KANISA LA FUGWA BAADA YA MCHUNGAJI KUFUMANIWA KANISANI


Mwanzoni mwa Mwezi July 2014, Mchungaji Michael Semeni wa Kanisa la 
Living Word Ministry lililopo Ukonga-Majumba Sita jijini Dar es Salaam 
alifumaniwa live akijiandaa kuvunja amri ya sita na muumini 
wake ambaye ni mke wa mtu ndani ya ofisi yake.
Mchungaji Semeni alinaswa akiwa na mwanamke huyo aitwaye Erizabert Kisanda, 
mkazi wa jijini Mwanza ambaye alifika Dar kuonana naye kwa ajili ya 
kumwombea maombi maalum ya kiroho 'deliverance' kutokana na matatizo 
ya mke huyo kushika mimba na kutoka kila wakati."Huyu mwanamke alikuja 
Dar kwa mchungaji kwa lengo la kuombewa apate mtoto. Alikuwa na tatizo 
la uzazi kwani kila alipopata ujauzito, akikaribia kujifungua tu mimba 
inaharibika."Kutokana na tatizo hilo, ndipo akashauriwa akamwone 
mchungaji huyo ndipo akafunga safari kwenda kumuona na kumweleza 
tatizo lake, mchungaji akamwambia ni tatizo dogo sana
kwake."Anasimulia shuhuda wa mkasa huo.Ilizidi kudaiwa kwamba, 
ahadi ilipangwa ambapo mwanamke huyo alitakiwa kurudi siku hiyo ya 
tukio.Siku ya tukio, mwanamke huyo alifika kuombewa ambapo mchungaji 
huyo alizama kiroho zaidi kwa muda wa saa mbili."Baada ya kumaliza 
maombi hayo ndani ya kanisa ndipo mchungaji huyo akamchombeza kwa 
kumwambia wazame chumbani akamwombee zaidi,"chanzo kilisema.Habari 
zaidi zinadai kuwa wakiwa chumbani sasa, mke hana nguo, mchungaji 
akiwa ndani ya kipensi tu, mwanaume aliyedaiwa ni mume na dada yake 
walitokea kusikojulikana na kuwavaa, hali iliyosababisha tafrani 
kubwa.Kuhusu kilichotokea baadaye baada yafumanizi hilo ni kwamba 
kanisa hilo limefungwa. Mara baada ya waumini wake kuona fumanizi la 
baba mchungaji huyo walisusa kwenda kanisani hapo.Habari zilizonaswa 
kutoka kanisani hapo kutoka kwa muunini mmoja zilidai kuwa baba 
mchungaji huyo ameingia mitini na hajulikani alipo."Ilikuwa ni aibu 
kubwa sana kwa mtumishi wa Mungu. Baada fumanizi lile, baba mchungaji 
hajaonekana tena na kanisa limefungwa,"alisema mmoja wa waumini hao




:
Powered by Blogger.