Kimbunga chafanya uharibifu Vanuatu
Kimbunga kikali kimekumba kisiwa cha Vanuatu katika kile umoja wa
mataifa unasema kinaweza kuwa janga baya zaidi kuwahi kulikumba eneo la
pacific.
Kuna hofu kuwa huenda idadi ya watu waliokufa ikaongezeka.Kimbunga hicho kwa jina Pam kilikuwa na upepe unaovuma kwa kasi ya kilomita 250 kwa saa , mvua nyingi na upepo mkali.
Kimeng'oa paa za nyumba na miti na kukata nguvu za umeme.
Mawasiliano yametatizika na huenda uharibifu sehemu zingine utajulikana baada ya siku kadhaa.
Maelfu ya watu walikimbilia usalama kwenye kambi za muda lakini wengine walisalia makwao.
Kimbunga hicho tayari kimesababisha uharibifu mkubwa maeneo mengine ya kusini mwa pacific vikiwemo visiwa vya kiribati na Solomon.