Nadharia ya Ukuaji wa Lugha
Kuna mambo mbalimbali yanayofanya lugha yoyote ikue. Mambo hayo ni kama vile matumizi ya lugha katika shughuli mbalimbali kama vile:
· Shughuli za utawala na kampeni za kisiasa.
· Shughuli za kibiashara ndani na nje ya nchi.
· Maswala ya Elimu.
· Mikutano ya nchi (kitaifa) na kimataifa.
· Shughuli mbalimbali za kiutamaduni, muziki, sherehe, nk.
· Matumizi ya lugha katika vyombo vya habari kama vile magazeti, redio, televisheni, nk.
· Urahisi wa lugha yenyewe katika kueleweka na kuweza kuchukua maneno ya kigeni au maneno ya utamaduni wa mataifa mengine bila mgogoro.
Urahisi huo wa lugha waweza kuwa katika:
(i) Matamshi yake
(ii) Msamiati
(iv) Miundo
(v) Maana-:mfano neno moja kuwa na maana zaidi ya moja, nk.
(vi) Mwingiliano wa tamaduni mbalimbali na uhamiaji wa kigeni.
(vii) Vita-husababisha kuchangamana kwa watu wengi pamoja na hivyo huweza kusababisha lugha ya utamaduni fulani kuenea na kukua haraka ukilinganisha na lugha za tamaduni nyingine.
(viii) Usanifishaji-husababisha lugha fulani iteuliwe kutumika katika nyanja fulani kama elimu, utawala, biashara, nk. Na hivyo lugha hiyo hukua. Kutokana na usanifishaji ndipo tunapata lugha rasmi na lugha ya taifa.
Hivyo kukua kwa lugha ni hali ya kuongezeka kwa msamiati. Msamiati ni jumla ya maneno yanayotumiwa katika lugha fulani. Ili lugha yoyote ikue lazima msamiati wake ukuzwe.
Sababu za uundaji wa msamiati/maneno ni kama zifuatazo:
(a) Kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambayo huchukua
sura mpya kila siku.
(b) Kwa ajili ya kuweza kutafsiri mengi kutoka lugha yako kwenda lugha ya kigeni au kutoka lugha ya kigeni kuingia katika lugha yako.
© Ili kupata msamiati unaokubalika na shughuli mahsusi kama vile benki, forodhani, Jeshini, nk.
(d) Kwa ajili ya matumizi ya utamaduni wa watu wa taifa hili
au hata taifa jingine. Jambo la muhimu ni kuona msamiati wa Kiswahili unaendelezwa ili kukidhi haja ya watumiaji wa Kiswahili katika kupokea maingiliano ya fani mpya za utamaduni wa kigeni.
(e) Ili kukidhi msamiati wa masomo yote katika lugha yako, ambayo hapa ni Kiswahili.
3.2 Njia za Uundaji wa Msamiati
Njia zinazojitokeza katika uundaji wa msamiati ni kama ifuatavyo:
Njia ya kutumia mpangilio tofauti wa fonimu au vitamkwa: Kila lugha ina fonimu au sauti za msingi ambazo hutumika kujenga silabi ambazo nazo hujenga maneno yote ya lugha husika. Maneno mengi katika lugha huweza kupatikana kwa kubadili mpangilio wa vitamkwa/sauti-fonimu za lugha husika.
Kwa mfano:
Sauti-fonimu /a/, /o/, /n/ zikibadilishiwa mpangilio kwa namna mbalimbali zinaweza kuzalisha maneno kama vile:
(i) o-n-a => ona (ii) => noa (iii) => oana.
Njia ya miambatano yaani kuunganisha maneno: Hapa maneno mawili yanaunganishwa na kuwa neno moja. Kuna aina mbalimbali za miambatano:
(i) Miambatano kati ya jina huru na jina huru.
mwana hewa
mwanahewa
mwana + nchi mwananchi
Afisa + misitu Afisamisitu
(ii) Miambatano kati ya Nomino na Kivumishi.
Mla + mbivu Mlambivu#000000 solid;margin:15px;width:95%;">
Mwana + kwetu Mwanakwetu.
(iii) Miambatano kati ya jina tegemezi na jina huru. Jina tegemezi linatokana na kitenzi.
Mpiga + maji Mpigamaji.
Mpiga + mbizi Mpigambizi
(iv) Miambatano kati ya kitenzi na jina.
Piga + mbizi pigambizi
Pima + maji pimamaji
Kutohoa maneno: Kila lugha ina uwezo wa kuchukua maneno kutoka kwenye lugha nyingine ili kukidhi haja ya mawasiliano kulingana na maendeleo ya jamii. Kiswahili nacho kimechukua maneno kutoka lugha mbalimbali za kigeni na lugha za Kibantu na kuyatohoa ili kusadifu misingi ya sarufi yake.
