Mh.Zitto Kabwe amesema hana taarifa za kufutwa uanachama Chadema.


Siku moja baada ya mahakama kuu kutupilia mbali ombi la mbunge wa Kigoma kaskazini Mh Zitto Kabwe kujadiliwa na vikao vya Chadema kuhusu hatma ya uanachama wake na kutakiwa kulipagharama za kesi hiyo mbunge huyo amedai kuzisikia taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari lakini hana taarifa rasmi.
Hayo ndio yalikuwa majibu ya awali ya mbunge huyo wa Kigoma kaskazini alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
 
Mara baada ya mahakama kutoa uamuzi wake haraka mwanasheria mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Mh Tundu Lisu akazungumza na vyombo vya habari kuhusu Chadema kutomtambua Mh Zitto kama mwanachama wa chama hicho ambapo ili kusikia kauli ya Mh Zitto kuhusu suala hilo ITV ikafika katika ofisi ndogo za bunge zilizoko jijini Dar es Salaam na kumshuhudia Mh Zitto akiongoza vikao vya kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu ya mashirika ya uma PAC ambapo baada ya kumalizika kwa kikao hicho akazungumzia maamuzi hayo ya mahakama na Chadema baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari.
 
Aidha kutokana na madai hayo Mh Zitto amesema kwa kuwa hana taarifa rasmi ijumaa ya wiki hii atakwenda jimboni kwake kuzungumza na wananchi wa jimbo lake kama mbunge na kisha jumanne ya wiki ijayo atahudhuria vikao vya bunge kama kawaida na kuongeza kuwa tukio hilo linamkomaza kisiasa na kwamba siasa zake ni zakujadili masuala na si watu kama walivyo baadhi ya wanasiasa wenzake.
 
Pia amezungumzia hatma ya mustakabali wake kisiasa na kuelezea mahusiano yake na chama cha demokrasia namaendeleo Chadema kwa sasa.
 
Powered by Blogger.