SARUFI YA KISWAHILI NA SINTAKSIA
Jina la somo: SARUFI YA KISWAHILI NA SINTAKSIAUfafanuzi wa kozi Sarufi ya Kiswahili na sintaksia ni kozi inayochambua sarufi ya Kiswahili kwa kuzingatia nadharia za sintaksia kama zilivyoasisiwa na wanazuoni wa isimu. Sintaksia ni tawi la isimu linalohusu namna maneno yanavyounda virai na sentensi za Kiswahili. Sintaksia inahusu tungo za lugha ambazo zaweza kuwa ni maneno, virai, vishazi na sentensi. Japokuwa neno ni kipashio cha maumbo, linasadifu kuingia katika sintaksia ya lugha kwani lenyewe lina muundo wake unaotokana na viambajengo vinavyoliunda ambavyo ni mzizi na viambishi. Kozi hii itachunguza nadharia kadha za sintaksia. Awali tutaanza na ubainishaji wa kategoria za maneno tukizingatia umuhimu wake katika sintaksia na muundo wa virai au sentensi. Kozi hii itazingatia zaidi nadharia za msingi za sintaksia kama vile sarufi miundo virai, sarufi zalishi, Nadharia ya ungoekaji na uambatishaji (government and binding). Katika kozi hii virai na sentensi vitachanganuliwa ili kubaini miundo yake. Malengo ya kozi Katika kozi hii wanafunzi wanatarajiwa kufanya yafuatayo: a)Kuelewa maana ya sintaksia b)Kutambua kategoria kuu na kategoria ndogo za sintaksia c)Kueleza umuhimu wa kategoria za sintasia katika kujifunza sintaksia d)kufahamu nadharia mbalimbali za sarufi miundo:Sarufi miundo virai, sarufi patanishi na uteuzi na nadharia X-bar e)kuchanganua sentensi kwa mujibu wa nadharia za sarufi miundoMaudhui ya kozi 1.0 Maana ya lugha na sarufi Lugha ni nini? Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa na watu ili kupashana habari