vijembe vya Putin kwa mataifa ya Ulaya
Vijembe vya Putin kwa mataifa ya Ulaya
Rais
Vladmir Putni wa Urusi ametumia hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa
kushambulia mataifa ya Magharibi ambayo amesema yamekuwa na unafiki
mkubwa juu ya hali ilivyo nchini Ukraine.
Bwana Putin alisema kuwa
kama pasingekuwa na matatizo Ukraine wakati huu mataifa ya Magharibi
bado yangalikuja na swala lingine la kujaribu kudhibiti Urusi.Alisema pia kuwa Urusi haitakubali kusambaratika jinsi ilivyofanyika katika taifa la Yugoslavia.
Bwana Putni alisema kuwa Uchurmi wa Urusi unakabiliwa na changamoto nyingi siku za mbeleni, lakini akasisitiza kuwa vikwazo hivyo vitasaidia Urusi kuunda mbinu mwafaka za kujitegemea.
Rais aliwahimiza waekezaji kurudi tena Urusi kwa kutangaza kuwa hakutakuwepo na upekuzi juu ya uhalifu wa fedha au kama kulikuwepo na wizi wa kodi juu ya rasilmali itakayoingizwa nchini.
Alisema Urusi ni mahali salama zaidi kwa Warusi kuhifadhi pesa zao.
chanzo;bbcswahil