tofauti ya mhusika mmoja akitazamwa na Mkristo au Mwislamu. Majagina huzuka katika mazingira fulani na katika kipindi maalum, ili kutekeleza jukumu maalum katika jamii. Hii ndiyo sababu wanajamii humtazama shujaa wao kama zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hivyo, katika utafiti wetu imetulazimu kuangazia mazingira ya kihistoria ambamo mashujaa hawa wanapatikana. Tumejaribu kufafanua usuli wa jumuiya wanamopatikana Fumo Liyongo na Nabii Isa, ili kuwaelewa majagina hawa kwa kina. Ni katika kuuelewa muundo na hali halisi za kijamii, ndiposa tunaweza kuelewa na kufasili masuala yanayomzunguka shujaa. Kutokana na uelewa wa hali halisi ya kijamii, tunaweza kupata majibu ya maswali yafuatayo: Ni kwa nini shujaa huzuka katika kipindi fulani katika historia ya jamii fulani? Ni sifa zipi ambazo jagina ako nazo na ambazo wanajamii wengine hawana? Mchango wa shujaa katika jamii yake ni upi? 9 1.7 Msingi wa Kinadharia Katika utafiti huu tumeongozwa na nadharia ya Uhakiki wa Vikale. Nadharia ya vikale imetumikizwa katika ulinganishi wa sifa za shujaa Liyongo na Nabii Isa, kwa mujibu wa sifa bia za mashujaa, na vilevile katika kuelezea umuhimu wa shujaa Isa na Fumo Liyongo katika mfumo mzima wa jamii zao. Kulingana na Wafula na Njogu (2007), vikale ni picha kongwe zinazotokea mara kwa mara katika kazi za fasihi.Vikale hivi vinaweza kuwa taswira, wahusika, miundo ya usimuliaji na kadhia zingine zinazopatikana katika fasihi popote pale ulimwenguni. Vikale humwezesha mhakiki wa fasihi kubainisha uhusiano uliopo kati ya fasihi za aina mbalimbali. Abrahams (1981:11-12) kama alivyonukuliwa na Mutiso (2004:21), anaeleza nadharia ya uhakiki wa vikale kwa mitazamo miwili. Ameeleza kuwa chimbuko la nadharia hii ni kutokana na kazi ya James G.Frazer katika kitabu cha “The Golden Bough” (1890-1915), kilichotolewa katika idara ya Anthropolojia Linganishi, chuo kikuu cha Cambridge. Abrahams (khj), anaeleza kuwa kitabu hiki kilifuatilia ruwaza za kimsingi za visasili na za kitambiko ambazo alidai hujirudiarudia katika visakale na taratibu nyingi katika tamaduni anuwai. Kwa upande mwingine, ameeleza kuwa nadharia ya vikale ilitokana na maelezo ya Carl G. Jung kuhusaina na akili-laza. Jung alikuwa mwanafunzi wa Sigmund Freud, mtaalamu aliyeasisi taaluma ya Uchanganuzi nafsia, lakini walitofautiana kimawazo. Wakati ambapo Freud alisisitiza akili-laza ya kibinafsi, naye Jung alisisitiza kuhusu akili-laza jumuishi. Jung alitumia istilahi ya vikale kwenye taswira za asili za kumbukumbu zinazorudiwarudiwa kutokana na tajiriba katika maisha ya tangu mababu zetu wa kale. Alisisitiza kuwa, taswira hizi hurithiwa na kutiwa kwenye akili- 10 laza jumuishi ya jamii ya watu na ambazo hudhihirika katika visasili, ndoto, mawazo ya binadamu mathalan, katika vipengele vyote katika maisha ya binadamu wote duniani na pia katika kazi za kifasihi. Nadharia ya uhakiki wa vikale kwa hivyo, inaeleza kuwa binadamu wote ni sawa popote walipo. Tofauti ni ndogo na za kufikirika ambazo husababishwa na tofauti za kihistoria na za kimazingira. (Mutiso 1999:2), anasema kwa jumla vikale hurejelea ruwaza za kimsingi. Ruwaza jumla au bia za aina moja au nyingine ambazo aghalabu hudhihirika katika jamii