Misamiati
Misamiati
Majina ya Ukoo
- Baba - mzazi wa kiume
- Mama - mzazi wa kike
- Dada - Ndugu wa kike (hutumika sanasana kurejelea ndugu wa kike mkubwa)
- Kaka - Ndugu mkubwa wa kiume.
- Babu – Baba wa babako au mamako
- Nyanya - Mamake mama au baba.
- Shangazi – ndugu wa kike wa Baba
- Mjomba – ndugu wa kiume wa mama
- Mpwa – mtoto wa nduguyo wa kike/kiume
- Umbu – jina wanaloitana ndugu wa kike na wa kiume
- Amu – ndugu wa kiume wa Baba
- Wifi – jina linalotumika baina ya mke na ndugu wa kike wa mume
- Mkaza mjomba – mke wa mjomba
- Binamu – mtoto wa shangazi/mjoma/amu
- Mkwe - mzazi wa mkeo.
- Mavyaa – mama mkwe
- Bavyaa – Baba mkwe
- Mkaza mwana – mke wa mwanao
- Mvyele – mzazi
- Mwana - mtoto wako (hasa wa kiume)
- Binti - mtoto wako wa kike
- Mjukuu - mtoto wa mwanao
- Kitukuu - mtoto wa mjukuu
- Kilembwe - mtoto wa kitukuu
- Kining’inia - mtoto wa kilembwe
- Shemeji - jina linalotumika baina ya mwanamke na ndugu za mumewe.
Ulemavu
1. Kiwete - asiyeweza kutembea wala kusimama
2. Kibongoyo - asiye na meno
3. Kigugumizi - aliye na shida za kutamka maneno
4. Bubu - asiyeweza kuongea
5. Kiziwi - asiyeweza kusikia
6. Kipofu – asiyeona
7. Matege - mwenye miguu iliyopinda
Malipo
1. Ada - malipo kwa mganga au ya hospitali
2. Karo - malipo kwa ajili ya mafunzo (shuleni)
3. Nauli - malipo ya kusafiri
4. Kiingilio - malipo yanayotozwa watu ili kushiriki katika jambo Fulani
5. Marupurupu - pesa za matumizi ya kila siku
6. Ushuru - malipo kwa serikali
7. Fidia - malipo kwa mtu baada ya kumkosea
8. Kiinua mgongo - malipo anayotoa mtu kama shukrani kwa jambo alilotendewa au analotaka kutendewa
9. Riba – malipo ya ziada yatokanayo na mkopo
10. Mtaji – Kianzio katika bihashara inaweza kuwa pesa au rasilimali
11. Kodi - malipo ya pango au uendeshaji wa biashara,bidhaa au kifaa
Kazi
1.dobi: hufanya kazi ya kuosha nguo
2.karani: anayeangalia matumizi ya pesa katika benki au kampuni fulani
3.katibu: anayeweka rekodi za mambo na orodha mbalimbali katika kampuni au idara fulani
4.kungwi: hufunza vijana jandoni
5.mchuhuzi: anayeuza bidhaa kutoka nyumba hadi nyumba
6.mfinyanzi: hufinyanga udongo kutengeza vyombo kama vyungu, n.k
7.mhandasi: anayefanya kazi ya kuunda au kurekebisha injini/mashine mbalimbali
8.mhasibu: mtu anayefanya kazi ya hesabu
9.mhunzi: hufua vyuma
10.mkatabi: anayeweka rekodi za vitabu katika maktaba, na kuwasaidia wanaotaka kuomba vitabu.
11.tabibu: anayetibu watu
12.topasi: kazi ya kuosha vyoo