CUF yasema Ukawa imeanza kuleta matumaini ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
CUF yasema Ukawa imeanza kuleta matumaini ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba amesema
umoja wa vyama ulioundwa wakati wa mchakato wa katiba mpya marufu Ukawa
umeanza kuleta matumaini ya kushinda katika uchaguzi mkuu ujao hapo
mwakani baada ya kufanya vizuri katika uchaguzi wa serekali za mitaa
ulio malizika hivi karibuni.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadahara ulio hudhuriwa na umati
mkubwa wa wananchi wa mkoa kaskazini Pemba kwenye uwanja wa Jadida wete
amesema umoja huo umepata mafanikio makubwa licha ya kasoro nyingi
zilizo jitokeza katika uchaguzi huo wa serekali za mitaa.
Kwa upandewake katibu mkuu wa chama hicho Malim Seif Sharif Hamad
amesema ingawa uchaguzi huo niwamara ya kwanza lakini mungano huo wa
vyama umeweza kuonyesha umoja na mshikamano na kuleta mafanikio.
Mapema mwakilishi wa jimbo chakechake Omar Ali Shehe aliwataka wana
chama wachama hicho kufata utaratibu ulio wekwa kwa masheha kuchukua
vitambulisho vyao vya mazanzibar mkaazi iliwajiweke tayri kujiandikisha
katika daftari lakudumu la wapiga kura nae makamo mwenyekitu wa CUF Juma
Duni Haji amewataka wananchi kuhakikisha wanajiandisha ilikuweza kila
moja wao kuwa mpiga kura.