Mlinzi wa Dr. Slaa Akanusha tuhuma za kutaka Kumuua Dr. Slaa
Khalid Hamada Kangezi aliyekuwa mlinzi wa Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willbroad Slaa,
amekanusha taarifa iliyotolewa na viongozi wa chama hicho kwamba alitaka
kumdhuru kiongozi huyo na akasisitiza yeye ndiye aliyenusurika kifo
baada ya kufungiwa chumbani kwa zaidi ya saa sita na viongozi wa chama
hicho wakiwa wanamsulubu akiwa uchi wa mnyama.
Amesema
alifanyiwa hivyo akishinikizwa asaini karatasi ya maelezo
kuwa ana njama na watu wa usalama wa taifa (TISS) kutaka kumpa sumu Dk.
Slaa ambapo alisaini karatasi hiyo ili asiuawe kwani tayari kulikuwa na
begi
lenye visu vilivyoonekana kutaka kutumiwa dhidi yake.
Juzi uongozi wa Chadema ulitoa taarifa kwamba mlinzi huyo anahusika
pamoja na watu wengine, wakiwemo viongozi wa Chama Cha Mapianduzi (CCM)
na Usalama wa Taifa katika njama za kumdhuru na kumuua Dk. Slaa.