Mfano:
(a) Kiingereza:
(i) tractro => trekta => trekita => terekita
(ii) plaugh => plau => pulau
(iii) shirt => sheti => shati
(iv) geography =>jiografia => jografia
(v) machine => mashine
(b) Kiarabu:
(i) laki => pokea
(ii) ahadi => milele
(iii) dhaifu => nyonge
(iv) ila => isipokuwa
© Kireno:
(i) bibo => bibo
(ii) roda => roda
(ii) mesa => meza
(iii) copa => kopa
(d) Kiajemi:
(i) bandar => bandari
(ii) dirisha => dirisha
(iii) kod => kodi
(iv) pilao => pilau.
(e) Kihindi:
(i) achari => achari
(ii) biyme => bima
(iii) ghati => gati
(iv) lakh => laki
(f) Kijerumani:
(i) schule => shule
(ii) hella => hela
(g) Kutoka Lugha za Kibantu
(i) faculty => kitivo <kipare/kisambaa.
(ii) composite => kivung <kipare
(iii) state house => ikulu <kigogo/kisukuma
(iv) national assembly => bunge<kigogo/kisambaa
(v) fluid => ugiligili <kinyakyusa
Njia ya urudufishaji: Hii ni njia ya kurudia neno, likawa neon moja.
Mfano:
(i) kimbele => kimbele mbele
(ii) pole => pole pole
(iii) kinyume => kinyume nyume
(iv) kimya => kimya kimya
(v) kizungu => kizungu zungu
Kwa njia ya kufupisha maneno: Njia ya kufupisha maneno inachukua ama herufu ama silabi ya kwanza ya kila neno lililojitokeza katika jina zima la mahali au kitu funi.
Mfano:
(i) Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili => TUKI
(ii) Baraza la Kiswahili Tanzania => BAKITA
(iii) Chama Cha Mapinduzi => C.C.M
(iv) Baraza la Mitihani la Taifa => BAMITA
nk.
Njia ya kutumia mnyambuliko na uambishaji: Neno jipya huundwa kwa kuunganisha viambishi kwenye mzizi au shina la neno. Njia hii hukuza lugha bila taabu kwani maneno ya lugha nyingi yanaweza kunyumbuliwa na kuambishwa, kama ifuatavyo:
(a) Mnyambuliko wa Majina:
(i) taifa => taifisha => taifishwa => taifishiwa. nk.
(ii) soma => somea => somesha => someshea => someshwa => someshewa => somesheka => , nk.
(b) Mnyambuliko wa Vitenzi:
(i) piga => pigana => pigisha => pigishwa => pigishia => pigia => pigiana, pigika, nk.
(ii) cheza => chezana => chezesha => chezeshwa => chezeshea => chezeana => chezwa => chezeka, nk.
© Mnyambuliko wa Vivumishi:
(i) fupi => fupisha => fupishia => fupishwa => fupishiwa => => fupishana => fupishika, nk.
(ii) safi => safisha => safishana => safishia => safishiana => safishika, nk.
(d) Mnyambuliko wa Vielezi:
(i) haraka => harakisha => harakishana => harakishika => harakishia => harakishiana, nk.
Njia ya Kutumia Uambishaji
(i) taifa => utaifa, mataifa, utaifishaji, nk.
(ii) piga => kupigana, anapiga, nk.
(iii) safi => msafi, wasafi, nk.
(iv) haraka => kuharakisha, nk.
Njia ya kufananisha sauti/umbo: Baadhi ya maneno ya Kiswahili yametokana na mwigo wa sauti au dhana ya kitu fulani.
Mfano:
(i) Piki-piki- piki-piki => pikipiki,
Neno ambalo limetokana na mwigo wa sauti (mlio) wa chombo husika.
(ii) tu-tu-tu => mtutu (wa bunduki)
neno ambalo limetokana na mwigo wa sauti ya risasi inapotoka kwenye bunduki baada ya kufyatuliwa.
(iii) kifaru
Hii ni zana ya kivita ambayo imepewa jina hilo kutokana na umbo lake lililofanana na mnyama aitwaye kifaru.
Njia ya vijenzi/viundaji: Mara nyingi vijenzi huunda neno ambalo huwa nomino. Vijenzi hupachikwa mwishoni mwa kitenzi ili kiwe nomino. Maneno yanayojitokeza huwa na maana na ngeli tafauti tafauti.
Vijenzi vitumikavyo ni kama ifuatavyo:
Kijenzi Kitenzi Nomino
{i} jenga mjenzi
linda mlinzi
soma msomi
panda mpanzi
{ji} winda mwindaji
soma msomaji
sema msemaji
cheza mchezaji
linda mlindaji
{o} soma somo/masomo
sema msemo/misemo
cheza mchezo
{u} kua ukuu
tulia utulivu /mtulivu
tukuka utukufu/mtukufu
choka uchovu
{e} teua mteule
tuma mtume
kata mkate
umba kiumbe
3.3 Vigezo Vitumikavyo Kupima Ukuaji wa Lugha
Vigezo vitumikavyo kupima ukuaji wa lugha ni kama ifuatavyo:
(i) Matumizi katika nyanja mbalimbali kama vile elimu, dini, utawala, biashara, nk.
(ii) Kupanuka kwa msamiati wenyewe.
(iii) Kupanuka kwa miundo katika lugha.
(iv) Kupanuka katika maana na maneno.