Repoa: Wananchi wachoshwa na ukata, wataka fursa za kujikwamua
Dar es Salaam. Taasisi ya Utafiti wa Kupunguza Umasikini
(Repoa) imeiomba Serikali kutoa nafasi kwa wananchi waweze
kutoa maamuzi katika mambo yanayowagusa ili kuwakwamua kiuchumi na
kuwapunguzia machungu ya umasikini.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar-es-salaam Mtafiti Mwandamizi
wa repoa, Lucas Katela alisema wamefanya utafiti huo ili kujua
uhusiano uliopo kati ya kukua kwa uchumi na huduma za kijamii.
Aliongeza
kuwa utafiti huo uliofanyika mwaka 2014 ulionyesha ongezeko la
uchumi kwa asilimia 7 huku hali za wananchi zikiwa mbaya.
“Serikali
imekuwa ikisifika kuwa uchumi umeongezeka kwa kiasi kikubwa
lakini kama uchumi umeongeza Serikali itakuwa na rasilimali za
kutosha na huduma kwa jamii zitakuwa zakutosha,”alisema Katela.
Aidha
Katela aliongezea kuwa wananchi wana machungu kuona baadhi
ya pesa zinapotea kiujanja huku wananchi wakikosa huduma za
kijamii.
“Wananchi hawafurahii ukuaji wa uchumi
kutokana na kudorora kwa huduma za jamii , Serikali kutokuwa wazi
kutoa matumizi ya fedha, wananchi wanaona kama rushwa
imeongezeka kila sekta,” alisema.
Katela
alisisitiza kuwa Serikali iwe wazi na matumizi ya fedha pamoja
na kuboresha huduma za jamii na kodi zinazo kusanywa zitumike
kwa busara kutoa huduma bora kwa wananchi.