za watu mbalimbali duniani. Anashikilia kuwa vikale humvuta msomaji vikitumiwa vizuri katika kazi ya kifasihi (Mutiso 1996: 20 - 23 na Gichamba 2005: 6-7). Kulingana na Wamitila (2002: xi na 2008: 45), fasihi huwa na sifa bia ambazo huzipa uwezo wa kiulinganishi. Anadai kuwa msingi wa fasihi zote duniani ni jamii kwani jamii mbalimbali zimeundwa na binadamu. Kwa hivyo, fasihi mbalimbali duniani huingiliana. Mwingiliano katika masuala anuwai katika maisha ya binadamu ndio huwezesha fasihi kulinganishika. Aidha, ulinganishi huu unatokana na sababu kwamba, fasihi zote ulimwenguni hutumia lugha kama malighafi yao na lugha zote duniani huwa na sifa zinzoshahibiana. Pili, fasihi zote duniani huchota maudhui yake kutoka katika jamii za wanadamu. Wanadamu wote duniani huwa na sifa zinazofanana. Tatu, fasihi hulenga kutekeleza dhima fulani katika jamii, kama vile kuelimisha, kuonya, kufariji, kuburudisha, kuzindua, kuadilisha, kuhamasisha, n.k. Isi 11 Ingawaje kutokana na maelezo ya Abrahams (khj:11-12) kuwa mtazamo wa kisaikolojia pia unaweza kutumiwa kuhalalisha kufanana kwa sifa bia na kushabihiana kwa umuhimu wa mashujaa wote duniani, somo letu limeegemea zaidi katika upande wa anthropolojia. Hebu tujiulize hili swali, kwa nini ruwaza za visasili na matambiko hujitokeza katika visakale na taratibu nyingi za watu mbalimbali duniani? Kujibu swali hili ni sharti tuchukue mtazamo wa kijumla kuhusiana na uelewa wa hulka za kila binadamu katika dunia. Madai kuwa wanadamu wote duniani ni sawa ni ya wazi. Gichamba (2005:8-9) na Mutiso (1999:2) wanaeleza kuwa jamii zote duniani huwa na vipengele vya kimaisha vinavyolandana. Kwa mfano hakuna jamii ya watu duniani isiyokuwa na mavazi, lugha, dini, sheria, katiba (iwe imeandikwa au haijaandikwa) mapenzi, kilimo ∕ ufugaji, wizi, utu, talaka, fasihi , elimu, uuguzi, ukahaba, uchochezi, ufisadi, utabaka, mayatima, ndoa, malezi, muziki, wajane, mapishi, namna ya kufanya mazishi, nk. Vipengele hivi huwa na umuhimu ulio sawa katika jamii zote. Kwa mfano, uamilifu wa mavazi ni kusetiri uchi wa binadamu. Sheria ipo kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika jamii yeyote ile. Hata hivyo, ingawa uamilifu wa vipengele hivi ni sawa, tofauti ni katika utendakazi au utekelezaji wao. Kila jamii ina njia mahususi ya kutekeleza masuala na matamanio mbalimbali kutegemea kiwango cha teknolojia na mazingira ya jamii husika. Werner (1968:18) katika kuchunguza visasili na visakale vya wabantu, alithibitisha uhusiano uliopo katika mila, desturi na lugha zao, dhana ya kuwepo kwa Mungu mmoja, licha ya kwamba wengine hawatofautishi baina ya mawingu au jua, kuamini katika maisha ya baada ya kifo, na kuwa na mawazo kwamba roho za waliokufa zinaweza kuaathiri hali zao za kimaisha kwa kiwango chochote kile. Kutokana na maelezo haya, ni wazi kuwa katika kulinganisha visasili, 12 visakale na matambiko ya jamii tofautitofauti, kuna uhusiano katika ruwaza ya sifa za visasili na matambiko katika tamaduni za jamii mbalimbali. Mutiso (1996:24), akimnukuu Eliade (1957:15–17), anadai kuwa visaasili hufichua muundo wa kweli na anuwai wa hali za wanadamu duniani. Kwa sababu hii, visasili huwa vielezo bora kwa tabia za wanadamu na zinafichua hadithi