Papa Francis na alyiekuwa papa Benedict
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amedokeza kwamba huenda akafuata nyayo za mtangulizi wake Papa Benedict kwa kujiuzulu.
Akihojiwa na runinga moja ya nchini Mexico katika sherehe za maadhamisho yake ya pili tangu achaguliwe,Papa Francis amesema kuwa anahisi kwamba uongozi wake katika kanisa hilo hautaendelea kwa kipindi kirefu.
Amesema kuwa hatua ya Benedict kujiuzulu mwaka 2013 ni ya ujasiri na haifai kuchukuliwa kama ya kipekee.
Papa Benedict ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo kujiuzulu tangu papa Gregory wa 12 mwaka 1415.
Papa Francis anasema kuwa anatamani maisha yake ya kuwa muhubiri na angependelea kuzuru maeneo kadhaa bila kujulikana.