Mvua kubwa isiyotabirika yaja, TMA yatahadharisha wananchi
Mvua kubwa isiyotabirika inatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika ukandMvua kubwa isiyotabirika inatarajiwa kunyesha katika maeneo mbalimbali
nchini hasa katika ukanda wa Pwani ya Kaskazini, maeneo ya Dar es
Salaam, Tanga, Unguja na Pemba; pia katika ukanda wa Kaskazini Mashariki
kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Dar es Salaam. Mvua kubwa isiyotabirika inatarajiwa kunyesha
katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika ukanda wa Pwani ya
Kaskazini, maeneo ya Dar es Salaam, Tanga, Unguja na Pemba; pia katika
ukanda wa Kaskazini Mashariki kwa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na
Manyara.
Akitoa taarifa ya hali ya hewa jana kwa
Januari na Februari mwaka ujao, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania (TMA), Dk Agness Kijazi alisema mvua ya msimu katika
maeneo hayo inatarajiwa kwisha leo.
Hata hivyo, alisema
mvua kubwa ya nje ya msimu inatarajiwa katika kipindi cha Januari,
2015. Dk Kijazi alisema hali kama hiyo pia itaikumba mikoa ya Kagera,
Mwanza, Shinyanga na Geita.
“Maeneo mengine yanayopata
msimu mmoja wa mvua kwa mwaka yatakuwa na mvua ya wastani. Maeneo hayo
ni Mbeya, Rukwa, Katavi, Iringa, Lindi, Dodoma na Mtwara.
Dk
Kijazi alisema mvua hiyo inasababishwa na ongezeko la joto
linalolifanya anga kushindwa kutengeneza unyevunyevu ambao hugeuka kuwa
mvua. “Ninawashauri wananchi kuchukua hatua ya kujikinga na athari za
kiafya na mazingira zinazoweza kusababishwa na ongezeko la joto
linaloendelea sambamba na mvua kubwa inayonyesha,” alisema Dk Kijazi.
Juzi,
mvua kubwa ilinyesha jijini Dar es Salaam kwa saa mbili na kusababisha
vifo vya watu wawili katika Wilaya ya Kinondoni kuleta kero kwa wasafiri
wanaotumia vyombo vya moto na watembea kwa miguu.
Mitaa ya Azikiwe, Bibi Titi na Morogoro ambayo juzi ilijaa maji, jana ilionekana kuwa mikavu baada ya maji yote kukauka.
huku watumiaji wa barabara wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.
Yusuph
Said, mmoja wa wafanyabiashara wa magezeti Mtaa wa Azikiwe, alisema
eneo hilo hujaa maji kila mvua inaponyesha na kuwasababishi kufanya kazi
yao katika mazingira magumu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni, Camillius Wambura aliliambia gazeti hili jana kuwa hakuna
madhara zaidi yaliyotokea ukiacha matukio ya watu wawili kufariki dunia
kutokana na mvua hiyo.
Naye Kamanda wa Polisi Ilala,
Mary Nzuki alisema: “Mkoani kwangu sijapokea taarifa yoyote ya maafa
yaliyosababishwa na mvua mpaka sasa.” Kamanda Kihenya Kihenya wa Mkoa wa
Kipolisi Temeke naye alisema hajapokea taarifa yoyote ya maafa.
Akizungumzia
matukio ya mvua kipindi cha Oktoba – Disemba, 2014, Dk Kijazi alisema
maeneo mengi ya nchi yalipata mvua za wastani hadi juu ya wastani
isipokuwa maeneo machache ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Dodoma
(Hombolo), Kilimanjaro (Same), Njombe, Mtwara na Lindi ambayo yalipata
mvua za chini ya wastani.
Mkurugenzi huyo aliongeza
kuwa matukio ya mvua hizo ambayo yaliambatana na vipindi vifupi vya
upepo mkali, yalisababishwa na kuimarika kwa ukandawa mvua magharibi mwa
nchi ambao uliambatana na kuwepo kwa makutano ya upepo.
“Wananchi
wajenge pia utamaduni wa kupanda miti ili kusaidia kupunguza kasi ya
upepo unaombatana na mvua kubwa ambazo zinaweza kusababisha uharibifu wa
mali na madhara kwao,” alisisitiza Dk Kijazi.
Peter Elias, Bakari kiango na Hadija Salum.