za kweli. Anashikilia kuwa kwa sababu hiyo, visasili haviwezi kuwa mahsusi, binafsi au vya pekee kwani huchukuliwa kama kielezo mwafaka kwa wanadamu wote duniani. Mutiso (1996: 23), na Gichamba (2005: 9), wanasema kuwa mashujaa, wawe wa kweli au wa kufikirika tu wana jukumu katika uumbaji wa vijana wa huko Ulaya na hasa kutokana na uigizaji wa sifa na tabia za wahusika kwenye ngano zilizo na vitushi vyenye hatari na majabari ya kivita miongoni mwa masuala mengine sawa na hayo. Eliade (khj: 27 – 29), anaendelea kudai kuwa, baadhi ya sherehe zinazoadhimishwa leo zingali zikihifadhi muundo na majukumu ya visasili, na binadamu hufanya hivi kupitia kwa akili laza bila yeye kujua. Kwa mfano, maadhimisho ya mwaka mpya, sherehe za kuzaliwa, ujenzi wa nyumba, sherehe za kupalilia, kuvuna, sherehe za nyimbo. Kwa mfano, Wabajuni kuimba nyimbo za vave, watu kuimba nyimbo za kazi, mazishi n.k ni ishara kuwa binadamu anarudia ya kale (za Adamu na Hawa) bila kujua, kwa jina la mwanzo mpya, mvuko mpya au kubatizwa.Binadamu huzaliwa upya hata wakati anapopewa jina. Katika uponyaji kwa mfano, anarudi kutumia miti shamba. Hata Amri kumi ambazo zimo katika Bibilia zimo katika sheria zetu za kitamaduni. Anashadidi kuwa, (uk. 9) kuna mambo mja anashindwa kuelezea na kwa hivyo anatumia visasili na visakale. 13 Njogu na Wafula (2007: 81 – 82) wakiwanukuu Jung (1972), Cuddon (1997) na Wamitila (2001) wanadai kuwa Jung, akifanya utafiti juu ya njozi na ndoto, alichukulia kikale kama aina ya mtiriko au picha kongwe inayojitokeza mara kwa mara katika tajiriba anayopitia mwanadamu. Wanashikilia kwamba, mtu na utamaduni wake ni nakala ya wanadamu wengine waliokuwepo kabla yake miaka mingi iliyopita. Maoni ya Jung ni kwamba hata kama utu na mtu ni wa kibinafsi, mtu huyu huathiriwa na jamii inayomzunguka. Hawezi kamwe kuepukana na athari zake. Matambiko muhimu anayopitia mtu katika maisha yake, kama vile, sherehe za kumpa mtu jina, za kuingia jandoni na unyagoni, za ndoa na sherehe zinazohusu maziko baada ya mtu kuaga dunia huathiri maisha ya mtu binafsi. Baadhi ya sifa kongwe za mtu zimeazimwa kutokana na wanyama wa porini kama vile, paka, sungura, mbweha, dubu miongoni mwa wanyama wengine. Katika fasihi, mtunzi ataonyesha utu wake, mambo anayopenda na mambo anayochukia kupitia vikale. Kutokana na maelezo ya Gunnep (1960), matambiko mbalimbali ambayo hukumba binadamu wote duniani yana uamilifu sawa kutoka enzi za zamani za mababu zetu hata ikiwa huwa utekelezaji wao ni tofautitofauti kulingana na jamii mbalimbali husika. Matambiko haya ni kama ujauzito na kuzaliwa kwa watoto, kipindi cha utotoni, kushiriki kwa wanadamu katika hafla mbalimbali katika jamii, tohara au jando, kuoa au kuolewa na hata kifo. Kutokana na madai haya, tunaweza kuchukulia kuwa kila jamii duniani huwa na shujaa wao ambaye mara nyingi hupewa sifa zilizo karibu sawa. Tujuavyo ni kuwa, shujaa ni mtu wa kawaida. Lakini kutokana na fikra zilizo katika akili laza za wanajamii mbalimbali tangu jadi, anachukuliwa kama kiumbe asiye wa kawaida na mwenye sifa za kiajabu ajabu. Sifa hizi apewazo shujaa kutoka jamii mbalimbali wengine wote (Gichamba 2005: 9-10 na 1996: 20-23).


>>>>>>ITAENDELEA>>>>>>> 
Powered by Blogger.